Vituko jeshini

Kuna rafiki mmoja ambae amenizidi umri aliniadithia kwamba kipindi yupo JKT MAKUTOPORA kuna afande ambae alikuwa kiongozi wa makuruti jina lake alikuwa anaitwa NUSU MUNGU. Aliniambia kuwa afande huyu alikuwa na vituko sana.Naomba kwa wale waliopitia JKT MAKUTOPORA wanipe vituko vyake.
 
Adhabu za jeshi ni sulubu usipime.
Unaweza juta kwa nini hukua mkulima tu. Mana adhabu nyingi ni za kukomoana.
 
Tehe tehe tehe !
Kwa baba zangu wadogo wakurya hadi leo akizaliwa mtoto wa kiume wanakusifia," Poti hongera umezaa lijeshi !"
 
Kuna jamaa yangu alishawahi kunisimulia! Kuna mkurya alipata kazi Tanesco akarudi kwao akawaambia amepata kazi Tanesco bac kwao wote wakashangaa Mura Tenesco ndo jeshi gani tena hilo!
 
mkurya moja kapata ajari eneo la jeshi nakulazwa Lugalo,cha ajabu kamwita nesi nakumlizia baisikeli na tireyi za mayayi
 
hapo Lugalo(Makongo)...miaka ya nyuma kuna konda na dereva wake walikamatwa wakipakia madenti...adhabu waliyopewa na wale maMP eti walipewa kila mmoja mche wa sabuni halafu wakaoge kwenye bwawa moja lilikuwepo pale Makongo Sec....
 
hapo Lugalo(Makongo)...miaka ya nyuma kuna konda na dereva wake walikamatwa wakipakia madenti...adhabu waliyopewa na wale maMP eti walipewa kila mmoja mche wa sabuni halafu wakaoge kwenye bwawa moja lilikuwepo pale Makongo Sec....

Hizo zipo sana na unatakiwa hiyo sabuni iishe. Utashangaa kama una nywele fupi hata kalamu haizami unaambiwa umefuga rasta.
 
Katika kikosi fulani mkoa wa Tanga tulitakiwa kwenda kulima. Majembe yakaisha afande akaleta majembe yaliyokatika nusu (upande wa makali haupo). Makuruta waliosema haiwezekani kulimia wakaambiwa wasimame pembeni. Yalipoisha hayo majembe wale walioambiwa wasubiri pembeni wakapewa sululu zenye ncha nyembaba wakalime kama hawawezi watangulie main gate wapewe extra drill
 
Nawish niende jeshin, naombeni ushauri!Ni mda mrefu naota kuwa mwanajeshi napenda sana bt nasikia tetes nying hko!Vp ntatokaje?
 
Kuna afande mmoja alitupa kazi ya fatiki kulimia majani kuzunguka kambi,lakini wote tukala kona tukajifungia mabwenini,sikia sasa alivyokuwa anamjulisha mkuu wa kambi kupitia cm za ndani ya kambi' alisema hivi,"afande haya makuruta nimeyapa kazi ya usafi lakini yame obey order yote yamerudi mabwenini afande"!
 
Namkumbuka mkuu wangu wa jkt pale Ruvu,alikuwa akimtongoza kuruti wa kike alimwambia"twende tukafanye parfomance".
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom