Vodacom Kumlipa Fidia ya Mabilioni aliyebuni Huduma ya "Tafadhali Nipigie"

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
80
96
Vodacom yaamriwa kumlipa fidia ya Mabilioni aliyebuni Huduma ya "Tafadhali Nipigie"

Mahakama ya juu ya Rufaa Nchini Afrika Kusini imetupilia mbali rufaa ya Vodacom dhidi ya mbunifu wa Huduma ya “Tafadhali nipigie”, Kenneth Makate ambaye alikuwa Mfanyakazi wa Vodacom

Aidha, Mahakama imeiamuru Vodacom imlipe Makate kati ya asilimia 5 hadi 7.5 ya jumla ya mapato yaliyotokana na Huduma hiyo kwa zaidi ya Miaka 18 iliyotumika, pamoja na riba.

Makate alikuja na wazo hilo zaidi ya Miaka 20 iliyopita alipokuwa na uhusiano wa mbali na Mkewe, ambaye wakati huo alikuwa Mwanafunzi. Mzozo kati yake na Vodacom ulianza Mwaka 2007

Mtendaji Mkuu wa zamani wa Vodacom alimuahidi Makate fidia kwa ubunifu wake, lakini baadaye Kampuni ilisitisha Mpango wa kufanya hivyo pale Huduma hiyo ilipofanikiwa.

Wazo la "Please Call Me" linamsaidia Mtumiaji asiye na muda wa Maongezi kuweza kutuma ujumbe wa Maandishi kwa mwingine ili kumshawishi ampigie Simu.
 
bilionea mpya huyo
 
Back
Top Bottom