Idd Amin Dada

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,776
Idi Amin Dada alizaliwa 1923 na alifariki mwezi wa nane 2003 alikua raisi wa tatu wa Uganda, alitawala 1971 mpaka 1979. Amin alijiunga na jeshi la kikoloni la Mwingereza likitumikia Kenya na Uganda. Amin alipanda haraka ngazi kufikia cheo cha umeja wakati huo ni baada ya uhuru ikijulikana kama jeshi la Uganda, alikua kamanda kabla ya kufanya mapinduzi mwaka 1971 na kumpindua Milton Obote. Baadae alijipandisha cheo kua field marshal akiwa raisi.
images


Amin hakuwahi kuandika kitabu cha historia yake wala hakuwahi kumruhusu mwandishi yeyote kuandika habari ya maisha yake. Hii inamaanisha hakuna uhakika ni lini na ni wapi alizaliwa. Maandishi mengi kuhusu amini yanaeleza alizaliwa Koboko au Kampala mnamo 1925. Habari nyingine zisizo na uhakika zinaeleza Amin alizaliwa 1923 na nyingine zinasema 1928.

Mtoto wa Amin aitwae Hussein anasema baba yake alizaliwa Kampala mnamo mwaka 1928. Fred Guweddeko wa Makerere University, anasema Idi Amin ni mtoto wa Andreas Nyabire alieishi kati ya 1889 na 1976. Nyabire ni mmoja wa kabila la Kakwa ambalo lilibadili dini kutoka Ukatoliki kwenda Uisilamu mwaka 1910 na kubadili jina kuwa Amin Dada. Yeye mwenyewe alikuwa mtoto wa kwanza kuzaliwa.

Iddi Amini alitengwa na malezi ya baba akiwa mdogo, Idi Amin alikua na mama yake katika kijijini kwa shughuli za kilimo kaskazini magharibi mwa Uganda. Guweddeko anasema mama yake Amin aliitwa Assa Aatte alizaliwa 1904 na alifariki 1970, na alikuwa mganga wa kienyeji aliewatibu familia ya kifalme ya Buganda kati ya wateja wake.

Amin alijiunga na shule ya Kiislam ya Bombo mwaka 1941, aliacha shule akiwa na elimu ya darasa la nne kwa elimu ya Mwingereza na alifanya vibarua kabla ya kujiunga na jeshi la Mwingereza na kuwa ofisa wa jeshi.
small_torgb_5584990.jpg


Amin alijiunga na Jeshi la Mwingereza la King's African Rifles (KAR), mwaka 1946 kama msaidizi wa mpishi. Baadae alidai mwenyewe kuwa alilazimishwa kuingia jeshini wakati wa vita kuu ya pili ya dunia World War II na aliwahi kupelekwa Burma.

Alihamishiwa Kenya kwa mafunzo maalumu mwaka 1947 na alikua sehemu ya kikosi cha 21 ca tattaalion Gilgil, Kenya mpaka 1949. Mwaka huo kikosi chake kilikwenda kupigania Kenya zidi ya Wasomali vita ya Shfta. Mwaka 1952 Brigadia yake ilipigana dhidi ya Mau Mau wa Kenya na alipandishwa cheo kuwa koplo mwaka 1953

feb-24-2012-idi-amin-e12phm.jpg


Mnamo mwaka 1959, Amin alipewa cheo cha Afande Afisa Mteule (warrant officer), hiki kilikua cheo cha juu zaidi kwa askari Mweusi wa |Kiafrika katika jeshi la Mkoloni Mwingereza wakati huo. Amin alirudi Uganda mwaka huo huo, na mwaka 1961 alipewa cheo cha luteni na kuwa mmoja kati wa Waganda wawili kuwa na maafisa maalum (Commissioned Oficers).

Alipangiwa kusuluhisha mapigano ya Karamojong na kabila la Turkana la Kenya uliohusu ngo'mbe. Kufuatia uhuru wa Uganda kutoka kwa Mwingereza, Amin alipandishwa cheo kuwa kapteni na 1963 kuwa meja. Aliteuliwa kua Afisa wa pili wa majeshi ya Uganda mwaka 1970.

images



Amin alikuwa mwanamichezo mzuri sana wa enzi zake kote katika Jeshi la Mwingereza na Jeshi la Uganda. Akiwa na urefu wa sentimeta 193 au futi 6 na inchi 4 na tambo lililo jaa, hivi vilimfanya kuwa nyota katika michezo. Alikuwa mwanamasumbwi wa uzito wa juu, muogeleaji, pia alicheza rugby kwa uwezo wa hali ya juu. Katika miaka ya 1950 alichezea Nile RFC.

