Visa vya CCM vyaanza kuonekana Dar es Salaam

Visa vya CCM vyaanza kuonekana Dar es Salaam

Kwa waliyofanywa na CCM kule Zanzibar kwa wananchi wake ,kauli ya JPM kwa wenzie wana CCM wakubaliane na demokrasia ilikuwa na alama nyingi sana za mimi kujiuliza hivi inawezekanaje Shetani akageuka kuwa Malaika ghafla...!!?
 
Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) jijini Dar es Salaam vimeanza kufilisiwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mpango wa Serikali ya Rais John Magufuli kupoka vyanzo muhimu vya mapato ambavyo awali vilitumika kuendesha halmashauri za jijini humo, umekamilika na sasa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndiyo inayotarajiwa kuwa mbadala katika ukusanyaji mapato.

Vyama vinavyoumizwa na hatua hiyo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF) ambavyo ndivyo vilivyo na wabunge na madiwani Dar es Salaam.

Charles Kuyeko, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pia Diwani wa Kata ya Bonyokwa (CHADEMA) amesema, tayari manispaa yake imearifiwa kwamba, kodi ya majengo kwenye manispaa hiyo itakusanywa na TRA na sio manispaa kama ilivyokuwa awali.

Hatua hiyo anasema itazuia shughuli ama ahadi zao kutotekelezeka kwa namna ambavyo walitaka iwe huku akikosoa hatua hiyo na kuihusisha na uhasama wa kisiasa jijini humo.

Hata hivyo amesema, wapo kwenye mazungumzo na serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kwamba, serikali haioneshi dhamira ya kubadili msimamo wake.

Kuyeko amesema, ni vema serikali ikaachana na suala hilo kwani itakuwa chanzo cha kurudisha maendeleo nyuma na kuvuruga bajeti iliyopangwa na manispaa hiyo.

“Kwanza tunasikitishwa na hatua hiyo ambayo imeanza kutekelezwa baada ya Umoja wa Katiba ya Wananchi – UKAWA kuingia madarakani. Siku zote walikuwa wapi? Ni dhairi kuwa nia yao ni kutaka kuturudisha nyuma ili bajeti yetu ikwame.

“Kodi ya mapango ndio chanzo kikuu cha mapato katika kila wilaya ukiacha kodi za mabango na ushuru wa wafanyabiashara,” amesema Kuyeko.

Hata hivyo, utaratibu wa kukusanya kodi za majengo utaanza katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na baadaye kwenye manispaa zote.

Kuyeko amesema, manispaa yake imepanga kufikia bajeti ya Sh. 85 Bilion na zaidi kwa mwaka 2016/17 na kwamba kama serikali itatekeleza hatua yake ya kupoka kodi za majengo, itakuwa imevuruga bajeti hiyo.
WEWE NYUMBU WAAMBIE NA NYUMBU WENZIO KAMA MLIVYOKATAA FEDHA ZA MAGUFULI,MKILETEWA NA RUZUKU KWENYE HALMASHAURI ZENU ZIKATAENI.
 
Kwa waliyofanywa na CCM kule Zanzibar kwa wananchi wake ,kauli ya JPM kwa wenzie wana CCM wakubaliane na demokrasia ilikuwa na alama nyingi sana za mimi kujiuliza hivi inawezekanaje Shetani akageuka kuwa Malaika ghafla...!!?
WEWE MWAMBIE NYUMBU MKUU MBOWE AWEKE DEMOKRASIA KWANZA KWENYE CHAMA CHAKE KABLA YA KUKURUPUKA NA ZERO YAKE YA IHUNGO.#DEMOKRASIA ZIANZIE NDANI YA VYAMA
 
W

UNAJIPA MOYO! sasa hivi waliongia MKENGE na kuwakubali UKIWA wanjuuuuutah! Kisirisiri ongea na wananchi walioipigia kura hilo GENGE la WAPIGA DEAL usikie....... UKAWA IMEBAKI KWENYE KANDA ZA JAMII ZENYE ROHO YA PAKA TU!

Tunakushukuru kwa kututukana na kutufananisha na paka ,lakini kumbuka sisi pia ni sehemu ya jamii na ni binadamu kama walivyo binadamu wengine wenye itikadi za CCM...

Ungejadili hoja iliyo mezani ingependeza tungeona walau chembe ya busara uliyo nayo.
 
WEWE MWAMBIE NYUMBU MKUU MBOWE AWEKE DEMOKRASIA KWANZA KWENYE CHAMA CHAKE KABLA YA KUKURUPUKA NA ZERO YAKE YA IHUNGO.#DEMOKRASIA ZIANZIE NDANI YA VYAMA

Nimekuelewa mkuu nntaufikisha ujumbe ,lakini kumbuka kwanza kutoa boriti ndani ya jicho lako sbb vipo vipande vingi sana nnaviona machoni pako...

Lakini mkuu hili ningeona ni vema ukalianzishia uzi wake
 
Umeuliza swali la maana sana kuhusu sheria. Pia umetoa hoja nzuri kwa njia ya swali kama ccm wanafanya wanavyojisikia. Labda pia ungeuliza nini nafasi ya vyama vya upinzani kuona ccm haiendeshi nchi kwa matakwa ya watu binafsi bali kwa kuzingatia katiba na sheria? Kulalamika? Kuwaelewesha wananchi ili wao waiwajibishe ccm au kutumia tukio hilo kutunga uongo na hisia za kuuburudisha mioyo za wafuasi wao mbumbumbu ambao kwao habari ni 'chama adui' yao kushindwa?
mkuu mimi siziwezi hoja nzito kama hizi za kwako, nasepa zangu taratibu msije nitoa macho bure. kwa heri.
 
Naichukia sana ccm..... Siwez kuipenda

Mungu iangamize ccm watanzania tupone

Mungu hawezi kuwa upande wa shetani! ndio maana taaratibu anawaangamiza CHADOMO na UKAWA slowly but sure! HUKU CHAMA KUBWA KINAZIDI KUIMARIKA!
 
Back
Top Bottom