Ukiachana na VPN na TOR hii njia pia inaweza kukusaidia ku-access blocked sites au apps kwenye internet kwa kubadili DNS Servers

kali linux

JF-Expert Member
May 21, 2017
1,996
5,045
Hello bosses.......

Kuna muda matumizi ya internet yanabanwa kiasi fulani hivyo kufanya watu wengi waishie kutumia VPN. Japo matumizi ya VPN yanaonekana kuaminiwa sana ila kiukweli mara nyingi hizi free au cheap VPN haziko safe sana sana kwenye privacy yako kwa sababu wao wanapata browsing history yako yote. Kiufupi unapotumia VPN ni kwamba unaiomba computer fln ilioko nchi nyingine ikusaidie kutafuta kitu fln kwenye internet kisha ikikipata inakuletea. Kwa mechanism hio haiitaji kuelezewa pages nyingi kwamba privacy yako iko matatani.

Kuna njia mbadala kadhaa unazoweza kutumia kusolve hii issue ya blocked sites au apps, zamani nilielezea njia ya kutumia TOR ambapo kwa watumiaji wa kawaida wanaweza kuitumia kwa kudownload ORBOT App kutoka Playstore na ni Bure kabisa coz TOR ni opensource project na iko very secure. Maelezo zaidi kuhusu hio njia unaweza yapata kwenye huu uzi wangu Tumia TOR kama mbadala wa VPN

Ukitumia TOR kuna changamoto pia ya kuwa blocked kwa sababu IP address nyingi zinazotolewa na TOR zimekuwa blacklisted na baadhi ya server kwa matumizi mabaya. IP Address ichukulie kama namba ya simu unayotumia ukiwa una-access internet. Sasa kuna baadhi ya hackers hutumia TOR kufanya attacks zao na ndio maana server nyingi zinablock hizo IP.

Hivyo leo nimeamua kuleta njia nyingine kwa wale wanaotumia Routers au Home Internet, njia hii itaweza kuwasaidia kuepuka baadhi ya blocks kutoka kwa ISP. Kiukweli njia hii ni kama by product ya DNS Poisoning. Na kuielewa zaidi inabidi uwe na uelewa kidogo khs namna Internet inavyofanya kazi na mifumo baadhi inayosaidia kutimiza hilo. So nitaelezea kwanza hayo mambo mawili kiufupi na kiurahisi kabisa hapa chini.

HOW INTERNET SURFING IS ACHIEVED
--> Internet ni mkusanyiko wa server ama computer nyingi zilizounganishwa na zinazotoa huduma mbali mbali. Hizi ni machine***(note this). Ukitaka kutafuta kitu fln kutoka kwenye internet unafanya kutafuta computer (server) ambayo imebeba na inatoa hicho kitu unachotafuta. Hizo computer hazina majina kama ilivyo kwetu binadam kwa kuwa zenyewe ni machine. Servers hizo (computers) zinatumia address maalum iliopo kwenye mfumo wa numbers na ni rahisi kwa machine kudeal na numbers kuliko text. Hizo address kwa kitaalamu zinaitwa IP ADDRESSES. Sasa kwakuwa hizo namba ni ngumu kuzikariri(coz kuna watu hata namba zao za simu hawajakariri) ndio maana yanakuja matumizi ya DOMAIN NAMEs. Domain name ni kama vile jamiiforums.com ama facebook.com hio inakusaidia kupata website fln moja kwa moja na kukusaidia kupata kitu unachokitaka kutoka kwenye internet.

--> Lakini kumbuka nimesema servers ni machines na zinatambuana na kutambulika kwa IP Addresses na sio majina ama hizo domain names. So lazima kuna njia ya kuzitafsiri hizo domain names kuja kuwa IP ADDRESSES. Chukulia hii kama phonebook ya sim yako. Unatunza jina na namba then unakua unasearch kwa jina tu. Hio kazi ya kutafsiri DOMAIN NAMES kuwa IP ADDRESSES inafanywa na servers maalum zinaitwa DNS SERVERS, Na hapa ndipo ilipo njia mojawapo (Kati ya nyingi) ambayo hutumiwa na mitandao ya simu kublock sites au apps ambazo haitaki wewe uzione.

--> Hizo DNS Servers zichukulie kama ndio phonebook yako coz zimejaza records kwamba mtu akiandika domain name fln basi inamaanisha IP Address fln. So kitu cha kwanza kabisa kinachofanyika unapoenda kuandika domain name kwenye browser yako mfano jamiiforums.com ni kwamba hio domain inapelekwa kwenye DNS server unayotumia kisha DNS server inarudisha IP Address na browser yako inaendelea kukuconnect kwa kutumia hio IP Address.

--> Unapotumia mtandao wa simu basi huo mtandao ndio ISP wako (Internet Service Provider). Na Ndio anakua na control kwa DNS Server ipi wewe mtumiaji utaitumia. Wengi wanalazimisha utumie DNS servers wao na percent kubwa ya wanaofanya hivyo ndio hutumia njia nnayoenda kuelezea hapo chini kublock baadhi ya sites usizione wewe mtumiaji.

