Vita ya kugombea mali za aliyekuwa Mchungaji, Marehemu Getrude Rwakatare sasa imeshika kasi

Wanajipanga.Mzazi wala haandiki hata hisia

Ingekuwa waarabu watoto wote wangekaa kikao pamoja kujipanga namna ya kuendesha hizo mali.Wangechaguana mmoja awe mkurugenzi mtendaji ,mwingine wa utawala,mwingine wa fedha nk na kuziendesha hizo mali pamoja wakawa wanalipana mishahara kila mwezi na wanagawana faida mwisho wa mwaka

Lakini mitoto ya kiswahili pasua kichwa yaani mali zote zile zinasambaratika kwa muda mfupi .Muda si mrefu hao watoto wa Lwakatare watakuwa maskini wa kutupwa
Na usishangae nyuma ya hawa vijana kuna pisi kali zinachochea mali ziuzwe, mali zikikauka vijana watakuta wamezeeka bila mke wala Mali.
 
Utajiri level ya mama wakatare. Ni wa kugombea mali kweli

Yaani watoto tumbo moja na baba mmoja bado mnagombea mali za mabilioni.

Yaani hata mgawane vipi bado kila mtu ana qualify kuwa bilionea ila bado mnagombana tu.

Wahindi na waarabu wanatumia ujanja gani kumudu mirathi kwa amani
 
Utajiri level ya mama wakatare. Ni wa kugombea mali kweli

Yaani watoto tumbo moja na baba mmoja bado mnagombea mali za mabilioni.

Yaani hata mgawane vipi bado kila mtu ana qualify kuwa bilionea ila bado mnagombana tu.

Wahindi na waarabu
Inategemea Mali ilipatikana vp?

Ova
 
Tukawaulize Kakobe, Lusekelo, Mwingira na Gwajima wamejipangaje kurithisha mali kwa kanisa na si kwa familia.
 
"Kifo na kiheshimiwe unajitaabisha wee kukusanya kwa jasho nguvu nyingi zikiwemo za giza lakini mwishowe ni umauti na kusahaulika tu"
What's the meanings of life? Where are we going after death?, which are the target of living hood?.....
°sometimes wealth can be useless, over "Holy death"
Na ndio maana nchini spain ipo mila inakabudu kifo as holy death.
 
VITA ya kugombea mali za aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God - Mlima wa Moto, Marehemu Mchungaji Getrude Rwakatare sasa imeshika kasi huku ikizidi kuwagawa watoto wake.

Taarifa za kuwepo kwa vita hii zimekuja ikiwa ni miezi kadhaa baada ya mtoto mkubwa wa kiume wa Marehemu Rwakatare, anayefahamika kwa jina la Tibe Kenneth Rwakatare kumuandikia barua Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, akimueleza jinsi ndugu zake wanavyokiuka sheria kwa kutenda makosa ya jinai, akiwatuhumu kughushi nyaraka za mauzo ya baadhi ya mali za marehemu mama yake, Mchungaji Rwakatare.

Tibe Kenneth Rwakatare aliandika barua hiyo Disemba 31, 2021 ikiwa na kichwa cha maneno kinachosomeka ‘mauzo batili plot no 259 Udindifu Bagamayo.’

Katika barua hiyo, Tibe aliandika kumweleza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa uuzwaji wa kiwanja hicho umehusisha nyaraka za kughushi pamoja na kutolipwa kwa kodi stahiki za Serikali.

Akithibitisha kuandika barua hiyo, Tibe aliiambia Tanzania PANORAMA Blog kuwa amedhulumiwa haki yake na ndugu zake hivyo hakuwa na jingine zaidi ya kuandika barua hiyo.

Wakili kiongozi wa Kampuni ya Uwakili ya Haki Kwanza Advocates, Alloyce Komba ambaye ametoa ufafanuzi kuhusu tuhuma zilizotolewa na Tibe dhidi ya ndugu zake, amesema adhabu itakayowakabili watuhumiwa wakibainika mahakamani kutenda jinai hiyo ni kifungo.