Kuna usemi wa mjini kuwa alichaguliwa kama mchezaji wa ziada kaitka michezo ya Afrika Mashariki kwenye mechi dhidi ya British Lions. Amin hatahivyo hakutokea kwenye picha za mchezo huo wala jina lake halikua kwenye orodha ya wachezaji. Kutokana na maongezi na askari wenzake wa kizungu Amin alianza kujenga ushabiki na timu ya mpira ya Hayes, ushabiki huo uliendelea maisha yake yote.

images


Mwaka 1965, Waziri mkuu Milton Obote na Amin walishutumiewa katika mpango wa kuingiza meno ya tembo na dhahabu nchini Uganda kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mpanga huu mbao Generali Nicholas Olenga, rafiki wa aliekua kiongozo wa serikali ya Kongo Patrice Lumumba, alikuwa mmoja wa washiriki ili kusaidia majeshi ya upinzani dhidi ya serikali ya Kongo kwa siri kufanya biashara ya dhahabu na meno ya tembo, kubadishana silaha na mpangaji mkuu wa mpango huu akiwa Amin kwa Uganda.

Bunge la Uganda lilidai utafiti ufanyike dhidi ya shutuma hizi. Mwaka 1966 Obote alifuta sherehe za kiraisi zilizofanywa na Mfalme Kabaka Mutesa II wa Buganda, na kujitangaza kuwa yeye mwenyewe ni raisi na kumtangaza Amin kuwa Kiongozi wa Majeshi. Amin aliongoza mapigano dhidi ya jumba la kifalme la Kabaka na kumfanya Kabaka na familia yake kukimbilia hifadhi ya ukimbizi nchini Uingereza ambako aliishi mpaka mauti yanamkuta mwaka 1961.

idi-amin-president-of-uganda-with-president-mobutu-sese-seko-of-zaire-picture-id2634497


Amin alianza kuingiza watu wa kabila lake la Kakwa na Lugbara kutoka Kusini mwa Sudani na makabila mengine kutoka Magharibi mwa eneo la Nile linalopakana na South Sudan. Watu wa Sudani ya Kusini walihamia Uganda tangia karne ya 20, walikuja kujiunga na jeshi la mkoloni. Jeshi la Amin lilijaa watu wa Sudan ya Kusini na wengi wao waliishi katika nchi zote mbili.

Milton Obote ndiye aliyekuwa raisi wa pili wa Uganda ambae alipinduliwa na Idi Amin mnamo mwaka 1971. Ugomvi kati ya Obote na Amin ulianza baada ya Amin kuwa na nguvu na kubwa jeshini kutokana na kuajiri watu wa kabila lake. Hii pia ilisaidia kusaidia majeshi ya waasi wa serikali ya Sudani ya Kusini pia jaribio la kumuua Obote mwaka 1969. Oktoba 1970 Obote alichukua madaraka makubwa jeshini na kumpunguzia Amin nguvu aliyoanza kuifurahia jeshini kwa miezi michache.

MTE5NDg0MDU1MDg4NTYzNzI3.jpg


Milton Obote.
Alipogundua kuwa Obote anampango wa kumfunga kwa hujuma ya kupotea kwa pesa za jeshi, Amin alimuwahi kwa kumpindua mnamo 25 January, 1971. Obote alikua katika kikao cha Jumuia ya Madola nchini Singapore. Wanajeshi waliomuunga mkono Amin walizingira kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Entebe, walizingira nyumba ya Obote na walifunga barabara.

Walitangaza redioni kuwa serikali ya Obote haiko madarakani kwa shutuma za kutumia madaraka vibaya na ufujaji wa mali pia iliendesha serikali kwa upendeleo, hasa kupendelea watu wa mkoa wa Lango. Watu walisikika wakishangilia kwenye barabara za Kampala,

Idi Amin alisema wazi kuwa yeye si mwanasiasa bali yeye ni askari mwanajeshi. Alisema pia uongozi wake utakuwa ni wa muda mpaka hapo serikali ya kidemokrasia itakapopatikana ki halali. Amin aliahidi kuwafungua wafungwa wote wa kisiasa.

Amin alimfanyia mazishi ya kitaifa Mfalme Kabaka wa Buganda na raisi wa kwanza wa Uganda Bwana Edward Mutesa aliefia ukimbizini nchini Uingereza. Mazishi haya yalifanyika mwezi April 1971, kitendo hiki kiliwapendeza sana Waganda. Pia aliwafungua wa kisiasa kama alivyoahidi na aliahidi kuleta uchaguzi huru na wa haki katika muda mfupi.

images
the-flagdraped-coffin-of-king-freddie-first-president-of-uganda-and-picture-id480432783


Mazishi ya kitaifa ya Sir Edward Mutesa, Mfalme wa Buganda na raisi wa kwanza wa Uganda 1971.

