Vituko vya chitchat: A day in JF

Vituko vya chitchat: A day in JF

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
368,313
Reaction score
851,963
Asubuhi: Ma-Don wa Chai ya Rangi

Siku inaanza saa kumi na moja alfajiri kwa nyuzi za kujimwambafai.

Raia wanaanzisha mada za "Niko Five star hotel Dubai..nakunywa capuchino ya Brazil huku nawaza ninunue kiwanja gani wiki hii." Kumbe ukweli ni kwamba mleta mada amejifunika shuka la neti huku aking’atwa na mbu, na capuchino yenyewe ni ile ya mia mbili ya kijiweni.

Watoa maoni hawachelewi kumpiga spana: "Kaka, plasta imebubujika hapo ukutani kwako, jenga kwanza kabla ya kuwaza Brazil!"

Mchana: Soko la Kupigwa Chabo
Saa nne asubuhi hadi saa sita mchana, jukwaa linageuka kuwa chumba cha mahojiano.

Watu wanatafuta "connections" na kuanzisha mada za uongo na kweli ili mradi tu wavutie watu (attention).

Kila anayeweka uzi wa maana anakutana na swali la dokezo: "punguza C&P nk"

Hapa ndipo wabishi wa keyboard wanapoanza kunyoshana vidole huku kila mtu akijifanya anajua kila kitu kuliko mwenzake.😂

Adhuhuri:
Mlipuko wa Jukwaa la "Selfika"Hapa ndipo jukwaa linapochanika msamba! Saa saba mchana, uzi maarufu wa Selfika unalipuka kwa picha.

Wadada wanaweka picha za magoti, vikuku, au mikono yenye kucha ndefu, huku kaka zao wakiweka picha za vishikwambi au usukani wa magari ya watu.😁
PM (Private Messages) zinajaa kufurika; kila mtu anajifanya "Don" anayetaka kutoa ofa ya chakula cha mchana,
wakati kiuhalisia wengi wao wanasubiri bajaj ya buku jiko iwafikishe wanakokwenda.

Jioni: Udaku wa Ubuyu Moto
Saa kumi na moja jioni, watu wakiwa kwenye foleni za daladala na hasira za hapa na pale, wanahamishia hasira zao kule Chitchat.

Mtu anakuja na "ubuyu" usio na miguu wala mikono: "Niko hapa Posta namwona msanii fulani analia baada ya kuachwa." Ndani ya dakika tano, wataalamu wa kudukua picha wanakuja na ushahidi kuwa msanii huyo yuko mkoani.

Mleta mada anapoona spana zimezidi, anazima data na kujifanya bando limeisha.

Usiku: "Midnight Crew" na Kupoteza ID
Saa sita usiku, watoto wamelala na jukwaa linabaki na watu wazima pekee. Hapa ndipo ID fake zinapofanya kazi yake; watu wanakuja na siri zito za chumbani na matatizo ya mahusiano ambayo hawawezi kuyasema hadharani.
Kila mtu anakuwa mshauri wa mapenzi na daktari wa kienyeji, huku wengine wakivizia kule Selfika kuona kama kuna picha za usiku wa manane zitakazovuja kabla ya kufutwa alfajiri!

*A day in JF what an amazing life😂😂😂
tanzanian-konyagi-a-spirit-drink-based-on-molasses-made-from-sugarcane-FCWP8J.jpg
250dbc72-f116-4467-aac5-84094de559d1.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom