Vituko vya Waziri Muhongo

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospiter Muhongo, anaweza kuwa waziri mwenye vituko kuliko wote kwa mwaka uliopita 2013 na mwaka huu mpya wa 2014.

Mbali ya kituko cha mwaka jana cha kukataa kupanda ndege akipinga kuwekwa kwenye daraja la kawaida, safari hii waziri huyo ameanza mwaka kwa kituko kingine cha kumshambulia na kumuumbua Kamishna wa Madini, Injinia Ally Samaje mbele ya ujumbe wa Waziri wa Mafuta, Gesi na Madini wa Algeria, Youcef Yousif.

Tukio hilo lilitokea juzi wakati Waziri Yousif alipokuwa na mazungumzo na ujumbe wa Wizara ya Nishati na Madini nchini, wakiongozwa na Waziri mwenye dhamana, Profesa Sospiter Muhungo.

Chanzo cha tukio hilo kilikuwa hivi: Vyanzo vyetu vya habari kutoka ndani ya kikao hicho nyeti, vilisema kuwa baada ya wageni hao kuwasili ndani ya ukumbi wa mikutano wa wizara, Kamishna wa Madini alikuwa na kazi ya kuwasilisha mada kuhusu sekta ya nishani na madini, hususani masuala ya gesi.

"Akiwa katikati ya mada yake, Waziri Muhongo alisimama kutoka kwenye kiti chake na kuanza kumfokea Kamishna Samaje kwamba mada aliyokuwa anawasilisha ni ya kijinga na haikuwa na hadhi ya kuwasilishwa mbele ya ugeni ule.

"Alisema kwa lugha ya Kiingereza na kwa kupaza sauti na kila mgeni aliyekuwapo ukumbini alisikia. Lilikuwa tukio la aibu na kituko cha mwaka, na kamishna alijisikia vibaya sana," alisema mtoa habari wetu.

Kwa mujibu wa habari hizo, hata baada ya kutolewa maneno ya kukatisha tamaa, Kamishna aliendelea na mada yake hadi mwisho na alipokuwa anazungumzia changamoto zinazoikabili sekta ya madini nchini, Waziri Muhongo alimshambulia tena mbele ya wageni kwa kusema hizo sio changamoto.

Waziri Muhongo atoa ufafanuzi

Akijibu tuhuma hizo, Waziri Muhongo alisema kwa uzoefu wake wa kufanya kazi sehemu mbalimbali duniani, hawezi kukubali kuona uwasilishaji wa mada usiokidhi viwango akaendelea kuunyamazia.

Waziri Muhongo alisema katika uwasilishaji wa mada yoyote, lugha inayotumika ni kitu muhimu, hivyo mada ya kamishna wake ilikuwa na tatizo la lugha kwani ingesababisha wasikilizaji kushindwa kuifuatilia na kuijadili.

Majibu yake kwa ujumla yalikuwa hivi

Mara ya kwanza Waziri Muhongo alipopigiwa simu, hakuipokea na badala yake alituma ujumbe mfupi wa maandishi kuwa yupo katika mkutano.
Hata hivyo, gazeti hili lilimuandikia ujumbe mfupi ukimuuliza kama tukio hilo la kumfokea mwenzake hadharani haliwezi kushusha hadhi ya nchi mbele ya wageni, na kama hali hiyo haimaanishi kutokuwepo mawasilino mabaya katika wizara hiyo.

Katika majibu yake ya awali kupitia ujumbe mfupi wa simu yake ya mkononi, Waziri Muhongo alisema wasomi wazuri wanajua mada zinazowasilishwa, zinakuwa na majadiliano na siyo kufokeana.

Alisema katika uwasilishaji huo, elimu nzuri na uelewa mzuri ni kitu muhimu huku akiainisha kuwa lugha ni tatizo hata kushindwa kufuatilia mijadala.
Baada ya kutuma ujumbe huo, Profesa Muhongo alipiga simu na kulalamika kuwa gazeti hili limekuwa haliisaidii jamii kwa kuandika vitu vinavyoonekana tofauti na mitazamo ya serikali na kwamba hata tukio linalodaiwa kuwa amemfokea Kamishna wa Madini mbele ya wageni haliwezi kuisaidia jamii kama watapata taarifa hiyo.