Wiki moja baada ya mapinduzi 02 February 1971 Amin alijitangaza kuwa yeye ndiye rais wa Uganda, Mkuu wa Majeshi pia ni Katibu Mkuu Kiongozi wa serikali ya Uganda. Aliitisha kikako cha maofisa wa jeshi, yeye mwenyewe akiwa mwenyekiti na aliweka sheria za jeshi juu ya sheria za nchi.

Maafisa wa jeshi walipewa madaraka makubwa serikalini na aliunda baraza la mawaziri ambalo lilifuata sheria na nidhamu za jeshi. Ikulu aliibadilisha jina kuwa The Command Post na alifuta idara ya upelelezi ya serikali iliyopita na kuipa jina State Research Bureau (SRB), ikiwa na makao makuu kando ya Kampla eneo la Nakasero, kwa kifupi hii ndio ilikua kitengo cha utesaji unyongaji na uuaji kwa kipindi chote cha utawala wa Amini.

images


Obote alikimbilia Tanzania, alipewa hifadhi ya ukimbizi wa kisiasa na Rais Julius Nyerere. Obote alijiunga na Waganda 20,000 waliokimbia nchi yao na walifanya jaribio la kumpindua Amin mwaka 1972, jaribio hili lilishindwa kutokana na mipango mibovu.

Amin alikasirishwa sana na jaribio hili la kuvamia nchi yake lililopangwa na wakimbizi wa kisiasa. Aliwaondoa jeshini wale wote waliomuunga Obote hasa wale wa kabila la Acholi na Lango. Wanajeshi wa Acholi na Lango waliuwawa kikatili katika kambi ya Jinja na Mbarara.

Mwanzoni mwa mwaka 1972 wanajeshi takriban 5,000 wa Acholi na Lango na raia wasio julikana idadi kamili waliuwawa na wengine walipotea na hakuna aliejua walikwenda wapi mpaka leo hii. Wahanga wa jaribio hili walikua pamoja na viongozi wa dini, waandishi wa habari, viongozi wa kuu serikalini, wasanii, wanasheria, majaji, wanafunzi, wanafalsafa, wanauchumi, majambazi walioshukiwa na raia wa kigeni. Katika hali hii visa vya kikatili vilifanyika na miili mingi ilitupwa mto Nile.

Mauaji haya, yalichochewa haswa na ukabila, sababu za kisiasa na uchumi, na yaliendelea kwa muda wote wa miaka nane wa utawala wa Idi Amin. Hakuna mtu anaejua idadi halisi ya watu waliouwawa. Jumuia ya kimataifa ya wanasheria inakisia idadi ya watu waliouwawa kuwa ni kati ya 80,000 na 300,000. Idadi ya wakimbizi na Amesty International inakisia idadi ya waliouwawa kuwa inafika 500,000.

Katika waliouwawa alikuwa Benedicto Kiwanuka, ambae alikuwa waziri mkuu na Mwanasheria Mkuu Janani Luwum, Askofu wa kanisa la Anglicana Joseph Mubiru, Gavana wa benki kuu ya Uganda Frank Kalimuzo, Makamo wa mkuu wa Makerere University Byron Kawadwa, na mwandishi ns mtunzi pia mawaziri wawili kutoka kwenye serikali yake Erinayo Wilson Oryema na Charles Oboth Ofumbi.

Amin aliajiri watu wengi kutoka kabila lake la Kakwa na watu kutoka Sudani ya Kusini. Kufikia mwaka 1977 watu hawa walikuwa asilimia 60 ya magenerali wa jeshi na aslimia 75 za mawaziri. Wakati huo huo, Waislamu walikuwa asilimia 80 katika serikali ingawa kwa idadi ya raia wa Kiislamu ilikuwa asilimia 5 tu nchi nzima.

Hii inajidhihirshia sababu kwa nini kulikua na majaribio nane ya kumpindua Amin katika miaka nane aliyotawala. Askari wengi wa Amin walitokea Sudani ya Kusini na Kongo na asilimia 24 tu ya askari walikuwa Waganda hawa pia wengi wao walikuwa kabila la Kakwa na ni Waislamu.

images


'Tuna lengo la kutengeneza Mganda wa kawaida kuwa mwongozaji wa maendeleo yake na juu ya yote afurahie utajiri wa nchi yake. Nia yetu ni kuhamisha uchumi wa Uganda uwe mikonini mwa Waganda kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu.' Idd Amin.

