Vitambulisho vya Taifa (NIDA) havitambuliwi na BOT

Vitambulisho vya Taifa (NIDA) havitambuliwi na BOT

Serikali ya CCM katika hali ya ubora wake uliotia fora!!

tanzania-ID.jpg
a247driving-licence.jpg
passport.jpg

Niliona makundimakundi yakijiandikisha mwakajuzi kipindi cha kiangazi kwa ajili ya vitambulisho hivyo, huku kukiwa na mchanganyiko mkubwa wa weusi, wahindi na waarabu kwa makundi. Nikitokea kituo cha Mkapa cha biashara za kimataifa pale barabara ya Mandela, nikasimama kidogo pale Buguruni ndipo nilipobaini zoezi zima linavyoendeshwa na kwa utafiti niliona kasoro nyingi ambazo zinaweza kusababisha kitambulisho kisiwe halali baadaye tokana na mapungufu kadhaa.

Nilishawishiwa nijiandikishe, lakini niliwakatalia kwamba kwa sasa napenda kuangalia kwanza zoezi linavyoendelea na ubora wake, kwa vile ninacho tayari kitambulisho kingine cha driving licence kinachotambuliwa na kutolewa na serikali hali kadhalika passport ambayo ni kitambulisho kikuu kitaifa kinachotambuliwa kimataifa pia sikuona kupaparikia vitambulisho hivyo, na leo nashuhudia madhaifu hayo, bora nilisitisha kuingia kicha kichwa tu.
 
Benki kuu ya Tanzania imetoa muhtasari wa kutokutambua vitambulisho vya taifa kwa kuwa vina mapungufu makubwa kama kutokuwa na date of issue , signature of the ID holder, Place of issue etc etc.... na hivyo kutkufaa kwenye matumizi yeyote ya kibenk ikiwemo kufungua account na kufanya transaction zozote zile za kibenk.
Taarifa zaidi zitawajia..

Huu ni mwendelezo tu wa namna tunavyokurupuka kama taifa kufanya maamuzi ya zima moto kweye mambo ya msingi...... naangalia namna tunavyoandaa vitambulisho vya kuipiga kura, katiba mpya , Bara bara za lami, shule za kata, umeme nk.....

1. Date of issue: ni siku tangazo la waziri au Rais lilipotoka kwenye gazeti la serikali,
2. Signature of the ID holder: vidole, vidole vyetu vili-scan-iwa hivyo BoT wa-link na database ya NIDA,
3. Place of issue: Tanzania na sio Kenya wala Vanuatu

NB: Anayekikataa amechanganyikiwa!
 
12.gif
ID%20cards.jpg
images
142376_max.jpg
images
9k=
9k=
president.png

Tunapojadili hili tuangalie kwa ulinganifu na vitambulisho vya kitaifa vya mataifa mengine barani Afrika na mabara mengine duniani.
  • Nini kinakosekana ambacho katika vitambulisho vya matafa mengine wanavyo?
  • Draft ya vitambulisho haikufanyiwa uhakiki kulinganisha na vitambulisho vinavyotumiwa na mataifa mengine?

Ninavyojua mimi kitambulisho cha kitaifa ni short form ya passport, hivyo mfumo ni ule unaoonekana kwenye passport unatakiwa uwekwe wazi kwenye kitambulisho. Haiwezekani imformation zibaki kwenye data base wakati zinahitajika wakati anapojitambulisha kwa njia yo yote.

CC,
mfianchi

Mkuu tuko pamoja. Angalia hivyo vitambulisho kadhaa vya mataifa tofauti ulivyoviweka hapo uone ni vingapi
havina expiry date. Cha South Africa hakina, cha Rwanda hakina. Sasa sijui ni kwa nini unafanya conclusion kwamba expiry date ni lazima.

Tiba

Pole kwa kutotambua hilo kuhusu mwisho wa matumizi.
Kitambulisho cha kitaifa ni short form ya passport. Tarehe ya kuzaliwa, mahali ulipozaliwa, majina yote matatu kirefu, tarehe ya kutolewa na mahali ilipotolewa, mwisho wa matumizi ingawa haina maana kutotolewa tena ila inamaanisha renewal, TIN number, mahali na address unapoishi, namba ya kadi, bila kusahau picha na sahihi ya mwenye kitambulisho. Kuna viashiria vya siri pia ndani ya kitambuliso kwa ajili ya kuhakiki utapeli.

