Vodacom yahonga Wabunge Blackberry

Vodacom yahonga Wabunge Blackberry

Vodacom hata mimi wananipa simu mpya kila mwaka mwaka wa nne huu, kwa sasa ni BB ya tatu na kila wakinipa simu mpya wananipa na maongezi ya bure. Kwa kuwa ni mteja wao mzuri na hawataki nihame.

Dunia zingine sasa hivi simu ni bure bora utumie mtandao wao tu, kwa sasa hapa kwetu zinakwenda kwa "targeted market" lakini itafika huko kwa bure kwa wote ushindani ukizidi. Biashara ni matangazo, ujuwe hizo zinatoka kwenye bajeti yao ya matangazo, hiyo inaitwa "directional promotion" na si hongo hilo.

zomba cursed!
 
mmh.sijui kama kwelikwelii,jamani hawa vodacom c wangewapa japo manesi au maaskari zikawasaidia ktk utendaji kazi wao!?
 
Katika hatua ambayo imeibua mjadala mzito katika kipindi hiki cha Bunge la Bajeti, Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom imemwaga Blackberry kila moja ikiwa na thamani ya Shilingi laki 7 na muda wa maongezi wa Shilingi 100, 000 ka wabunge 23 wa kamati ya Miundombinu akiwemo Spika wa Bunge Anna Simamba Makinda.

Baadhi ya Wabunge wameripotiwa kukataa simu hizo huku Mwenyekiti wa Kamati hiyo Peter Serukamba na Spika Anna Makinda wakidaka ofa hiyo kiulaini.

Source; Gazeti la MWANAHABARI la leo

My Take:
Si kwamba huu ni mkakati wa Vpdacom kuzima kelele za Wabunge ambao wamekuwa wakidai kuwa makampuni ya simu yamekuwa yakiwakamua wananchi vya kutosha na yamekuwa yakilipa kodi kiduchu?

Kama habari hii ni ya kweli basi bunge letu linanuka rushwa na kuna kila sababu ya kujisafisha katika hili.
Tulianza na kuelezwa na Kafulila kwamba kuna baadhi ya wabunge waliomba rushwa katika halmashauri lakini spika wa bunge akaitia kapuni hoja hiyo.
Baada ya muda mfupi mbunge mmoja, miongoni mwa watuhumiwa wa Kafulila akakamatwa na kushitakiwa na Takukuru kwa mashitaka ya kuomba na kupokea rushwa.
Sasa kama wabunge wengine nao wamepokea simu kutoka vodacom, wakati huu ambapo wananchi tunahitaji serikali kuhakikisha kwamba makampuni ya simu yanachangia pato la taifa kwa kulipa kodi stahili, wao wameamua kugawa simu kwa wabunge, basi hakuna sababu ya kutoamini kwamba hiyo ni rushwa ya waziwazi, na katika hili nategemea Takukuru ifanye kazi yake kikamilifu wala isisubiri mashinikizo.
 
Mi hata niliposikia Vodacom hawako ktk orodha ya walipa kodi wakubwa sikushangaa, Mtu yeyote makini angetegemea voda kutolipa kodi inavyositahili, Kwani Watanzania waliona hisa voda wametajwa kwenye UFISADI na mwingine alijivua Gamba ccm, Pili kuhonga wabunge hizo simu si ajabu kwani Spika wa bunge Pius Msekwa aliwahipewa Uenyekiti wa Boi ya Vodacom, na watu wakalalamika inakuaje spika kuwa mwenyekiti wa bodi ya vodacom. Sasa ktk mazingira haya Unategemea nini toka Vodacom, eti kampuni inayoongoza kuwa na wateja wengi Tanzania then isiwemo ktk walipa kodi wakubwa, na sasa hiyo ni Rushwa kuwaziba mdomo wabunge
Katika hatua ambayo imeibua mjadala mzito katika kipindi hiki cha Bunge la Bajeti, Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom imemwaga Blackberry kila moja ikiwa na thamani ya Shilingi laki 7 na muda wa maongezi wa Shilingi 100, 000 ka wabunge 23 wa kamati ya Miundombinu akiwemo Spika wa Bunge Anna Simamba Makinda.

Baadhi ya Wabunge wameripotiwa kukataa simu hizo huku Mwenyekiti wa Kamati hiyo Peter Serukamba na Spika Anna Makinda wakidaka ofa hiyo kiulaini.

Source; Gazeti la MWANAHABARI la leo

My Take:
Si kwamba huu ni mkakati wa Vpdacom kuzima kelele za Wabunge ambao wamekuwa wakidai kuwa makampuni ya simu yamekuwa yakiwakamua wananchi vya kutosha na yamekuwa yakilipa kodi kiduchu?
 
Kwanini wasiulizwe hao wala rushwa, na ni kwanini kwa kamati hiyo tu.
 
Kwani spika naye yuko kwenye kamati ya miundombinu au,kama walitaka kutoa wangetoa kwa wabunge wote tujue sio hii ya kulenga.
 