Mnamo August 1972, Amin alitangaza vita ya uchumi, aliweka policies pamoja kutaifisha ma mali zote azilizomilikiwa na Wazungu na Wahindi. Wahindi wapatao 80,000 wengi wao walitokea wengine walizaliwa Uganda wazazi wao walikwenda Uganda miaka mingi iliyopita wakati Uganda ikiwa koloni la Mwingereza,

wengi wao walikua na biashara kubwa na zilikuwa moja ya uti wa mgongo wa uchumi wa taifa. August 04/08/1972, Amin aliwafukuza Wahindi wapatao 60,000 ambao ni raia wa Uganda. Wengi wao walikua na passport ya Mwingereza. Baadae zoezi hili lilibakisha Wahindi wenye taaluma kama daktari, wanasheria, walimu na wengineo.

Karibia Wahindi 30,000 walihamia Uingereza. Wengine walikwenda Canada, Autralia, India, Kenya, Pakistani, Sweden, Tanzania na Marekani. Amin alitaifisha biashara zote na kuwapa wale waliomuunga mkono. Wengi wao hawakuwa na uwezo wa kuendesha biashara, matokeo yake nyingi zilikufa na uchumi kutikisika.

Refugees1.jpg


Wahindi wakiwa wanaondoka Uganda 1972.

Mwaka 1977, waziri wa afya Henry Kyemba ambae pia alifanya kazi katika serikali ya Obote aliachia madaraka na kwenda Uingereza kuishi kama mkimbizi. Aliandika nakala isemayo Nchi ya Damu.

idi-amin-3.jpg


Amin alipata ushirikiano mkubwa kutoka nchi za Magharibi kama vile Uingereza, Ujerumani, Israel, kipindi hiki kilikua ni cha vita baridi kati ya nchi za kijamaa na kibepari, Obote alishaonesha nia ya kufuata siasa za kijamaa na hili halikuwafurahisha sana watu wa Magharibi.

Obote alitaifisha makampuni 80 ya waingereza na hii ilionyesha kabisa nia yake ya kuifanya Uganda kuwa Soviet Union. Kutokana na nidhamu ya Jeshi la Mwingereza alilojiunga nalo Amin, alikuwa na imani kubwa na Waingereza. Wengine wanasema Waingereza walimtengeneza Amin kuwa mtawala wa Uganda tangu 1966.

3325002-1st-august-1975-ugandan-soldier-and-dictator-gettyimages.jpg



M15ba4cb9376b1aca16707403b9fd158e.jpg

Amin aliwaamuru wafanyabiashara Waingereza wambebe kama mfalme huko Kampala.

Kufuatia kufukuzwa kwa raia wenye asili ya Kihindi nchini Uganda mwaka 1972 ingawa wengi wao walikua na hati za kusafiria za Uingereza lakini asili yao ilikuwa India, hivyo India mwaka huo ilikatisha mawasiliano ya kidiplomasia na Uganda, mwaka huo huo, Amini alitaifisha makampuni 85 ya Kiingereza. Mwaka huo huo Israel ambayo ilikua nchi mfadhili kwa silaha za kijeshi Uganda walichukizwa na maamuzi ya Amin.

Amin hakusikitika kwakua alimpata rafiki mpya mwenye uwezo wa fedha Muammar Gaddafi aliekua raisi wa Libya, Urusi ilimuahidi vifaa vya kijeshi. Amin alikemea kile alichoona si haki aliyotendewa na Israel wazi na hii ilipelekea Gaddafi kumpa msaada wa kifedha. Amin alijiandaa kuivamia kivita Israel kwa kutumia askari wa parachute, mabomu na silaha zenye sumu.

Inaelekea Amin alipata ushirikiano mkubwa kwenye jambo hili, Urusi ilimpelekea silaha, Ujerumani Mashariki ilitoa mafunzo kwa askari wa upelelezi Uganda State Research Bureau, hizi ajensy mbili ziliogopewa sana ya Ujerumani Mashariki na ya Uganda. Wakati wa vita ya Tanzania na Uganda, Ujerumani mashariki alikanusha kabisa kujihusisha na Idd Amin.

IIn June 1973, Balozi wa Marekani nchini Uganda Thomas Patrick Melady, alipendekeza nchi yake kupunguza ushirikiano na Uganda. Balozi Melady alielezea serikali ya Amin kuwa ni ya kibaguzi, ya kikatili ya isiyotabirika, Marekani walifunga ubalaozi wao mjini Kampala. Kabla ya hapo CIA ilifanya kazi sana na serikali ya Amin ikisaidia kutoa silaha na mabomu kwa jeshi la Amin katika mipango mingi ya kijeshi na wanajeshi wa Uganda wakiwa watekelezaji.

Mnamo June 1975, Amin aliruhusu ndege ya shirika la ndege la Ufaransa iliyotekwa na vijana wa Popular Front for the Liberation of Palestine - External Operations (PFLP-EO) na watu wawili kutoka kikundi cha Ujerumani Revolutionare Zellento kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa Entebe.

