Eeh bhana eeh!!!! Ni abo ndio bana Congo.
1.Bongo hawaichukulii poa ni kama sisi tunavyoiona nchi kama South Afrika.
2.Papuchi wanawake wanauza balaaa.
3. Apo kwenye kisa cha bodaboda ni kwaida mtu kukodi boda kwa umbali mrefu kama Dar-Moro. Nimeshuhudia Kalemie bodaboda ilitumika kusafirisha mwili wa marehemu kwa mazishi kijijini kwao.
4.Si chakula safi tu ,mlo ni mmoja saa 10 hioni mpaka saa 10 jioni. Hili si kwa watu wenye kipato cha chini pekee bali ni kwa asilimia kubwa ya raia na ata watoto iyo hali wameizoea.
5.Kujichubua hakuchagui jinsia wenyewe wanakwambia "mwekunda"kumaanisha mtu mwenye rangi iyo.
6.Dolla inatumika kama kawaida unaweza lipa dukani kwa pesa ya Congo chenji ukapewa Dolla yenye thamani ya salio lako na pesa ya Congo ao vice versa.
7.kuongea kiswahili ni kitambulisho cha "born town" hakuna anaetaka kuonekana wakijijini.
8.Pombe apo ndio penyewe acha na na za kiwandani Primus,Amstel,Skol n.k. Gongo inanyweka sana ata Bar unapata wanaita cinq cent (senk nsa) yaani Jero (mia tano)
Lingine: Wana import vyakula kama unga, mchele,ndizi, nyama, mafuta ya kupikia na packed vinywaji baridi kama soda, juice n.k ata nyanya,vitunguu kutoka Kigoma japo nasikia serikali imedhibiti wana Kigoma kufanya biashara izo.
..... Niliyoyashuhudia Kalemie.....