Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

Chagua ugonjwa wako
1657230539-picsay.jpg
 
WAPELELEZI WA DCI WASIMULIA JINSI MWANAFUNZI WA MATIBABU ALIVYOJITEKA ILI KUPATA PESA KUTOKA KWA WAZAZI.

'Mwanafunzi wa udaktari mwenye umri wa miaka 23 katika Chuo cha Mafunzo ya Tiba Makindu, yuko chini ya ulinzi katika kituo cha polisi cha Kayole, baada ya kuandaa utekaji nyara wake ili kukamua pesa kutoka kwa wazazi wake

. Edwin Kamau ‘alitoweka’ Jumapili iliyopita kabla ya kumbloke babake na kumpigia simu mamake akidai kutekwa nyara. Alimweleza kuwa watekaji nyara walitaka fidia ya Sh70,000, ili kumwachilia huru kabla hajamkata simu. Wazazi wake waliokuwa wamechanganyikiwa waliripoti kisa hicho kwa maafisa wa polisi ambao mara moja walianzisha msako wa kuwasaka watekaji nyara.

Hata hivyo, simu hizo ziliendelea huku Kamau akimwambia mamake kuwa watekaji nyara wake walikuwa wakielekea kumuangamiza. Wakiwa wamedhamiria kuokoa maisha ya mwana wao, walituma Sh10,000 jana kupitia MPESA na Sh40,000 za ziada leo. Mara baadabya Kamau kupokea Sh10,000 za awali, alienda kwenye klabu moja mjini Thika kumwagilia maji koo na kufurahi pamoja na mtoto mzuri ambaye alikutana naye.

Kumbe mwanamke huyo ni malaya ambaye alimwekea madawa kwenye kinywaji chake na kuiba pesa hizo. Leo baada yakupata fahamu alipiga simu tena na wazazi wake wakatuma Sh40,000 zaidi ambazo alizitoa na kuzisunda kwenye viatu vyake.

Kumbe wapelelezi walikuwa wanamfuatilia hivyo walimkamata. Alipohojiwa, Kamau alisema kwamba alikuwa amefuja pesa za karo ya shule ya muhula wake wa mwisho na alikuwa akishangaa jinsi angechangisha pesa za kufanya mitihani yake, na akaja na mbinu ya kutekwa

Aidha alifichua kuwa ‘alitekwa nyara’ pamoja na wanafunzi wengine wawili ambao wazazi wao walikuwa wamelipa fidia. Maafisa wa upelelezi walipata Sh38,600 kutoka kwa mwanafunzi ambaye sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Koyole akisubiri kufikishwa mahakamani

Good morning Kenya
FB_IMG_1657247727236.jpg
 
Back
Top Bottom