Entebe watekaji waliungana na watatu wengine hii inamaana Amin alijua mipango inavyoendelea. Baada ya hapo watu 156 ambao si Waisrael waliruhusiwa kuondoka, Wayahudi 83 na raia wa Israel na wengine 20 waliokataa kuwaacha pamoja nao alikua kaptani wa ndege na cabin crew waliwekwa mateka. Waisrael walifanya mpango wa kuwaokoa waliouita Thunderbolt (radi) Operation Entebe.

Kati ya 3-4 July, kikundi cha makomando wa Israel walikwenda kwa ndege na kuteka eneo la uwanja wa ndege Entebe, waliwaokoa karibu mateka wote. Mateka watatu walikufa wakati wa pambano na wengine kumi walijeruhiwa; watekaji 7 na askari 45 wa Uganda, pamoja na askari 1 wa Israel Yoni Netanyahu waliuwawa.

Mateka wanne aliekuwa na umri wa miaka 75 Dora Bloch, bibi mzee Myahudi na Mwingereza alipelekwa hospitali kuu ya Mulago Kampala kabla ya kuanza kwa mashambulizi, aliuwawa wakati akiwa anarudisha fahamu hospitali. Tukio hili lilizidisha hali mbaya ya uhusiano na ilipelekea Uingereza kufunga Ubalozi wake Kampala.

Uingereza ilipositisha uhusiano huo Amin alitangaza amewashinda Waingereza na alijipa title ya "CBE" kwa maana ya "Conqueror of the British Empire" kwenye majina ya vyeo vyake. Baadae Radio Uganda ikatoa vyeo vyote vya Raisi kama ifuatavyo; His Excellency President for Life Field Marshal Alhaj Dr. Idi Amin Dada, VC, DSO, MC, CBE.

Uganda chini ya utawala wa Amin ilijenga jeshi lenye nguvu sana, hii ilikua tishio kwa nchi jirani ya Kenya. Mwanzoni mwa mwezi June 1975 maofisa wa Kenya walizuia shehena kubwa ya silaha zilizotengenezwa Soviet Union zikielekea Uganda katika bandari ya Mombasa. Hali kati ya Kenya na Uganda haikuwa nzuri kutokea hapo,

Amin alisema anahakikisha ardhi ya Sudani ya Kusini na Magharibi mpaka kati kati ya Kenya vinarudi kuwa sehemu ya Uganda. Serikali ya Kenya ilijibu kwa kusema Kenya haitapunguza hata inchi moja ya mipaka yake. Amin aliamua kukaa kimya baada ya Kenya kupeleka wanajeshi na silaha katika mpaka wa Kenya na Uganda.

Baadae Idi Amin alitangaza kuwa Kagera ni sehemu ya Uganda, hii ilisababisha vita ya Uganda Tanzania ambayo ilimaliza utawala wa miaka nane wa Amin na hatimae Amin alikimbilia Libya na baadae Saudi Arabia ambako aliishi mpaka mauti yalipomkuta tarehe 18 August 2003.

Kufikia mwaka 1978, idadi ya watu waliomuunga mkono Amin ilipungua sana na alikua anakabiliwa na upinzani kutokana na kushuka kwa uchumi nchini Uganda pia miundo mbinu haikufuatiliwa. Askofu Luwum, na mawaziri wawili Oryema ana Oboth Ofumi mwaka 1977, waganda wengi walikimibia nchi yao.

November 1978, baada ya makamu wa raisi Generali Mustafa Adrii kuumia katika ajali ya gari, wanajeshi wengi wa Amin walianza kuasina kukimbilia nchi jirani ya Tanzania, Amin alipeleka majeshi kupigana na wanajeshi wake walioasi katika mipaka ya Tanzania

Amin alianza kumshutumu rais wa Tanzania Julius Nyerere kwa kuanzisha vita na Uganda, Amin aliendelea kusema kuwa hata Kagera ambayo iko kwenye mpaka wa Tanzania na Uganda ni sehemu ya Uganda, rais Nyerere alitangaza vita baada ya kauli hiyo..

Janurary 1979, Nyerere alituma majeshi ya Jeshi la Wananchi na kuanza mashambulizi, Jeshi la wananchi lilipata ushirikiano wa majeshi ya msituni yaliyokuwa yakimpinga Amin kama Uganda National Liberation Army (UNLA). Majeshi ya Amin yalipata kipigo kikali sana, pamoja na msaada mkubwa aliopata Amin kutoka kwa rais wa Libya Muammar Gaddafi, ilibidi Amin akimbie nchi kwa kutumia helikopta 11 April 1979 wakati Kampala iliposhikiliwa na majeshi ya Tanzania.

