Voda na Halotel mtuonee huruma

Voda na Halotel mtuonee huruma

Hahahaha eti aizike kabisa. Ila ni bora kuwa na universal modem kwa hali ya mitandao ya nyumbani.[
Hivi mpaka leo mnatumia modem huoni kama unaingia gharama mara mbili yaani kifurushi cha line ya kwenye modem na ya kwenye simu, kwa nini usitumie simu ukawasha WiFi hotspot kisha ukatumia internet hiyo kwenye computer?
 
Nashauri mtu kama hana hizi pc za kisasa zenye sehemu ya kupachika laini atumie Wi-fi ambayo anaweza kuipata kwa kununua kirouter kidogo au kuigeza smartphone yako kuwa router kwa kuwasha Hotspot
 
Duh! Cheki navyo kula bata kwa mrija,yani vodacom speed yake ni 7mb/s na halotel ni 15mb/s..Pole mkuu
Mtafute Magu atumbue hilo jipu
 
Huwa nikinunua bundle ya Tsh.500/= VodaCom,napewa 150 MBs plus Doubled 150 MBs nyingine (ofa ya ongea deilee)...Ila ajabu zikiisha zile 300 MBs naendelea kutumia internet hadi 5 to 6 GB bila kukata japo tayari sms ya kunitaarifu kwamba "bundle niliyoinunua imeisha" inakuwa imeshatumwa...
MAMBO YOTE HAYA NI KUANZIA ASUBUHI HADI SAA TISA KAMILI ALASIRI...

Je, Hii ni ofa ya huku Mbeya au ni ya wateja wote? Nina wiki ya pili tangu nigundue hii kitu, ....nina-download movies,games,music hadi PC inataka kujaa...
youtube,TV online ndo nimepatia pa kuzichekia!
HEBU JARIBUNI NA NYIE, labda hii ni OFA ya "kimyakimya"
NB: (natumia modem ya Airtel inayokubali LINE zote za simu)
 
Voda miyeyusho mi nipo arusha nazo modem mbili bahati mbaya zote voda kinachoniboa inasoma hspa au 3g na mashine ipo stationery inakuwaje mara edge mara gprs mi sielewi yaani full kuboreka.Kama ishu ni speed wanatupa bundle labda 1gb au whatever kitumike kiishe ninunue kingine.Mbwembwe za nini?Hata kwenye simu yaleyale.
 
Mkuu kuigeuza smartphone ku-access internet ktk PC kunaua betri. Battery life cycles zinakwisha kwa kasi ya kimbunga. Labda utumie occassionally.
 
wandugu, nilikuwa mbeya, wiki nzima kila nikinunua kifurushi cha internet (kutumia kwenye computer sio simu), hela yangu inaenda bure, network iko chini mno na hela inaisha tu bure. ninaanza na modem ya voda, inasumbua sana iko chini sana network, nikija halotel ambayo wameniuzia garama kuliko hata hizo nyingine, nayo iko chini sana. ninyi wafanyakazi wa voda na halotel tafadhali, kuweni na huruma, mmetuuzia hizi modem zenu za nii kama network ndio hii:

wakuu kwa wale walioko tigo, zantel na airtel, mtusiadiie, hasa wale wanaoishi mbeya, mtandao ukoje, manake nahisi hizi modem mbili nitazitupa.
Nenda na laptop yako duka la Airtel waulize kama unaweza kupata network nzuri, ikiwezekana wakupe yao ujaribu. Vile vile network inakuwa chini kutokana na eneo unaloishi kama ni bondeni taabu utaipata au kama upo mbaaaalii sana na mnara. Ok jaribu njia hizo bro
 
hivi moderm nzuri ni ipi, wataalam mtueleze tafadhali.
Universal modem ndiyo nzuri, ambayo inakubali laini yoyote. Kwa hali ya mitandao ya nyumbani ni vema kuwa na modem aina hiyo. Lakini pia, vema kuwa na inayokubali 3g na 4g. Mfano kuna hizi zinaitwa HSDPA ni nzuri sana na bei nafuu.
 
Mkuu kuigeuza smartphone ku-access internet ktk PC kunaua betri. Battery life cycles zinakwisha kwa kasi ya kimbunga. Labda utumie occassionally.
Nunua power bank kuliko kuwa na modem gharama inazidi zaidi
 
Back
Top Bottom