Kiranga ili tukuthibitishie kuwa Mungu yupo unataka tukuoneshe kitu gani au tukuthibitishie kwa mrengo upi ili uamini uwepo wake?
ebu jibu kwa ufasaha na straight hili swali,sitaki uzunguke zunguke...
Shukurani nyingi sana zikufikie kwa kutaka kuweka msingi wa uthibitisho utakaokubalika kabla ya kurukia kuthibitisha.
Kwa haraka haraka tu hili linanieleza kwamba unataka majadiliano yenye kina na yanayotaka kufikia makubaliano na hata ukweli.
Nakusihi sana, chonde chonde, tuzungumze kwa upole, tupime neno kwa neno. Nina Imani kwamba una akili na uwezo wa kufanya hivi, kwa sababu swali ulilouliza, kwa anayeelewa, si dogo. Ni la mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri.
Uthibitisho ninaoutaka mimi ni wowote ambao haujipingi wenyewe (non-contradiction, logical consistency) na angalau unaweza kueleweka katika akili za kibinadamu (humanly comprehensible).
Nasema uthibitisho usijipinge kwa sababu kama uthibitisho unaweza kujipinga, huo si uthibitisho. Ni uchafuzi wa uthibitisho.
Nasema angalau uweze kueleweka katika akili za kibinadamu kwa sababu mungu hawezi kujificha asiweze kuthibitika katika akili za binadamu, hususan kama ana nguvu zote, uwezo wote na upendo wote na atahukumu binadamu ambao hawakumjua.
Vinginevyo, kama uthibitisho wa kuwepo kwa mungu unaweza kujipinga wenyewe katika akili za binadamu, au unaweza kuwa umejificha usijulikane katika akili za binadamu, huyu mungu atakosa haki ya kuweza kumuhukumu binadamu kwa kutomjua mungu.
Atamhukumu vipi binadamu kwa kutomjua mungu kama hajampa nafasi ya kumjua mungu vilivyo huyu binadamu?
Kwa msingi huu, uthibitisho wowote unaojikita katika msingi wa ""god works in mysterious ways" hautafaa, kwa sababu utakuwa ni uchafuzi wa uthibitisho kwa maana ya kwamba hauejielezei ulivyo, unazika kuelezea ulivyo.
Unaweza kuthibitisha uwepo wa mungu kwa msingi hii miwili ?
Asante tena na shukurani nyingi kwa usomi uliouonyesha kwa kuuliza aina ya uthibitisho unaotakiwa kabla hata ya kutaka kutoa uthibitisho.
Ningefurahi sana kama wengi wangeweza kufikiri kama wewe na kuuliza maswali kama haya kabla hata ya kutaka kujibu.