Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,505
- 51,107
Nimepita maeneo ya feri Dar es Salaam kwa ajili ya kuvuka kwenda upande wa Kigamboni. Nilichokiona pale kwa kweli kimenifikirisha na kunitafakarisha sana na kunifanya niwaze sana juu ya mustakbali wa nchi hii.
1. Kuna dalili kampuni ya Azam imepewa dili kinyemela kufanya kazi ya kuvusha watu feri
Mwanzoni, walitupiga changa la macho eti kuna tatizo la hali ya hewa, na hivyo kivuko cha Azam kimeletwa ili kusaidiasaidia. Cha ajabu mpaka leo hii hivyo vivuko vinaendelea kufanya kazi, wakati vile vivuko vya MV Kigamboni na MV Magogoni ni vizima.
2. Vivuko vya MV Magogoni na MV vipo na vinaendeshwa polepole Makusudi ili kuvipa nafasi vivuko vya Azam
Inaelekea kuna mpango mkakati wa kuwafanya watu wavizoee vivuko vya Azam pale feri. Nilichokishuhudia, Pale kuna vivuko vinne, Viwili ni vya Azam na viwili ni vya serikali(MV Magogoni na MV Kigamboni), Cha ajabu, Vivuko vya serikali vinaendeshwa polepole kuliko ilivyokuwa zamani.
Yaani nimeshuhudia MV Kigamboni ikikaa upande wa feri kwa takriban dakika 40, bila kuondoka huku Kivuko cha Azam kikiwa kimepiga trip mbili kwenda na kurudi kigamboni. Hii kama siyo hujuma kwa Vivuko vya serikali ni nini?.
3. Maisha ya wananchi yanawekwa hatarini kwa jinsi wanavyotolewa ndani ya sehemu ya kusubiria vivuko na kupangwa nje karibu na ukingo wa maji kusubiri vivuko vya Azam
Kikawaida watu huwekwa ndani ya hall la kusubiria kivuko, kikishafika geti linafunguliwa na kivuko kikishashusha watu na Magari ndo geti linafunguliwa na watu kuruhusiwa kuingia. Cha ajabu nilichokishuhudia leo, kwa kuwa vivuko vya Azam ni vidogo basi askari anawatoa watu nje ya hall ya kusubiria watu mapema kabisa kabla watu wanaoshuka hawajaisha. Maana yake ni iwamba Ujio wa kivuko cha Azam umeondoa hata kusudio la yale mahall ya kusubirisha abiria. Na hata usalama wa Abiria.
4. Ninachokiona
Huenda Kampuni ya Azam, inapewa dili na wakubwa wachache serikalini ili itoe huduma ya kuvusha watu licha ya kuwa vivuko vya serikali vipo pale.
Kampuni ya Azam kupewa kandarasi ya kutoa huduma siyo tatizo iwapo
1. Tenda inatangazwa kwa uwazi
2. Usalama wa wanajchi unazingatiwa ipasavyo
3. Serikali inapata faida
Kilicho dhahiri inaelekea Azam ya Mzee Bakhressa inapigiwa pande kinyemela ktk hii ishu, ambayo dhahiri shahiri kuna harufu za watu kuwa na 10% zao pale.
Hapa Chini ni picha ambayo wananchi wametolewa kwenye hall ya kusubiria kivuko, wamepangwa nje foleni wakisubirie kwa nje. Hii ni hatari sana, na ni very local
Hapa Chini, Kivuko cha MV kigamboni kimekalishwa zaidi ya dakika 40, huku kikiwa na watu ndani na magari huku Kivuko cha Azam kikipiga trip tu kwenda na kurudi, Sijui hawa Azam wanalipwa kwa idadi ya Trips wanazopiga?