Visa vya CCM vyaanza kuonekana Dar es Salaam

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) jijini Dar es Salaam vimeanza kufilisiwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mpango wa Serikali ya Rais John Magufuli kupoka vyanzo muhimu vya mapato ambavyo awali vilitumika kuendesha halmashauri za jijini humo, umekamilika na sasa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndiyo inayotarajiwa kuwa mbadala katika ukusanyaji mapato.

Vyama vinavyoumizwa na hatua hiyo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF) ambavyo ndivyo vilivyo na wabunge na madiwani Dar es Salaam.

Charles Kuyeko, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pia Diwani wa Kata ya Bonyokwa (CHADEMA) amesema, tayari manispaa yake imearifiwa kwamba, kodi ya majengo kwenye manispaa hiyo itakusanywa na TRA na sio manispaa kama ilivyokuwa awali.

Hatua hiyo anasema itazuia shughuli ama ahadi zao kutotekelezeka kwa namna ambavyo walitaka iwe huku akikosoa hatua hiyo na kuihusisha na uhasama wa kisiasa jijini humo.

Hata hivyo amesema, wapo kwenye mazungumzo na serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kwamba, serikali haioneshi dhamira ya kubadili msimamo wake.

Kuyeko amesema, ni vema serikali ikaachana na suala hilo kwani itakuwa chanzo cha kurudisha maendeleo nyuma na kuvuruga bajeti iliyopangwa na manispaa hiyo.

“Kwanza tunasikitishwa na hatua hiyo ambayo imeanza kutekelezwa baada ya Umoja wa Katiba ya Wananchi – UKAWA kuingia madarakani. Siku zote walikuwa wapi? Ni dhairi kuwa nia yao ni kutaka kuturudisha nyuma ili bajeti yetu ikwame.

“Kodi ya mapango ndio chanzo kikuu cha mapato katika kila wilaya ukiacha kodi za mabango na ushuru wa wafanyabiashara,” amesema Kuyeko.

Hata hivyo, utaratibu wa kukusanya kodi za majengo utaanza katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na baadaye kwenye manispaa zote.

Kuyeko amesema, manispaa yake imepanga kufikia bajeti ya Sh. 85 Bilion na zaidi kwa mwaka 2016/17 na kwamba kama serikali itatekeleza hatua yake ya kupoka kodi za majengo, itakuwa imevuruga bajeti hiyo.
 
CCM iache siasa siasa za kukomoana kwenye mambo ya kimaendeleo maana haisaidii zaidi inabomoa ..
 
Uandishi wako unafaa kuuza magazeti. Sioni tatizo ili mradi fedha haitaingia katika hazina ya CCM bali ya taifa kwa manufaa ya wananchi. Kuyeko hajui kuwa kila zama na kitabu chake? Ajipange kuleta maendeleo kwa atakachokusanya.
 
Haya ndo mojawapo ya mambo huwa yanafanya watu wengi wenye uelewa waone, CCM haina jambo jipya zaid ya siasa tu, hii nchi ina matatizo sana kutoka itatuchua karne kama nne hiv, wakati nchi nyingine duniani zikielekea kwenye devolution, sis ndo kwanza tunaimarisha central system, sehemu kubwa ya mapato yanatakiwa yabaki halmashaur, serikalin ziende hela kidogo tu.
 
Hao hao TRA walishawahi kupewa kazi ya Kukusanya kodi ya Majengo kwa Mkoa wa Dar Es Salaam, lakini kwa nini kazi hiyo ilirejeshwa kwa halmshauri za Manispaa, mimi na wengine kama wapo, hatujui. Vilevile TRA miaka ya nyuma walikuwa wanakusanya kodi toka kwa makampuni/watu wanaofanya biashara ya michezo ya kubahatisha (bahati nasibu, Casinos etc). Baadaye Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ikaanza kukusanya hayo maduhuli na mapato yaliongezeka kwa kiwango kikubwa. Mimi nina mashaka kama kutakuwa na ufanisi wa makusanyanyo ya kodi ya majengo chini ya TRA. Nasubiri nione.
 
Walivyokuwa wanafisadi sasa wameona huduma za wananchi zitakuwa nzuri kwa kuwa mapato yataonekana wameamua kubana, CCM ni janga kuu.
 
Hili jambo ni la zamani sana na mimi as a banker back then niliwahi kufungua TRA Collection Account couple of years ago na tangu hapo watu wakawa wanaambiwa kulipia majengo bank lakini pesa ilikuwa haiingii kwenye account za Halmashauri bali za TRA.

Hata hivyo, I also know kuna baadhi ya Manispaa walikuwa wagumu kuachia ulaji... ilikuwa ni sawa na mishahara kwa maaskari!
 
Kwani sheria imebadilishwa lini? Na kwanini ni manispaa moja na siyo miji yote? Au nchi imeachwa kuongozwa na sheria inaongozwa kwa matamko? Hatufiki kokote kichumi kwani taratibu nyingi zinakiukwa kuukomesha upande fulani. Waziri mwenye dhamana akae chonjo kwani suala hili litamletea shida bungeni hasa akizingatia wabunge ni wajumbe kwenye vikao vya counsel vya miji na majiji. Je, wamepewa vyanzo vingine mbadala ili kucompasate mapato waliyotarajiwa? Tuache mihemko tufuate sheria na taratibu. Wabunge pingeni hili kwa nguvu zote. Badala ya tra kukusanya kodi ya majengo wakusanye vat kwa wenye nyumba za kupangisha.
 
akusanya nani WATAJUA WENYEWE wanainchi tunataka MAENDELEO TU ! Barabara zipitike,Maji 48 Hrs, UMEME wa kumwaga, papuchi ziwe bei chee, nk.
 
Back
Top Bottom