Vitu gani vilikufanya ubadilishe mtazamo wako juu ya kitu ama jambo fulani..?

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
35,744
Reaction score
86,370
Sisi kama binadamu kuna vitu vingi tunapitia nakuwa na uzoefu katika vitu hivyo!, Navyo hutupelekea kubadilisha njia ama mtazamo juu ya kitu fulani je, wewe ni vitu gani hivyo vilikufanya ubadili mtazamo juu ya kitu fulani..?

Binafsi ni kazi.
Nina hulka ya introvert, ila kazi niifanyayo inakinzana na hiyo hulka!.
kivipi..? katika namna hii.
kazi niifanyayo inahitaji uwe na interaction nawatu mbalimbali na kila mmoja umpokee na hulka yake na si hivyo tu!, inahitaji upendezeshe kazi yako kwamaana ili mtu huyo yeye na hali yake na hulka yake anahitaji kuifurahia kazi yako!.

Sasa kwa jambo kama hilo kwa aina ya watu ambao ni introvert ni ngumu!,maana wao si watu wazuri sana kwenye kuhusiana na watu tena zaidi wasiowajua!.
asikuambie mtu ni ngumu hii hali mpaka uizoee!, kwani pasipo na maongezi unahitajika ufanye maongezi kitu ambacho kwa aina ya introvert ni ngumu kuanza wao maongezi!..
na hata unaweza usianzishe wewe maongezi ila ulienae akawa anahitaji maongezi sasa hapo shughuli ndipo inapoanzia kuwa tafrani!..😂

Haiishi hapo unaweza ukakutana na mtu aidha yeye anapenda miziki ya aina fulani na wewe huipendi so inakupasa wewe uisikilize hata kama hauhitaji!, na vibe lake anataka liwe kwako!..
Hivyo ni vichache katika mengi ila hoja yangu ya msingi hapa ni vile nimeweza kulandana na watu wa aina mbalimbali bila kujali itikadi zao, uwezo wao, vitu wanavyopenda na wasivyovipenda... So unajikuta unatakiwa ku balance "hulka yako na zao!", ni sentensi ndogo sana kwa kuisoma ila kuishi ni kitu chengine!.

Jambo hilo limenibadili nini katika mitazamo yangu..?
kwanza nimejua aina nyingi za watu, pili hulka ya introvert na extrovert zinatakiwa ziwe katika uwiano sawasawa!, kwa maana ya ujue ni wapi u tune nakuonyesha tabia zipi ambazo ktk mazingira hayo zinaweza kukupatia faida!.
Hapa nitawapa msemo mmoja "Kama unatafuta njia basi ongea na watu maana watu ndo wanazijua njia!".

Kuwa na mitazamo huru!.
Ikitokea akaja mtu mpya kwenye kazi yako, ama popote maishani akakufunza kitu fulani basi usiwe wakupinga tu ama kupambana nae!, jitahidi kujifunza hicho kipya alichokuletea na pia jitahidi kuchakata nini chakuchukua na kipi chakutokuchukua!, maana hata mtu mmbaya unaweza kupata funzo kutoka kwake hata kwa huohuo ubaya wake!.

Jua hisia zako na zipime kwa mitazamo huru/akili.
Unaweza ukamchukia mtu bila au kwasababu ambayo si ya nguvu sana so hizo hisia za chuki usiziendeleze!. jaribu kuzi challenge kwa akili maana binadamu muda mwengine huwa tunahisia tu kitu pasipo hali yoyote ya mantiki so, ili kujiepusha na migongano isiyo lazima penda kufanya hivyo!.
kwa maana nyengine naweza kusema uwe "emotional intelligent!".

