Vita ya kugombea mali za aliyekuwa Mchungaji, Marehemu Getrude Rwakatare sasa imeshika kasi

Unajua hii vita naweza sema kaisababisha mama mwenyewe tukirudi kwenye historia ya hizo mali zake hazikuwa zake zilikuwa za kanisa la TAG wakati yeye akiwa mchungaji huko hizo shule zilikuwa chini ya usimamizi wa TAG na kanisa lilimuamini kama msimamizi na kulikuwa na makunaliano na shule,na kanisa lkn alichokuja kukifanya huyo mama ni utapeli mkubwa alinadili kanisa kuwa mali yake na usimamizinwa shule fungu likawa.linaenda kwake vita ilikuwa kubwa kanisa likaaamua kuachana nae tu kwamba Bwana aamue mwenyewe hyo kesi ona sasa wazungu wanasema unachokifanya kiwe kizuri au kibaya unajifanyia mwenyewe tu kwa hyo hiyo vita ya watoto kasababisha mama mwenyewe.

Mama ameanza kumiliki shule kabla ya kuwa mchungaji.

Maana shule ni za zamani sana. 90s kati kati st marys zilianzishwa
 
Wakili ni Alloyce Komba? Basi mmepigwa, wakili anaandika barua kwa Waziri? Ndio utaratibu wa sheria? Sio kwa Msajili wa hati kupeleka caveat au kuripoti Polisi au kufungua shauri mahakmaa ya ardhi/mirathi?
Wakili wa vichochoroni plus mchongo
 
Mama ameanza kumiliki shule kabla ya kuwa mchungaji.

Maana shule ni za zamani sana. 90s kati kati st marys zilianzishwa
St mary sio shule zake mama alikuwa mwangalizi wa hzo shule akiwa TAg akipenda sana huduma ya kutembelea wanafunzi mashuleni na wkt huo akijifunza utumishi badae ndio alianzisha za kwake hzo za kentoni high school.lkn chanzo ni baada ya TAG kupewa usimamizi wa st mary na wao.kumchagua mama rwakatare ndio na yeye akafanya yake huko
 
Hivi njia nzuri ya ku uhifadhi wasia ni ipi?

Safe Deposit Box, cabinet locker, Kwa msimamizi, sehemu za kutunza nyaraka, Wakili (hapo inabidi uwe makini sana), Benki.

Popote unapoona ni salama kwako. Muhimu kumwambia mtu mmoja unayemwamimi
 
VITA ya kugombea mali za aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God - Mlima wa Moto, Marehemu Mchungaji Getrude Rwakatare sasa imeshika kasi huku ikizidi kuwagawa watoto wake.

Taarifa za kuwepo kwa vita hii zimekuja ikiwa ni miezi kadhaa baada ya mtoto mkubwa wa kiume wa Marehemu Rwakatare, anayefahamika kwa jina la Tibe Kenneth Rwakatare kumuandikia barua Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, akimueleza jinsi ndugu zake wanavyokiuka sheria kwa kutenda makosa ya jinai, akiwatuhumu kughushi nyaraka za mauzo ya baadhi ya mali za marehemu mama yake, Mchungaji Rwakatare.

Tibe Kenneth Rwakatare aliandika barua hiyo Disemba 31, 2021 ikiwa na kichwa cha maneno kinachosomeka ‘mauzo batili plot no 259 Udindifu Bagamayo.’

Katika barua hiyo, Tibe aliandika kumweleza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa uuzwaji wa kiwanja hicho umehusisha nyaraka za kughushi pamoja na kutolipwa kwa kodi stahiki za Serikali.

Akithibitisha kuandika barua hiyo, Tibe aliiambia Tanzania PANORAMA Blog kuwa amedhulumiwa haki yake na ndugu zake hivyo hakuwa na jingine zaidi ya kuandika barua hiyo.

Wakili kiongozi wa Kampuni ya Uwakili ya Haki Kwanza Advocates, Alloyce Komba ambaye ametoa ufafanuzi kuhusu tuhuma zilizotolewa na Tibe dhidi ya ndugu zake, amesema adhabu itakayowakabili watuhumiwa wakibainika mahakamani kutenda jinai hiyo ni kifungo.