“Kosa la kughushi, adhabu yake iwapo mahakama ikimtia hatiani mtu kwa ushahidi usio na shaka yoyote ni kufungwa kwa mujibu wa kifungu cha 337 cha sheria ya kanuni za adhabu, sura ya 16 ya sheria za Tanzania, toleo la 2019.

“Mtu anapaswa kuripoti polisi kosa lolote la jinai linalofanywa na mtu yoyote ili mradi awe na ushahidi wa kutosha.

“Ni kosa pia kunyamazia kosa la jinai. Ndiyo maana mtu hukosa kwa kutenda (commission) au kutotenda (omission), mfano kutomzuia mtoto kutumbukia kisimani wakati unaona anacheza karibu na kisima,” alisema Wakili Komba.

Mwanasheria mwingine aliyezungumza na PANORAMA kwa sharti la jina lake kuhifadhiwa alisema tuhuma zilizotolewa na Tibe dhidi ya ndugu zake ni nzito na iwapo zitathibitika mahakamani hawatakwepa mkono wa sheria.

“Sheria zipo lakini inashangaza watu wanatenda makosa ya makusudi kama haya ambayo adhabu yake ni kali.

“Huyu anayewatuhumu wenzake naye hayuko salama kwa sababu ni wazi anajua vema jinsi ndugu zake walivyotenda hiyo jinai, walivyoghushi kwa sababu ni ndugu zake hivyo alipaswa kutoa taarifa polisi.

“Sasa inashangaza kijana msomi kukaa kimya huku akijua kuna jinai inafanyika. Kwa vile kalipeleka kwa waziri tumpe nafasi ya kulifanyia kazi,” alisema.

Kwa mujibu wa kifungu cha 338 cha sheria ya kanuni ya adhabu, sura ya 16 ya sheria za Tanzania, toleo la 2019 ambayo Tanzania PANORAMA Blog imeiperuzi inaeleza kuwa mtu akibainika mahakamani kwa kughushi wosia, hati za umiliki ardhi, hundi n.k adhabu yake ni kifungo cha maisha jela.

Hilo likiwa halijapoa, mtoto mwingine wa kiume wa Marehemu Mchungaji Rwakatare anayefahamika kwa jina la Muta Robert Rwakatare ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) alizungumza na mwandishi wa Tanzania PANORAMA Blog na kumshutumu ndugu yake Tibe Kenneth Rwakatare kwa kutwaa kimabavu Shule ya Sekondari ya St. Mary’s International School, Dodoma Campus ambayo ni mali waliyoachiwa na marehemu mama yao.

Muta alieleza kuwa shule hiyo ni miongoni mwa shule zilizokuwa zikimilikiwa na Marehemu Mchungaji Rwakatare enzi za uhai wake lakini hivi sasa Tibe imeibadilisha jina na kutwaa umiliki wake.

Alisema ikiwa chini ya umiliki wa mama yao, ilikuwa ikijulikana kwa jina la St. Mary’s International School, Dodoma Campus, lakini sasa baada ya kubadilishwa jina inafahamika kwa jina la St. Mary’s Dodoma.

Muta alisema Tibe sasa anachukua mapato yote ya shule hiyo na eneo ilipojengwa nalo amelibadilisha jina na kuweka la kwake.

Watu walio karibu na familia hiyo wameeleza kuwa chanzo cha mzozo wa umiliki wa shule hiyo baada ya Marehemu Mchungaji Rwakatare kufariki ni mmoja wa watoto wake kuwazunguka wenzake na kuhamisha fedha zote zilizokuwa kwenye akaunti ya shule kwenda akaunti yake binafsi na pia akaanza kuchukua mapato yote ya shule hiyo.

Kwamba baada ya hilo kubainika, Tibe aliamua kuitwaa shule hiyo, akaibadilisha jina na majina ya akaunti za benki, hatua ambayo sasa inalalamikiwa na ndugu zake.