Vilevile kutokana na kuwasoma watu hulka zao nimejikuta najua na naweza kuchambua watu fulani wanapenda nini, kuamini nini na kwanini watu wa namna hiyo wanapenda nakuamini hicho wanachokiamini!.
Niwaambie ukweli kuna watu mnakwaruana nao kwasababu hujawajua vyema, watu unaohusiana nao penda kuwasoma hata kama huwapendi wewe wasome tu!, sio kisa huwapendi ndo usiwasome no change that!.
Kumsoma mtu nakumjua ki hulka si dhambi ni itakusaidia wewe na pia unaweza kujiepushanae ambapo unaona mnaweza kuleteana shida!.

Pia kazi hiyohiyo imenifanya nijue watu wengi haswa sisi waafrika hawana staha, uwajibikaji na ubora!. ila kwenye hili kuna sababu za sisi binafsi na kimazingira!.

kwa sasa niishie hapo ila kadri mada itakavyokuwa ikiendelea nitazidi kuweka hiyo mitazamo myengine!, nawe itakuwa vyema ukishiriki ktk hili ili tujifunze kwa pamoja uzoefu mbalimbali tunaopitia!.
 
Vitu Kama hivi vilinifanya nibadili mitazamo yangu mingi
downloadfile.jpg
 
Pia kazi hiyohiyo imenifanya nijue watu wengi haswa sisi waafrika hawana staha, uwajibikaji na ubora!. ila kwenye hili kuna sababu za sisi binafsi na kimazingira!.🤔🥺😔
 
Niliamini mke wangu ananipenda kupita maelezo ilifuka kipindi hadi akaunt ya benki tulikuwa tunatumia moja,,yani nilikuwa na deposit kwake then mtu akiwa na shida anaenda ATM.
Picha likaanza sasa mwaka juzi kuna kipindi nilikosa kazi yoyote yeye ndio kidogo akawa ana income aise nilishuudia dharau,kejeli game sikupewa mpaka uombe wiki nzima na vingine vingine
Sasa bana maokoto yalivyorudi daah anaisoma namba kweli kweli yani nimekuwa mtu AmBAe hata sieleweki kwake yani nimekuwa kama vampire tu yani hahah mapenzi nyoko
 
Mnazidi kuwapa points kataa ndoa..😂
 
Nakumbuka kipindi hapo nyuma nilikuwa naogopa kujudge issue ambazo zinaleta mkanganyiko haswa kwenye Maswala ya kidini

Kwa kuogopa kuhoji kwamba hili lipoje na hili lipoje lakini

Sina umri mkubwa sana nipo kwenye 20s za kati

Siogopi kuuliza pale napoona pana kasoro,nimekuwa na imani Yangu ya kivyangu,,,ambayo jamii yangu nikiwahusisha kuhusu ninacho amini kuhusu dini na Mungu kwa sasa

Wamekuwa wakihisi nimechanganyikiwa au nakufuru

Wengivwamekuwa wakitishia kuhusu kifo lakini end of the day wote tunakufa

NAISHI KWA KUFANYA MEMA PIA KUWAFANYA WENGINE WAFANYE MEMA KATIKA MEMA NA MABAYA HAPO NDIPO KUNA SHETANI NA MUNGU

SIHITAJI DINI KUTAMBUA BAYA NA JEMA
 
Pia nina ndugu nilihisi wananipenda sana na ni kweli hapo zamani walikuwa wakinipenda sana lakini

Mtazamo wangu kuhusu ule upendo umeanza kubadilika pale yule bibi yangu mdogo aliyekuwa akinipenda sana

Ana watoto pia wana maisha mazuri kuliko mimi lakini,kwa sasa amekuwa akilalamika,na kunionesha chuki iliyondani kabisa chuki ya kizee ambayo inatisha sana kwa ukicompare na ule upendo niliwahi oneshwa kwa sababu anasema hajawahi kula hela yangu

Ingali mama yangu hajawahi kula pesa za watoto wake

Hakika mtazamo wangu kuhusu ndugu ulibadilika mazima

Ndugu zangu ni Baba yangu,mama yangu na wadogo zangu
 
Back
Top Bottom