Visa vya CCM vyaanza kuonekana Dar es Salaam

Visa vya CCM vyaanza kuonekana Dar es Salaam

H

kuna haja gani ya kujadiliana na mtu asiyefikiri kama wewe? TRA itakusanya kodi za majengo nchi nzima au pale ambapo wapinzani wanaongoza halmashauri?

Kama kuna ujinga mkubwa mwanadamu anaweza kufanya basi ni kugoma kujifunza kutoka kwa wengine. Kama halmashauri mliyoiongoza kwa miaka leo inashikwa na mwingine, huku ni kutapatapa kuogopa kuwa watakusanya zaidi na mtaumbuka, na mbili mtashindwa kufanya propaganda. Nukta

Kama kweli wewe unajua kufikiri jibu basi maswali yangu ya kijinga niliyomuuliza mwanahabarihuru.Swali kwako ni moja tu, je kwa kufanya hivyo inavyotaka kufanya serikali ya ccm inavunja kifungu kipi cha katiba au sheria ipi? Maana ukilalamikia suala ambalo sheria inaliruhusu huku ukiwa na uwezo wa kufikiri basi wewe ni hayawani, ungekuwa hujui na labda huna tafakuri nzuri angalau ungekuwa mjinga tu
 
ama kweli ccm hawaishiwi vituko. kwani sheria inasemaje juu ya hilo? au siku hizi ccm wakiamka ni kubadilisha tu kwa jinsi wanavyojisikia? makubwa haya.

Umeuliza swali la maana sana kuhusu sheria. Pia umetoa hoja nzuri kwa njia ya swali kama ccm wanafanya wanavyojisikia. Labda pia ungeuliza nini nafasi ya vyama vya upinzani kuona ccm haiendeshi nchi kwa matakwa ya watu binafsi bali kwa kuzingatia katiba na sheria? Kulalamika? Kuwaelewesha wananchi ili wao waiwajibishe ccm au kutumia tukio hilo kutunga uongo na hisia za kuuburudisha mioyo za wafuasi wao mbumbumbu ambao kwao habari ni 'chama adui' yao kushindwa?
 
Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) jijini Dar es Salaam vimeanza kufilisiwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mpango wa Serikali ya Rais John Magufuli kupoka vyanzo muhimu vya mapato ambavyo awali vilitumika kuendesha halmashauri za jijini humo, umekamilika na sasa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndiyo inayotarajiwa kuwa mbadala katika ukusanyaji mapato.

Vyama vinavyoumizwa na hatua hiyo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF) ambavyo ndivyo vilivyo na wabunge na madiwani Dar es Salaam.

Charles Kuyeko, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pia Diwani wa Kata ya Bonyokwa (CHADEMA) amesema, tayari manispaa yake imearifiwa kwamba, kodi ya majengo kwenye manispaa hiyo itakusanywa na TRA na sio manispaa kama ilivyokuwa awali.

Hatua hiyo anasema itazuia shughuli ama ahadi zao kutotekelezeka kwa namna ambavyo walitaka iwe huku akikosoa hatua hiyo na kuihusisha na uhasama wa kisiasa jijini humo.

Hata hivyo amesema, wapo kwenye mazungumzo na serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kwamba, serikali haioneshi dhamira ya kubadili msimamo wake.

Kuyeko amesema, ni vema serikali ikaachana na suala hilo kwani itakuwa chanzo cha kurudisha maendeleo nyuma na kuvuruga bajeti iliyopangwa na manispaa hiyo.

“Kwanza tunasikitishwa na hatua hiyo ambayo imeanza kutekelezwa baada ya Umoja wa Katiba ya Wananchi – UKAWA kuingia madarakani. Siku zote walikuwa wapi? Ni dhairi kuwa nia yao ni kutaka kuturudisha nyuma ili bajeti yetu ikwame.

“Kodi ya mapango ndio chanzo kikuu cha mapato katika kila wilaya ukiacha kodi za mabango na ushuru wa wafanyabiashara,” amesema Kuyeko.

Hata hivyo, utaratibu wa kukusanya kodi za majengo utaanza katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na baadaye kwenye manispaa zote.

Kuyeko amesema, manispaa yake imepanga kufikia bajeti ya Sh. 85 Bilion na zaidi kwa mwaka 2016/17 na kwamba kama serikali itatekeleza hatua yake ya kupoka kodi za majengo, itakuwa imevuruga bajeti hiyo.
chama chenyewe mumemuuzia mtu kwa hela halafu mnaitambia ccm kuleta maendeleo wakati wao ndio wameshika dola. hata ingekua mimi singewaamini ningewakaba koo.
 
ungeweka hapa hilo agizo tuone content yake then tujadili,, hatuwezi kujadili kwa hisia bila kuona agizo lenyewe, maana ninauhakika kua agizo litakua limebeba maelekezo yote..
Kumbe comment ya kwanza ulikuwa hujaanza kujadili
 
Ningeshangaa kama hili suala lisingeingia fitina ya kisiasa. Fitina hizi za kisiasa ni mambo ya kawaida sana kwenye nchi zetu za kiafrika. Hivyo sisi waafrika kukosa maendeleo ni matokeo ya tabia zetu za fitina kwa kila kitu, na hili halibagui toka wasomi mpaka wasiosoma.
 
