Fadhila Thomas Kiria wa USA River, Arusha amepotea katika mazingira ya kutatanisha akiwa mjini Moshi, asubuhi ya tarehe 4/3/2024 na hadi leo hajulikani halipo. Tarehe tajwa hapo juu Fadhila alikua dukani anapofanya kazi, Moshi mjini. Akalalamika kichwa kumuuma, akaacha simu na pochi juu ya meza dukani, akatoka kwenda kununua dawa. Lakini hakurudi mpaka leo. Ameacha mtoto mchanga wa wa miezi 5 anayenyonya.
Juhudi za kumtafuta maeneo mbalimbali ya Moshi na Arusha hazijazaa matunda. Taarifa imetolewa Polisi lakini bado hajaonekana. Ndugu wamemtafuta hospitali zote za Moshi, ikiwa ni pamoja na vyumba vya kuhifadhia maiti (mochwari) lakini hawajampata. Haijulikani kama yu hai au amefariki, au labda alipata tatizo la afya ya akili kutokana na maumivu ya kichwa. Tunaomba yeyote atakayemuona awasiliane na mama yake kwa simu nambari; 0762122114 au dadaye Berha: +255765688085. Asanteni na Mungu awabariki
View attachment 2927750