Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,589
- 1,679
- Thread starter
- #61
Niseme kwa ufupi sana kwa sababu maalum. Nimewahi kushiriki kwenye technology panel ya Pentagon ambapo tulishirikiana kwa karibu sana na IDF. Inabidi tukubali kuwa wenzetu wako mbali sana; uwezekano wa Hizbollah au Iran kupata Technolgy ya Drone au long range missiles ni mambo waliyokwisha yaona zamani na kazi iliyokuwa mbele yao ni namna ya kuwadhibi; yaani walikuwa wanatafuta namna ya kuwadhibiti wairani na hizbollah kabla hata hao mahasidi wao hawajafikia uwezo huo. Nina wasiwasi sana na kila sababu ya kuamini kuwa iwapo Irani au nchi yoyote eneo la mashariki ya Kati itajipatia silaha hizo za nyukulia na ikajulikana kuwa ziko wapi basi silaha hizo "zitawalipukia" wenyewe ! Inabidi wawe makini sana na namna wanavyopata teknologia hatari za namna hiyo
Hapa unazungumza kitu kinachowezekana sana. Kwa kweli Wairan pia wanajua uwezo mkubwa wa Waisraeli na nyuma yake Wamarekani. Isipokuwa falsafa ya Iran juu ya ulinzi ni ya kujitegemea kwa kutengeneza zana zao wenyewe. Ingawaje itawachukua muda mrefu kufikia kiwango cha nchi hizo mbili, isipokuwa kujitegemea katika kuunda silaha kwenyewe ni 'deterrence' kwa vile itakuwa vigumu kwa nchi nyingine ku 'decipher' mali yao. Wairan hawa waamini Warusi. Urusi pia ipo chini ya influence ya Wayahudi (fuatilia majina ya wale walio katika shirika la Rosoboronexport), vile vile natumaini wajua Urusi imekataa kuiuzia Iran makombora ya S-300 ingawaje Iran ilikwishayalipia, kutokan na shinikizo za Israel na Marekani.
I am sure, Wairan nao they don't leave anything to chance. Labda hii ndiyo sababu hasa, kwa nini Israeli na Marekani haijaishambulia Iran hadi sasa. Ni kwa vile wanaogopa kupata surprises!