Amin alikimbilia kwanza Libya ambako aliishi mpaka 1980. Baadae familia ya kifalme ya watu wa Saudi Arabia walimpa hifadhi pia walimpa pesa nzuri tu ya kujikim. Kwa miaka mingi Amin aliishi kwenye maghofa ya ju ya hoteli ya Novotel barabare ya Palestine mjini Jeddahn.

Katika mahojiano yote Amin aliyoyafanya akiwa ukimbizini aliamini Uganda inamhitaji. Hakuonyesha masikitiko yeyote kwa aliyoyafanya wakati wa utawala wake. 1989 Amin alipanga kurudi Uganda kuongoza majeshi ya Kanali Juma Oris, alifika Kinshasa Zaire ambako Raisi Mobutu Sese Seko alimwamuru arudi Saudi Arabia.

Kifo chaa Idd Amin.
Mnamo 19 July, 2002, mmoja katika wake wa Amin Madina alieleza kuwa Amin ni mgonjwa mahtuti na anakaribia kukata roho katika hospitali ya Mfalme Faisal. Amin alikuwa na matatizo ya figo. Madina alimuomba rais Yoweri Museveni, aruhusu Amin arudishwe Uganda ambako ndiyo asili yake.

Museveni alijibu kuwa Amin akirudi tu Uganda anashitakiwa kwa yote aliyoyafanya wakati wa utawala wake. Familia ya Amin iliamua kusimamisha mashine zilizomuongezea uhai akiwa hospitalini. 16 August 2003 Amin alizikwa kwenye makaburi ya Ruwais Jeddah, yalikuwa mazishi ya kawaida.

Maisha binafsi ya Idi Amin.
Amin aliamini ndoa ya wake wengi na katika maisha yake aliishi na wanawake wasiopungua watano, watatu kati yao aliwapa talaka. Aliwaoa wake zake wawili wa kwanza Malyamu na Kay mwaka 1966. Mwaka uliofuatia alimuoa Nora na baadae alumoa Nalongo Madina mwaka 1972.
2012_6largeimg214_Jun_2012_124401800-703x422.jpg


Malyam na Kay
Mwaka 9174 Amin alitangaza katika Radio Uganda kuwa amemuacha Malyamu, Nora na Kay. Malyamu alikamatwa baadae Tororo ambako ni mpaka wa Uganda na Kenya akiwa anakimbilia Kenya na jora la kitambaa. Baadae alihamia London ambako alifungua mgahawa London Mashariki (East London).

Kay alifariki katika kifo cha kutatanisha katikati ya miaka ya 1970 na mwili wake ulikutwa ukiwa umekatwa katwa. Nora alikimbilia Zaire mwaka 1979 na hakuna anaejua habari zake zaidi.

Mwezi August 1975, wakati wa mkutano wa Wakuu wa Umoja wa nchi za Afrika (OAU), Amin alimuoa Sarah Kyolaba, bwana wa Sarah ambae aliishi nae kabla ya kukutana na amin alipotea na hakuonekana tena. Sarah alikua mcheza katika jeshi la Uganda, kikundi hicho cha jeshi kilitumbuiza wageni wa OAU baada ya sherehe kuisha mmoja alitunukiwa u firt lady.

kufikia mwaka 1993, Amin alikua anaishi na watoto wake tisa wa mwisho na alikua na mke mmoja, Mama Chumaru ambae inasadikika alikua mke wa sita na mama wa watoto wake wanne wadogo. Mtoto wake wa mwisho alikua binti aliyepewa jina Iman alizaliwa 1992.
29A70D2E00000578-0-image-a-87_1434430298503.jpg


Harusi ya Sarah na Idi Amin iligharimbu shilingi million 2 za Uganda miaka hiyo. Inasadikika mpaka mauti yanamkuta Amin alibarikiwa kupata watoto 45.

Amin alifunga ndoa na Saraha Kyolaba aliekua na umri wa miaka 19. Sahara alikuwa mchezaji wa go-go katika jeshi la Uganda, harusi yao iligharimu pesa ya Uganda shi million 2 kwa wakati huo, harusi ilifanyika wakati wa mkutano wa OAU uliofanyika Kampala na mwenyekiti wa Palestine Leberation Organisation,

Yasser Arafat alikuwa best man wa Amin.i Wanandoa hawa walijaliwa kupata watoto wanne na Amin alipenda sana kufanya mazoezi ya mashindano ya magari katika gari yake aina ya Citroen SM, na Sarah akiwa navigator. Sarah baadae alikuja kuwa msuka nywele Tottenham London mpaka maout yalipomkuta mwaka 2015.

