Visa vya CCM vyaanza kuonekana Dar es Salaam

yaani hii mijitu ina roho mbayaaa..
kama sura zao..
 
Sheria ni msumeno. TRA itakusanya kodi ya majengo kwa miji yote bila kujali chama kinachoongoza miji hiyo. Think positively mkuu.

Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) jijini Dar es Salaam vimeanza kufilisiwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mpango wa Serikali ya Rais John Magufuli kupoka vyanzo muhimu vya mapato ambavyo awali vilitumika kuendesha halmashauri za jijini humo, umekamilika na sasa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndiyo inayotarajiwa kuwa mbadala katika ukusanyaji mapato.

Vyama vinavyoumizwa na hatua hiyo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF) ambavyo ndivyo vilivyo na wabunge na madiwani Dar es Salaam.

Charles Kuyeko, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pia Diwani wa Kata ya Bonyokwa (CHADEMA) amesema, tayari manispaa yake imearifiwa kwamba, kodi ya majengo kwenye manispaa hiyo itakusanywa na TRA na sio manispaa kama ilivyokuwa awali.

Hatua hiyo anasema itazuia shughuli ama ahadi zao kutotekelezeka kwa namna ambavyo walitaka iwe huku akikosoa hatua hiyo na kuihusisha na uhasama wa kisiasa jijini humo.

Hata hivyo amesema, wapo kwenye mazungumzo na serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kwamba, serikali haioneshi dhamira ya kubadili msimamo wake.

Kuyeko amesema, ni vema serikali ikaachana na suala hilo kwani itakuwa chanzo cha kurudisha maendeleo nyuma na kuvuruga bajeti iliyopangwa na manispaa hiyo.

“Kwanza tunasikitishwa na hatua hiyo ambayo imeanza kutekelezwa baada ya Umoja wa Katiba ya Wananchi – UKAWA kuingia madarakani. Siku zote walikuwa wapi? Ni dhairi kuwa nia yao ni kutaka kuturudisha nyuma ili bajeti yetu ikwame.

“Kodi ya mapango ndio chanzo kikuu cha mapato katika kila wilaya ukiacha kodi za mabango na ushuru wa wafanyabiashara,” amesema Kuyeko.

Hata hivyo, utaratibu wa kukusanya kodi za majengo utaanza katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na baadaye kwenye manispaa zote.

Kuyeko amesema, manispaa yake imepanga kufikia bajeti ya Sh. 85 Bilion na zaidi kwa mwaka 2016/17 na kwamba kama serikali itatekeleza hatua yake ya kupoka kodi za majengo, itakuwa imevuruga bajeti hiyo.
 
Mpango Kabambe waja
Think loud . omba omba kutoka DODOMA ccm inakotawala wamekimbipa DAR ES SALAAM jiji linaloongozwa na UKAWA. Jiulize sasa mbona ccm mmeshindwa hata kuwasaidia watu Wa DODKMA mpaka wanakuja DAR jiji LA ukawa? Mwana habari huru hawa LUMUMBA hawana fikira au?
 
Hili suala linahusu halmashauri zote Tanzania, na ambazo nyingi zinaongozwa na Ccm. Inawezekana TRA wamejipanga zaidi kukusanya hii kodi kuliko halmashauri. Mtaa ninao kaa mimi huwa naambiwa nikalipe hii kodi kwa mtendaji wa mtaa aniandikie kirisiti cha makaratasi, baada ya kuona hivyo sijalipa toka 2010 na hakuna anayenigusa. Labda kwa sasa TRA watanifikia wachukue 27,000- yao
 
Huu ni uamuzi wa kukomoa upinzani ambao ni wananchi wameamua
 
Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) jijini Dar es Salaam vimeanza kufilisiwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mpango wa Serikali ya Rais John Magufuli kupoka vyanzo muhimu vya mapato ambavyo awali vilitumika kuendesha halmashauri za jijini humo, umekamilika na sasa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndiyo inayotarajiwa kuwa mbadala katika ukusanyaji mapato.

Vyama vinavyoumizwa na hatua hiyo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF) ambavyo ndivyo vilivyo na wabunge na madiwani Dar es Salaam.

Charles Kuyeko, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pia Diwani wa Kata ya Bonyokwa (CHADEMA) amesema, tayari manispaa yake imearifiwa kwamba, kodi ya majengo kwenye manispaa hiyo itakusanywa na TRA na sio manispaa kama ilivyokuwa awali.

Hatua hiyo anasema itazuia shughuli ama ahadi zao kutotekelezeka kwa namna ambavyo walitaka iwe huku akikosoa hatua hiyo na kuihusisha na uhasama wa kisiasa jijini humo.

Hata hivyo amesema, wapo kwenye mazungumzo na serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kwamba, serikali haioneshi dhamira ya kubadili msimamo wake.

Kuyeko amesema, ni vema serikali ikaachana na suala hilo kwani itakuwa chanzo cha kurudisha maendeleo nyuma na kuvuruga bajeti iliyopangwa na manispaa hiyo.

“Kwanza tunasikitishwa na hatua hiyo ambayo imeanza kutekelezwa baada ya Umoja wa Katiba ya Wananchi – UKAWA kuingia madarakani. Siku zote walikuwa wapi? Ni dhairi kuwa nia yao ni kutaka kuturudisha nyuma ili bajeti yetu ikwame.

“Kodi ya mapango ndio chanzo kikuu cha mapato katika kila wilaya ukiacha kodi za mabango na ushuru wa wafanyabiashara,” amesema Kuyeko.

Hata hivyo, utaratibu wa kukusanya kodi za majengo utaanza katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na baadaye kwenye manispaa zote.

Kuyeko amesema, manispaa yake imepanga kufikia bajeti ya Sh. 85 Bilion na zaidi kwa mwaka 2016/17 na kwamba kama serikali itatekeleza hatua yake ya kupoka kodi za majengo, itakuwa imevuruga bajeti hiyo.
ccmni taka ngumu
 
Mimi sioni tatizo hapo jee muheshimiwa ana mikakati gani kuhusu Tanzania kuwezesha kibiashara kwanza naona Hilo ndio muhimu na sisi wadogo siku zote twaonekana hatuna lakuchangia lakini mapato yatakujaje Bila ya wafanya biashara kunawiri na kuwa wengi hivyo ndio vyanzo vyamapato
 
Mimi licha ya nimpinzani lakini laukweli nalikubali yaani raisi wetu amefanya makubwa na mazuri kipindi kidogo tu mimi na mkubaali saaaaana tena saanaa
 
Back
Top Bottom