Vodacom: Mgodi wanadai mkopo kwa fujo sana

Vodacom: Mgodi wanadai mkopo kwa fujo sana

Mfumo wao hauko vizuri.

Wanataka eti niwalipe KWANZA Songesha hiyo 250k, halafu nikiwa sina deni Songesha...ndio mfumo wao uruhusu kukata 10k.

Sasa bro, sasa hivi 250k naitoa wapi Mimi...aah sio kweli bhana!!
Mgodi hawakati mpaka ulipe mwenyewe. Ila ukipitiliza muda deni linaongezeka.

Wananidai 150k
Ila mie nawalipa + uwa na save kwenye kakibubu kao.
 
Mgodi walinikopesha 15500, wanadai jamani sio poa nilikaa miezi 5 nikaja lipa sasa hivi wamenifungia kukopa.

Siku moja walipiga simu nikampa apokee mtoto aseme mama hayupo nae akasema " mama amesema hayupo" [emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Basi yule baba akamwambia mtoto mwanangu usiwe mwongo kama mama yako ni dhambi kwa Mungu mama si yupo hapo akajibu eeeh yupo. Nilijisikia aibu sana siku hiyo
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Straight to the point:

Line zangu mbili za VODACOM zina mikopo ya:

1. Songesha (250,000 Tsh)
2. Mgodi (10,000)

Daah hawa jamaa MGODI sijui Wana njaa. Aisee wanadai mkopo wao vibaya sana.

Nilishapigiwa simu na wao kwà namba tofauti tofauti zaidi ya mara 5 , wanataka 10,000 yao.

You guys (MGODI) kama mmo humu, asee ebu niacheni kidogo kwanza asee.

Mbona Songesha hawajawahi nipigia simu na wananidai pesa nyingi tu? Why you? Aah sio kweli bhana!
hao wote cha mtoto,kopa MPAWA,mkopo wa mwezi mmoja,yakipita masaa 2,tangu wakukopeshe,wanaanza kukumbusha kulipa deni..
 
Tatizo wao, hata pesa ikiingia MPESA hawachangamki kuitoa chap kama wafanyavyo songesha.

Mgodi wamelala sana. Ningekua nishawalipa kitambo sana.
Mimi singesha nilisikia bado wanazonikata kila siku. Sasa wanajikuta 6500 kila.mwezi wanasema Vodacom Bima. Sijawahi ugua ila wananikata. Ngoja wajichanganye kwenye huduma ya mkopo wowote ndio nitarudisha pesa zangu. Naanza na chomoka kesho au keshokutwa niweke wewe la 25000 wanaloniambia kwenye gari kisha itakuja nyingine then mwaka mzima sitaweka wala kutoampesa kwenye Mpesa zaidi ya kupiga na kupokea hadi wanisamehe kama walivyonisamehe kwenye songesha. Pumbavu sana.
 
Kuna dogo aliniomba atumie line yangu ya mpesa sasa kawapiga matukio yaani songesha ni takriban 360k na wezesha ni 900+k sasa nifanyeje jamani sasa hivi wananisumbua mimi japo niko mbali na dogo aliye na line??
Pole sana
 
Straight to the point:

Line zangu mbili za VODACOM zina mikopo ya:

1. Songesha (250,000 Tsh)
2. Mgodi (10,000)

Daah hawa jamaa MGODI sijui Wana njaa. Aisee wanadai mkopo wao vibaya sana.

Nilishapigiwa simu na wao kwà namba tofauti tofauti zaidi ya mara 5 , wanataka 10,000 yao.

You guys (MGODI) kama mmo humu, asee ebu niacheni kidogo kwanza asee.

Mbona Songesha hawajawahi nipigia simu na wananidai pesa nyingi tu? Why you? Aah sio kweli bhana!
😂😂😂Kwa sasa Kuna Kampuni za Kenya ndo zinafanya hii online mikopo.Kule kwao Ruto aliwakimbiza so wamekuja huku.Sio mgodi tu Kuna hawa wengine na hivi vi app vyao,wanapigia mpaka ukoo wako mzima wakuimize ulipie deni la buku 10.🤣🤣
 
Nimeingia mgodi nimechukua 100000 maajabu wamenipa 82000 hii imekaaje
 
Mbongo ni mtu ambaye anapenda sana kupokea kuliko kutoa, ni watanzania wachache sana ambao wanatambua nini maana ya deni/mkopo.

Wengi Huwa wanachukua tu pesa uku wakikubaliana na mashariti, lakini hawajui kulipa na ukimkumbusha kulipa deni anaona ni kero kubwa sana.

Mtanzania kutokulipa au kukwepa deni kwake anaona ni ujanja au akili na anajivunia kabisa kama tunavyoona kwenye huu Uzi hapa.

Huu utamaduni wa kukwepa na kukimbia madeni umepelekea taasisi nyingi za mikopo kufa kila uchwao. Ni utamaduni Fulani hivi wa ovyo sana lakini wabongo ndio kwanza mnajivunia.

Binafsi sasa hivi sishauri kabisa mtu yeyote au kampuni yoyote itoe huduma za mikopo kwa wabongo, wabongo ni watu wa ovyo sana.
 
Mgodi walinikopesha 15500, wanadai jamani sio poa nilikaa miezi 5 nikaja lipa sasa hivi wamenifungia kukopa.

Siku moja walipiga simu nikampa apokee mtoto aseme mama hayupo nae akasema " mama amesema hayupo" [emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Basi yule baba akamwambia mtoto mwanangu usiwe mwongo kama mama yako ni dhambi kwa Mungu mama si yupo hapo akajibu eeeh yupo. Nilijisikia aibu sana siku hiyo
"Simu Iko chaji mama hayupo"..... "Mama Yuko bafuni"...."mama kaenda kumuona mgonjwa"...

Na hii ndio kawaida yenu, kumpa mtoto aongee uongo kwa niaba yako matokeo yake vitoto vyenu vinakuwa viongo viongo tu kama nyie mama zao!

Imagine huyo mwanao akija kufikia umri kama wako atakuwaje? Si atakuwa muongo hata ibilisi nyoka anasubiri.

Ni mara kumi ukapokea tu simu ukaongea tu huo uongo wako wewe mwenyewe.
 
Back
Top Bottom