Vodacom: Mgodi wanadai mkopo kwa fujo sana

Vodacom: Mgodi wanadai mkopo kwa fujo sana

Sawa, lakini naona kama hawakujipanga vizuri. Mbona M-PAWA wameikuta na haina issue za kukopesha pesa kirahisirahisi.

Mimi sikua nimesave chochote MGODI, nashangaa, kukopa 10,000 kitu kikaitika. Na Wana bahati cause kiwango changu cha kukopa kilikua 60k.

Note: M-PAWA huwezi kukopa kama haujasave chochote
We jamaa unachekesha, M-pawa
Wengi wenu mmewatapeli sana ..
 
Mgodi walinikopesha 15500, wanadai jamani sio poa nilikaa miezi 5 nikaja lipa sasa hivi wamenifungia kukopa.

Siku moja walipiga simu nikampa apokee mtoto aseme mama hayupo nae akasema " mama amesema hayupo" [emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Basi yule baba akamwambia mtoto mwanangu usiwe mwongo kama mama yako ni dhambi kwa Mungu mama si yupo hapo akajibu eeeh yupo. Nilijisikia aibu sana siku hiyo
Unakopaje mgodi? Mm niliomba nikaambiwa niweke 1000 lakin bado inakataa nikitaka kukopa na line iko vizur kwenye miamala

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Unakopaje mgodi? Mm niliomba nikaambiwa niweke 1000 lakin bado inakataa nikitaka kukopa na line iko vizur kwenye miamala

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Sidhani kama lazima uweke hela ninachojua ukikopa ukalipa mapema ndio wanakuongezea mkopo. Mimi walinikopesha bila kuweka hata cent jaribu tena. Menu ya mpesa namba 5 mikopo na akiba, nenda mgodi halafu angalia kiwango wanachoweza kukukopesha
 
Straight to the point:

Line zangu mbili za VODACOM zina mikopo ya:

1. Songesha (250,000 Tsh)
2. Mgodi (10,000)

Daah hawa jamaa MGODI sijui Wana njaa. Aisee wanadai mkopo wao vibaya sana.

Nilishapigiwa simu na wao kwà namba tofauti tofauti zaidi ya mara 5 , wanataka 10,000 yao.

You guys (MGODI) kama mmo humu, asee ebu niacheni kidogo kwanza asee.

Mbona Songesha hawajawahi nipigia simu na wananidai pesa nyingi tu? Why you? Aah sio kweli bhana!
Hahaha vipi kuhusu pesa X weeee niliwazungusha mpaka sasa hawapigi tena
 
Unakopaje mgodi? Mm niliomba nikaambiwa niweke 1000 lakin bado inakataa nikitaka kukopa na line iko vizur kwenye miamala

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Mpaka ukiwa na shida maalum. Inakubali bila kuweka hata buku.

Nasikia jamaa hukutizama kupitia camera iliyopo mbele ya simu Yako.

So unapokua una apply mkopo.....FANYA kama unasikitika hivi....
 
Kuna hawa wengine wa kuitwa Mpawa. Wanatuma msg za kibabe na vitisho pamoja na kupiga simu
 
Attachments

  • Screenshot_20230912_184851_Messages.jpg
    Screenshot_20230912_184851_Messages.jpg
    38.3 KB · Views: 7
Sidhani kama lazima uweke hela ninachojua ukikopa ukalipa mapema ndio wanakuongezea mkopo. Mimi walinikopesha bila kuweka hata cent jaribu tena. Menu ya mpesa namba 5 mikopo na akiba, nenda mgodi halafu angalia kiwango wanachoweza kukukopesha
Umemsikia MzeeKipusa kwamba inabid usikitike ni kweli

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom