Vitu nilivyojionea nikiwa ndani ya nchi ya Congo

Vitu nilivyojionea nikiwa ndani ya nchi ya Congo

Wanawake wa Congo siyo wazuuuri km unavyosema,
Sema wanajipodoa kupitiliza,
Suala la kiswahili ni kweli maana nimewahi Fanya daladala nzima ikanyamaza sababu tu nilivyokuwa nataka Maelezo ya konda,
Kuhusu vyakula ni kweli hovyo kabisa,niliwahi kula kichwa cha mbuzi kilichopondwa pondwa wakachanganya na kisamvu,
Wanawake wao wanaongea sana,wanamidomo mno,
Mkuu mji gani hasa umerenga
Hahaaaaa hapo Kwenye midomo hujawaonea Kabisa
 
Mleta mada ninakusifu. Umetuonesha FURSA nyingi sana:
1. Uhaba wa maji ya kunywa - mjasiriamali anaweza kupeleka maji ya chupa mf. maji afrika,uhai, k'njaro, lulu n.k.
2. Biashara ya pombe
3. Biashara ya huduma ya afya mfano hospitali, duka la madawa ( hao wanaojipitisha kwenye malori, makahaba - uwezekeno wa magonjwa ya ...),
4. Biashara ya pikipiki na vipuri vyake
5. Walimu wa kufundisha lugha ya Kiswahili
6. Biashara ya Mama Lishe yenye ubora wa hali ya juu
Maisha unajaribu popote mfano Zambia, Malawi hawajui kujenga sehemu zingine hawajui machinga hawa wa kutembeza vitu majumbani, hivo ukiwa Fundi mzuri wa Ujenzi, nguo,Magari, nk unaweza ukapata fursa maana ni nadra sana kutajirika ulipozaliwa,cha msingi tu utafute vibali vya sehemu husika.Wamasai wametengeneza sana Pesa Zambia kwa kusuka na kuuza vitu vya asili.
 
Eeh bhana eeh!!!! Ni abo ndio bana Congo.


1.Bongo hawaichukulii poa ni kama sisi tunavyoiona nchi kama South Afrika.

2.Papuchi wanawake wanauza balaaa.

3. Apo kwenye kisa cha bodaboda ni kwaida mtu kukodi boda kwa umbali mrefu kama Dar-Moro. Nimeshuhudia Kalemie bodaboda ilitumika kusafirisha mwili wa marehemu kwa mazishi kijijini kwao.

4.Si chakula safi tu ,mlo ni mmoja saa 10 hioni mpaka saa 10 jioni. Hili si kwa watu wenye kipato cha chini pekee bali ni kwa asilimia kubwa ya raia na ata watoto iyo hali wameizoea.

5.Kujichubua hakuchagui jinsia wenyewe wanakwambia "mwekunda"kumaanisha mtu mwenye rangi iyo.

6.Dolla inatumika kama kawaida unaweza lipa dukani kwa pesa ya Congo chenji ukapewa Dolla yenye thamani ya salio lako na pesa ya Congo ao vice versa.

7.kuongea kiswahili ni kitambulisho cha "born town" hakuna anaetaka kuonekana wakijijini.

8.Pombe apo ndio penyewe acha na na za kiwandani Primus,Amstel,Skol n.k. Gongo inanyweka sana ata Bar unapata wanaita cinq cent (senk nsa) yaani Jero (mia tano)

Lingine: Wana import vyakula kama unga, mchele,ndizi, nyama, mafuta ya kupikia na packed vinywaji baridi kama soda, juice n.k ata nyanya,vitunguu kutoka Kigoma japo nasikia serikali imedhibiti wana Kigoma kufanya biashara izo.

..... Niliyoyashuhudia Kalemie.....
Kwa njia ya panya vinaenda walindao ni watu pia Kigoma Bandari bubu ni nyingi kuliko idadi ya walinda mipaka.
 
Kuhusiana na hilo mkuu wala hawaulizwi, sheria zao wanazijua wenyewe, kubwa ni kukea gari lako tu maana na watu wanapanda mpaka juu.
Ukiamua ununue canter lako au fuso kisha uweke nafasi nyuma si unapiga pesa huko, ama?
 
Yaani wanaishi wanavyotaka, Hakuna sheria za barabarani, ukiwa katikati ya mji si ajabu kuona carina imepakia nondo za futi kumi nyingi za kutosha juu kwenye roof
 
Kinshasa (mji mkuu wa DRC) na Brazzaville (mji mkuu wa republic of Congo) ndiyo miji mikuu ya nchi mbili iliyo karibu zaidi. Inatazamana. Ni umbali wa km 36 tu, 1hr drive au dakika 5 kwa ndege.


Ardhi ya Congo yote yani yote kwa ujumla wake ni mali, karibu kila kitu kinapatikana Congo na hii ndo sababu hawana amani. Kwa utajiri wa rasilimali naamini ni nchi ya kwanza duniani
Yes ndo ya kwanza duniani kwa raslimali,dini lolote,mafuta,gas,udongo, nk takataka zote zitakiwazo duniani ziko Kongo. Wabongo tulinyimwa uwezo wa kubuni au kujiongeza kuhusu fursa tungetumia Bandar yetu kwa maslai ya kibiashara na Congo tungekuwa mbali sana.
 
Yaani wanaishi wanavyotaka, Hakuna sheria za barabarani, ukiwa katikati ya mji si ajabu kuona carina imepakia nondo za futi kumi nyingi za kutosha juu kwenye roof
Ahahahahahah ,,amani ipo nasi tukatembee
 
Hapo unataka kumuuza, ni sawa ataingia Kongo kwa rushwa siku ya kutoka na kupitia nchi nyingine akidaiwa passport ataeleza nini?
Ukitaka kuinjoi au kutafuta nchi za watu msipende short cut mambo ya maghumasi yaachieni bongo huku unaweza malizana na wabongo wenzio,nchi za watu jela zao mbaya utalishwa vyakula usivovizoea pia utarudi kwenu kwa miguu,maana mtaji wote utauacha kule, muwe na documents halali
 
Back
Top Bottom