monotheist
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 720
- 943
Mimi sio mtumiaji sana wa mtandao wa vodacom mnamo mwaka 2022 nilihamasika kusajili laini ya vodacom kutokana na masuala ya miamala hivyo ilinilazimu kusajili laini ya voda na baada ya kumaliza zoezi langu sikuitumia tena
Nikarudi tena kuitumia mwaka 2023 sababu ya visa card huwa natumia kulipia bidhaa alibaba na AliExpress pia mimi si mpenzi wakukopa pesa kwenye mitandao ya simu kwa kifupi sijawahi kukopa pesa mtandao wowote wa simu
Wiki mbili zilizopita nilirushiwa pesa na mteja wangu huwa ninatabia ya kutoa hizo pesa na kuweka bank basi baada ya kupokea sms ya muamala kutoka kwa mteja hapohapo zilifuata sms 3 zote zikionyesha nimekatwa pesa kutoka songesha
Nilihamaki sana ikabidi nipige customer care wakanipa jibu kwamba kiasi kilichokatwa hakijakatwa kimakosa kwani nilikopa songesha 04/01/2021. Duu nilishikwa na mshangao ikabidi niwapigie tena sasa wakarudi nyuma zaidi wanadai nimekopa tarehe 08/12/2020 na poukweli ni kwamba nimesajili laini mwaka 2022 na sijawahi kukopa songesha
Huu ni utapeli wa wazi kabisa mnanilazimisha nikubali deni ambalo halinihusu mtafuteni aliyewakopa mpeni deni lake na mimi mnirudishie pesa yangu la sivyo huu ndo utakua mwisho wa kutumia vodacom mimi na vizazi vyangu kama master card hata tigo na airtel wanayo