Kitambulisho cho chote cha kumtambulisha mtu iwe kitaifa au kimataifa mwisho wa matumizi yake ni miaka kumi, kwa vile binadamu anazaliwa, anakua, anazeeka na mwisho hufa, hivyo sura na umbo hubadilikabadilika, hali kadhalika makazi pia, ndio maana lazima vitu hivyo vyote muhimu viwemo na kwamba kila baada ya miaka kumi abadilishe kupata kitambulisho kipya.

Soma bandiko langu katika mada hii #97 ambalo nimeambatanisha taswira za vitambulisho vya kitaifa Tanzania na mataifa mengine, kisha linganisha mapungufu tajwa katika kitambulisho chetu kwa ulinganifu na vitambulisho vya mataifa mengine.

CC;
mfianchi

Ndugu yangu mbona unapinga hata ushahidi uliouweka wewe mwenyewe hapa?

Tiba
 
Marekani hawana vitambulisho vya taifa, inabidi utumie driving license au passport.
 
1. Date of issue: ni siku tangazo la waziri au Rais lilipotoka kwenye gazeti la serikali,
2. Signature of the ID holder: vidole, vidole vyetu vili-scan-iwa hivyo BoT wa-link na database ya NIDA,
3. Place of issue: Tanzania na sio Kenya wala Vanuatu

NB: Anayekikataa amechanganyikiwa!
Ni mjadala huru huu mkuu kinachotakiwa ni kuwaelekeza wale ambao unadhani wamechanganyikiwa maana hata shule na vyuoni watu wote wangekuwa tofauti na uelewa wa wengine wanaitwa hivyo sidhani kama tungekuwa na taifa ambalo leo hii tupo kwenye keyboard
 
benki kuu ya tanzania imetoa muhtasari wa kutokutambua vitambulisho vya taifa kwa kuwa vina mapungufu makubwa kama kutokuwa na date of issue , signature of the id holder, place of issue etc etc.... Na hivyo kutkufaa kwenye matumizi yeyote ya kibenk ikiwemo kufungua account na kufanya transaction zozote zile za kibenk.
Taarifa zaidi zitawajia..

Huu ni mwendelezo tu wa namna tunavyokurupuka kama taifa kufanya maamuzi ya zima moto kweye mambo ya msingi...... Naangalia namna tunavyoandaa vitambulisho vya kuipiga kura, katiba mpya , bara bara za lami, shule za kata, umeme nk.....

ona sasa...kiko wapi? Hii nchi inaendeshwa kitutusa na mitutusa ya ccm.
 
Niliwahi kuuliza hapa ni kwa nini hivyo vitambulisho vya taifa (nafikiri tungekuwa tunaviita vitambulisho vya utaifa sio taifa) kwa nini vina expiry date? Ina maana inafika uraia wa mtanzania utakuwa unakoma? Nimeviona vitambulisho vya jirani zetu hapo Kenya, havina expiry date. Na ukipoteza kitambulisho chako, hakitolewi kipya, you can only get a duplicate of your original ID. Sasa hivi vya kwetu eti vinaisha muda wake.

No wonder muandikishaji wa vitambulisho kwenye eneo langu alikataa kuitambua passport yangu kama utambulisho kamili akataka nilete barua ya balozi. Niliamua kuachana na hivyo vitambulisho, na leo eti taasisi za serikali hazivitambui. Hiki ni kichekesho.

Tiba

Mkuu TIBA vikisha expire ni business ukienda kurenew unalipa au kikipote unalipa kutengenezewa kingine kama driving license vile. Chezea bongo tambaraleee!
 
Mkuu TIBA vikisha expire ni business ukienda kurenew unalipa au kikipote unalipa kutengenezewa kingine kama driving license vile. Chezea bongo tambaraleee!

Kwani hivyo vitambulisho ni kwa watu mjini tu? Mtu aliyeko huko vijijini anapata wapi muda na nauli kwenda mjini ku-renew hicho kitambulisho?

Huu ni utani.

Tiba
 
Kwani hivyo vitambulisho ni kwa watu mjini tu? Mtu aliyeko huko vijijini anapata wapi muda na nauli kwenda mjini ku-renew hicho kitambulisho?

Huu ni utani.

Tiba

Vijijini wataanzishiwa NIDA(RIDA) yao kama vile REA. Only in Bongo :rockon:
 
Niliwahi kuuliza hapa ni kwa nini hivyo vitambulisho vya taifa (nafikiri tungekuwa tunaviita vitambulisho vya utaifa sio taifa) kwa nini vina expiry date? Ina maana inafika uraia wa mtanzania utakuwa unakoma? Nimeviona vitambulisho vya jirani zetu hapo Kenya, havina expiry date. Na ukipoteza kitambulisho chako, hakitolewi kipya, you can only get a duplicate of your original ID. Sasa hivi vya kwetu eti vinaisha muda wake.

