YAKATAE HAYA UNAPOENDELEA KUSHEREHEKEA PASAKA.
●Usikubali kwenda kwenye dhambi.
●Usikubali kwenda kwenye mwaliko wa kufanya uovu.
●Usikubali kwenda kwenye kumbi za starehe.
●Usikubali kwenda kumtukuza shetani
●Usikubali kumpa shetani utukufu wote wa pasaka kwa kumtii katika matendo yako.
●Usikubali kuwa na utakatifu wa pasaka tu bali uwe mtakatifu siku zote za maisha yako.
●Usikubali kufanya machukizo ili tu kuwafurahisha wanadamu.
●Usiende disko wala kokote kwenye tamasha la nyimbo za kidunia.
●Kataa ahadi ya kwenda kufanya dhambi ambayo mliahidiana na yeyote.
●Usikubali kujinajisi kwa sababu tu ya siku ya sikukuu na mapumziko.
Mtii Bwana YESU KRISTO katika maisha yako yote.
Zaburi 1:1-3 " Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa."
Nakutakia Pasaka njema sana BWANA aliye MUNGU akulinde na kukuepusha na mabaya yote.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.