Mfahamu Nkosana Makate, mvumbuzi wa huduma ya Please Call Me

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
13,773
20,165
Nkosana Makate ni raia wa Afrika Kusini ambaye alivumbua huduma maarufu ya ‘Please Call Me’ ama ‘Tafadhali Nipigie ‘, uvumbuzi ambao mpaka sasa kesi bado ipo mahakamani kufuatia kutokukubaliana fidia na mtandao wa simu ya Vodacom.

650.jpeg

Makate anadai jumla ya bilioni 75 za Kitanzania ikiwa ni kama fidia kutoka katika kampuni hiyo ya Vodacom nchini Afrika Kusini
Kampuni ya Vodacom mwanzoni ilikuwa imekubali kulipa Makate Milioni 354 za Kitanzania ambayo mvumbuzi huyo wa Please Call Me alikataa.

Mzozo wa kampuni hiyo na mvumbuzi Makate upo Mahakamani. Huduma ya ‘Tafadhali Nipigie’ ililetwa sokoni kwa mara ya kwanza mnamo 2001.

Hii ni huduma ya sms ya bure ambayo inaruhusu wateja kutuma ujumbe kwa mtumiaji mwingine anayeomba apigiwe simu. Mvutano kati ya Makate na Vodacom umekuwepo kwa zaidi ya miaka 20 sasa.

Mahakama imetakiwa kutathmini upya fidia aliyopewa kama ilivyohesabiwa na Mtendaji Mkuu wa Vodacom Shameel Joosub. Hii ilifuata uamuzi wa Mahakama ya Katiba mnamo 2016 ambapo Vodacom iliamriwa kufanya mazungumzo na Makate ili kupata fidia ya haki.
 
amevumbua nini? Nikisema Nakojoa/nakunya/natema mate etc , mfano, nimegundua nini hapo
Acha kujitoa akili! Umeambiwa amevumbua mfumo wa huduma ya please call me katika mawasiliano ya simu. Ukisema unakunya/ unakojoa si kinywa chako tu kinakuwa kimeamua kuropoka! Yaweke hayo maneno yako machafu katika mfumo rasmi wa mawasiliano ambapo kila anayehitaji kuyatumia hatalazimika kuyaandika ila atabofya codes flan then ujumbe unafika ulipokusudiwa.
 
Muda mwingine mpumbavu hujibiwa kwa upumbavuu safii sana.
 
Amevumbua nini? Nikisema Nakojoa/nakunya/natema mate etc, mfano, nimegundua nini hapo, au sielewi nieleweshe

Ungelijua kiasi gani mvumbuzi wa JUST DO IT usingesema maneno hayo bali ungelikuwa unachakarika kuvumbua neno nawe ule mpunga wa maana.
 
Back
Top Bottom