Latent chaos
JF-Expert Member
- Jul 15, 2024
- 1,501
- 3,101
Nimekuwa nikiona mara kwa mara nyuzi zinazoulizia wanachama ambao wamepotea jukwaani kwa muda mrefu, wengine miaka mitano, minane au zaidi. Sasa naelewa kwa nini jambo hili hutokea.Najua ukimya ungeweza kutosha lakini nimeona bora niache maelezo mafupi kuliko kuacha maswali na kama JamiiForums ingeweka option ya kufuta akaunti kabisa, ningechagua njia hiyo badala ya kuaga kwa maandishi.
Kwa muda wa takribani mwezi mmoja nimekuwa nikitafakari uamuzi huu, na hatimaye nimeamua kuchukua mapumziko marefu kutoka JamiiForums kwa miaka kadhaa ijayo.
Nilipokuja hapa nilikuja kama mtu mwenye hamu ya kujifunza, ku-share mawazo na kubadilishana mitazamo na watu mbalimbali. Nimekutana na watu wenye mawazo tofauti, nimejifunza mambo mengi, nimecheka, nimejadili na wakati mwingine nimeingia kwenye mijadala mikali na baadhi members .
Lakini tunavyojua kadri maisha yanavyosonga, mtu hugundua kuwa kila kipindi kina vipaumbele vyake. Muda na umakini ni rasilimali adimu, na kuna wakati inabidi mtu achague kuelekeza nguvu zake kwenye mambo mengine muhimu zaidi: kujenga, kujifunza, familia na maisha nje ya mitandao.
Uamuzi huu si kwa sababu ya chuki, ugomvi au kupunguza thamani ya jukwaa hili. Ni kwa sababu tu nimefika kwenye hatua ambayo nahitaji kufungua ukurasa mwingine. Hivyo basi ndugu zangu nipende kuchukua nafasi kuwaaga rasmi.
Kwa wapenzi wa
Kwa wale wa
Kwa wale ambao tumewahi kutofautiana, kukosoana au kutokuona mambo kwa jicho moja, nawapa salamu pia. kutofautiana maoni hakupaswi kumfanya mtu ashindwe kumtakia mwenzake mema
Kwa wale ambao hawapo hapa kwa sababu mbalimbali, wakiwemo
Kama wahenga wasemavyo hakuna marefu yasiyo na ncha, kuna wakati nilikuja hapa kama mgeni, nikawa sehemu ya jamii hii, na sasa ni wakati wa kuondoka.Ahsanteni sana
, kwakherini 👋.
Kwa muda wa takribani mwezi mmoja nimekuwa nikitafakari uamuzi huu, na hatimaye nimeamua kuchukua mapumziko marefu kutoka JamiiForums kwa miaka kadhaa ijayo.
Nilipokuja hapa nilikuja kama mtu mwenye hamu ya kujifunza, ku-share mawazo na kubadilishana mitazamo na watu mbalimbali. Nimekutana na watu wenye mawazo tofauti, nimejifunza mambo mengi, nimecheka, nimejadili na wakati mwingine nimeingia kwenye mijadala mikali na baadhi members .
Lakini tunavyojua kadri maisha yanavyosonga, mtu hugundua kuwa kila kipindi kina vipaumbele vyake. Muda na umakini ni rasilimali adimu, na kuna wakati inabidi mtu achague kuelekeza nguvu zake kwenye mambo mengine muhimu zaidi: kujenga, kujifunza, familia na maisha nje ya mitandao.
Uamuzi huu si kwa sababu ya chuki, ugomvi au kupunguza thamani ya jukwaa hili. Ni kwa sababu tu nimefika kwenye hatua ambayo nahitaji kufungua ukurasa mwingine. Hivyo basi ndugu zangu nipende kuchukua nafasi kuwaaga rasmi.
Kwa wapenzi wa
siasa, endeleeni na uchambuzi wenu na mijadala yenu. Kwa wapenzi wa mpira, endeleeni kutetea timu zenu kwa moyo wote, hata pale takwimu zinapowapa changamoto.Kwa wale wa
kula tunda kimasihara, all the best, play safe. Kwa wale wa selfika thread, endeleeni ku-selfika ila jitahidini kupunguza vi-emoji kwenye sura zenu. Kwa wapenda nyuzi za binti wa kale, chit chat, pombe , kobazi, single-mothers na kila kona nyingine ya jukwaa, nawatakia kila la heri pia.Kwa wale ambao tumewahi kutofautiana, kukosoana au kutokuona mambo kwa jicho moja, nawapa salamu pia. kutofautiana maoni hakupaswi kumfanya mtu ashindwe kumtakia mwenzake mema
Kwa wale ambao hawapo hapa kwa sababu mbalimbali, wakiwemo
waliopigwa ban, nawawatakia mema pia.Kama wahenga wasemavyo hakuna marefu yasiyo na ncha, kuna wakati nilikuja hapa kama mgeni, nikawa sehemu ya jamii hii, na sasa ni wakati wa kuondoka.Ahsanteni sana
, kwakherini 👋.