Utaratibu upi kuhakikisha makusanyo yatarudi kwenye manispaa?
 
Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) jijini Dar es Salaam vimeanza kufilisiwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mpango wa Serikali ya Rais John Magufuli kupoka vyanzo muhimu vya mapato ambavyo awali vilitumika kuendesha halmashauri za jijini humo, umekamilika na sasa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndiyo inayotarajiwa kuwa mbadala katika ukusanyaji mapato.

Vyama vinavyoumizwa na hatua hiyo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF) ambavyo ndivyo vilivyo na wabunge na madiwani Dar es Salaam.

Charles Kuyeko, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pia Diwani wa Kata ya Bonyokwa (CHADEMA) amesema, tayari manispaa yake imearifiwa kwamba, kodi ya majengo kwenye manispaa hiyo itakusanywa na TRA na sio manispaa kama ilivyokuwa awali.

Hatua hiyo anasema itazuia shughuli ama ahadi zao kutotekelezeka kwa namna ambavyo walitaka iwe huku akikosoa hatua hiyo na kuihusisha na uhasama wa kisiasa jijini humo.

Hata hivyo amesema, wapo kwenye mazungumzo na serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kwamba, serikali haioneshi dhamira ya kubadili msimamo wake.

Kuyeko amesema, ni vema serikali ikaachana na suala hilo kwani itakuwa chanzo cha kurudisha maendeleo nyuma na kuvuruga bajeti iliyopangwa na manispaa hiyo.

“Kwanza tunasikitishwa na hatua hiyo ambayo imeanza kutekelezwa baada ya Umoja wa Katiba ya Wananchi – UKAWA kuingia madarakani. Siku zote walikuwa wapi? Ni dhairi kuwa nia yao ni kutaka kuturudisha nyuma ili bajeti yetu ikwame.

“Kodi ya mapango ndio chanzo kikuu cha mapato katika kila wilaya ukiacha kodi za mabango na ushuru wa wafanyabiashara,” amesema Kuyeko.

Hata hivyo, utaratibu wa kukusanya kodi za majengo utaanza katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na baadaye kwenye manispaa zote.

Kuyeko amesema, manispaa yake imepanga kufikia bajeti ya Sh. 85 Bilion na zaidi kwa mwaka 2016/17 na kwamba kama serikali itatekeleza hatua yake ya kupoka kodi za majengo, itakuwa imevuruga bajeti hiyo.
Kwani ni Dar pekee au ni nchi nzima?
 
Ni sahihi kabisa, kuhakikisha hakuna mgongano wa mahesabu baina ya munispaa na TRA, mkakati mzuri kabisa.
Baada ya kukusanywa na TRA kwa hiyo halmashauri wakipanga matumizi waombe Tena hela serikali kuu
 
TRA imefanya ukusaji wa Jodi za majengo manispaa ya kinondoni lakini haikufanikiwa wananchi wanataka maendeleo CCM inataka kuwacheleweshea maendeleo Kwa siasa za chuki Na hasira za kisiasa
 
TRA imefanya ukusaji wa Jodi za majengo manispaa ya kinondoni lakini haikufanikiwa wananchi wanataka maendeleo CCM inataka kuwacheleweshea maendeleo Kwa siasa za chuki Na hasira za kisiasa
Hivyo nini visa na visasi na ccm lakini watashindwa tu
 
Hao hao TRA walishawahi kupewa kazi ya Kukusanya kodi ya Majengo kwa Mkoa wa Dar Es Salaam, lakini kwa nini kazi hiyo ilirejeshwa kwa halmshauri za Manispaa, mimi na wengine kama wapo, hatujui. Vilevile TRA miaka ya nyuma walikuwa wanakusanya kodi toka kwa makampuni/watu wanaofanya biashara ya michezo ya kubahatisha (bahati nasibu, Casinos etc). Baadaye Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ikaanza kukusanya hayo maduhuli na mapato yaliongezeka kwa kiwango kikubwa. Mimi nina mashaka kama kutakuwa na ufanisi wa makusanyanyo ya kodi ya majengo chini ya TRA. Nasubiri nione.
Ni mambo ya kijinga tu ndo yanarudisha nchi nyuma kabisa! TRA lazima isukwe upya na ajira zivute wasomi. siyo hawa wa divisheni 5 na vyeti vya chuo cha kodi.

Manispaa zote CCm huwa ni kufa kupona kwa sababu ndo chanzo chao kikubwa cha kuchota pesa na kuzipeleka kwenye chama. Kila wanapopoteza manispaa, wanapata kiwewe! kumbuka walivyohangaika na Mwanza na Arusha.

Bajeti za CCM na mahitaji yao ni makubwa na mara zote wanaishia kuchota pesa za serikali kupitia kwa wakurugenzi. Kuna hisia pia hata baadhi ya wafanyakazi wa ofisi za chama wako kwenye payroll ya serikali na ndo wafanyakazi hewa hao! Kwa kunyang'anywa Dar, wana kiwewe na maisha yao.
 
Back
Top Bottom