Vita ijayo mashariki ya kati

Imebidi niandike makala hii baada ya tukio la kihistoria la siku tatu zilizopita juu ya anga ya Israel, na kuona kuwa huenda wengi hapa hawatakuwa na nyenzo au taarifa zitakazowasaidia kuli-analyse ipasavyo tukio hilo. Ni dhahiri kuwa SAI iliyoweza kupenya mazindiko ya anga (radar) ya Israel yasiyo na mfano popote duniani, na kusafiri kwa zaidi ya saa tatu hadi kwenye ncha ya vituo vya nuklia vya Israel....hii si hatua ndogo hasa ukiangalia uwezo mkubwa wa Israel na Marekani.
Ni dhahiri, baada ya bw Nasrallah kukiri kuwa ni Hizbullah kwa msaada wa Iran ndio waliotuma UAV, au SAI (Unmanned Aerial Vehicle- Safina ya Angani Ijiendeshayo = SAI), hakuna mtu atakayetia shaka sasa juu ya uwezo mkubwa wa Kiteknolojia walio nao Waajemi (Wa-Irani). Kwani kwa anayefuatia mambo, ni mara nyingi sasa Iran imetuonjesha weledi wake wa kiteknolojia. Chukua kwa mfano vita ya 2006 ya Hizbullah na Israel, ambapo kwa kweli Hizb ilimwendesha puta Mwisraeli kwa kuvunja vifaru maarufu vya Merkava (Kitanda cha Mungu:kutokana na wanavyoamini kuwa kina amani), na pia kuishambulia na kuichoma kwa kombora Meli ya kisasa zaidi Saur kwenye mwambao wa Lebanon, ambayo Waisrel waliamini hakuna yeyeto angeweza kuigusa na ndiyo maana wakaiegesha kando ya Lebanon.
Pili ni hekaya mashuhuri ya Iran kuitungua 5-generation SAI ya Marekani, Sentinel RQ-170 (the beast of Kandahar: mnyama wa Kandahar) ambayo haigunduliwi na Radar (kiasi iliposhiriki katika mauaji ya Osama huko Pakistan, Wapakistan hawakuwa na habari yeyote)--ambayo Wairan waliitungua kwa teknolojia bila ya kufyatua kombora na kuweza kuishusha ikiwa na mikwaruzo midogo dogo tu, jambo lililowatia aibu kubwa Wamarekani.
Tatu ni uwezo wa Wairan kupigana na kushinda virusi vikali vya Komputa (tarakilishi) viitwavyo Stuxnet na Flame bila ya msaada wa yeyote.
Nne kutuma kwao, kwa kulipiza kisasi, virusi vilivyofuta kumbukumbu zote za mashirika mawili makuu ya petroli katika Saudi Arabia na Qatar na kuambukiza komputa zaidi ya elfu 40 za mashirika hayo na hadi leo si Wamarekani wala Waarabu wameweza kuviondoa virusi hivyo, kiasi Leon Panetta, Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Alhamisi ilibidi awaite wafanyibiashara wakuu wa Marekani na kuwaonya juu ya vita ya kibemasa (tafsiri yangu ya cyberwarfare, kama mchezo wa kibemasa)!
Yote haya yananionesha kuwa Iran, katika baadhi ya nyanja za Teknolojia, iko mbele hata ya Marekani (Jambo hili si rahisi kulichuuza maana watu wengi bado twawaangalia wazungu kama miungu watu, hawashindwi!).
Natija ninayotoka nayo ni kuwa vita ijayo itageuza kabisa sura ya Mashariki ya Kati, ikiwa si dunia nzima. Kwa kweli kuna nchi zitafutika kabisa katika uso wa dunia zizaliwe nyingine mpya- yaani haidhuru eneo litakuwepo lakini mfumo mzima kama tunavyoujua sasa hautakuwepo. Mithili ya yaliyotokea baada ya vita kuu za dunia ya kwanza na ya pili na vita vya hivi karibuni vya Balkani, ambapo nchi mpya zilizuka. Jambo muhimu zaidi, mfumo wa dunia 'world sytem' kama tunavyoujua hivi sasa, nao pia utatoweka.
Jee, una idea nchi gani zitatoweka na zipi zitabakia?

Ndugu, unachokiamini kamwe hakitatokea. Kumbuka vita vya siku sita, Israel pia ilionekana kuwa dhaifu, what happened? Mungu atalilinda taifa lake siku zote hata mbele ya mwisho wa dunia hii! Mungu si mwanadamu hata aseme uongo, na kila alichomuahidi Ibrahim, Isaka na Israel kitatimizwa.
 
uSIWASIFIE HISBOLLAH KWA SABABU HISBOLLAH wao hawavai uniform za jeshina kama wanavaa uniform basi wasingekuwepo duniani! Wao huvaa kiraia na huja kama raia wema huku wameficha siraha, sasa Israel ni Taifa huru na linaloheshimu utu wa mtu, hivyo hawawezi kumlenga mtu asiye na nguo za kijeshi wakati wanapigana.