MITANDAO INATUMIAJE DNS SERVERS KUBLOCK SITES
--> Kama nilivyosema hapo juu hii ni njia mojawapo kati ya nyingi ambayo mitandao inatumia kublock hizo sites, njia nyingine ni kama kutumia firewalls, packet filtering etc...
Kwa kuwa Mtandao unakua umesha kusetia DNS Server ya kutumia na hio DNS server mara nyingi huwepo ndani ya infrastructure zao basi pale browser inapotuma request ya kutambua IP Address ya domain name fln (unayotaka kusearch) hio DNS Server itaangalia kama hio domain name ni blacklisted kisha kutuma invalid response kwa browser na hivyo browser kushindwa kuendelea na request, browser itakachofanya ni kukwambia 'Cannot connect to this server' kwa sababu imepata invalid response kutoka kwa DNS Server. Ni kama vile utumie namba ambayo sio sahihi kumpigia mtu ukidhani hio namba ni sahihi (Tukilinganisha na mfano wa phonebook).

NAMNA YA KURUKA HICHO KIZUIZI
--> Kwa kuwa mchezo mzima unahusisha DNS servers basi njia rahisi ya kuruka hicho kizuizi ni kubadili DNS Server unayotumia. Kwa watumiaji wa moja kwa moja wa internet (Wale mnaotumia line zenu kwenye simu directly) inakua ngumu kubadili hizi DNS settings. Lakini kwa wale mnaotumia Routers au Modems manaweza fanikisha hilo kwa kubadili address ya DNS Server kifaa chako kinayotumia.

--> Siwezi sema hapa namna ya kubadili hizo settings kwenye kila aina ya Router na Modem coz kuna brands nyingi lkn nitakupa basics za kufuata. Modems na Routers nyingi zinakuja na option ya 'Use automatic DNS Server selection' na baadhi kati ya hizo zinaruhusu user kubadili DNS Server address manually. Hio option mara nyingi ipo kwenye network configuration upande wa routers.

DNS SERVER IPI YA KUTUMIA BADALA YA HIZI ZITOLEWAZO NA MITANDAO YA SIMU(ISP)
--> Google wana DNS server zao ambaz ndizo narecommend zitumike kwa sababu ya uhakika wa usalama. IP Address za hizo DNS Servers zao ni 8.8.8.8 na 8.8.4.4. Kwa wale mnaoweza kubadili DNS Server setting option kwenye Router zenu mnaweza kujaribu kutumia DNS Server za google na endapo kama mtandao wako wa simu umeblock hizo sites kwa njia hii basi sites zitaweza kufunguka bila shida.


MWISHO:
Kama nilivyosema kuna njia nyingi ISP hutumia kublock sites ambazo hawataki watumiaji waone. Endapo njia ilotumiwa na ISP inahusisha filtering upande wa DNS Server wanayotumia basi hii njia nloelezea hapa itafanya kazi lkn kama wametumia njia nyingine kublock basi ni vema kutafuta njia nyingine ili uweze kuaccess internet bila bugdha. Vile vile hii njia inafaa kwa watumia wa routers na modem. Japo kuna uwezekano kidogo wa watumiaji wa simu pia kuweza kutumia hii njia lkn inahitaji research zaidi.


Peace.
~Kali Linux
 
Kuna chimbo langu moja ilikua free ni website ila saivi wameweka malipo...sasa mkuu ukipata namna dondosha uzi jinsi ya kuaccess website za kulipia
 
Samahani wakuu nje ya mada kidogo!

Nimeibiwa simu pamoja na laini zangu, kwa maana hiyo nimepoteza namba za simu nyingi sana nilizokuwa nawasiliana nao.

Je, kuna namna ya kufanya kuweza kuzipata?

Nawasilisha.
 
Samahani wakuu nje ya mada kidogo!

Nimeibiwa simu pamoja na laini zangu, kwa maana hiyo nimepoteza namba za simu nyingi sana nilizokuwa nawasiliana nao.
Je kuna namna ya kufanya kuweza kuzipata?

Nawasilisha.
Kama ulikua umeweka account ya google(gmail) unayoikumbuka mara nyingi google inasync contacts zako so ukinunua simu mpya ukaweka hiohio account ya google contacts zitarudi.

Pia kama ulikua unatumia fb kwenye namba mojawapo kati ya hizo na ulisync contacts zako fb basi utaweza zipata tena ukinunua simu mpya na ukalogin kwa hio hio fb account
 
Jamani nimeomba msaada mwenye kujua jinsi kufanya ili nizipate hizo contacts

cc kali linux
 
Kuna siku moja jamaa mmoja aliweka link hapa ukiifungua tu unazikuta contact zako za miaka nenda rudi ambazo zimehifadhiwa fb.

Nimeshindwa namna ya kuitafuta hiyo link mwenye ujuzi naomba msaada
 
Kuna siku moja jamaa mmoja aliweka link hapa ukiifungua tu unazikuta contact zako za miaka nenda rudi ambazo zimehifadhiwa fb.

Nimeshindwa namna ya kuitafuta hiyo link mwenye ujuzi naomba msaada
umejaribu ulichoelekezwa hapo juu comment #13 ?
 
Back
Top Bottom