vitambulisho na leseni mpya za kisasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

vitambulisho na leseni mpya za kisasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ubungoubungo, Sep 17, 2010.

 1. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  wakubwa, hivi vitambulisho vya utaifa (na vya ukaazi kwa wale wasio raia) mwisho wake umefikia wapi? manake tunaona nchi zingine wameshafanya hivyo, na inakuwa rahisi sana hata kukamata wezi kwasababu kile kitambulisho kinakuwa kimewekwa kwenye database ya mtandao wa selikali hivyo ukiingiza namba yako popote pale iwe bank,iwe kituo cha polisi, iwe popote pale nchini unatambulika wewe ni nani...hii inasaidia kukamata wezi na wahalifu wengine na kucontrol watu waishi kwa usalama. sasa hapa tz wanatuletea vitambulisho vya aina gani na leseni za udereva za aina gani, tunataka ziwe na hadhi zaidi ya passport. kama Masha unanisikia hapa nataka ufanye hivyo haraka sana, hatutaki kuwa nyuma tu kila mwaka...wasomali na wakenya wamejaa hapa pamoja na wanyarwanda hadi wanagombea uongozi, kuna siku tutakuwa na rais msomali hapahapa tz...Mungu ibariki Tanzania.
   
 2. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2010
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Vitambulisho + Leseni za kisasa bila miundombinu ya kisasa haina maana....
   
 3. bona

  bona JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  nilishangaa jana kwenye taarifa ya habari ya TV leseni mpya itakua elf 40, cjui wenzangu is this price justifiable? au ndo mpango wa serikali ii vivu kutaka kujiongezea mapato? maana tunajua jinsi wasivyo wabunifu kutafuta pesa wanachojua ni kumkamua maskini tu! kilichonifanya niamini ni ishu ya pesa zaidi kwani kamisshna mkuu wa TRA alikua mbele kuliongelea ili suala kwenye media i thought lilikua zaidi suala la usalama barabarani kwa iyo polisi ndio wangekua mbele kulizungumzia!
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  jana nimeangalia news watu wanne wamepata leseni bila interview na wala hawakurudisha za zamani. Binti aliyekuwa anaelekeza, waziri, mkuu wa TRA na Mkuu wa traffic. Je hizo leseni ni halali?????
   
 5. Sabasaba

  Sabasaba Member

  #5
  Sep 17, 2010
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 88
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15
  .

  Hizi leseni si halali maana hazijafata hata masharti ambayo yanaongelewa na TRA na police, au kuwa waziri wa mambo ya ndani huruhusiwi kufata sheria?, manake wenyewe wanasema hakuna mkato kwenye kupata hizi leseni
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Siku ya kwanza nne sio halali kwa mwaka itakuwaje?

  Tanzania tanzania nakupenda kwa moyo wote.

  Alivyozungumza waziri sivyo ilvyokuwa mpaka akapewa leseni na nimeangalia wala hazikuandikwa sample in red kukatisha kwenye hizo leseni za mfano
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Bei ya leseni imepanda.
  Angalia hii nchi hii. wanapandisha gharama kwa melfu wala sio kwa makumi au mamia. Sijui hii serikali inaendeshwa na wasomi kweli hii?
   
 8. f

  friendsofjeykey Senior Member

  #8
  Sep 17, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona zabuni hatukuona zikitangazwa? au PPA haihusiki kweye haya?
   
 9. nkosikazi

  nkosikazi JF-Expert Member

  #9
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 11, 2010
  Messages: 354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nimeanza kuona NIDA wakianza kutangaza kuhusu vitambulisho vya taifa na faida zake kama kupata mikopo ya kibiashara kwa wau wote pamoja na wakulima na wamachinga napia mikopo kwa wanafunzi na kupanuka kwa biashara as if card hiyo ni magic wand kwamba all of a sudden life will be ok na as if sasa mambo hayaendi shauri ya vitambulisho! Nadhani ifike mahali watu wa vyama vya upinzani na wote wapenda maendeleo ya nchi hii waseme enough is enough! Huu ni wizi tu na hamna lolote la maana! Nani mwenye akili timamu atakayeweza kutumia mabilioni ya fedha kutoa vitambulosho kwa wanachi waishio kwenye vibanda na wala hawana mitaa wala vijiji vya kuweza kuwatambua? Utawekaje vipaumbele uchwara kama hivi wakati hamna umeme na viwanda vimesimama kuzalisha shauri ya umeme na uchumi unaporomoka? Watoto wanakufa kwa kukosa dawa wewe unaongea kuhusu vitambulisho vya smart card vinavyogharim trilioni? Hiingii akilini kuwa baraza la mawaziri pamoja na wabunge wetu hawaoni kuwa hiki si kipaumbele chetu? Hivi mnajua kuwa serikali imewakopa wananchi wake wanaotoa services na gooda kwa serikalisababu haina hela ya kuwalipa ikiwa ni pamoja na wakandarasi waliojenga barabara za umma kwa fedha zao na serikali imeshindwa kuwarudishia hela walizotumia na sasa tunaongelea kuhusu miradi ya ovyo kama vitambulisho!
  Lets stand up and be counted! Huu upuzi na ulaji wa wachache tusiukubali! Tulionywa kuhusu IPTL kuwa ni mradi fake hatukusikia na matokeo yake tumeyaona! Tulionywa kuhsu rada na waingereza wenyewe walioitengeneza kwamba msiinunue lakini hatukusikia! Tumeona wenyewe matokeo yake!
  Umefika wakati wa kusimama kama taifa la watu wenye akili na hekima hata kama ni wachache wetu tu na hata kama wenye akili hao inaexclude mawaziri wanaotumia matumbo kufikiria badala ya ubongo!
  LETS SAY NO TO THIS USELESS ID CARDS SCAM!
   