Kabla ya hajakutana na Amin alikuwa akiishi na bwana wake, Jesse Gitta, alipotea na mpaka leo hakuna anaejua kama alinyongwa, alifungwa au alitoroka kuelekea Kenya.

Mpaka ilipofika mwaka 1993, Amin aliishi na watoto wake tisa wa mwisho na mke mmoja, Mama a Chumaru, ambae inasadikika alikwa mke mpya wa sita na mama wa watoto wake wanne wamwisho, mtoto wa mwisho wa Amin ni binti aliyepewa jina la Iman, alizaliwa 1992 na mama yake aliolewa na Amin miezi michache kabla ya kifo chake.

Habari zinatofautiana kuhusu idadi kamili ya watoto wa Amini, kuna wanaosema alipata watoto 30 wengine wanasema walifika 45. Mpaka 2003, Taban Amin aliyezaliwa 1955 ambae ni mtoto wa kwanza wa kiume wa Iddi Amin alikuwa kiongozi wa West Nile Bank Front (WNBF), kikundi kilichopinga serikali ya Museveni lakini baadae Museveni alimpa kinga ya kisiasa na pia alipewa kazi kama Kaimu Mkurugenzi wa Usalama .

Mtoto mwingine wa Amin Haji Ali Amin aligombania nafasi ya umeya Mji wa Njeru mwaka 2002 lakini hakuchaguliwa. Wakati cinema iliyopata sifa za kimataifa The Last King of Scotland inatoka, Jaffar Amin ambae inasadikika kuwa ni mtoto wa 40 wa halali wa Amin kutoka kwa wake zake saba,alisema ataandika kitabu kusafisha jina la baba yake alipohojiwa.

03 August 2007, mtoto wa Amin kutoka wa mke wake Sarah aitwae Faisal Wangita aliyezaliwa mwaka 1983 alishitakiwa kwa mauwaji mjini London.
Mmoja wa marafiki wa karibu sana wa Amin ni Mwingereza Bob Astles, ambae wengi wanaamini alikuwa na urafiki wa kinafiki kuliko ilivyodhaniwa na Amin mwenyewe. Issac Malyamungu alikuwa mtendaji wa mipango yote ya Amin na ni afisa aliyeogopewa kuliko wote katika jeshi la Amin.

Tabia za ajabu za Amin
Tabia za ajabu za Amin zinahusishwa na uvumi kuwa alikuwa na ugonjwa wa akili, tabia hii isiyotabirika ilileta mtafaruku mkubwa wakati wa utawala wake, Amin alikuwa na hasira za karibu, pia mchangamfu sana, kutoka kwenye uchangamfu kufikia hasira vililikua haraka bila hata tahadhari, hakuna aliyetegemea anaweza kufanya nini dakika chache zijazo.

Wengi wanasema tabia hii inawezekana ilisababishwa na ugonjwa wa syphilis uliodumu muda mrefu bila kutibia au bipolar disorder. Kadiri miaka ilivyokwenda tabia ya Amin ilizidi kushangaza watu.

Wakati wa utawala wake, mashirika mengi maarufu ya habari yalimngenezea taswira ya mchekeshaji mwenye tabia za ajabu. Gazeti la Times lilimuandika kama "muuaji na mchekeshaji, binadamu wa ajabu mwenye moyo mzuri, ambae anataka kuonyesha umaarufu wake kwa cheo chake".


Kyalow
 
Nyerere kupitia kwa Wasemaji wake wa RTD wakati huo kina Mzee Paul Sozigwa walitufundisha kuwa Amin alikuwa anakula watu jee hizi taarifa ni kweli?
 
Nyerere kupitia kwa Wasemaji wake wa RTD wakati huo kina Mzee Paul Sozigwa walitufundisha kuwa Amin alikuwa anakula watu jee hizi taarifa ni kweli?
Hii stori angeandika Mohamed Said najua lazma mngeanza kwa kumpinga hivi sababu haswa ya kupigana vita nao ni vile alimtungua mtoto wa mchonga, alimtukana mchonga, alivamia kagera au nini vitabu vingi vinanipeleka chaka
 
Nyerere kupitia kwa Wasemaji wake wa RTD wakati huo kina Mzee Paul Sozigwa walitufundisha kuwa Amin alikuwa anakula watu jee hizi taarifa ni kweli?

Hizo ni propaganda tupu tukiaminishwa tu ili kuhalalisha kuivamia uganda. Sisi ndo tuli ikosea uganga kwa kuweka kambi za waganda kwa ajili ya kumpindua. Kina museveni walipewa kila msaada.
Amin alikua dictator lkn ilibidi iwe hivo kwani hali ya usalama haukua nzuri kwani alikabiliwa na upinzani wa ndani ma nje
 
Aisee!!!