“Huyu ndugu yetu anashangaza sana kuanza kuandika barua kwa viongozi wa Serikali akitutuhumu kwa kukiuka sheria za nchi, eti tunaghushi nyaraka wakati yeye ndiyo bingwa wa kughushi nyaraka kuanzia Brela mpaka ardhi na anayemtumia kufanya hizo kazi za kughushi anafahamika, ni kijana aliyesoma kwenye moja ya shule zetu. Anachotaka amiliki yeye mali zote za mama.

“Ana madudu mengi mno lakini sie hatujishughulishi naye matokeo yake akiona tunamzuia kuchukua kila kitu anatafuta huruma nje ya familia kwa kutuchongea serikalini.

“Amejimilikisha shule ya Dodoma na kuibadili jina na akaunti za benki wakati shule hiyo ina mkopo wa benki moja kubwa nchini. Wewe unaweza kubadili umiliki wa mali ambayo ina mkopo wa benki kweli? Muulizeni na yeye hilo kalifanikishaje?

“Anamiliki mali nyingi sana za mama ambazo mapato yake yote yanaingia mfukoni mwake na hakuna anayemsumbua lakini yeye jambo dogo tu analalamika na kuandika barua huku na kule.

“Tulipouza hizo ardhi nyingine na kugawana mbona hakusema lolote? Kamuulizeni anataka nini hasa maana shule aliyotupora baada ya kuibadilisha jina imeondolewa kwenye orodha ya mali za marehemu mama. Hivi sasa anaimiliki yeye bila ridhaa ya sisi ndugu wengine.

“Nyumba za kupangisha za marehemu mama, zile ‘Appartments’ za Tabata zaidi ya 25, vyumba vya biashara 20, kote anachukua kodi yeye na pia mgodi wa dhahabu Chunya nao kachukua lakini bado anatupiga vita,” alisema Muta.

Alipoulizwa Tibe kuhusiana na madai hayo alisema hana muda wa kuyazungumzia.

Tanzania PANORAMA inaendelea kumtafuta Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kulizungumzia hilo.

Source: Tanzania-Panorama
Kosa la mama Rwakatare ni kutowaarithisha watoto wake maadili mema na upendo ndio maana yote haya yanatokea.
 
Urithi mzuri usio na migogoro kwa sasa ni PESA tu. Ukiondoka watoto wanapigiana pasu, kila mtu anatawanyika. Lakini miundombinu? Watagombana tu; mara, ooh, mimi nyumba niliyogawiwa ni mbaya, n.k.
 
Mitoto yote minne ya Marehemu Getrude Lwakatare ni ya hovyo mno. Hivi bado kanisa lipo? Hizo Mali zitapukutika kama maua. Na Kwa kuwa ni mivivu siyo wawekezaji watakuwa maskini wa kutupwa.
 
Mkuu labda ndo masharti wanayopewa wakienda kutafuta uchungaji wao huko Nigeria..
 
Wakristo matajiri wanakosea sana kulea watoto kwenye mambo ya mali

Hata wakiwa tumbo moja bado wanagombania mali.

Tazama matajiri wa kiislam wakifariki mifarakano hakuna.

Kafa baba wa gsm kimyaa.. kafa sumry kimyaa.. kafa patel kimyaa.. kafa zakaria kimyaaa.. kafa ali mafuruki kimyaaa husikii familia zikigombea mali.

Ila wakristo kafa mengii mgogoro, kafa lwakatare mgogoro, kafa bilionea msuya mgogoro mpaka wanachinjaaana mtu na wifi yake... yaani balaa tupu
 
Mara nyingi misiba ya waislamu huwa wanatumia sheria za mirathi za kiislamu katika kugawa mali.. Sasa shida ni kwamba hakuna sheria za mirathi za wakristo.. wanatumia sheria za kiserikali ambazo zinakaribisha magomvi mengi..
 
Back
Top Bottom