Vita ya kanisa vs freemason

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,123
FreeMason.jpg v C_Freemason_001.jpg



.
MCHEZO ULIVYOANZAAkizungumza na mapaparazi wetu juzikati, jijini Dar, Mchungaji Mwamkamba alisema awali alitoa matangazo na pia kutuma ujumbe mfupi wa simu ‘SMS’ kwa watu mbalimbali akiomba mchango wa fedha ili aweze kujenga kanisa lake, lakini bila matarajio yake, namba zake ziliangukia mikononi mwa watu hao.
“Nilitarajia kupanua kanisa langu hivyo nilihitaji mchango wa fedha kwa ajili ya ujenzi, nikatoa tangazo kwa watu mbalimbali pamoja na kutuma SMS kwa marafiki zangu.
“Siku moja nilipigiwa simu na watu nisiowajua, wakaniambia wanataka kukutana na mimi ili wanisaidie fedha za ujenzi wa kanisa langu.
“Nilikubali, nikaenda kukutana nao pale Ubungo. Walianza kunieleza jinsi walivyoamua kunisaidia kujenga hekalu la Mungu huku wakisema wananipa fedha za kutosha na kuagana na umaskini,” alisema Mchungaji Mwamkamba.
Aliendelea kudai kuwa watu hao walisema lengo lao ni kumpa kiasi chochote cha fedha ambacho kilikuwemo kwenye ‘brifkesi’ kwa ajili ya ujenzi huo.
“Waniliambia wananipa kiasi chochote cha fedha ninachokihitaji, lakini iwe siri yangu na wao, halafu wakasema waumini katika kanisa langu wataongezeka
pesaaa.jpg
Pesa za Freemason wanazo zitoa


MCHUNGAJI AZIDI KUFICHUA
“Wakaniambia wamefanya hivyo kwa watumishi wengi wa Mungu hapa Tanzania ambao kwa macho ya kawaida huwatambuliki kama ni wafuasi wa Freemason na wanafanya ishara na miujiza mingi huku makanisa yao yakiwa na idadi kubwa ya waumini.”APEWA MKATABA
Baada ya mazungumzo ya muda mrefu na kabla mchungaji huyo hajasema ndiyo au hapana, alipewa mkataba wenye maelekezo ya jinsi ya kujiunga ili aanze kula mema ya nchi na kuuaga umaskini kwa muda mfupi.
“Walinipa mkataba, una nembo ya Freemason, lakini wakaniambia ni lazima nibadili dini, nianze kuvaa nembo ya mwewe na nyoka na kumtoa kafara mke wangu au mwanangu nimpendaye kama sadaka ya shukrani kwa mungu wao,” alisema mchungaji.
AWACHOMOLEA WAZI
“Niliposikia masharti hayo, ghafla nilisikia uchungu moyoni, nikakataa, nilisimama haraka sana na kuondoka kwa mwendo wa haraka, kama nakimbia. Wakaanza kunizomea huku wakitoa ishara ya kuvunja vidole viwili ambayo ni moja ya alama za Freemason,” alisema mchungaji huyo.
KWA NINI NI VITA?
Hivi karibuni, Mchungaji wa Kanisa la Good News for All Nations, Mark Diganyeka alitoa alama za kuwatambua watumishi wa Mungu ambao ni waumini wa dini ya Freemason na kusema kuwa waumini wawe makini kuwabaini.
Miongoni mwa alama hizo alisema ni pamoja na kuvunja vidole kwa haraka wakati wakihubiri na kuvaa pete kubwa kwa ajili ya kufanyia miujiza wawapo madhabahuni.
Kwa tafsiri ya Mchungaji Diganyeka na hayo aliyokutana nayo Mchungaji Mwamkamba, ni dhahiri makanisa yameingiliwa na Freemason hivyo kuanza kutimia kwa yale maneno kwamba, imani hiyo itawavaa watumishi wa Mungu kabla ya kurudi kwa Yesu Kristo.
NI VITA... - Global Publishers

 
Hivi hawa Freemanson wao wanapataje pesa? Ni swali tu ndugu zangu nataka kujua msinishambulie!!!!

Tiba

hao ndio wanatengeneza pesa,viongoz wakuu wa kibenk,marais,wafanyabiashara wakubwa,wana nguvu ya kiuchumi na kiutawala,sasa watakosaje pesa?
 
FREEMASON = Wonderful marketing tool for UDAKU newspapers.

Nimeipenda hii.
Ni kweli sasa hivi vyombo vya habari hususani hivi....Vimebadilisha mfumo wao wa kuandika habari kutoka kuzungumzia habari za kishirikina na kuzigeuza kuwa habari za kifreemason.
 
Nimeipenda hii.
Ni kweli sasa hivi vyombo vya habari hususani hivi....Vimebadilisha mfumo wao wa kuandika habari kutoka kuzungumzia habari za kishirikina na kuzigeuza kuwa habari za kifreemason.

wanaangalia trend ya soko,,,kwa sasa watu wanaongea sana abt masoni so media za udaku zinalalia hukohuko na wanauza......
Wajinga ndio............
 
2b1ask1!!hakuna anayekufuata kukuomba ujiunge nao,njaa zako mwenyewe ndio zitakupeleka,hawa wachungaji wanatafuta publicity,kwa kutumia jambo ambalo wanatambua wazi kuwa wengi wa waumini wao hawana uelewa wa kutosha juu yake,uelewa ambao pia yaweza kuwa vigumu kwetu sote kuupata,hata huyo mchungaji mwenyewe.
 
2b1ask1!!hakuna anayekufuata kukuomba ujiunge nao,njaa zako mwenyewe ndio zitakupeleka,hawa wachungaji wanatafuta publicity,kwa kutumia jambo ambalo wanatambua wazi kuwa wengi wa waumini wao hawana uelewa wa kutosha juu yake,uelewa ambao pia yaweza kuwa vigumu kwetu sote kuupata,hata huyo mchungaji mwenyewe.
wapuuzi sana wanafananisha ushirikina na freemason wachungaji njaa sana
 
Walete pesa hizo kwangu nazitaka
Utajiunga nao ? Watakupatia pesa ila masharti yao ni mazito kama una mke wako au mtoto wako au mama yako au baba yako au kaka yako au dada yako lazima umtoe Sadaka ndipo upate kuwa FreeMason uko teyari kuwa Mwanachama wa FreeMason mkuu Baba V?
 
i hate freemansons staki hata kuwaona maalama yao mana yananikumbusha adhabu za mwisho wa dunia u karibu wakati mi bado natamani kula lager dame them
 
Back
Top Bottom