Vitu 10 kumhusu bae Suzy wa Vagabond

Krikichino

JF-Expert Member
Oct 5, 2019
651
1,098
Nisijifanye namfahamu sana Bae Suzy. Of course nimeangalia movie yake moja inaitwa ASHFALL amefanya na Lee Byung Hun { bonge la chemistry}

Kwenye upande wa series nilimuona kwenye GU FAMILY BOOK na ile kali kuliko yote VAGABOND ya mwaka 2019 aliyoshirikiana na Lee Seung Gi.

Ninachopenda kwa Bae Suzy ni namna ambavyo halazimishi character akiwa anaigiza anyway kama unamfaham au umfaham basi leo naleta kwenu vitu 10 usivyovijua kuhusu mwanadada huyu.

10) Mwaka 2015 alikuwa kwenye mahusiano na Lee Min Ho baada ya muda waliachana kwa sababu ya kila mtu kuwa busy na ratiba zake.

9) Ana uzito wa 47 Kg na urefu wa 160 cm na pamoja na kuwa na uzito kidogo Bae Suzy hapendi vyakula vya mbogamboga.

8) Suzy aliingia kwenye kiwanda cha burudani baada ya kuchaguliwa kuwa kama Model wa shopping mall moja huko mjini Seoul akiwa na miaka 15 tu.

7) Anapenda rangi ya Pink na inasemekana hata chumba chake kimepambwa na rangi ya pink.

6) Bae Suzy ni mojwapo ya watu wenye followers wengi kwenye mtandao wa twitter huko nchini South Korea.

5) Ukiachana na uigizaji Suzy pia ni mtangazaji mzuri tu alikuwa ni mtangazaji wa kipindi cha Music Core! kuanzia mwaka 2010.


Pia hata tuzo za BAEKSANG ARTS AWARDS zilizofanyika trehe 13 May 2021 Suzy alikuwa kama MC wa sherehe hii

4) Suzy ana urafiki wa karibu na muimbaji na muigizaji Lee Ji Eun (IU). Ukaribu huo ulianza baada ya Suzy kumpigia simu IU siku ya Birthday yake.

3) City Hunter ya 2011 starring Lee Min Ho ndio series bora yake muda wote.

2) Suzy amesoma Seoul Perfoming Arts high school shule maalum ambayo pia mastaa kama Sulli na Kim Ji Soo toka kundi la Black Pink pia walisoma hapo.

1) Suzy pia anafanya muziki ana EP 2 ikiwemo YES OR NO? Pamoja na Faces of Love.

Kipi kingine unakifahamu kutoka kwa Suzy?

b6f69549e61d4e998dca32a803ca5292.jpg
vbYKLHYI.jpg
1194bb2fe104631e2479fce186d8409f.jpg
 
Mmmmmmhmn, haya matamthiriya ya kikorea ndio yalinifanya nitupe king'amuzi cha startimes nikaweka Dstv.Maana wameyajaza kila kona kwenye channels za startimes......
 
Back
Top Bottom