Marais wa kwanza na wa pili wa Uganda ni kina nani?
1.Kabaka Mutesa
2.Milton Obote
3.Idd Amin Kaidada
4.Prof Yusuf Kironda Lule
5.Geofrey Lukongwa Binaisa
6.Paul Muwanga
7.Milton Obote
8.Kanali Tito Lutwa Okelo
9.Major General Yower Museven

Sky Eclat tunafurahi sana kwa elimu hii!Mm binafsi napenda historia!Habari nzuri umetupa

kwa kuongezea tu hapo baada ya jaribio la kumuua Obote la mwaka 1969 kushindwa na Idd Amin akiwa Mkuu wa Majeshi ya Uganda kukimbia nyumbani kwake Bamunanike na kwenda kujificha ktk kambi ya Jeshi ya Bombo na huko kufichwa na mkuu wa Kambi Lt Kanal Nyangweso,Jeshi la Uganda likahusishwa moja kwa moja ktk jaribio hilo

Serikali ikaanzisha uchunguzi, na moja kwa moja ripoti ikawa inamtaja Amin kama alihusika na jaribio hilo!Ripoti hiyo ikawa isomwe tarehe 25,1970 lkn haikusomwa kwani usiku wa tarehe 24 huko ktk kambi ya jeshi ya Guru,aliyekuwa mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Uganda Brigedier msomi tena kijana Pierino Okoya aliuwawa akiwa nyumbani kwake!

Rais Obote akaunda tena tume kuchunguza mauaji ya Brig Okaya,pia akaagiza kuwa akirudi toka Singapore lzm apate ripoti ya matumizi ya hovyo ya pesa za serikali ktk kununua vifaa vya jeshi!Ili kuonyesha kuwa sasa Amin hatapona,Rais Obote akatenganisha vitengo kadhaa ktk jeshi la nchi kwa kumteua Brigedia Mohamed Hussein kuwa mkuu wa utawala jeshini na Kanali Tito Okelo kuwa mkuu wa kambi yenye nguvu ya Mbarara!Amin akabaki kama figurehead tu

Amin ikawa hana cha kufanya zaidi ya kunyakua madaraka hapo January 25,1971 asubuhi ya saa 1!Alichokifanya kwa nchi ya uganda hamna asiyejua!

Sky Eclat tunashukuru sana,tupe zaidi
 
1.Kabaka Mutesa
2.Milton Obote
3.Idd Amin Kaidada
4.Prof Yusuf Kironda Lule
5.Geofrey Lukongwa Binaisa
6.Paul Muwanga
7.Milton Obote
8.Kanali Tito Lutwa Okelo
9.Major General Yower Museven

Sky Eclat tunafurahi sana kwa elimu hii!Mm binafsi napenda historia!Habari nzuri umetupa

kwa kuongezea tu hapo baada ya jaribio la kumuua Obote la mwaka 1969 kushindwa na Idd Amin akiwa Mkuu wa Majeshi ya Uganda kukimbia nyumbani kwake Bamunanike na kwenda kujificha ktk kambi ya Jeshi ya Bombo na huko kufichwa na mkuu wa Kambi Lt Kanal Nyangweso,Jeshi la Uganda likahusishwa moja kwa moja ktk jaribio hilo

Serikali ikaanzisha uchunguzi, na moja kwa moja ripoti ikawa inamtaja Amin kama alihusika na jaribio hilo!Ripoti hiyo ikawa isomwe tarehe 25,1970 lkn haikusomwa kwani usiku wa tarehe 24 huko ktk kambi ya jeshi ya Guru,aliyekuwa mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Uganda Brigedier msomi tena kijana Pierino Okoya aliuwawa akiwa nyumbani kwake!

Rais Obote akaunda tena tume kuchunguza mauaji ya Brig Okaya,pia akaagiza kuwa akirudi toka Singapore lzm apate ripoti ya matumizi ya hovyo ya pesa za serikali ktk kununua vifaa vya jeshi!Ili kuonyesha kuwa sasa Amin hatapona,Rais Obote akatenganisha vitengo kadhaa ktk jeshi la nchi kwa kumteua Brigedia Mohamed Huasein kuwa mkuu wa utawala jeshini na Kanali Tito Okelo kuwa mkuu wa kambi yenye nguvu ya Mbarara!Amin akabaki kama figurehead tu

Amin ikawa hana cha kufanya zaidi ya kunyakua madaraka hapo January 25,1971 asubuhi ya saa 1!Alichokifanya kwa nchi ya uganda hamna asiyejua!

Sky Eclat tunashukuru sana,tupe zaidi

Asante sana, this is very interesting part of the story. Nitaendelea nipeni muda. Kuna Maisha ya binafsi ya Amini.
 
Back
Top Bottom