No wonder muandikishaji wa vitambulisho kwenye eneo langu alikataa kuitambua passport yangu kama utambulisho kamili akataka nilete barua ya balozi. Niliamua kuachana na hivyo vitambulisho, na leo eti taasisi za serikali hazivitambui. Hiki ni kichekesho.

Tiba

Ili uweze kuupdate taarifa zako, Baada ya miaka hiyo vitu vingi vinakuwa vimebadilika pamoja na sura yako mama.
 
Mwisho matumizi ni tarehe ya kifo cha mhusika.

Hapana huwa vina kwisha baada ya miaka 10 kama ilivyo hati ya kusafiria. Labda waseme hivi ni miaka 20! Usijeshangaa watu waliopewa mwanzo vikaisha muda wake wengine bado hawajapewa.
 
yawezekana tatizo ni serikali kwa ujumla, wametengeneza kitu lakini hawakuweka mazingira ya kukifanya kifanye kazi wameawaachia nida au wizara husika peke yao.

ilitakiwa mpango mzima wa vitambulisho vya taifa uwe kama ilivyofanya mashine za TRA (EFD) au kuingia katika digital kwa taasisi husika kutoa tamko la kufikia tarehe fulani lazima taasisi zote zinazotumia vitambulisho ziwe zimehamia kwenye vitambulisho vya taifa na hii ni pamoja na kuwa na mashine hizo husika.

lakini si kuwaacha wapuuzi wachache hawa wanadiscourage project hii ya taifa eti kwa kuvikataa na kuonyesha leseni za udereva na kitambulisho cha kupiga kura ni bora zaidi.

kwanza nadhani ingewekwa tarehe maalumu kwa mtu kupata huduma yoyote katika taasisi yoyote lazima kitumike kitambulisho cha taifa, usajili wa mali zote ufanyike kutumia kitambulisho cha taifa.

serikali hapa nadhani imelala

Signature zimo ndani ya chip, hata mahali, tarehe ya kuzaliwa, kutolewa na kuhishwa zipo, lakini benki zinatakiwa kuwa na kifaa cha kusomea taarifa hizo. Na kimsingi asasi nyingine zinatakiwa kulipia taarifa hizi ili NIDA iwezekujitegemea kwa kukusanya retention/maduhuli.
 
jibu lako ni la kizamani kwa nini isiwe kila kitu kinachoingizwa kwenye data base kinapobadilika unaenda nida ku update taarifa badala ya kusema eti mpaka kifikie ukomo alafu ndio kubadili taarifa.

mimi nadhani kama mtu alijiandikisha amemaliza form six siku akipata degree anakwenda nida anapeleka cheti wanaongeza katika taarifa zake. kukaa miaka yote hiyo mpaka kifikie ukomo nadhani kitambulisho hiki hakitakuwa na maana kama wengi wanavyodhani ni sawa na taasisi nyingi wamefungua website lakini hawaweki taarifa zinazoendana na wakati hivyo kutosaidia.

vitambulisho hivi vingefaa kudhibiti kodi ya mapatao lakini kama hakuna taarifa pale mtu anapohama kutoka kwa mwajiri mmoja kwenda kwa mwingine wakwepa kodi watambuliwaje?

ingefaa kama mtu amefanya kosa na amekimbia polisi wanaweka taarifa zake kwenye mtandao hivyo hawezi kupata huduma yoyote bila kutumia kitambulisho na popote atakapotoa kitambulisho anatambulika kuwa anatafutwa na polisi sasa nyie kwa utaratibu wenu wa ku update taarifa za sasa mpaka 2024 hamuoni hamjui matumizi ya vitambulisho hivyo bali mnafikiria kuvitumia tu kama visitors ID cards.

kama mnatengeneza project kama hiyo sio kukaa mkatengeneza chips zenu huku taasisi nyingine wakiwa hawajui na mnataka eti waje wawaulize nyinyi, mlitakiwa kuwaandaa hawa wadau kwenda kuwapa mawazo yenu na nyinyi muwasikilize na kuona kama mawazo yenu yanaendana na kile wanachokitegemea.

yaani unategemea mtu kaja na kitambulisho na vitu unavyotaka kuviona huvioni unaenda kumuuliza aliyetoa kitambulisho au ni kumwambia mwenye kitambulisho ninavyovitaka hapa havipo lete kitambulisho kingine.

kama watu wanatembea na data wakati hawajui ni umbumbu wenu nida, kama taasisi haziwezi kusoma data zenu ni umbumbu wenu nida kwa maana wote mwenye kitambulisho na anayetakiwa kukisoma wanahitaji kuelimishwa na ninyi mnaotengeneza sasa je mmefanya hivyo au mnatengeneza mnavyojua na kukaa kimya?