“Kosa la kughushi, adhabu yake iwapo mahakama ikimtia hatiani mtu kwa ushahidi usio na shaka yoyote ni kufungwa kwa mujibu wa kifungu cha 337 cha sheria ya kanuni za adhabu, sura ya 16 ya sheria za Tanzania, toleo la 2019.

“Mtu anapaswa kuripoti polisi kosa lolote la jinai linalofanywa na mtu yoyote ili mradi awe na ushahidi wa kutosha.

“Ni kosa pia kunyamazia kosa la jinai. Ndiyo maana mtu hukosa kwa kutenda (commission) au kutotenda (omission), mfano kutomzuia mtoto kutumbukia kisimani wakati unaona anacheza karibu na kisima,” alisema Wakili Komba.

Mwanasheria mwingine aliyezungumza na PANORAMA kwa sharti la jina lake kuhifadhiwa alisema tuhuma zilizotolewa na Tibe dhidi ya ndugu zake ni nzito na iwapo zitathibitika mahakamani hawatakwepa mkono wa sheria.

“Sheria zipo lakini inashangaza watu wanatenda makosa ya makusudi kama haya ambayo adhabu yake ni kali.

“Huyu anayewatuhumu wenzake naye hayuko salama kwa sababu ni wazi anajua vema jinsi ndugu zake walivyotenda hiyo jinai, walivyoghushi kwa sababu ni ndugu zake hivyo alipaswa kutoa taarifa polisi.

“Sasa inashangaza kijana msomi kukaa kimya huku akijua kuna jinai inafanyika. Kwa vile kalipeleka kwa waziri tumpe nafasi ya kulifanyia kazi,” alisema.

Kwa mujibu wa kifungu cha 338 cha sheria ya kanuni ya adhabu, sura ya 16 ya sheria za Tanzania, toleo la 2019 ambayo Tanzania PANORAMA Blog imeiperuzi inaeleza kuwa mtu akibainika mahakamani kwa kughushi wosia, hati za umiliki ardhi, hundi n.k adhabu yake ni kifungo cha maisha jela.

Hilo likiwa halijapoa, mtoto mwingine wa kiume wa Marehemu Mchungaji Rwakatare anayefahamika kwa jina la Muta Robert Rwakatare ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) alizungumza na mwandishi wa Tanzania PANORAMA Blog na kumshutumu ndugu yake Tibe Kenneth Rwakatare kwa kutwaa kimabavu Shule ya Sekondari ya St. Mary’s International School, Dodoma Campus ambayo ni mali waliyoachiwa na marehemu mama yao.

Muta alieleza kuwa shule hiyo ni miongoni mwa shule zilizokuwa zikimilikiwa na Marehemu Mchungaji Rwakatare enzi za uhai wake lakini hivi sasa Tibe imeibadilisha jina na kutwaa umiliki wake.

Alisema ikiwa chini ya umiliki wa mama yao, ilikuwa ikijulikana kwa jina la St. Mary’s International School, Dodoma Campus, lakini sasa baada ya kubadilishwa jina inafahamika kwa jina la St. Mary’s Dodoma.

Muta alisema Tibe sasa anachukua mapato yote ya shule hiyo na eneo ilipojengwa nalo amelibadilisha jina na kuweka la kwake.

Watu walio karibu na familia hiyo wameeleza kuwa chanzo cha mzozo wa umiliki wa shule hiyo baada ya Marehemu Mchungaji Rwakatare kufariki ni mmoja wa watoto wake kuwazunguka wenzake na kuhamisha fedha zote zilizokuwa kwenye akaunti ya shule kwenda akaunti yake binafsi na pia akaanza kuchukua mapato yote ya shule hiyo.

Kwamba baada ya hilo kubainika, Tibe aliamua kuitwaa shule hiyo, akaibadilisha jina na majina ya akaunti za benki, hatua ambayo sasa inalalamikiwa na ndugu zake.

