Vita ijayo mashariki ya kati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita ijayo mashariki ya kati

Discussion in 'International Forum' started by Sijali, Oct 13, 2012.

 1. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,057
  Likes Received: 411
  Trophy Points: 180
  Imebidi niandike makala hii baada ya tukio la kihistoria la siku tatu zilizopita juu ya anga ya Israel, na kuona kuwa huenda wengi hapa hawatakuwa na nyenzo au taarifa zitakazowasaidia kuli-analyse ipasavyo tukio hilo. Ni dhahiri kuwa SAI iliyoweza kupenya mazindiko ya anga (radar) ya Israel yasiyo na mfano popote duniani, na kusafiri kwa zaidi ya saa tatu hadi kwenye ncha ya vituo vya nuklia vya Israel....hii si hatua ndogo hasa ukiangalia uwezo mkubwa wa Israel na Marekani.
  Ni dhahiri, baada ya bw Nasrallah kukiri kuwa ni Hizbullah kwa msaada wa Iran ndio waliotuma UAV, au SAI (Unmanned Aerial Vehicle- Safina ya Angani Ijiendeshayo = SAI), hakuna mtu atakayetia shaka sasa juu ya uwezo mkubwa wa Kiteknolojia walio nao Waajemi (Wa-Irani). Kwani kwa anayefuatia mambo, ni mara nyingi sasa Iran imetuonjesha weledi wake wa kiteknolojia. Chukua kwa mfano vita ya 2006 ya Hizbullah na Israel, ambapo kwa kweli Hizb ilimwendesha puta Mwisraeli kwa kuvunja vifaru maarufu vya Merkava (Kitanda cha Mungu:kutokana na wanavyoamini kuwa kina amani), na pia kuishambulia na kuichoma kwa kombora Meli ya kisasa zaidi Saur kwenye mwambao wa Lebanon, ambayo Waisrel waliamini hakuna yeyeto angeweza kuigusa na ndiyo maana wakaiegesha kando ya Lebanon.
  Pili ni hekaya mashuhuri ya Iran kuitungua 5-generation SAI ya Marekani, Sentinel RQ-170 (the beast of Kandahar: mnyama wa Kandahar) ambayo haigunduliwi na Radar (kiasi iliposhiriki katika mauaji ya Osama huko Pakistan, Wapakistan hawakuwa na habari yeyote)--ambayo Wairan waliitungua kwa teknolojia bila ya kufyatua kombora na kuweza kuishusha ikiwa na mikwaruzo midogo dogo tu, jambo lililowatia aibu kubwa Wamarekani.
  Tatu ni uwezo wa Wairan kupigana na kushinda virusi vikali vya Komputa (tarakilishi) viitwavyo Stuxnet na Flame bila ya msaada wa yeyote.
  Nne kutuma kwao, kwa kulipiza kisasi, virusi vilivyofuta kumbukumbu zote za mashirika mawili makuu ya petroli katika Saudi Arabia na Qatar na kuambukiza komputa zaidi ya elfu 40 za mashirika hayo na hadi leo si Wamarekani wala Waarabu wameweza kuviondoa virusi hivyo, kiasi Leon Panetta, Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Alhamisi ilibidi awaite wafanyibiashara wakuu wa Marekani na kuwaonya juu ya vita ya kibemasa (tafsiri yangu ya cyberwarfare, kama mchezo wa kibemasa)!
  Yote haya yananionesha kuwa Iran, katika baadhi ya nyanja za Teknolojia, iko mbele hata ya Marekani (Jambo hili si rahisi kulichuuza maana watu wengi bado twawaangalia wazungu kama miungu watu, hawashindwi!).
  Natija ninayotoka nayo ni kuwa vita ijayo itageuza kabisa sura ya Mashariki ya Kati, ikiwa si dunia nzima. Kwa kweli kuna nchi zitafutika kabisa katika uso wa dunia zizaliwe nyingine mpya- yaani haidhuru eneo litakuwepo lakini mfumo mzima kama tunavyoujua sasa hautakuwepo. Mithili ya yaliyotokea baada ya vita kuu za dunia ya kwanza na ya pili na vita vya hivi karibuni vya Balkani, ambapo nchi mpya zilizuka. Jambo muhimu zaidi, mfumo wa dunia 'world sytem' kama tunavyoujua hivi sasa, nao pia utatoweka.
  Jee, una idea nchi gani zitatoweka na zipi zitabakia?
   
 2. M

  Masauni JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2012
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  P.U.M.B.A.V.U Hujuhi unachoongea wewe.
   
 3. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Umeongea kiushabiki zaidi,print copy za kutosha na ukazisambaze kwenye misikiti!
   
 4. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  una madharau ya kiseng,e,sasa kama hajui analoongea hebu lete point yako kuhusiana na vita inayokuja
   
 5. M

  Masauni JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2012
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haukuna nchi itakayoweza kuipiga Israel. Teknolojia ya Israel na iran ni sawa na kufananisha mbingu na ardhi, Israel iko mbali sana kuliko Irani, Hilo jamaa linaongea kishabiki
   
 6. Root

  Root JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,242
  Likes Received: 12,961
  Trophy Points: 280
  Iran inatapa tapa sasa waulize dollar ecchange ni rial ngapi,pia detection ya UAV inamaana radar iko active na kama ingekuwa weak hakika isingekuweza detect.
  Pili tuweke ushabiki pembeni cyber war najua iko active sio kiasi cha wao kushindwa toa hao virus

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,349
  Likes Received: 19,530
  Trophy Points: 280
  makala ya kujifurahisha. Chemical ali type.
   