Ili uweze kuupdate taarifa zako, Baada ya miaka hiyo vitu vingi vinakuwa vimebadilika pamoja na sura yako mama.
 
  • Thanks
Reactions: 911
[h=1]NIDA HAYA MAKOSA MPAKA VITAMBULISHO VYA TAIFA VINATOKA HAMKUYAONA?[/h]Kuna wakati unapoandika vitu vya msingi kama hivi hasa unapoongelea swala linalogusa tabaka tawala unaonekana kama umetumwa na chama pinzani au una malengo fulani ambayo si mazuri ya kuikosoa serikali iliyoko madarakani. Kwa kuwa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ibara ya 18, ibara ndogo ya (1) inanipa uhuru na nguvu ya kutoa mawazo kama mwananchi bila ya kuathiri sheria za nchi. Sheria inasema hivi " Bila ya kuathili sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta na kupokea na kutoa habari na dhana zozote na chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.

Napenda kuangazia jicho langu katika makosa yaliyojitokeza katika vitambulisho vya Taifa, vitambulisho hivi vimechua takribani mwaka mmoja mpaka sasa hivi kuanza kutolewa katika jiji la Dar Es salaam kwa wananchi wa kawaida, usajili wa vitambulisho hivi ulianzia kwanza kwa watumishi wa serikali waliopo jijini Dar Es Salaam kabla ya mikoa mingine. Zoezi la usajili kwa sasa lipo mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara. Serikali inatakiwa kupongezwa kwa hatua waliofikia japo imechelewa kuvitoa ukilinganisha nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Kwa jinsi mchakato wake ulivyoendesha ulikuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi, wananchi walidamka mapema sana kuwahi maeneo ya kujiandikishia walichokikuta uko ni siri yao, foleni zilikuwa ndefu kuliko hata zile za benki tulizozizoea, wengine waliambulia matusi kutoka kwa wafanyakazi wa NIDA mpaka hivi juzi wakati wa kuvipokea mambo yaliendelea kuwa vile vile, badala ya wafanyakazi wa NIDA kutumia lugha ya ukarimu na kutoa maelekezo kwa wananchi lakini eneo la kuvigawa ikawa ni uwanja wa matusi, aibu gani hii tena unakuta kijana mdogo na mzee ndio wanarushiana maneno mazito mazito na matusi juu.

Hapa ndipo hasa napenda kupaangalia kwa undani zaidi,napenda kunukuu neno kutoka kwa mkurugenzi Mkuu Bwana Dickson Maimu kutoka katika tovuti ya mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA. "Mfumo huu unalenga kujibu maswali makuu manne ambayo ni nani ni nani, yuko wapi, anafanya nini na anamiliki nini? kuwapo kwa mfumo na teknolojia ya smart card ambayo inatumika kutengenezea Vitambulisho vya Taifa ni chachu ya maendeleo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kutaimarisha ulinzi, amani na usalama wa nchi Tanzania".
Baada ya kutoa vitambulisho hivi vya Taifa kuna taarifa muhimu na za msingi kabisa hazipo na zinaonekana kutojibu maswali makuu manne kama yalivyosema na Mkurugenzi mkuu.
katika kitambulisho hiki, napenda kusema kwamba nimebaini makosa makuu 4 yaliyofanywa kwa uzembe na mamlaka husika NIDA, imefikia hatua sasa unaona kabisa kile kitambulisho cha mpiga kura bado kinaonekana kuwa bora kwa kuwa na taarifa sitahiki na muhimu zote zimewekwa katika kitambulisho hicho. Kwa uzembe huu uliotokea kwa vitu vidogo vidogo kama hivi kusahaulika msishangae kabisa kuona watu wasio watanzania kuwa na vitambulisho vya Taifa.