Halafu nawashukuru sana watanzania wanaounga mkono Israel. CCM na serikali yake walitulazimisha sana kuichukia Israel wakati wa ukomunisti. Leo hii watanzania tunajua ukweli kuwa hiyo yote ilikuwa ni chuki ya bure ili kuwaliwaza waarabu na azama zao za kutaka kuiteketeza israel.

Mungu ibariki Israel! shemaa alehemu alehemu adonai! maranataaa maranataaa!

Are u sure Israel ineheshimu utu wa mtu? Umewahi kufika Palestina na kuona vile inavyowatendea Wapalestina?
Apartheid imekufa Afrika kusini lakini inashamiri Israel.
 
uSIWASIFIE HISBOLLAH KWA SABABU HISBOLLAH wao hawavai uniform za jeshina kama wanavaa uniform basi wasingekuwepo duniani! Wao huvaa kiraia na huja kama raia wema huku wameficha siraha, sasa Israel ni Taifa huru na linaloheshimu utu wa mtu, hivyo hawawezi kumlenga mtu asiye na nguo za kijeshi wakati wanapigana.

Halafu nawashukuru sana watanzania wanaounga mkono Israel. CCM na serikali yake walitulazimisha sana kuichukia Israel wakati wa ukomunisti. Leo hii watanzania tunajua ukweli kuwa hiyo yote ilikuwa ni chuki ya bure ili kuwaliwaza waarabu na azama zao za kutaka kuiteketeza israel.

Mungu ibariki Israel! shemaa alehemu alehemu adonai! maranataaa maranataaa!

Mara nyingi nashangazwa na wale wanaoishabikia Israel. Kwa sabu ikiwa ni kwa sababu za kidini, Waisraeli ni Wayahudi si Wakristo na wala hawapendi Ukristo.
Inabakia labda kwa sababu za kuwachukia tu Waarabu kwa vile aidha ni Waislamu (hii pia si sahihi, Waarabu wengi pia ni Wakristo huko Palestina, Lebanon, Syria na Iraq) au kwa sababu za Kihistoria na hadithi za utumwa- ambapo kwa wasomi, tunajua biashara kuu ya utumwa ilifanywa na Mayahudi 100%. Meli zote za ufukwe wa Mashariki wa Marekani ambazo zilikuwa ndio zinasafirisha watumwa, 99% zilikuwa zinamilikiwa na Wayahudi isipokuwa marubani ni Wa Scot na wengine. Mwarabu alikuwa mchuuzi tu kama walivyokuwa wafalme wa Kiafrika.
Waisraeli pia ni ma- racist wakubwa wa watu weusi. Umesahau Ehud Barak aliitukana Tanzania na akakataa kuomba msamaha? Au hujaskia Israel ilikuwa inaisaidia Afrika Kusini ya Ubaguzi kutengeneza bomu la nuklia? Wadhania nani walikuwa wakusudiwa kuteketezwa, Waeskimo?
Ndiyo maana napenda sana mtu anayesapoti Israeli anieleze sababu zake: huenda akawa na sababu nzuri na mimi sizijui. Jee, waweza kunielimisha ndugu?

Kuhusu uniform za Hizbollah, tafadhali, kabla ya kuzungumza cheki fact zako. Hizi hapa tena mpya za mwaka huu 2012:

Hezbollah is getting close to be looks like Marines in new uniforms 2012 !!! - YouTube
 
Ktk Top 10 ya majeshi yenye nguvu duniani,israel ipo na cha kushangaza ina wanajeshi wachache kupindukia,kombora dogo kuliko yote duniani limevumbuliwa na israel mwaka huu na wamemuuzia teknolojia mrusi kombora lenyewe lina uzito wa kilo nne na ni dogo kama rula na effect zake ni kama kombora linalobebwa na magari makubwa ya kijeshi...toa udini wako hv ufikirii kwa middle east nchi zinazoizunguka israel zikiweka silaha chini amani itakuja,ila israel akiweka silaha chini kifo kitamjia,for years wamemshindwa,sasa subiri soon uone iran itakavyobamizwa baada ya hapo mataifa ya kiarabu pamoja na urusi watakapovamia israel na kuharibiwa kabla ya kuingia mpinga kristo

Mkuu, moshi bar kwa uncle wazima?
 
Wewe pimbi mwezako kajitahidi instead of give him credits unamcrush,au kwa vile amewasifia wa iran,angemsifia cameroon naona kile kimdudu ulichonacho cha shamran kinge kushtuka ungefunga jf uende ukakinyamazishe.
 
Nyie wagalatia,kama mnaona iran ni cha mtoto,mbona huyo basha wenu mu esrael chupi imembana,ana mbembeleza bi mkubwa (u.s.a),wakati mwenzake amesha upima mziki akauona hauchezeki.nyie subirini vita na hawa ma gardener wetu wanyasa tuwatoe nishai.
 