 8. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mbona haya yote unayoyasema hapa inaonekana unayafahamu wewe peke yako? Hayajatangazwa kwenye vyombo vya habari vya kiarabu (mashariki ya kati) wala vya magharibi. wewe umeyatoa wapi? Au ndivyo mnavyotiana moyo mkiwa huko misikitini?
   
 9. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Unachomekwa vijiti? Mbona unaandika kama unawashwa? Mleta mada amejitahidi kuandika anachokiona yeye kuhusu mashariki ya kati, saa zingine sio lazima uchangie...
   
 10. Fyong'oxi

  Fyong'oxi JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Msimvamie mtoa mada kwa matusi ya kishabiki, mimi nadhani mngemuomba alete link ya hizo information, na kama ni mambo ya millitary confidential alizipataje.Wakati mwingine sio lazima ziletwe Topic zinazowafurahisha tuu!
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Prisoner exchange admits Israeli defeat in 2006 Lebanon war

  Lebanese government noted correctly that Hezbollah pushed Israel to the very same terms it refused before the 2006 Israeli war with Lebanon. Hezbollah was asking Israel to release Samir Kuntar. After Israel’s repeated refusals Hezbollah attacked an IDF outpost, took Regev and Goldwasser prisoners, and now exchanged their bodies for Kuntar.
  Had Israeli government released Kuntar in early 2006, more than a hundred Israelis including Regev and Goldwasser would have been alive.

  Source: Israeli News: Prisoner exchange admits Israeli defeat in 2006 Lebanon war
   
 12. kirumonjeta

  kirumonjeta JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 3,083
  Likes Received: 492
  Trophy Points: 180
  Mhhh!!!tunasubiri wenye data wazilete hapa tupime wapi pazito
   
 13. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,544
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Utamu njoo uwongo njoo.
   
 14. GREAT VISIONAIRE

  GREAT VISIONAIRE Senior Member

  #14
  Oct 13, 2012
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 179
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ktk Top 10 ya majeshi yenye nguvu duniani,israel ipo na cha kushangaza ina wanajeshi wachache kupindukia,kombora dogo kuliko yote duniani limevumbuliwa na israel mwaka huu na wamemuuzia teknolojia mrusi kombora lenyewe lina uzito wa kilo nne na ni dogo kama rula na effect zake ni kama kombora linalobebwa na magari makubwa ya kijeshi...toa udini wako hv ufikirii kwa middle east nchi zinazoizunguka israel zikiweka silaha chini amani itakuja,ila israel akiweka silaha chini kifo kitamjia,for years wamemshindwa,sasa subiri soon uone iran itakavyobamizwa baada ya hapo mataifa ya kiarabu pamoja na urusi watakapovamia israel na kuharibiwa kabla ya kuingia mpinga kristo
   
 15. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Thread inaongea ukweli mtupu, na habari zote zinapatikana :poa
   
 16. Elijah

  Elijah JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 1,671
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  kabla ya kuingia mpinga kristo??hebu dadavua
   
 17. Elijah

  Elijah JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 1,671
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Inawezekana kweli kuwa muisrael ameishiwa nguvu na hana mvuto tena na ushawishi kwenye jumuia za kimataifa,hilo ni kawaidia kabisa.Mrusi naye halikadharika keshachoka.Sasa tunazungumzia EU ambaye juzi kapewa noble price,ni ukweli usiopingika kuwa amani ya dunia sasa itashikiliwa na muungano wa nchi za ulaya,nchi za mashariki ya kati zitalazimika kufuata mkumbo na zitatii kwa kulazimishwa na america chini ya utawala wa roma
   
 18. Kilimo

  Kilimo JF-Expert Member

  #18
  Oct 13, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 780
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Please ongea ukweli, nikwamba hiyo UAV au SAI ilionekana mapema wakati inakaribia southern border ya Israel nawao walikuwa tayari washajua na hawakutaka kuitungua mapema vile sababu ya makazi ya watu, wenzetu wanajali utu, hivyo walisubiri mpaka eneo lisilo na makazi ya watu ndipo waitungue.

  vita ya hizbullah na Israel, Hizbullah wanajichanganya kwenye makazi ya watu-walebanoni, raia, kwahiyo ulitaka IDF iue raia??

  Unajua nini juu ya DEMONA REACTOR?? angekuwepo Rais ambaye marehemu, Rais Kennedy angekueleza na kwanini hadi leo rais anayeingia madarakani wa marekani lazima aiheshimu Israel??

  Tusiwe washabiki wa upande wowote!
   
 19. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #19
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,796
  Likes Received: 36,820
  Trophy Points: 280
  Busara ni jambo la muhimu sana,
  Sijaona sababu ya wewe kupanic kiasi hichi.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 20. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #20
  Oct 13, 2012
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Udini unaingiaje hapa
   
Loading...