KOSA LA KWANZA: kitambulisho hakina tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa wa mwenye kitambulisho, kwa kawaida kitambulisho chochote cha taifa, passport, leseni ya udereva, kitambulisho cha mpiga kura kinapaswa kuonyesha tarehe ya kuzaliwa na mwaka waziwazi, lakini kitambulisho hiki ambacho serikali imetoa mabillion ya pesa hata hiki kimesahaulika,na kama sio kusahaulika labda hizi namba nyingi zilizopo yawezekana zikawa zimefichwa zisijulikane kwa haraka ,sasa picha tu na jina ndio litaridhisha? Kwa nini passport, leseni ya udereva na kitambulisho cha mpiga kura wameweka? Kitambulisho hiki ndicho mama kinatumika sehemu nyingi katika upataji wa huduma, mfano shule, afya, mawasiliano, huduma za kifedha, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), BRELA, mifuko ya hifadhi ya jamii kama NSSF,PPF,PSPF, mahakama, polisi, nk kuna wakati wanataka kujua umri wa mtumiaji wa kitambulisho hicho. NIDA kuna lolote la kujitetea hapa, obvious watasema iko kwenye system sasa sijui ili tuweze kuona umri hizo mashine zitakuwa kila ofsi ili kujua.
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Tarehe na mwaka wa kuzaliwa hiki ni cha Uganda[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

KOSA LA PILI: Kitambulisho hakionyeshi makazi rasmi ya mwenye kitambulisho,(Permanent residence) hata ili hamkuliona kwenye vitambulisho vya mwanzo kabisa, kitambulisho hiki kilipasa kuonyesha mtumiaji wake anakaa Mkoa gani, wilaya ipi, kata ipi, mpaka mtaa na nyumba namba, hata kama amepanga siku akiama eneo ilo lakini taarifa zake zitakuwepo kwenye nyumba aliyokuwa akiishi itakuwa rahisi kumpata. Swala la kuonyesha makazi katika kitambulisho ni muhimu sana mfano wakati wa ajali,kupata huduma za kifedha kama mikopo lazima taasisi za kifedha ijue mteja wao anaishi wapi lakini pia pindi kitambulisho kinapo potea inakuwa ni rahisi kukirudisha eneo au mkoa husika kwa kuwa watu wanasafiri kila siku kutoka sehemu moja kwenda nyingine, kuna swala la majanga, Serikali hupata changamoto kubwa ya kuwalipa fidia au kuwasaidia pindi wananchi wake wanapopatwa na majanga mbalimbali, mfano mabomu ya Mbagala, Gongo la Mboto na mafuriko ya Kilosa, mwisho wa siku watu wanaotakiwa kupata msaada hawaupati lakini kitambulisho hiki kiwekwa taarifa zake za makazi pale juu inakuwa rahisi kuhudumiwa, vipi kuhusu mtu anapojihusisha na vitendo vya kiuharifu polisi inawasaidia kufanya upelelezi kirahisi kuanzia sehemu anapoishi na kujua mwenendo wake eneo la makazi sio tena kwenda NIDA kitambulisho chake kinamsaidia afsa wa jeshi la polisi kufanya upelelezi.
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Sample ya Marekani wameweka mpaka group la damu, shughuli ufanyazo,mahali unapoishi, rangi ya nywele[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

KOSA LA TATU: Kitambulisho hakina sahihi ya mtumiaji, basi hata kama mwananchi haujui kusoma na kuandika lipo dole gumba, Bank wameanza kuvikataa kwa kuwa hakuna sahihi ya mwenye kitambulisho,kwa taratibu za kibenki inapaswa kuoanisha sahihi iliyopo kwenye kitambulisho chako kama passport, leseni ya udereva na kile kinachotumika benki, sasa kutokana na mapungufu haya imefikia hatua hata benki yenyewe kuona hakifai.
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]sehemu ya sahihi na dole gumba imewekwa, hiki ni cha KENYA.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

KOSA LA NNE: Kitambulisho kina mwisho wa matumizi yake (EXPIRE DATE)Hapa napo pameniachana na maswali mengi bado sijapata jibu kamili labda mpaka litakapotolewa ufafanuzi tena ukaniingia, leseni za udereva ni sawa kabisa kwani kuna kuwa na utaratibu wa kubadilisha madaraja sasa tukirudi kwenye hoja ya msingi kulikuwa kuna maana gani ya kuweka expire date? Ina maana ndio siku mwenye kitambulisho anakufa!! jibu hakuna Mungu ndie anayejua siri hii, au ndio mwisho wa dunia!!!.........bado najiuliza basi tuseme ndio utakuwa ukomo wa kuwa wananchi wa Tanzania labda nchi itakuwa chini ya mwekezaji na kuamua kubadilisha jina nacheka kimoyo moyo, haya yote ni mawazo tu niliyonayo mimi Nyanja juu ya kuweka expire date huku taarifa za msingi mnaziacha, lakini mwishoni nimepata jibu si watarudishwa tena ikifika mwaka huo 2023 kupata tena tenda ya kutengeneza vipya ili watengeneze tena madudu yao na serikali iingine gharama mpya kwa maana kwamba vitakuwa vimefikia ukomo wa matumizi yake, havitakuwa halali tena. Japo kuna baadhi ya nchi nyingine wanatumia na ukiona kwenye specimen wameonyesha lakini swala linabaki kwa nchi yangu na tayari makosa yanaonekana hapo.

