Vitambulisho vya Taifa (NIDA) havitambuliwi na BOT

Vitambulisho vya Taifa (NIDA) havitambuliwi na BOT

LorenzoA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Posts
5,889
Reaction score
17,753
Benki kuu ya Tanzania imetoa muhtasari wa kutokutambua vitambulisho vya taifa kwa kuwa vina mapungufu makubwa kama kutokuwa na date of issue , signature of the ID holder, Place of issue etc etc.... na hivyo kutkufaa kwenye matumizi yeyote ya kibenk ikiwemo kufungua account na kufanya transaction zozote zile za kibenk.
Taarifa zaidi zitawajia..

Huu ni mwendelezo tu wa namna tunavyokurupuka kama taifa kufanya maamuzi ya zima moto kweye mambo ya msingi...... naangalia namna tunavyoandaa vitambulisho vya kuipiga kura, katiba mpya , Bara bara za lami, shule za kata, umeme nk.....
 
Kisichokuwa na sifa hakiwezi kupewa sifa. Aje msemaji wa serikali atueleze vizuri
 
Hivi kumbe vipo?au watu walishapiga deal imetoka hiyo
 
kitambulisho cha taifa...

ipo tarehe ya kuzaliwa ambayo inaonyesha mwanzo wa utaifa wa mwenye kitambulisho.
 
kitambulisho cha taifa...

ipo tarehe ya kuzaliwa ambayo inaonyesha mwanzo wa utaifa wa mwenye kitambulisho.

Inatakiwa tarehe iliyotolewa na lini hicho kitambulisho hakita tumika.
Kama vingekuwa vyatolewa siku yakuzaliwa ndio ungesema hayo uliyosema.
 
kama taasisi au mtu hakiwa anapingamizi kwa hivi vitambulisho aende mahakamani...

kuzuia mchakato wote.
 
kama tunataka maendeleo na kuwaondoa wababaishaji katika utendaji ambao mambo ya kitaifa wanayachukulia kama ni sehemu yao ya kufanya dili ni lazima mkurugenzi mkuu wa NIDA awajibike kwa hilo.

tunatumia gharama kubwa kutengeneza matoi ya vitambulisho?

ila kama taarifa hizi ni za kweli.

Benki kuu ya Tanzania imetoa muhtasari wa kutokutambua vitambulisho vya taifa kwa kuwa vina mapungufu makubwa kama kutokuwa na date of issue nk.... na hivyo kutkufaa kwenye matumizi yeyote ya kibenk ikiwemo kufungua account.....
Taarifa zaidi zitawajia..

Huu ni mwendelezo tu wa namna tunavyokurupuka kama taifa kufanya maamuzi ya zima moto kweye mambo ya msingi...... naangalia namna tunavyoandaa vitambulisho vya kuipiga kura, katiba mpya , Bara bara za lami, shule za kata, umeme nk.....
 
Mkuu sio BOT tu hata benki ya BOA haivitambui ,nilipata mshtuko nilipoenda kuchukua hela niliyotumiwa kwa Western Union,nikaacha passport na kuchukua hicho kitambulisho naam nikaambiwa wao kama benki hawakitambui kwanza kwa kuwa hakina saini ndivyo aliniambia karani ,sikuamini nikaenda kwa meneja wa tawi nae akaniambia hivyo hivyo akadai au niende napassport au kitambulisho cha kupigia kura au cha NSSF au leseni ya udereva.Pamoja na yote ikabidi niende Benki ya Posta ndio nikapata hela bila longolongo.
Kifupi pamoja na hayo mapungufu mi nadhani kwa kutotambua hicho kitambulisho cha taifa ni makosa kwani saini pekee yake kwenye kitambulisho sio muhimu kwani saini ipo kwenye data base na saini peke yake ya kwenye kitambulisho haifanyi ndio kitambulisho kiwe na sifa,mimi nadhani hizi benki zetu au taasisi zingine zingejiunga kwenye mtandao wa NIDA ili mtu akitoa kitambulisho aweze kutambuliwa,jamani lazima tuwe na plan B kunapokuwa na mapungufu,tusiwe kama Tanesco ambao mitambao yao ya LUKU ikibuma basi umeme nao unabuma,tufikirie nje ya tulipo.
 
Hakuna hata umuhimu wa kuvifuatilia manake unapoteza muda na takataka usikuja itumia milele
 
Nililiona hili mapema sana. Jinsi walivyokuwa wanadai viambatanishi kibao, nikasema hapa mambo lazima yaharibike tu. na kweli.
 
Kwa hapa tulipo, kitambulisho hiki kitaonekana kama hakijakidhi kama hakitakuwa na jina kamili,tarehe ya kuzaliwa, mahali ulipozaliwa na Picha ya mmiliki( Yaani mwenye majina yake kwenye kitambulisho). Kama vitu hivyo vinne vyote vipo basi ni valid ID. Sahihi sidhani kama inaweza kukibatilisha kitambulisho.
Binafsi sikumbuki kama kitambulisho hiki kina mahali pa kuzaliwa.
 
Sasa kitambulisho eti cha Uraia kipo kama visitor I.d ya kuingia ofisi za wachina. Hahaha
 
Wa TZ kwa kulalamika kwa vitu wasivyovijua ni hodari. Uliza ujibiwe na NIDA.
 
Wa TZ kwa kulalamika kwa vitu wasivyovijua ni hodari. Uliza ujibiwe na NIDA.

Waulize NIDA ili iweje? unategemea hao NIDA wako watasema ni kweli havifai? Kuna watu wametoa ushuhuda hapo juu jinsi walivyokwamishwa na hivi vitambulisho vya NIDA. Mimi mwenyewe nilijua baada ya hivi vitambulisho kutoka basi mambo ya kuwa na 'mzigo' wa vitambulisho kwenye pochi yatakuwa yameisha kumbe ndiyo yamaeongezeka,nilishawahi pia kukataliwa bank kutumia hicho kitambulisho cha hao NIDA wako na sikuwa mbishi kwa sababu ni kweli havina sahihi. Taarifa zilizopo ni 1.Namba ya kitambulisho 2. Jina la mwenye kitambulisho (majina matatu) 2. Jinsi (gender) 3. Mwisho wa matumizi (expiry date)
 
Back
Top Bottom