Tiba
JF-Expert Member
- Jul 15, 2008
- 4,607
- 3,191
Nimeweka vitambulisho hivyo kuonyesha kasoro mbalimbali ambazo zinasababisha kutotambulika, ndio maana unaona vitambulisho vya nchi za kiafrika vina makosa kadhaa mengi tofauti na mabara mengine, hii ni kutokana na nchi za kiafrika ndio zinaanza kutumia mfumo huo, na tatizo hawakuwa makini kuangalia vitambulisho vya nchi nyingine zenye uzoefu wa muda mrefu katika kutumia vitambulisho vya kitaifa. Lengo ungejifunza badala ya kuendelea kubisha kitu ambacho kipo wazi. Angalia hoja ya msingi kitambulisho kina muda maalumu si kwa maisha kama ilivyo group ya damu yako. Unabadilikabadilika tokana na kuzaliwa, kukua, kuzeeka hadi kuwa kikongwe huwezi kuwa na picha ile ile ya teenage. Makazi hubadilika, occupation hubadilika, nk. Wengine hufa bila kupeleka taarifa kwenye mamlaka husika za msajili wa vizazi na vifo, hivyo mpango huo ni kuhakiki na kuthibiti idadi ya wenye vitambulisho.
Tukubali makosa yaliyomo kwenye vitambuliso hivyo na yasahihishwe ili wananchi wapate vitambulisho vilivyokamilika si mradi kuwa na kadi ambayo haikupi utambulisho unaokubalika. Hata cadi za bank zitumikazo ATM zina muda maalumu, Driving lisence ina muda maalum, Passport ina muda maalum, kitambulisho cha mpiga kura kina muda maalum, nk. Hoja yako ni nini sasa kujenga utetezi wako mdau?
Kama haujaielewa hoja yangu mpaka sasa hivi, basi hautakaa unielewe. Amini unachokiamini na mimi nitaendelea kuamini ninachokiamini. Nimetoa mifano ya nchi ambazo vitambulisho vya uraia havina expiry date na nikaeleza ni kwa nini kitambulisho cha utaifa hakipashwi kuwa na muda wa kwisha kutumika, bado hunielewi. Shikiria unachokiamini.
Tiba