The CCM is a crime syndicate, Most members and MPs of CCM are corrupt. No conceince, No brains no nothing, just bunches of criminal and theft. Corruption cost mlalahoi in street.:embarassed2:--------Mzalendo
 
Vodacom hata mimi wananipa simu mpya kila mwaka mwaka wa nne huu, kwa sasa ni BB ya tatu na kila wakinipa simu mpya wananipa na maongezi ya bure. Kwa kuwa ni mteja wao mzuri na hawataki nihame.

Dunia zingine sasa hivi simu ni bure bora utumie mtandao wao tu, kwa sasa hapa kwetu zinakwenda kwa "targeted market" lakini itafika huko kwa bure kwa wote ushindani ukizidi. Biashara ni matangazo, ujuwe hizo zinatoka kwenye bajeti yao ya matangazo, hiyo inaitwa "directional promotion" na si hongo hilo.

Directional promo ni sawa ila nadhani tatizo analoliona mleta uzi ni hasa kuhusu NANI kapewa na kapewa katika muktadha upi. Hawa waheshimiwa wapo katika kamati ambayo inawamulika hawa Vodacom
 
Hata kama ni wema na uungwana ndoo utolewe kipindi hiki cha bunge la bajeti jamani???? Kwa kweli binafsi kama kweli wamepewa kuna mantiki kuhisi kwamba hii ni rushwa
 
Rushwa ni rushwa tu iwe ndogo au kubwa. Na hii ni aina moja wapo warushwa.

Kimsingi ni kuwa Vodacom wameonyesha tu namna Wabunge wetu walivyokuwa hawana uelewa wa mambo. Katika nchi nyengine hii ingechukuliwa kama tusi kwa Wabunge, kupewa zawadi za aina hii ambazo sio zinakaribia kuwa rushwa, bali rushwa dhahir' shahir'
 
Basically Hawa Voda through M pesa Wamepora Kabisa Kazi za mabenk ambao wengi ni walipa Kodi!! Mbaya zaidi hawa mabwana Hawalipi Kabisa Kodi Kwenye Hiyo Biashara!! Hawa Watunga Budget wamekaa tu hawaoni hata Hiyo ni big source ya Mapato / Kodi!! Tangu lini mlipakodi halali anakwenda Bungeni Kuwapooza Wabunge?? Hapa Ujue Kuna Wizi mkubwa sana!! Mbona sijawaona Airtel wala TBL Wakijipendekeza Bungeni ili hali ni walipakodi Wakubwa!! Shame on this people!! Wanatoa Vinawati Hamsini na kukwepa kodi ya Mabilioni!!

Hapana si kweli.

Transaction zote za wakala wa Mpesa zinapitia bank. Hao wamewapatia bank kazi nzuri sana na wateja wapya wengi sana.
 
Kama Spika na mwenyekiti wa kamati ya bunge inayohusika na miundo mbinu hawatasimama bungeni na kutoa kauli ya kukanusha hii taarifa basi watanzania wanayo haki ya kuamini bunge letu na hasa Spika na Mwenyekiti wamepokea rushwa toka Vodacom.

Wanatakiwa watoe kauli loud & clear kama wamepokea simu toka Vodacom, kwanini wamepokea simu, na ilikuwaje wakapokea simu. Ni muhimu wananchi wawe na imani. Hizi taarifa zinachafua bunge kuanzia kiti cha Spika.
 
Vodacom hata mimi wananipa simu mpya kila mwaka mwaka wa nne huu, kwa sasa ni BB ya tatu na kila wakinipa simu mpya wananipa na maongezi ya bure. Kwa kuwa ni mteja wao mzuri na hawataki nihame.

Dunia zingine sasa hivi simu ni bure bora utumie mtandao wao tu, kwa sasa hapa kwetu zinakwenda kwa "targeted market" lakini itafika huko kwa bure kwa wote ushindani ukizidi. Biashara ni matangazo, ujuwe hizo zinatoka kwenye bajeti yao ya matangazo, hiyo inaitwa "directional promotion" na si hongo hilo.
Mbona hatupewi sisi watu wa kawaida na ni wateja wao wa muda mrefu??
 
Inabidi ujiunge na "post paid" services, mbona ni wengi tu wanaopata hizo.

zomba, ina maana kati ya wabunge wote only kamati ya miundo mbinu na Spika ndio wamejiunga na 'post paid' services?
 
Hapana si kweli.

Transaction zote za wakala wa Mpesa zinapitia bank. Hao wamewapatia bank kazi nzuri sana na wateja wapya wengi sana.

Mkuu transaction zinapitaje benki? Can you explain? Maana wengi tunajua suala la M-PESA, Airtel Money, Tigo Pesa na Z-Pesa ni biashara ya mitandao hii.

Actually na mimi ni miongoni mwa watu wanaohoji sababu ya Serikali yetu kutokuchukua kodi kwenye transactions hizi. Kuna mapato maengi sana kwenye eneo hili.
 
Kama Ni kweli hiyo Ni Rushwa. Wanataka wawanyamazishe Midomo.
 
Mimi ningechukua Hiyo BB na Vocha juu. Na ningesimama kidete kuponda Walipe kodi.
 
Back
Top Bottom