Vitu nilivyojionea nikiwa ndani ya nchi ya Congo

Vitu nilivyojionea nikiwa ndani ya nchi ya Congo

Wala hujaongopa Dada hapa Jirani Naish na mkongo ni msafi Wa ndani mpk rahaaaa, anapenda kuvaa na kujiremba Sana
Shida nadhani hawajui deodorants/perfumes/mafuta/lotions za kike/kiume[emoji52][emoji52][emoji52]
 
Maisha unajaribu popote mfano Zambia, Malawi hawajui kujenga sehemu zingine hawajui machinga hawa wa kutembeza vitu majumbani, hivo ukiwa Fundi mzuri wa Ujenzi, nguo,Magari, nk unaweza ukapata fursa maana ni nadra sana kutajirika ulipozaliwa,cha msingi tu utafute vibali vya sehemu husika.Wamasai wametengeneza sana Pesa Zambia kwa kusuka na kuuza vitu vya asili.
Nakubaliana na wewe mkuu, nilikosa kwacha mji mmoja wa chipata eastern province nikaenda bank wakasema wanachange dollar na rand tu, nikaelekezwa kwa mmasai anazo nikabadili na akasema anafanya kwa hiyo miezi mitatu then anarudi manyara au boda anagonga tena anaingia
 
Habari za majukumu wakuu.

Tangu nisafiri kuja Congo kuna mambo fulani ambayo nimejaribu kuona kwa macho yangu mengine kwa hisia tu.
Pia kuna baadhi ya mambo ambayo nimeyafanyia utafiti mdogo na baada ya hapo nikajiridhisha kwa vitendo.
Ngoja niweke ambayo nilijionea mwenyewe:-

1. Ukiwa Mtanzania utalala na wengi:
Hapa nazungumzia kwa wale wenzangu nami wanaependa kuserereka na totoz, yaani ni kwamba wanapoona unazungumza kiswahili fasaha hujipendekeza na kuwa na wewe karibu.
Hauna haja ya kuanza kutingoza mda mrefu ni kuomba namba ya sim na mengine yatajileta yenyewe.

2. Kuna wadada wazuri mno ila wengi ni makahaba:
Hapa sijajua sababu kuu ni ipi ambayo inapelekea wadada wazuri wanapenda kazi hiyo.
Unapishana na wadada kama watatu wanne utakaemkuta usiumize kichwa chukua twende.

3. Boda boda nyingi:
Yaani kuna boda boda nyingi kuliko nchi zingine zote za afrika.
Hapa naweza kusema kumechangiwa na wingi wa watu wenyewe na nchi yenyewe ilivyo kubwa.

4. Chakula safi ni shida:
Kwa Mtanzania ambae umezoea vitu vizuri vizuri kwe 'restaurants' za Tz basi kwa huko utazunguka sana mwisho was siku utaambulia ugali (bada).
Chapati zao sio nzuri hawajui kupika supu hata samaki was kwao.
Siku Mtz akijitokeza kupika pilau au biriani basi ataondoka na utajiri usio na kifani.

5. Wanapenda kujichubua sana:
Kwao ni vitu vya kawaida na imeonekana 'fashion' kufanya hivyo mafuta yanayokatazwa Tz, Congo yapo sokoni.

6. Wanathamini dola kuliko hela ya kwao:
Yaani kila duka utakalotembelea ni dola dola hadi unachoka mwenyewe.
Sio kwamba hela ya kwao hawatumii, la hasha! Wanatumia sana ila dola ndo kila kitu mijini na vijijini.

7. Kiswahili wanakipenda sana:
Mara nyingi wanapenda kuongea kiswahili kuliko kilingala na kizulu. Hata kama utawakuta wapo wenyewe wanaongea lakini lazima waingize kiswahili.
Kiswahili walikipenda sana ila kifaransa kiliwapenda zaidi.

8. Pombe ni nyingi sana kuliko maji safi ya kunywa.
Hapa kila kona utakayozunguka utakuna na pombe aina ya bia zimesheheni, lakini ukija kwa upande wa maji ya kunywa sio mengi.

Kwa leo niishie hapo maana kuna mengine nimeyasahau ila kama kuna mtu ambae anafaham zaidi anaweza kujazia nyama.
Pia askari wao ni wala rushwa wakubwa,ndege zao ni kama daladala za kwenda Kivule,hazina usalama na watu hupanda na hata mbuzi wengine wakiwa wamesimama kama basi za Mwendo kasi,kwenye vyakula hawana tofauti na wachina,hula nyani,nyoka ,majongoo. Kuna jamaa yangu ameacha mapacha huko alienda kikazi akafanya vitu vyake,bahati mbaya kwake kazini wamemtemesha kwa hiyo ataishia kuwaona bana kongo kwa FB au WhatsApp tu
 
Hapo vipi?
 

Attachments

  • IMG_20180421_100831.jpg
    IMG_20180421_100831.jpg
    34.3 KB · Views: 104
Hii page ningependa uendelee kutupia vitu tofauti kutoka huko boy.. Shida na raha
 
Kama vipi mkuu ungependa nilete hapa?
Hususan mazingira yao, uvaaji, maduka yao labda yanafanana na ya mbeya duka la vyakula ukakuta na pombe vimepangwa pa1 na hawa wakongo tuonao huku kutoboa pua au kuweka kichuma kwenye ulimi na huko wapo..?
 
Hahaah naona hutak kuonesha una njaa ya kumla huyo demu mkuu
Leo nimeamua kumuhitimishia rafiki yangu, kaenda kumaliza mambo guest mimi nilikua nawasubiri walipomaliza tukaondoka.
Na wakati nawasubiri kuna mmoja nae akajipendekeza, kama wewe unamataka sema nikupasie na wewe.
 
Hususan mazingira yao, uvaaji, maduka yao labda yanafanana na ya mbeya duka la vyakula ukakuta na pombe vimepangwa pa1 na hawa wakongo tuonao huku kutoboa pua au kuweka kichuma kwenye ulimi na huko wapo..?
Kwa upande wa mazingira ni kama nyumbani tu.
Uvaaji nao pia ni kama nyumbani vile vile palivyo Dar ndo palivyo mji wowote Congo.
Kwa upande wa maduka pia ni hivyo hivyo, sema kwa upande vyakula wapo chini sana, ukisema nipeleke sehemu ya chakula asilimia kubwa utapelekwa bar.
Na la mwisho kuhusu kutoboa pua na vichuma kwa hapo kwa mimi binafsi sijawaona, ila nahisi wapo sana tu.
Ukiangalia maisha tunayoishi Tanzania ndo maisha wanayoishi Congo, Burundi, Kenya na Rwanda pia kasoro lugha tu.
 
Back
Top Bottom