 10. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  wakuu siamini kama inawezekana,hapa tunaangalia channel 10 je tutafika
  mkurugenzi wa vitambulisho vya taifa anasema watu wote wanaoishi tanzania watapewa vitambulisho
  awe mtanzania au mgeni
  swala ni kwamba sijawahi kuona nchi yoyote duniani kufanya upumbavu kama huo
  foreigner wote wanaoishi katika nchi wanapewa kitu kinaitwa permit
  work permit, residence permit and so on
  sasa hii ya watanzania kuwapa vitambulisho inamaanisha kwamba watanzania ni watu wenye upendo sana??
  kwa nini tusifanya kama nchi zingine?
   
 11. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Wageni wanaoishi Tz watapewa vitambulisho sio kwamba ni wananchi wa Tz bali vitambulisho vyao vitakuwa vya wageni wakazi wa Tz. Information zao zinahitajika na serikali including TRA. Hata nchi jirani ya kenya na kwengineko wana issue ID kwa wageni wakazi. Residence permit huwa wanagongewa kwenye passport zao na hakuna anaetembea na passport kila wakati.
   
 12. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu ndo mara yangu ya kwanzaa kusikia habari kama hiyo
  kwa nini wasishughulikie kwanza vitambulisho vya raia na kuachana na raia wa kigenI?
   
 13. M

  Manyovu Member

  #13
  Jul 26, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 15
  Episodes, Usishangae na kuchanganya mambo wageni watapata vitambulisho lakini details zao zitakuwepo kwenye hivyo vitambulisho. Mfano halisi mie niko nje ya nchi kwa sasa lakini ninacho kitambulisho nilichopewa hapa. Kitambulisho hiki kina majina yangu, uraia wangu, namba ya pasipoti, kazi ninayofanya na ni cha muda gani. Work permit na residence permit ni document zingine kabisa ambazo ziko kwenye pasipoti yangu. Kwa hiyo nikiwa hapa sihitaji kutembea na pasipoti yangu bali natemebea na kitambulisho hiki na kinatumika sehemu yoyote ninayohitaji huduma.
   
 14. D

  Dopas JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2011
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hata mimi nipo nchi nje kwa masomo, mbali na documents nyingine zote muhimu kama passport, res permit, pia nina kitambulisho cha nchi hii, ambacho kitaisha muda 2021.
  Kwa ujumla, taratibu zikifuatwa vizuri, mgeni kuwa na kitambulisho ni kitu cha kawaida isipokuwa hawezi kupata kitambulisho bila kuwa na documents zingine muhimu. Muda wa kuisha passport, res permit na documents nyingine hauna uhusiano na kitambulisho. Kila kimoja kinajitegemea. Kwa ujumla kwa nchi za ulaya ukiwa na kitambulisho husaidia kupata huduma nyingi kwa gharama nafuu, mf. tiket ya kusafiri mwaka mzima ndani ya mkoa husika ni euro 230/- kama una kitambulisho ni euro 150. Ungenunua reja reja ingeweza kuwa hata mara 4.
   
 15. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hao wageni wanalipa pesa nyingi kuchukua kitambulisho kuliko wewe raia...kwahiyo wao vile vile muhimu kupewa.
   
 16. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #16
  Jul 27, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280

  Wageni kinakuwa kimeandikwa kabisa kwamba yeye ni mgeni na sio mtanzania hakuna neno hapo nchi nyingi wanafanya hivyo.
   
 17. Kakati

  Kakati Senior Member

  #17
  Jul 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 151
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Msameheni bure hajui duniani watu wanafanyaje.
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,497
  Likes Received: 81,829
  Trophy Points: 280
  [h=2]Minister: Policy on citizenship in pipeline[/h]

  By Patrick Kisembo

  29th July 2011

  National IDs set to be issued by end of year

  Home Affairs minister Shamsi Vuai Nahodha

  The government is drafting a policy that will restrict the number of foreigners seeking citizenship, Home Affairs minister Shamsi Vuai Nahodha revealed in the House yesterday.
  Tabling the 2011/12 Home Affairs ministry budget estimates, the minister said the process has already started, adding: "The policy seeks to limits the number of foreigners granted citizenship by the government."

