Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

FB_IMG_1657162445949.jpg
 
Update: Pichani wanandoa hao ambao mume amepitwa miaka 37 na mke wake huyo wametangaza kutaka kupata mtoto ambapo watatumia shilingi milioni 333.7 na tayari wamempata mwanamke wa kumuajiri awabebee mimba

Mke huyo anaitwa Cheryl ana miaka si chini ya 61 wakati mume wake huyo anaitwa Quran McCain(24) ambapo kwasasa wanaishi Rome, Italia baada ya kufunga ndoa mwaka 2021

Cheryl tayari alishazaa watoto 7 na ana wajukuu 17 katika mahusiano yake ya mwanzo, lakini Quran yeye bado hana mtoto kwahiyo wameamua ili kulinogesha zaidi penzi na ndoa yao basi wapate mtoto ambapo mbegu tayari wameshapata mwanamke wa kumuajiri awabebee hiyo mimba na watatumia jumla ya gharama £120,000 ambazo si chini ya milioni 333.7 za Kitanzania

Wamesema wanapendana sana kila mmoja anamfurahia mwenzie ambapo penzi lao lilianza kipindi cha nyuma baada ya mwanamama huyo kuachia video mtandaoni akicheza muziki kisha watu kuanza kumchamba na kukosa furaha ambapo Quran alianza kumfariji na baadaye penzi kuchanua na hatimaye kufunga ndoa
FB_IMG_1657171028780.jpg
 
Jamaa kaenda kwa mke wa rafiki yake..
Jamaa: shemeji, nimekutamani mnooo!
Mke: hebu ondoka hapa.. unafikiri rafiki yako akikusikia atasemaje?!
Jamaa: nikikulipa sh milioni 1 je?
Mke: njoo kesho mchana wakati mume wangu yupo ofisini.
...Kesho yake jamaa katinga na sh 1m akampa mke wa rafiki yake, akatafuna mzigo wee kwa kujinafasi hadi akatosheka kabisaaa.. wakaagana, akaondoka.
Jioni mume akarudi..
Mume: vipi wife, kwema hapa?
Mke: salama..
Mume: okay.. Vipi, rafiki yangu ameleta sh milioni 1 hapa?
Mke: (kwa mshangao mzito na kusita sita) ....nd, ndi, ndi, ndiyo-o🙄
Mume: huyu rafiki yangu ndo ninapompendea hapo hapo.. Ni muaminifu sanaaa! Asubuhi kaja ofisini kuazima kwangu milioni 1, akaniahidi atarejesha hapa home kabla siku haijaisha, na kweli katimiza.. Safi Sana!😊
 
Update: Pichani wanandoa hao ambao mume amepitwa miaka 37 na mke wake huyo wametangaza kutaka kupata mtoto ambapo watatumia shilingi milioni 333.7 na tayari wamempata mwanamke wa kumuajiri awabebee mimba

Mke huyo anaitwa Cheryl ana miaka si chini ya 61 wakati mume wake huyo anaitwa Quran McCain(24) ambapo kwasasa wanaishi Rome, Italia baada ya kufunga ndoa mwaka 2021

Cheryl tayari alishazaa watoto 7 na ana wajukuu 17 katika mahusiano yake ya mwanzo, lakini Quran yeye bado hana mtoto kwahiyo wameamua ili kulinogesha zaidi penzi na ndoa yao basi wapate mtoto ambapo mbegu tayari wameshapata mwanamke wa kumuajiri awabebee hiyo mimba na watatumia jumla ya gharama £120,000 ambazo si chini ya milioni 333.7 za Kitanzania

Wamesema wanapendana sana kila mmoja anamfurahia mwenzie ambapo penzi lao lilianza kipindi cha nyuma baada ya mwanamama huyo kuachia video mtandaoni akicheza muziki kisha watu kuanza kumchamba na kukosa furaha ambapo Quran alianza kumfariji na baadaye penzi kuchanua na hatimaye kufunga ndoaView attachment 2283164
Duuh!
Itakuwa huyo bibi ana mpunga mrefuu, ambao ndo umekamatia hisia za huyo dogo Quran🤔
 
Mlevi:​

Jamaa mmoja mlevi ana mazoea ya kurudi home usiku sana. Juzi karudi mishale ya saa 9 usiku. Maongezi kati yake na mkewe yakawa hivi..
Mlevi: dear, umeweka balbu otomatiki msalani?!!!
Mke: hapana, ni ile ile ya siku zote..
Mlevi: siyo, mbona nikifungua mlango taa inawaka yenyewe, na nikifunga inazimika?!
Mke: oohooo, toba🙄
kumbe ushajisaidia tena ndani ya friji!!🤔
 
Pedeshee​

Pedeshe: dereva, hebu njoo na hilo freezer langu kubwa hapa Lidaz
Dereva: sawa mkuu..
.... Baada ya muda freezer likaletwa..
Dereva: mkuu, tayari tumeleta friza hapa.. ni la nini huku lakini?!!!
Pedeshe: aah! Nilisahau simu yangu juu ya hilo freezer 😊
 
Jamaa alikuwa anaumwa sana, mkewe akaita daktari..
Dokta alipofika akakuta jamaa amefumba macho..
Dokta: huyu mbona kasha kufa?!
Jamaa: Heeee! Sijafa bhana!
Mke: hebu nyamaza huko.. wacha ujuaji wa kubishana na wataalamu. Ashasema umekufa, sasa wewe unabisha ili iweje?!!!🙄
 
Back
Top Bottom