Tofauti za majina kwenye vyeti vya kitaaluma kutoka mamlaka husika ni usumbufu usio na ulazima

howardlite

JF-Expert Member
Jul 16, 2016
234
368
Kumekuwa na usumbufu usio na ulazima kwa baadhi yetu ambao tumewahi kukutana nao,inapotokea unatakiwa vyeti kwa lengo fulani mfano,fao la kustaafu,fao la uzazi,ajira nk.

Usumbufu unaojitokeza ni pale majina yako yanapotofautiana kwenye vyeti na nyaraka mbalimbali.

Unakuta mtu unaitwa John Alfred Mhina.

Unaandikishwa shule kwa jina hilo,unafanya uhakiki,lakini cheti cha O'level na A'level kinakuja na majina mawili la kwanza na la mwisho.

Ukienda chuo mfano UD transcript inakuja na majina yote matatu,cheti kinakuja na majina mawili.

Mwingine O'level na A'level majina matatu, chuo yanakuja mawili.

Mwingine O'level na A'level majina mawili chuo wanaweka initial katikati.

Kwangu ndio hatari, majina mawili mpaka chuo,cheti cha uongozi majina matatu,kazini documents za ajira sijui kuthibitishwa na vitu gani majina matatu nyingine mawili, nyingine initial katikati,nikasomea kitu kingine- airport yakaja majina mawili kwenye vyeti,ikaja leseni majina matatu,leseni ya udereva majina matatu,vyeti vya courses za kazini kwenye madini majina matatu.

Siku ikaja nimetakiwa vyeti,dah nikatakiwa kwenda kuapa,nikahesabu ni usumbufu sio kwangu tu lakini ni watu kadhaa wanapitia kadhia hii.

Kwanini tusiwe na mfumo rasmi wa majina kama ni matatu basi iwe hivyo kwa level zote za masomo kazi na vingine mpaka unakufa?

Hizi mambo za wanasheria na mahakama kula pesa za kuapa si kitu bali usumbufu na ni kosa la mamlaka zinazohusika na elimu,ajira nk.

Nyie mamlaka husika japo hili ni dogo lakini linaleta usumbufu.

Sasa mtu majina yako yanabadilishwa utafikiri unakwepa kodi au ni vyeti feki.

Na hili mkaliangalie.
 
nenda kaape tu au nenda deed pol badili jina uko huru sana
Sisi tunaapa kiapo cha majina (Affidavit) au hati ya usajili wa majina (Deedpoll) sawa(usumbufu)na watoto wetu au watoto wa watoto wetu waendelee na utaratibu wa aina hii ambao ni suala la kuamua tu kumaliza changamoto isiendelee mpaka kwa vizazi vingine?
 
Ni kweli tuliosoma zamani kulikuwa na hiyo changamoto, siku hizi hakuna majina mawili. Angalia matokeo ya darasa la nne na form 2. Mpaka chuo ni majina matatu.
 
Sisi tunaapa kiapo cha majina (Affidavit) au hati ya usajili wa majina (Deedpoll) sawa(usumbufu)na watoto wetu au watoto wa watoto wetu waendelee na utaratibu wa aina hii ambao ni suala la kuamua tu kumaliza changamoto isiendelee mpaka kwa vizazi vingine?
Hakikisha majina yako yanatumiwa pia na watoto wako wasipate usumbufu baadae
 
Sisi tunaapa kiapo cha majina (Affidavit) au hati ya usajili wa majina (Deedpoll) sawa(usumbufu)na watoto wetu au watoto wa watoto wetu waendelee na utaratibu wa aina hii ambao ni suala la kuamua tu kumaliza changamoto isiendelee mpaka kwa vizazi vingine?
NIDA imewekwa kurahisisha kila kitu lakini hawataki kuitumia vyema. Vitu kama vyeti vya taaluma nk vilitakiwa viwekwe kwenye mfumo wa NIDA mtu akiitisha namba yako anapata nyaraka zote zikuhusuzo, hizo tofauti ndogo za majina zinakuwa hazina ishu. Ila sasa NIDA yenyewe ndio watumiaji hawajielewi
 
Hii nchi kama kuna jambo limewahi kufanikiwa angarau kwa 75% ni campaign za uchaguzi tu.
 
UGANDA walifanikiwaje?
Mtoto wangu amemaliza darasa la saba na Jina la tatu sijui nani alikiandikisha na ni tofauti kabisa n majina aliyokuwa anatumia awali ikiwa ni pamoja na report card ya kila muhula...nauliza sasa yuko kidato cha pili ili aweze kuibadili Jina la tatu...mwalimu analeta tantarira nyingi kuwa haiwezekani.
Ujinga mtupu.
 
UGANDA walifanikiwaje?
Mtoto wangu amemaliza darasa la saba na Jina la tatu sijui nani alikiandikisha na ni tofauti kabisa n majina aliyokuwa anatumia awali ikiwa ni pamoja na report card ya kila muhula...nauliza sasa yuko kidato cha pili ili aweze kuibadili Jina la tatu...mwalimu analeta tantarira nyingi kuwa haiwezekani.
Ujinga mtupu.
inawezekana we achana na mwalimu huyo mdogo mnoo kwenye mfumo huo,nenda kaape then andik barua kwa Afisa elimu wilaya yeye ataleta maagizo tu hapo shuleni wakati anaendelea kupeleka taarifa hizo Mkoani mpaka baraza ukishindwa utasaidiwa
 
Hayo majina ulipokuwa unajisajili huko ilikuwa unaandikiwa au unaandika mwenyewe .
Hapo naona tatizo ni lako wakati unajisajili uwe unaandika majina yote matatu..
Nilivyosoma mwanzo nilifikiria chuo ndio kikosee kuandika Jina kwenye cheti, halafu ukute chuo vyeti vinaprintiwa nje ya nchi
 
MM PIA NI MDAU WA HILI. NILIANZA SHULE NA JINA NILILOPEWA NA WAZAZI MFANO TABU, SHIDA, MATESO, MASUMBUKO, N. K. SASA MAJINA HAYA KWENYE JAMII HAYALETI RAHA ILA UNAKUTA UNASITA KUJITAMBULISHA NA UNAPOTAZA WATU WANAKUCHEKA. TUNASHUKURU KUNA SHERIA YA KUBADILI JINA. NILIPOPATA AFFIDAVIT NINAPOIPELEKA TAASISI HUSIKA INAKATAA KUPOKEA NA KUBADILISHA MFANO MZUMBE SS, UDSM, NECTA NA KWENGINE. SASA INALETA USUMBUFU. NAUNGANA NA WENGINE KWENYE HOJA HII ILI MAMLAKA YA NCHI IUNDE MFUMO MMOJA WA KUSAWAZISHA MAJINA YA WOTE WENYE HAJA YA KUFANYA HIVYO. NASHAURI MAMLAKA KAMA LITA INAKUWA MRATIBU WA HILI NA HII MAMLAKA NDIYO IWASILIANA NA TAASISI NYINGINE ILI ZIBADILI AU KUREKEBISHA MAJINA KATIKA NYARAKA HUSIKA KAMA VYETI. KWA MIFUMO YA TEHAMA YA SASA HILO NIRAHISI.HATA KAMA ITAKUWA NA ADA KIDOGO IWE HIVYO. UFANANO WA MAJINA POPOTE NA MUDA WOTE NI MUHIMU SANA KULIKO KILA NYARAKA KUWA NA JINA TOFAUTI KIDOGO KWA MTU YULEYULE. ITAONDOA HILO TATIZO NA USUMBUFU WA KUAPA MARA KWA MARA.
 
Back
Top Bottom