"Kutofautiana katika mijadala ni jambo la kawaida, nyie Tanzania Daima hamuisaidii nchi, hivi unadhani mimi ambaye nimeshafanya kazi sehemu mbalimbali duniani nitakuwa radhi kuona uwasilishaji wa jambo usiokidhi viwango niendelee kuunyamazia? Lakini tambua mimi natafuta maslahi ya Watanzania na si kile mtu anachotaka, sasa wewe kama unataka kuandika habari hiyo andika unavyoweza. Kwanza mimi huwa sisomi hilo gazeti lenu," alisema Profesa Muhongo.

Tanzania Daima ilimueleza Profesa Muhongo kuwa habari inayotafutwa si kwa ajili yake bali ni kwa ajili ya wananchi ili wajue namna viongozi wao wanavyofanya kazi kwa kutoaminiana.

Baada ya hapo, alikata simu na kisha kutuma ujumbe mfupi wa maandishi ukiwa na alama ya kuuliza ambao ulisomeka: " CHADEMA?"
Mwishoni mwa mwaka jana, Profesa Muhongo aligoma kusafiri kwa ndege na Watanzania wenzake kwenda nchini Algeria kwa daraja la kawaida baada ya kukosa daraja la kwanza, hivyo kulazimika kuahirisha safari yake kwa siku moja.

Waziri Muhongo alikuwa aondoke na Ndege ya Shirika la ndege la Emirates namba EK 726 kupitia Dubai kwenda Algeria akiwa na tiketi ya daraja la kawaida bila kujua kabla ya kufika uwanjani hapo na kisha kuanza kumfokea kila aliyekuwa anamsemesha.

Muhongo ambaye amekuwa akionyesha kauli za vijembe na kejeli kwa Watanzania mara kadhaa, aligoma kusafiri katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam Novemba 24, 2013, saa 10.45 akiwa na wenzake tisa.

Safari ya Waziri Muhongo na ujumbe wake nchini Algeria, ndiyo iliyozaa safari ya ujumbe wa Waziri wa Nishati, Mafuta na Gesi wa Algeria nchini.
Moja ya kauli ya dharau aliyopata kuitoa Waziri Muhongo mwaka jana ni pale aliposema wafanyabiashara Watanzania wana uwezo wa kuwekeza kwenye soda na juisi badala ya gesi, na pia aliwahi kuwashambulia viongozi wa dini kwa kuwaita waongo.

Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, hivi karibuni alimwita Waziri Muhongo ni muongo na kwamba ataanza kuanika kauli zake alizodai za uongo.
Moja ya kauli yake inayotafsiriwa kuwa ni ya uongo ni pale alipowaahidi Watanzania kwamba umeme hautakatika tena.
 
Huyu muhongo, nadhani ana matatizo kichwani. Kama kwli hayo yametokea, nitaamini kabisa kwamba lipo tatizo! Kila wakati yeye anadhani ktk wasomi yeye hakuna mwingine. Sijui amekulia mazingira gani, lakini majibu yake na matendo ya aina hii, yananipa was kwamba kichwa chake hakiko sawa.
 
Muhongo yupo sahihi kabisa watanzania tunapenda kuendesha mambo kwa mazoea, ndiyo maana wafanyakazi wa serikali hawana jipy kichwani pamoja na kupelekwa semina kila kukicha. Ilikuwa ni mwaka 2011 kuna mtumishi 1, alinieleza kuwa semina ambazo huwanaenda kufanya iwe mikoani au nje ya nchi huwa wanaenda kupumzika tu huko hakuna mtu ambaye huwa makini kufuatilia.
Watanzania hatupendi kuelezwa ukweli, Ndiyo maana huwa nampenda Lowasa(Ingawa anaidhaifu wake upande wa ngawira) kwa kufanya usimamizi mzuri, nakumbuka wakati akiwa PM wakuu wa wilaya, wakurugenzi walikuwa matumbo moto. Nakumbuka alivyomsimamisha yule DC ambaye alituhumiwa kuchota mahindi ya msaada. Tumwache Prof. Muhongo ainyooshe wizara ile.
 