Nahitimisha kwa kusema kwamba,Mkurugenzi mkuu wa NIDA, Dickson Maimu pamoja na watendaji wenzake wa mamlaka hii angalieni makosa hayo kwa undani na mtafute suruhisho mapema kabla ya kuendelea kutengeneza vitambulisho vingine vyenye makosa, kwani kwa kuwa ni mkoa mmoja tu ambao mmeshatoa vitambulisho hivi na sio wote wameshavipata na bado zaidi ya mikoa 20 bado havijatolewa tafadhari chukueni hatua ya kurekebisha mapungufu hayo mapema.

Imeandikwa na Nyanja Kelvin Poti.
Mawasiliano: 0715 019393
Mail:kelvinnyanja@gmail.com
Twitter:nyanja255
instagram: nyanja255
Think positive to help your national.
 
NIDA HAYA MAKOSA MPAKA VITAMBULISHO VYA TAIFA VINATOKA HAMKUYAONA?

Kuna wakati unapoandika vitu vya msingi kama hivi hasa unapoongelea swala linalogusa tabaka tawala unaonekana kama umetumwa na chama pinzani au una malengo fulani ambayo si mazuri ya kuikosoa serikali iliyoko madarakani. Kwa kuwa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ibara ya 18, ibara ndogo ya (1) inanipa uhuru na nguvu ya kutoa mawazo kama mwananchi bila ya kuathiri sheria za nchi. Sheria inasema hivi " Bila ya kuathili sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta na kupokea na kutoa habari na dhana zozote na chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.

Napenda kuangazia jicho langu katika makosa yaliyojitokeza katika vitambulisho vya Taifa, vitambulisho hivi vimechua takribani mwaka mmoja mpaka sasa hivi kuanza kutolewa katika jiji la Dar Es salaam kwa wananchi wa kawaida, usajili wa vitambulisho hivi ulianzia kwanza kwa watumishi wa serikali waliopo jijini Dar Es Salaam kabla ya mikoa mingine. Zoezi la usajili kwa sasa lipo mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara. Serikali inatakiwa kupongezwa kwa hatua waliofikia japo imechelewa kuvitoa ukilinganisha nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Kwa jinsi mchakato wake ulivyoendesha ulikuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi, wananchi walidamka mapema sana kuwahi maeneo ya kujiandikishia walichokikuta uko ni siri yao, foleni zilikuwa ndefu kuliko hata zile za benki tulizozizoea, wengine waliambulia matusi kutoka kwa wafanyakazi wa NIDA mpaka hivi juzi wakati wa kuvipokea mambo yaliendelea kuwa vile vile, badala ya wafanyakazi wa NIDA kutumia lugha ya ukarimu na kutoa maelekezo kwa wananchi lakini eneo la kuvigawa ikawa ni uwanja wa matusi, aibu gani hii tena unakuta kijana mdogo na mzee ndio wanarushiana maneno mazito mazito na matusi juu.

Hapa ndipo hasa napenda kupaangalia kwa undani zaidi,napenda kunukuu neno kutoka kwa mkurugenzi Mkuu Bwana Dickson Maimu kutoka katika tovuti ya mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA. "Mfumo huu unalenga kujibu maswali makuu manne ambayo ni nani ni nani, yuko wapi, anafanya nini na anamiliki nini? kuwapo kwa mfumo na teknolojia ya smart card ambayo inatumika kutengenezea Vitambulisho vya Taifa ni chachu ya maendeleo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kutaimarisha ulinzi, amani na usalama wa nchi Tanzania".
Baada ya kutoa vitambulisho hivi vya Taifa kuna taarifa muhimu na za msingi kabisa hazipo na zinaonekana kutojibu maswali makuu manne kama yalivyosema na Mkurugenzi mkuu.
katika kitambulisho hiki, napenda kusema kwamba nimebaini makosa makuu 4 yaliyofanywa kwa uzembe na mamlaka husika NIDA, imefikia hatua sasa unaona kabisa kile kitambulisho cha mpiga kura bado kinaonekana kuwa bora kwa kuwa na taarifa sitahiki na muhimu zote zimewekwa katika kitambulisho hicho. Kwa uzembe huu uliotokea kwa vitu vidogo vidogo kama hivi kusahaulika msishangae kabisa kuona watu wasio watanzania kuwa na vitambulisho vya Taifa.

