Vitambulisho vya machinga vimezikwa na hayati Rais Dkt John Magufuli huko Chato?

Pesa za machinga aulizwe Doto James. Wamachinga waondolewe wote mabarabarani wajipange katika biashara rasmi kama watanzania wengine. Uchafu umejaa mno mpaka unajiuliza hivi Dar na Arusha wanastahili kuwa majiji?Miaka 60 baada ya uhuru bado ni sifa mtu kuitwa "mnyonge"?

Au ilikuwa lugha ya kutengeneza kichaka cha upigaji na kuunda kundi au tabaka kwa maslahi ya kisiasa kwa mwendazake? Tunajenga lami na mitaro kwa ajili ya kuwekea vibanda vya nyanya na mitumba?

Waondoke wote waende wanakojua na kila mtu afuate sheria. Mkiwaacha kesho mtakuwa na kundi la bodaboda, daladala, panya, daladala, nk nk na ni hatari kwetu sote kama nchi.
 
Mrisho Gambo aache siasa nyepesi ,jiji la Arusha zima limegeuka gulio kila mahali na hakika kila barabara zimezibwa na hawa chingas
Gambo aelezwe uchaguzi ujao mbeleko ya Magu haitakuwepo
 
Mji umekuwa mchafu ajabu, now wameanza kujenga kuelekea polisi kutokea mnarani.

Kule jirani na kibo palace hotel naona walikuwa wanajenga kwenda mbele ila naona wenye hotel wamewabomolea, yaani ni full uchafu hizi kitu.
Kama pale soko la madini nje ni uchafu mtupu. Hivi Gambo anafahamu gharama ya kuijenga km 1 ya lami?? Anatetea watu wenye mitaji mikubwa kwamba ni wamachinga.
 
Kama pale soko la madini nje ni uchafu mtupu. Hivi Gambo anafahamu gharama ya kuijenga km 1 ya lami?? Anatetea watu wenye mitaji mikubwa kwamba ni wamachinga.
Anafahamu sana ila ndiyo ukishakuwa upande huo lazima kichwa kibaki 👼na akili zikutoke kidogo.
 
TRA na maofisa biashara wa Halmashauri wapitie upya aina za biashara zisizo za kimachinga alafu watoze kodi /leseni kama ambavyo wafanyavyo kwenye viduka vidogo mijini.

Tarura katika miji mikubwa wanayo mamlaka ya kukataza kufanya biashara kwenye kingo za barabara /waweke tozo kama wafanyavyo kwenye parking za magari. mfano wanaweza kutoa leseni za parking /uwazi wa eneo kwa wenye maduka /ofisi ili kuzuia machinga kupanga/kuweka huduma /bidhaa zao.

Maofisa afya/TFDA wanayo mamlaka ya kuzuia biashara holela za vyakula katika maeneo yasiyo rasmi, ubora na viwango.

Wakurugenzi wa halmashauri katika miji mikubwa kwa kushirikiana na watendaji walio chini yao hasa mipango miji wana wajibu wa kutenga maeneo au kubuni njia mbadala za Machinga kufanya shughuli zao. mfano maduka /vibanda vinavyo tembea au kuteua mtaa mmoja kwa ajili ya machinga.

Wakuu wa mikoa /wilaya wana wajibu wa kuratibu maeneo na aina ya biashara ili kuondoa mwingiliano wa bidhaa na huduma kurundikana sehemu moja.

Jeshi la zimamoto linao wajibu wa kutoa elimu juu ya majanga ya moto ambayo yanweza sababishwa na ujenzi holela wa vibanda vya machinga au kuzagaa kwa machinga karibu na maeneo yenye vituo vya mafuta mijini.

Tume ya Ushindani na wakala wa vipimo na TBS nao wana wajibu wa kusimamia /kutoa elimu ya namna ya kuboresha biashara ndogo ndogo ili zikuwe na kuondoa dhana ya Umachinga wa wajasiriamali wadogo wadogo.
 
Back
Top Bottom