Eti nimesikia kua katika JK kuteua Mawaziri watano wanaokuja Waziri wa Mambo ya Ndani ni Edward Ngoyai Lowassa!
 
huyo kamuhongo ametukatia umeme toka asubuhi bila taarifa yeyote na kwasasa tunaishi kama popo! ukimuona huko kwenu mwambie huo si ungwana maana tuneshindwa kuchaji simu,kupasi.kutunza vinywaji na chakula, kunyoa,kusaga,nakupiga mziki utufariji kwamaisha magumu tuliyo pewa na maccm
 
sasa kama kamishna wa madini anawasilisha pumba muhongo asimwambie?tatizo sio muhongo tatizo lipo kwa aliyemteua huyo kamishna shallow in presentation.
heko muhongo kwa kumuumbua mteuzi wa huyo kamishna,aiwezekani mtu amuage pumba mbele ya wasomi aachwe hivi hivi,lazima apewe shit next time ajipange,ingaw kauli zako ni tata bw muhongo na sikupendi kwa kupandisha bei ya umeme lakini kwa hili nakupa tano
 
sasa kama kamishna wa madini anawasilisha pumba muhongo asimwambie?tatizo sio muhongo tatizo lipo kwa aliyemteua huyo kamishna shallow in presentation.
heko muhongo kwa kumuumbua mteuzi wa huyo kamishna,aiwezekani mtu amuage pumba mbele ya wasomi aachwe hivi hivi,lazima apewe shit next time ajipange,ingaw kauli zako ni tata bw muhongo na sikupendi kwa kupandisha bei ya umeme lakini kwa hili nakupa tano

waziri alipaswa kupitia paper zote zinazowasilishwa na wizara yake kabla ya kikao na ujumbe wa algeria hivyo angepata nafasi ya kuboresha hizo presentation. vyovyote vile ilivyo waziri amekosa weledi katika uongozi na tatizo linatokana na watu kuchanganya uwezo wa kiungozi na kiwango cha elimu ya mtu! naamini Prof. Muhongo anaweza kuwa mwalimu mzuri lakini si kiongozi mzuri.
 
nacholipendea tz daima ni kuwapa makavu laivu na wanashindwa kulishitaki sababu wana ushahidi na mambo yao..
 
huyu waziri hana busara kama haamini wenzie si aone hizo mada kabla ya kuwasilisha utafikri yuko kariakoo hivi ni mzaliwa wawapi huyu bwana? elimu yake haijamsaidia kabisa
 
Safi wabongo wamezoea kusifiwa hata wakichemsha wanataka kupigiwa makofi nosafi prof wachefue mpk watapike km anachemka mwagia maji apasuke kbb
 
Muhongo yupo sahihi kabisa watanzania tunapenda kuendesha mambo kwa mazoea, ndiyo maana wafanyakazi wa serikali hawana jipy kichwani pamoja na kupelekwa semina kila kukicha. Ilikuwa ni mwaka 2011 kuna mtumishi 1, alinieleza kuwa semina ambazo huwanaenda kufanya iwe mikoani au nje ya nchi huwa wanaenda kupumzika tu huko hakuna mtu ambaye huwa makini kufuatilia.
Watanzania hatupendi kuelezwa ukweli, Ndiyo maana huwa nampenda Lowasa(Ingawa anaidhaifu wake upande wa ngawira) kwa kufanya usimamizi mzuri, nakumbuka wakati akiwa PM wakuu wa wilaya, wakurugenzi walikuwa matumbo moto. Nakumbuka alivyomsimamisha yule DC ambaye alituhumiwa kuchota mahindi ya msaada. Tumwache Prof. Muhongo ainyooshe wizara ile.

hayupo sahihi amekosa hekima ya kuongoza na hili ni eneo ambalo watumishi wa Mungu wanapaswa kumuombea sana
 
huyo Muhongo mzigo ametukatia umeme toka asubuhi bila taarifa yeyote na kwasasa tunaishi kama popo! ukimuona huko kwenu mwambie huo si ungwana maana tumeshindwa kuchaji simu, kupasi. kutunza vinywaji na chakula, kunyoa, kusaga,nakupiga mziki utufariji kwamaisha magumu tuliyo pewa na maccm
 
hayupo sahihi amekosa hekima ya kuongoza na hili ni eneo ambalo watumishi wa Mungu wanapaswa kumuombea sana


Msijifanye kumtumia Mungu kuficha dhambi zenu, wakati mnaomlaumu wote ndo walewale wapenda vya bure, tatizo mkielezwa ukweli mnakasirika acheni kupenda ubwete
 
Back
Top Bottom