  The minister would not reveal the number of foreigners who have applied for Tanzanian citizenship, but it is understood that the move comes in the wake of a massive influx of aliens into the country.
  The minister said the government would put in place conditions specifying the number of people to be given citizenship every year.
  According to Nahodha, the ministry granted 90 foreigners citizenship last year after they met the set conditions.
  He told the House that most foreigners who were given citizenship were from India, Somalia, Rwanda, Lebanon, Finland, Yemen, Pakistan, Nigeria, Italy, Republic of Sudan, Zambia, Bangladesh and China.

  A total of 625,308 foreigners entered the country between July 2010 and April 2011 as compared to 664,037 foreigners, who entered the country in the previous year, Nahodha said.
  He requested the House to approve a total of 482.394bn/- for his ministry's 2011/12 financial year budget of which 283.638bn/- was for the police force, 3.025bn/- for fire brigade, 108.850bn/- prisons, 6.864bn/- the ministry headquarters and 80.015bn/- for the immigration department.

  Further, he said that 627,884 foreigners left the country between July 2010 and April 2011 compared to 638,376 in the previous year.
  "The number of foreigners who have entered the country has fallen at an average of 38,729, equal to 5.8 per cent due to reasons related to economic crisis," said the Minister.
  He told the House that in the 2010/11 financial year 12,563 foreigners were granted residential permits compared to 10,890, who got such permits in the previous year.
  The number of residential permits issued increased by 1,673, equivalent to 15.4 percent during the period, he said.

  "The main reasons for this were the progress made in the world economy and the promising investment environment in the country,' he said.
  The minister told the House further that 32 Tanzanians were granted citizenship in foreign countries, including Kenya, Germany, Norway, Denmark, Zambia, Britain, Australia, Namibia, Sweden, China and Singapore.

  Holding the government censured, the opposition camp in Parliament said there has been an increase in the flow of foreigners into Tanzania as if the country "has no rules and regulations to check the anomaly."
  The Shadow minister Godbless Lema made the remarks when tabling the alternative budget yesterday, saying illegal immigrants were openly moving in the country's urban streets.

  "They are running their businesses as if they are citizens," he said citing people from Somalia, Democratic Republic of Congo (DRC), Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda, Pakistan, Nigeria, Bangladesh, India and China.
  "Majority of these people are living in the country without legal permits allowing them to do business," Lema said.

  The opposition told the government that the habit of letting foreigners live in the country illegally, poses a big security threat especially in this era of terrorism.
  The Parliamentary committee on Foreign Affairs, Defence and Security proposed that the government address the challenges facing the immigration department, saying it has been lacking communications facilities.

  Mohamed Khatib (CCM) tabling the committee's report on behalf of its chairman, Edward Lowassa (Monduli, CCM) said the department needs to be empowered to cope with the challenges it is facing.
  Meanwhile, the minister said that issuance of the National Identity Cards (IDs) is expected to start at the end of this year.

  "It is going to start at the end of this year with the issuance of IDs to some segments of the country's population," the minister said.
  He mentioned those to be issued with the IDs as public servants, college and university students and businessmen.

  According to the minister, the IDs would help the possessor to solve many problems including checking ghost workers in the public service.
  They would also make it easy to identify higher-education students who qualify for government loans, strengthen security and simplify identification of voters.
  Nahodha said the National Identification Authority (NIDA), the government agency overseeing implementation of the project, has already finalised procedures to acquire plots for construction of its offices in all districts on the Mainland.

  The 355bn/- project would enable the government to widen revenue collections from the current 1,570,000 taxpayers to 12 million.
  "The government signed an agreement with IRIS Corporation Behard of Malaysia to implement the project on April 21 this year, and the firm has started working on the project," Nahodha said.
  He said that between 25milion and 26 million citizens will be given the IDs.
  The opposition camp reacting to the minister's speech blamed the government for the delays in issuing the IDs.

  Shadow minister Godbless Lema advised NIDA management to speed up the project in the interest of the nation so that by 2014 every Tanzanian who qualifies for the ID would have one.
  He also proposed that the electoral commission should make use of the IDs in the 2015 general elections.
  For its part, the Parliamentary Committee on Foreign Affairs, Defence and Security differed with the opposition, saying work on the IDs has been progressing well.

  SOURCE: THE GUARDIAN
   
 19. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #19
  Jul 29, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  watu wanatamani wakimbie bongo! hawa ndio wameomba uraia na kupewa !>. seriously! huyu mtu toka italy anaomba uraia wa bongo! sio bure!
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,497
  Likes Received: 81,829
  Trophy Points: 280
  Sijui ni vigezo vipi vinatumika mpaka mgeni akubaliwe maombi yake ya kuwa raia. Sidhani kama hata kulifanywa utafiti wa kina kuangalia nchi za wenzetu wanatumia vigezo gani ili kumpa mtu uraia ili nasi tuige baadhi ya vile ambavyo tunaviona vinafaa.

  Kuna nchi nyingine hupewi uraia mpaka uwe unazungumza lugha ya Taifa ya nchi hiyo na pia kuifahamu historia ya nchi hiyo na kuna mitihani ambayo ni lazima ufaulu ili uweze kupata uraia.
   
Loading...