KOSA LA KWANZA: kitambulisho hakina tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa wa mwenye kitambulisho, kwa kawaida kitambulisho chochote cha taifa, passport, leseni ya udereva, kitambulisho cha mpiga kura kinapaswa kuonyesha tarehe ya kuzaliwa na mwaka waziwazi, lakini kitambulisho hiki ambacho serikali imetoa mabillion ya pesa hata hiki kimesahaulika,na kama sio kusahaulika labda hizi namba nyingi zilizopo yawezekana zikawa zimefichwa zisijulikane kwa haraka ,sasa picha tu na jina ndio litaridhisha? Kwa nini passport, leseni ya udereva na kitambulisho cha mpiga kura wameweka? Kitambulisho hiki ndicho mama kinatumika sehemu nyingi katika upataji wa huduma, mfano shule, afya, mawasiliano, huduma za kifedha, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), BRELA, mifuko ya hifadhi ya jamii kama NSSF,PPF,PSPF, mahakama, polisi, nk kuna wakati wanataka kujua umri wa mtumiaji wa kitambulisho hicho. NIDA kuna lolote la kujitetea hapa, obvious watasema iko kwenye system sasa sijui ili tuweze kuona umri hizo mashine zitakuwa kila ofsi ili kujua.
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Tarehe na mwaka wa kuzaliwa hiki ni cha Uganda[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

KOSA LA PILI: Kitambulisho hakionyeshi makazi rasmi ya mwenye kitambulisho,(Permanent residence) hata ili hamkuliona kwenye vitambulisho vya mwanzo kabisa, kitambulisho hiki kilipasa kuonyesha mtumiaji wake anakaa Mkoa gani, wilaya ipi, kata ipi, mpaka mtaa na nyumba namba, hata kama amepanga siku akiama eneo ilo lakini taarifa zake zitakuwepo kwenye nyumba aliyokuwa akiishi itakuwa rahisi kumpata. Swala la kuonyesha makazi katika kitambulisho ni muhimu sana mfano wakati wa ajali,kupata huduma za kifedha kama mikopo lazima taasisi za kifedha ijue mteja wao anaishi wapi lakini pia pindi kitambulisho kinapo potea inakuwa ni rahisi kukirudisha eneo au mkoa husika kwa kuwa watu wanasafiri kila siku kutoka sehemu moja kwenda nyingine, kuna swala la majanga, Serikali hupata changamoto kubwa ya kuwalipa fidia au kuwasaidia pindi wananchi wake wanapopatwa na majanga mbalimbali, mfano mabomu ya Mbagala, Gongo la Mboto na mafuriko ya Kilosa, mwisho wa siku watu wanaotakiwa kupata msaada hawaupati lakini kitambulisho hiki kiwekwa taarifa zake za makazi pale juu inakuwa rahisi kuhudumiwa, vipi kuhusu mtu anapojihusisha na vitendo vya kiuharifu polisi inawasaidia kufanya upelelezi kirahisi kuanzia sehemu anapoishi na kujua mwenendo wake eneo la makazi sio tena kwenda NIDA kitambulisho chake kinamsaidia afsa wa jeshi la polisi kufanya upelelezi.
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Sample ya Marekani wameweka mpaka group la damu, shughuli ufanyazo,mahali unapoishi, rangi ya nywele[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

KOSA LA TATU: Kitambulisho hakina sahihi ya mtumiaji, basi hata kama mwananchi haujui kusoma na kuandika lipo dole gumba, Bank wameanza kuvikataa kwa kuwa hakuna sahihi ya mwenye kitambulisho,kwa taratibu za kibenki inapaswa kuoanisha sahihi iliyopo kwenye kitambulisho chako kama passport, leseni ya udereva na kile kinachotumika benki, sasa kutokana na mapungufu haya imefikia hatua hata benki yenyewe kuona hakifai.
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]sehemu ya sahihi na dole gumba imewekwa, hiki ni cha KENYA.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