“Huyu ndugu yetu anashangaza sana kuanza kuandika barua kwa viongozi wa Serikali akitutuhumu kwa kukiuka sheria za nchi, eti tunaghushi nyaraka wakati yeye ndiyo bingwa wa kughushi nyaraka kuanzia Brela mpaka ardhi na anayemtumia kufanya hizo kazi za kughushi anafahamika, ni kijana aliyesoma kwenye moja ya shule zetu. Anachotaka amiliki yeye mali zote za mama.

“Ana madudu mengi mno lakini sie hatujishughulishi naye matokeo yake akiona tunamzuia kuchukua kila kitu anatafuta huruma nje ya familia kwa kutuchongea serikalini.

“Amejimilikisha shule ya Dodoma na kuibadili jina na akaunti za benki wakati shule hiyo ina mkopo wa benki moja kubwa nchini. Wewe unaweza kubadili umiliki wa mali ambayo ina mkopo wa benki kweli? Muulizeni na yeye hilo kalifanikishaje?

“Anamiliki mali nyingi sana za mama ambazo mapato yake yote yanaingia mfukoni mwake na hakuna anayemsumbua lakini yeye jambo dogo tu analalamika na kuandika barua huku na kule.

“Tulipouza hizo ardhi nyingine na kugawana mbona hakusema lolote? Kamuulizeni anataka nini hasa maana shule aliyotupora baada ya kuibadilisha jina imeondolewa kwenye orodha ya mali za marehemu mama. Hivi sasa anaimiliki yeye bila ridhaa ya sisi ndugu wengine.

“Nyumba za kupangisha za marehemu mama, zile ‘Appartments’ za Tabata zaidi ya 25, vyumba vya biashara 20, kote anachukua kodi yeye na pia mgodi wa dhahabu Chunya nao kachukua lakini bado anatupiga vita,” alisema Muta.

Alipoulizwa Tibe kuhusiana na madai hayo alisema hana muda wa kuyazungumzia.

Tanzania PANORAMA inaendelea kumtafuta Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kulizungumzia hilo.

Source: Tanzania-Panorama
Ni vizuri sana kuandika urithi na kuita mkutano kujulisha urithi uliotoa( isiwe siri) kama mengi baada ya kuandika urithi, angeita kila muhusika na kuwajulisha , haya yote yadingetokea. Kama kupinga urithi, wangempinga marehemu wakati yuko hai
 
St mary sio shule zake mama alikuwa mwangalizi wa hzo shule akiwa TAg akipenda sana huduma ya kutembelea wanafunzi mashuleni na wkt huo akijifunza utumishi badae ndio alianzisha za kwake hzo za kentoni high school.lkn chanzo ni baada ya TAG kupewa usimamizi wa st mary na wao.kumchagua mama rwakatare ndio na yeye akafanya yake huko
TAG na mashule wapi na wapi.Tuwe kweli kama ni kipawa au karama TAG haina karama au kipawa cha mashule.

Sema tu labda mama Rwakatare alitumia tu makaratasi yao TAG kuanzisha shule kwa makubaliano fulani.Lakini kusema TAG eti ianzishe shule za hadhi ya hizo za St Mary's kuanzia majengo,quality ya Elimu nk ni uongo wa mchana kweupe .TAG hawana uwezo huo.Kwenye mashule huko uwezo hawana kabisa ni sifuri.
 
Ni kawaida ya mali za freemason kurudi kwao pindi mmiliki wake akishamaliza nao mkataba. Mali za freemason hazirithiki sababu huna mkataba nazo.Kwani za Kanumba bado zipo? Mtauza zote na pesa haikai itaisha tu na wanunuzi huwa ni member wa freemason kwa maana mali zao zina barcode kama sio member huwezi zimiliki. Barcodes inaconnect na kuzimu.
 
VITA ya kugombea mali za aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God - Mlima wa Moto, Marehemu Mchungaji Getrude Rwakatare sasa imeshika kasi huku ikizidi kuwagawa watoto wake.