Mungu wa Israe hashindwi,sasa sijui ninyi mtakimbilia wapi,maana nyie ndo itabidi mfutike kataika ramani ya Dunia
 
Mungu wa Israe hashindwi,sasa sijui ninyi mtakimbilia wapi,maana nyie ndo itabidi mfutike kataika ramani ya Dunia
Sa Mungu wa Israel sio ndo Mungu wa Warabu na Wafrika au kuna Mungu gani tena :biggrin:
 
Niseme kwa ufupi sana kwa sababu maalum. Nimewahi kushiriki kwenye technology panel ya Pentagon ambapo tulishirikiana kwa karibu sana na IDF. Inabidi tukubali kuwa wenzetu wako mbali sana; uwezekano wa Hizbollah au Iran kupata Technolgy ya Drone au long range missiles ni mambo waliyokwisha yaona zamani na kazi iliyokuwa mbele yao ni namna ya kuwadhibi; yaani walikuwa wanatafuta namna ya kuwadhibiti wairani na hizbollah kabla hata hao mahasidi wao hawajafikia uwezo huo. Nina wasiwasi sana na kila sababu ya kuamini kuwa iwapo Irani au nchi yoyote eneo la mashariki ya Kati itajipatia silaha hizo za nyukulia na ikajulikana kuwa ziko wapi basi silaha hizo "zitawalipukia" wenyewe ! Inabidi wawe makini sana na namna wanavyopata teknologia hatari za namna hiyo
 
Israel haitafutika katika uso wa dunia hata siku moja, na hakuna nchi itakayouweza muziki wa hawa jamaa. Kuharibiwa kwa Merkava ni moja kati ya "athiriko la kijeshi katika vita" na ndio maana halisi ya ile operation ijulikanayo kama "donna attack"
 
Aloo, katoe upuuzi huu kwenye mahafali ya dini yako siyo hapa mbele ya watu wazima wenye akili. Mungu huyu anayechagua aliowaumba ni yupi huyu. Kama hakuwataka wengine kwa nini aliwaumba, ebo?
Vitabu vyao ndo vinawadanganya vile :biggrin:
 
Haya ma nchi ya middle east mapumbavu tupu. Mambo yao yote lazima waweke kwamba ni vita vya kimungu, hata kama niya kishenzi kama kuunda bomu la nuklia mahala hata Mungu ahusiki. Hawana uwezo wa kuunda silaha yeyote ya maana wanatengeneza rejects zilizopitwa na wakati. Subiria aibu watakayo ipata watabaki kuwaita watu wasio kuwa na raha ya kuishi wajilipue. Hiyo ndio silaha yao inayo tishia amani kidogo.
 
Hizi hoja mgeweka imani pembeni ndo mgejadili kwa utulivu.
Israel pekeyake hawezi kumpiga muirani.ni mpaka america,uk,frech ,italy washiriki na hapa enter russia kila kitu kinafikia THE END.
 
Page not found

kama hujapata hiyo.naomba uende kwenye hii site.ni site ya maveterani wa shirika la kijasusi la israel mossad.humo utaipata hiyo cyber attack na issue ya hizbulah drone na wanavomlaumu obama kwa kutokubali kuipiga iran kwa sasa.google Debka.com english.
 
Please ongea ukweli, nikwamba hiyo UAV au SAI ilionekana mapema wakati inakaribia southern border ya Israel nawao walikuwa tayari washajua na hawakutaka kuitungua mapema vile sababu ya makazi ya watu, wenzetu wanajali utu, hivyo walisubiri mpaka eneo lisilo na makazi ya watu ndipo waitungue.

vita ya hizbullah na Israel, Hizbullah wanajichanganya kwenye makazi ya watu-walebanoni, raia, kwahiyo ulitaka IDF iue raia??

Unajua nini juu ya DEMONA REACTOR?? angekuwepo Rais ambaye marehemu, Rais Kennedy angekueleza na kwanini hadi leo rais anayeingia madarakani wa marekani lazima aiheshimu Israel??

Tusiwe washabiki wa upande wowote!

israel iko na multilayered airdefence system,kama rada,patriot,iron dome etc.
Hiyo system wameiweka kucounter missile attack toka nje ya israel.hivyo iko designed kushootdown incoming missile attack au warplane.
Kilichotokea ile drone speed yake iko below missile speed au ndege ya mashambulizi.SYSTEM IKASHINDWA KUDETECT hiyo drone wamekuja shituka drone inaambaa ambaa juu ya miji ya israel ikielekea jangwa la negev ilipo DIMONA.
Dimona ndo zilipo silaha za nuclear za israel.
Wakataka kuiteka kwa kielectroniki.hizbulah wakagundua,ilianza ligi ya kuigombea drone hiyo kati ya timu ya cyberwarfare wa israel na hizbula ilichukua kama nusu saa.
Baada ya israel kushinda kuishusha chini ikiwa nzima ndo wakatuma jetfighter wakai tungua.
 
Ndio shida ya Watz..badala mchambue hoja kwa uvivu wa kufikiri mlionao mnaona ni sawa kuanza kutoa mitusi..sasa hizo akili au matope?!! hoja hupingana na hoja sio matusi...
 
Back
Top Bottom