KOSA LA NNE: Kitambulisho kina mwisho wa matumizi yake (EXPIRE DATE)Hapa napo pameniachana na maswali mengi bado sijapata jibu kamili labda mpaka litakapotolewa ufafanuzi tena ukaniingia, leseni za udereva ni sawa kabisa kwani kuna kuwa na utaratibu wa kubadilisha madaraja sasa tukirudi kwenye hoja ya msingi kulikuwa kuna maana gani ya kuweka expire date? Ina maana ndio siku mwenye kitambulisho anakufa!! jibu hakuna Mungu ndie anayejua siri hii, au ndio mwisho wa dunia!!!.........bado najiuliza basi tuseme ndio utakuwa ukomo wa kuwa wananchi wa Tanzania labda nchi itakuwa chini ya mwekezaji na kuamua kubadilisha jina nacheka kimoyo moyo, haya yote ni mawazo tu niliyonayo mimi Nyanja juu ya kuweka expire date huku taarifa za msingi mnaziacha, lakini mwishoni nimepata jibu si watarudishwa tena ikifika mwaka huo 2023 kupata tena tenda ya kutengeneza vipya ili watengeneze tena madudu yao na serikali iingine gharama mpya kwa maana kwamba vitakuwa vimefikia ukomo wa matumizi yake, havitakuwa halali tena. Japo kuna baadhi ya nchi nyingine wanatumia na ukiona kwenye specimen wameonyesha lakini swala linabaki kwa nchi yangu na tayari makosa yanaonekana hapo.

Nahitimisha kwa kusema kwamba,Mkurugenzi mkuu wa NIDA, Dickson Maimu pamoja na watendaji wenzake wa mamlaka hii angalieni makosa hayo kwa undani na mtafute suruhisho mapema kabla ya kuendelea kutengeneza vitambulisho vingine vyenye makosa, kwani kwa kuwa ni mkoa mmoja tu ambao mmeshatoa vitambulisho hivi na sio wote wameshavipata na bado zaidi ya mikoa 20 bado havijatolewa tafadhari chukueni hatua ya kurekebisha mapungufu hayo mapema.

Imeandikwa na Nyanja Kelvin Poti.
Mawasiliano: 0715 019393
Mail:kelvinnyanja@gmail.com
Twitter:nyanja255
instagram: nyanja255
Think positive to help your national.

Acha kudanganya watu kwa maneno marefuuu. Angalia hicho kitambulisho cha JK Tarehehe ya kuzaliwa ipo : 10 / 07 / 1950 imeandikwa hivi 19501007 . Ndio maana nasema fanyieni uchunguzi mambo badala ya kulalama. Kayoka
 
Last edited by a moderator:
Inatakiwa tarehe iliyotolewa na lini hicho kitambulisho hakita tumika.
Kama vingekuwa vyatolewa siku yakuzaliwa ndio ungesema hayo uliyosema.

Basi kutakuwa na vitambulisho vya taita vya aina mbili, mimi cha kwangu kina tarehe ya mwisho wa matumizi. hakina tarehe ya kutolewa ila majina matatu yote yapo. Hakina saini!
 
Mkuu tuko pamoja. Angalia hivyo vitambulisho kadhaa vya mataifa tofauti ulivyoviweka hapo uone ni vingapi
havina expiry date. Cha South Africa hakina, cha Rwanda hakina. Sasa sijui ni kwa nini unafanya conclusion kwamba expiry date ni lazima.

Tiba

Ndugu yangu mbona unapinga hata ushahidi uliouweka wewe mwenyewe hapa?

Tiba

Nimeweka vitambulisho hivyo kuonyesha kasoro mbalimbali ambazo zinasababisha kutotambulika, ndio maana unaona vitambulisho vya nchi za kiafrika vina makosa kadhaa mengi tofauti na mabara mengine, hii ni kutokana na nchi za kiafrika ndio zinaanza kutumia mfumo huo, na tatizo hawakuwa makini kuangalia vitambulisho vya nchi nyingine zenye uzoefu wa muda mrefu katika kutumia vitambulisho vya kitaifa. Lengo ungejifunza badala ya kuendelea kubisha kitu ambacho kipo wazi. Angalia hoja ya msingi kitambulisho kina muda maalumu si kwa maisha kama ilivyo group ya damu yako. Unabadilikabadilika tokana na kuzaliwa, kukua, kuzeeka hadi kuwa kikongwe huwezi kuwa na picha ile ile ya teenage. Makazi hubadilika, occupation hubadilika, nk. Wengine hufa bila kupeleka taarifa kwenye mamlaka husika za msajili wa vizazi na vifo, hivyo mpango huo ni kuhakiki na kuthibiti idadi ya wenye vitambulisho.

Tukubali makosa yaliyomo kwenye vitambuliso hivyo na yasahihishwe ili wananchi wapate vitambulisho vilivyokamilika si mradi kuwa na kadi ambayo haikupi utambulisho unaokubalika. Hata cadi za bank zitumikazo ATM zina muda maalumu, Driving lisence ina muda maalum, Passport ina muda maalum, kitambulisho cha mpiga kura kina muda maalum, nk. Hoja yako ni nini sasa kujenga utetezi wako mdau?
 
Back
Top Bottom