Taarifa za kuwepo kwa vita hii zimekuja ikiwa ni miezi kadhaa baada ya mtoto mkubwa wa kiume wa Marehemu Rwakatare, anayefahamika kwa jina la Tibe Kenneth Rwakatare kumuandikia barua Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, akimueleza jinsi ndugu zake wanavyokiuka sheria kwa kutenda makosa ya jinai, akiwatuhumu kughushi nyaraka za mauzo ya baadhi ya mali za marehemu mama yake, Mchungaji Rwakatare.

Tibe Kenneth Rwakatare aliandika barua hiyo Disemba 31, 2021 ikiwa na kichwa cha maneno kinachosomeka ‘mauzo batili plot no 259 Udindifu Bagamayo.’

Katika barua hiyo, Tibe aliandika kumweleza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa uuzwaji wa kiwanja hicho umehusisha nyaraka za kughushi pamoja na kutolipwa kwa kodi stahiki za Serikali.

Akithibitisha kuandika barua hiyo, Tibe aliiambia Tanzania PANORAMA Blog kuwa amedhulumiwa haki yake na ndugu zake hivyo hakuwa na jingine zaidi ya kuandika barua hiyo.

Wakili kiongozi wa Kampuni ya Uwakili ya Haki Kwanza Advocates, Alloyce Komba ambaye ametoa ufafanuzi kuhusu tuhuma zilizotolewa na Tibe dhidi ya ndugu zake, amesema adhabu itakayowakabili watuhumiwa wakibainika mahakamani kutenda jinai hiyo ni kifungo.

“Kosa la kughushi, adhabu yake iwapo mahakama ikimtia hatiani mtu kwa ushahidi usio na shaka yoyote ni kufungwa kwa mujibu wa kifungu cha 337 cha sheria ya kanuni za adhabu, sura ya 16 ya sheria za Tanzania, toleo la 2019.

“Mtu anapaswa kuripoti polisi kosa lolote la jinai linalofanywa na mtu yoyote ili mradi awe na ushahidi wa kutosha.

“Ni kosa pia kunyamazia kosa la jinai. Ndiyo maana mtu hukosa kwa kutenda (commission) au kutotenda (omission), mfano kutomzuia mtoto kutumbukia kisimani wakati unaona anacheza karibu na kisima,” alisema Wakili Komba.

Mwanasheria mwingine aliyezungumza na PANORAMA kwa sharti la jina lake kuhifadhiwa alisema tuhuma zilizotolewa na Tibe dhidi ya ndugu zake ni nzito na iwapo zitathibitika mahakamani hawatakwepa mkono wa sheria.

“Sheria zipo lakini inashangaza watu wanatenda makosa ya makusudi kama haya ambayo adhabu yake ni kali.

“Huyu anayewatuhumu wenzake naye hayuko salama kwa sababu ni wazi anajua vema jinsi ndugu zake walivyotenda hiyo jinai, walivyoghushi kwa sababu ni ndugu zake hivyo alipaswa kutoa taarifa polisi.

“Sasa inashangaza kijana msomi kukaa kimya huku akijua kuna jinai inafanyika. Kwa vile kalipeleka kwa waziri tumpe nafasi ya kulifanyia kazi,” alisema.

Kwa mujibu wa kifungu cha 338 cha sheria ya kanuni ya adhabu, sura ya 16 ya sheria za Tanzania, toleo la 2019 ambayo Tanzania PANORAMA Blog imeiperuzi inaeleza kuwa mtu akibainika mahakamani kwa kughushi wosia, hati za umiliki ardhi, hundi n.k adhabu yake ni kifungo cha maisha jela.

Hilo likiwa halijapoa, mtoto mwingine wa kiume wa Marehemu Mchungaji Rwakatare anayefahamika kwa jina la Muta Robert Rwakatare ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) alizungumza na mwandishi wa Tanzania PANORAMA Blog na kumshutumu ndugu yake Tibe Kenneth Rwakatare kwa kutwaa kimabavu Shule ya Sekondari ya St. Mary’s International School, Dodoma Campus ambayo ni mali waliyoachiwa na marehemu mama yao.

