Wasanii watano kutokea South Korea ambao ni waigizaji na wanamuziki kwa pamoja

Krikichino

JF-Expert Member
Oct 5, 2019
651
1,098
Kwa hapa Tanzania wasanii hawa tungewafananisha na Nandy, Quick Rocca, Rommy Jones au Shilole. Kwenye futiboli tungeweza kuwaita viraka maana ukiachana na uigizaji wao mzuri pia wana uwezo mkubwa kwenye kuimba.

Leo nataka niwalete kwenu wasanii watano kutokea korea kusini ambao ni waigizaji pia wanafanya au walishafanya muziki

5.LEE MIN HO.
Kwa hapa Tanzania wengi tulimfaham kwenye Boys BOYS OVER FLOWERS kisha akaigiza kwenye CITY HUNTER natoka hapo akawa ni mmoja wa waigizaji kutokea nchini Korea wanaofuatliwa sana.

Habari njema ni kuwa Lee ni mwanamuziki yuko Chini ya Label ya STAHAUS na alitoa album yake ya kwanza May 23 2013, album hiyo ina nyimbo kama "Without You", "Love Motion" na "my Little Princess".

Juzi juzi hapa pia alitoa albamu mpya chini ya Universal Music, albam hiyo inaitwa SONG FOR YOU . Binafsi sijasikiliza bado album hiyo but naaamini naamini itakuwa kali yenye kiwango cha lami kwa sababu Min Ho hajawahi kuwaangusha mashabiki zake.

4. JANG HYUK
Kama umeangalia SLAVE HUNTER aka Chuno basi Jang hyuk utakuwa unamfaham.

Kama utakuwa hujamuona humo kwenye Slave Hunter basi utamkuta kwenye IRIS 2, THE VOICE na kwenye movies kama THE SWORDS MAN ya na THE FLU ya mwaka 2013.

Kikubwa nnachotaka kusema hapa ni kuwa Jang Hyuk ni Rapper mzuri tu. Mwaka 2000 alitoa abum yake ya kwanza na ya mwisho inayoenda kwa jina la TJ PROJECT kupitia Label ya LOEN ENTERTAINMENT.

Kwa sasa Hyuk ambae hana ukurasa rasmi kwenye mtandao wa kijamii ni kama amestaafu kuimba hip hop maana amejikita sana kwenye uigizaji maana hajatoa muziki au wimbo wowote miaka ya karibuni

3. LEE SEUNG GI
Juzi juzi hapa niliweka uzi hapa kumhusu Lee seung gi humu.


Fahamu mambo 10 usiyoyafahamu kuhusu Lee Seung gi aliyeigiza Vagabond

Tukisema kiukweli huyu mwamba ana sauti nzuri linapokuja kwenye suala la kuimba.

Tulianza kumjua sana kwenye GU FAMILY BOOK akiwa na Bae Suzy, kisha akafanya kazi nzuri kwenye MY GIRLFRIEND IS A GUMIHO, tukamuona tena kwenye KOREAN ODYSSEY na mwaka juzi tuliinua tena mikono baada ya kukutana na Bae Suzy kwenye VAGABOND.

Ukweli ni kwamba ukiachana na kazi hizo za uigizaji LEE ANA ALBUM NANE. Unaweza ukashangaa ila ndio hivyo hapa bongo hakuna msanii wa kipindi hiki mwenye album zote hizo.

Kitu kinachonishangaza sana ni namna ambavyo anaweza kumanage ratiba yake kati ya uigizaji na kuimba maana series alizozifanya ni nyingi.

2. LEE JI EUN - IU

Wakorea humuita "Nation's Little Sister"

Mwanadada huyu aliyeanza kuimba akiwa na miaka 16 ameonekana kama Leading actress kwenye series ya MOON LOVERS pamoja na HOTEL DE LUNA ambayo kuna uzi humu unaonesha kuwa series hiyo ni miongoni mwa series zilizotazamwa huko Korea kwenye Cable TV.

Kwa sasa IU naweza kusema uigizaji ni kama part time tu maana muda mwingi humkuta studio akitengebeza nyimbo kuliko kuigiza.

Ana jumla ya album tano na ya mwisho inaitwa LILAC imetoka March 2021, album hiyo imeenda number 1 kwenye Gaon Charts, pia imepata platinum certification ikiuza nakala takribani 373k hivyo unaweza kuona anakubalika kiasi kwenye suala zima la muziki.

1. BAE SUZY.
Bae Suzy tumemuona kwenye Movie kama ASHFALL akiwa na LEE BYUNG HUN lakini kama umeshaangalia series ya VAGABOND basi Suzy utakuwa unamfaham.

Ukiachana na kuigiza Suzy yupo kwenye kundi la muziki la MISS A na yeye binafsi hana album bado ila ana EP 2 ikiwemo YES? NO? (2017)

Je kuna msanii mwengine unamfahamu? Mtaje hapa
leeminho_1.jpg
e8f08a896f2949b49669f55283d651c3.jpg
B3RRqf.jpg
iu-lilac-photo-edam-entertainment%402000x1270-1.jpg
1194bb2fe104631e2479fce186d8409f.jpg
 
Jinsia zao?? Kwasababu zinachanganya sana hasa huyo wa kwanza pichani
 
Picha ya 4 huyo mdada, ni "so inae" kacheza movie ya Endkess love.
 
Likija swala la mambo ya filamu za Kikorea, na culture ya Kikorea, hauna mpinzani Krikichino

Emdelea kutupatia nondo.
 
Back
Top Bottom