Vitambulisho vya machinga vimezikwa na hayati Rais Dkt John Magufuli huko Chato?

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Wakuu Wamachinga wa soko la Samunge maarufu kama NMC jijini Arusha wameieleza kilio chao kwa mbunge Mrisho Gambo cha kulipa ushuru wa shilingi 50 kila siku huku wanaowatoza wakiambiwa kuwa vitambulisho vya machinga vimezikwa na hayati Rais Dkt John Magufuli huko Chato.


Machinga wa soko hilo wameyasema hayo Mbunge huyo alipowatembelea na kusikiliza kero zinazowakabili ambapo wakielezea kuwa kero kubwa ni ushuru wanaotozwa kila siku na wakiulizia vitambulisho vya machinga walivyokuwa wanatumia awali wanaambiwa vimezikwa Chato.

Je Hii Sio Dharau Kwa Hayati Magufuli? Kwa Nini Huyu Mchukua Ushuru ametumia Kauli Hii?
View attachment 1934903
 
Inawezekanaje mitaani watu wenye viduka vinavyouza 30,000 kwa siku walipe kodi TRA halafu machinga wanauza hadi 200,000 lakini wanalipa 20,000 ya kitambulisho,ni upuuzi.
 
Idadi ya wamachinga inaongezeka kila siku , ajira rasmi nazo zinazidi kupungua,vitambulisho vya JPM sio muarobaini,itafutwe njia nyingine ya kuwawezesha watu hao kufanya shughuli zao kwenye maeneo maalumu na salama Kibiashara.
 
Machinga wa Arusha wameanza kuisoma namba baada ya kuambiwa kuwa hakuna tena vitambusho vya machinga hivyo wanatakiwa kulipa Tshs 500/= kila siku.

Wafanyabiashara hao hata walipoulizia kuwa mbona tuliambiwa tuwe na vitambulisho vya wamachinga vya Tsh 20,000/=? walijibiwa kuwa vitambulisho vya wamachinga vilizikwa Chato na kuanzia sasa wanatakiwa kutafuta TIN namba na kulipa ushuru kama wafanyabiashara wengine na kama wanataka kuwa wamachinga basi wabebe bidhaa zao na kuzunguka nazo si kukaa nazo sehemu moja ...jambo hilo halipo kwa sasa.

Hata hivyo mbunge wa Arusha, Mrisho Gambo akiongea na wamachinga amesema kuwa akiwa bungeni Mh Waziri Mkuu alisema hadharani kuwa Serikali inavitambua vitambulisho vya wamachinga na wataviboresha na kuviweka picha ili viwe na sura na vimeshaanza kutolewa kwa elfu ishirini na mbunge huyo amesema wazi kuwa yeye yupo pamoja na wamachinga na hao wanaosema vitambulisho vimezikwa Chato basi ni wachonganishi na wanafiki.

Chanzo: EFM RADIO

NB: Leo ndio siku ya kuondolewa wamachinga jijini Dar es salaam kama alivyo agiza Amos Makala
 
Ndio maanake PESA YAKE HATUJAWAHI AMBIWA IKO KWENYE MFUKO GANI AU NDIO ILIKUWA INAJENGA CHATO ???
 
Waanze na hao waliobana barabara ya kutoka Kilombero kupitia Hospitali na mahakama kwenda, halafu vibanda vya florida kwenda stand kuu. Yaani kiujumla ili Arusha iwe na hadhi ya mji wa kitalii lazima iondoe Wamachinga kabisa.
 
Mji umekuwa mchafu ajabu, now wameanza kujenga kuelekea polisi kutokea mnarani.

Kule jirani na kibo palace hotel naona walikuwa wanajenga kwenda mbele ila naona wenye hotel wamewabomolea, yaani ni full uchafu hizi kitu.
 
Dsm limekuwa jiji la hovyo na chafu.......hakuna anayekataa machinga ila imekuwa too much
 
Nchi imesharudi kwa wenyewe.

Wanyonge hawana haki tena ndani ya nchi yao.

RIP Magufuli, you were the best.
Kila mtu alipe kodi, huwezi ukawa unapanga lundo la bidhaa barabarani halafu hulipi hata senti, eti wewe mnyonge..mentality za kipuuzi sana hizi

Walipe ushuru hata kama ni 200 kwa siku, ila sio kuwa free ni ujinga
 
Back
Top Bottom