Muta alieleza kuwa shule hiyo ni miongoni mwa shule zilizokuwa zikimilikiwa na Marehemu Mchungaji Rwakatare enzi za uhai wake lakini hivi sasa Tibe imeibadilisha jina na kutwaa umiliki wake.

Alisema ikiwa chini ya umiliki wa mama yao, ilikuwa ikijulikana kwa jina la St. Mary’s International School, Dodoma Campus, lakini sasa baada ya kubadilishwa jina inafahamika kwa jina la St. Mary’s Dodoma.

Muta alisema Tibe sasa anachukua mapato yote ya shule hiyo na eneo ilipojengwa nalo amelibadilisha jina na kuweka la kwake.

Watu walio karibu na familia hiyo wameeleza kuwa chanzo cha mzozo wa umiliki wa shule hiyo baada ya Marehemu Mchungaji Rwakatare kufariki ni mmoja wa watoto wake kuwazunguka wenzake na kuhamisha fedha zote zilizokuwa kwenye akaunti ya shule kwenda akaunti yake binafsi na pia akaanza kuchukua mapato yote ya shule hiyo.

Kwamba baada ya hilo kubainika, Tibe aliamua kuitwaa shule hiyo, akaibadilisha jina na majina ya akaunti za benki, hatua ambayo sasa inalalamikiwa na ndugu zake.

“Huyu ndugu yetu anashangaza sana kuanza kuandika barua kwa viongozi wa Serikali akitutuhumu kwa kukiuka sheria za nchi, eti tunaghushi nyaraka wakati yeye ndiyo bingwa wa kughushi nyaraka kuanzia Brela mpaka ardhi na anayemtumia kufanya hizo kazi za kughushi anafahamika, ni kijana aliyesoma kwenye moja ya shule zetu. Anachotaka amiliki yeye mali zote za mama.

“Ana madudu mengi mno lakini sie hatujishughulishi naye matokeo yake akiona tunamzuia kuchukua kila kitu anatafuta huruma nje ya familia kwa kutuchongea serikalini.

“Amejimilikisha shule ya Dodoma na kuibadili jina na akaunti za benki wakati shule hiyo ina mkopo wa benki moja kubwa nchini. Wewe unaweza kubadili umiliki wa mali ambayo ina mkopo wa benki kweli? Muulizeni na yeye hilo kalifanikishaje?

“Anamiliki mali nyingi sana za mama ambazo mapato yake yote yanaingia mfukoni mwake na hakuna anayemsumbua lakini yeye jambo dogo tu analalamika na kuandika barua huku na kule.

“Tulipouza hizo ardhi nyingine na kugawana mbona hakusema lolote? Kamuulizeni anataka nini hasa maana shule aliyotupora baada ya kuibadilisha jina imeondolewa kwenye orodha ya mali za marehemu mama. Hivi sasa anaimiliki yeye bila ridhaa ya sisi ndugu wengine.

“Nyumba za kupangisha za marehemu mama, zile ‘Appartments’ za Tabata zaidi ya 25, vyumba vya biashara 20, kote anachukua kodi yeye na pia mgodi wa dhahabu Chunya nao kachukua lakini bado anatupiga vita,” alisema Muta.

Alipoulizwa Tibe kuhusiana na madai hayo alisema hana muda wa kuyazungumzia.

Tanzania PANORAMA inaendelea kumtafuta Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kulizungumzia hilo.

Source: Tanzania-Panorama
Tatizo la familia zetu za Kitanzania ni hizi ukiwa na mali shida na ukikosa mali pia nishida haya sasa mamakafa watoto wanagombania mali hapo bado familia ndiyo inapokuwa ngumu.
 
Tibe amekuwa mtu wa matukio kitambo nilijua labda ameshakua. Kazi kweli kweli.
 
Hivi mtu Kama yule alishindwa kuacha hata maandishi kuhusu umiliki wa Mali endapo atatangulia mbele ya haki? Au alijua ataishi milele?
 
Back
Top Bottom