Vitu gani vya kijinga na hatarishi uliwahi kufanya katika maisha yako?

mwitasa

Senior Member
Dec 28, 2013
199
476
Kuna wakati maisha yanaweza kukubana na kukupelekesha kiasi cha kuchukua uamuzi wa kufanya jambo fulani ukasahau kutumia akili yako au elimu yako ya darasani kutoa uamuzi sahihi.

Baada ya kutekeleza jambo hilo na ukafanikiwa au ukafeli na kuumbuka ndipo unagundua ulichukua maamuzi ya kipumbavu kiwango cha lami na kila aliyeshuhudia matokeo ya ulichofanya anakushangaa.

Kwangu mimi
Nakumbuka kipindi korona ilipoingia Tanzania yaliwekwa masharti magumu yaliyoathiri mfumo wetu wa maisha.

Wataalamu walilikuuza jambo hili kiasi cha kutufanya watu wengine tuishi kwa hofu kuona kama ukikosea sharti moja ndiyo mwisho wa maisha yako.

Nawa maji tiririka, tumia sanitizer, epuka misongamano na vaa barakoa ni baadhi tu ya masharti magumu kila mtu aliyeingiwa na hofu kama mimi alikumbana nayo.

Sasa Nakumbuka nilisafiri kwenda Dar kutafuta maisha nilikaa huko kwa miezi 3 bila kukutana na mwanamke kimwili nikiogopa kupumliana na mwanamke nikihofia ataniambukuza korona.

Ikafika hatua uzalendo ukanishinda akili yangu ikaenda likizo. Kuna dada nilikutana naye tukabadilishana namba nikamtongoza akakubali. Tukapanga mechi. Nikakutana naye na kuingia kwenye mechi nikiwa nimejihami nyanja zote za kiafya ikiwemo kucheza mechi nikiwa nimevaa barakoa.

Bwana wee ilipofika katikati ya mechi nikahisi pumzi kukata, nguvu kuanza kuniishia na kuona maruweruwe.

Nashkuru yule dada alikuwa anajua ABC za huduma ya kwanza aligundua kuwa kuna kitu hakipo sawa kwangu akanitoa nje fasta kwenye hewa na kunivua barakoa na kuanza kunipepea na kanga na baada ya muda nikarudi katika hali yangu ya kawaida na akili kunirudia.

Nilijiona mpumbavu kuliko wapumbavu wote . Kwanza mechi iliishia njiani bila kufunga bao pili nilitaka kufa kijinga kama mtu ambaye hakuingia darasani. Tukio hilo nimenipa funzo ambalo sitakuja kulisahau.

Haya na wewe lete tukio la kijinga uliliwahi kulifanya katika maisha yako.
 
🤣🤣 ulikwepa moto ukataka kukanyaga moto ungekufa ila watu mnaakili za hovyo dah
 
Nikiwa na miaka 15 kuna mti nilikuwa naukata
unamiba unaitwa mgunga chuma ulimti
wakati unaanguka ukaja upande wangu nikakimbia lakini yale matawi ya juu kabisa
yalinizibua vyema kabisa.
basi ikawa ni kazi ya wana kijiji kunitoa miiba.
 
Kwenda na mke wa mtu stend kupokea mumewe. Ili nikifika stend nirudi na boda yeye achukue mumewe. Njia nzima nashikashika upaja. Ni wale wanandoa wanaoishi mbali. Kwa hiyo inakuwa kama umekaimishwa. Mapenzi ni upofu. Sitarudia tena.

Mimi sijasema kataa ndoa
 
Tukiwa watoto tunaogelea ziwa nyasa tulikuwa tunashindana kuzamia kuchukua mchanga, kadiri depth inavyoongezeka ndivyo watu wanavyopungua na lazima ukitoka kuzamia uoneshe wenzako mchanga uliochukua chini,tukabaki wawili mi nikajiapiza lazima nishinde tukasogea mbele,tulipoibuka hakuna aliyefanikiwa tukaenda tena.Nilijilazimisha mpaka nikaupata nikauweka jiganjani ili nikiibuka niwaoneshe,kilichotokea pumzi ikakata nikajiona nakufa nikauachia mchanga huku masikio yakilia mlio kama wa turbo hivi,nikafanikiwa kuibuka wenzangu wananisubiri niowaneshe mchanga wakaniuliza mchanga uko wapi wala hata sikuwajibu nikavaa nguo moja kwa moja nyumbani.Kwangu ule ulikuwa ujinga ambao sitausahau.
 
aahhahahhahah.........mkuu ulionana na zilaili mtoa roho
 
Back
Top Bottom