Visa vya CCM vyaanza kuonekana Dar es Salaam

Haya ndo mojawapo ya mambo huwa yanafanya watu wengi wenye uelewa waone, ccm haina jambo jipya zaid ya siasa tu, hii nchi ina matatizo sana kutoka itatuchua karne kama nne hiv, wakati nchi nyingine duniani zikielekea kwenye devolution, sis ndo kwanza tunaimarisha central system, sehemu kubwa ya mapato yanatakiwa yabaki halmashaur, serikalin ziende hela kidogo tu.
Ndio maana tunasema serekali hii niyamaigizo full
 
Kuna watu wanachangia kwa mihemko mikubwa. Kama wote tunafahamu hapo zamani kila kitu kilikua kinapangwa na serikali kuu ufanisi ukawa mdogo ndio zikaanzishwa serikali za mitaa.
Vikaanishwa vyanzo vya mapato vya serikali za mitaa ili ziweze kujikimu mathalaani ujenzi wa barabara za halmashauri zinategemea mapato hayo kwa Dar fuatilia barabara nyingi za mitaa kwennye bango la ujenzi ujje
 
Kwa utawala huu, makusanyo yasiposimamiwa vema na tra basi bajeti yetu ya kujitegemea asilimia 80 haitofanikiwa!
 
Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) jijini Dar es Salaam vimeanza kufilisiwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mpango wa Serikali ya Rais John Magufuli kupoka vyanzo muhimu vya mapato ambavyo awali vilitumika kuendesha halmashauri za jijini humo, umekamilika na sasa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndiyo inayotarajiwa kuwa mbadala katika ukusanyaji mapato.

Vyama vinavyoumizwa na hatua hiyo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF) ambavyo ndivyo vilivyo na wabunge na madiwani Dar es Salaam.

Charles Kuyeko, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pia Diwani wa Kata ya Bonyokwa (CHADEMA) amesema, tayari manispaa yake imearifiwa kwamba, kodi ya majengo kwenye manispaa hiyo itakusanywa na TRA na sio manispaa kama ilivyokuwa awali.

Hatua hiyo anasema itazuia shughuli ama ahadi zao kutotekelezeka kwa namna ambavyo walitaka iwe huku akikosoa hatua hiyo na kuihusisha na uhasama wa kisiasa jijini humo.

Hata hivyo amesema, wapo kwenye mazungumzo na serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kwamba, serikali haioneshi dhamira ya kubadili msimamo wake.

Kuyeko amesema, ni vema serikali ikaachana na suala hilo kwani itakuwa chanzo cha kurudisha maendeleo nyuma na kuvuruga bajeti iliyopangwa na manispaa hiyo.

“Kwanza tunasikitishwa na hatua hiyo ambayo imeanza kutekelezwa baada ya Umoja wa Katiba ya Wananchi – UKAWA kuingia madarakani. Siku zote walikuwa wapi? Ni dhairi kuwa nia yao ni kutaka kuturudisha nyuma ili bajeti yetu ikwame.

“Kodi ya mapango ndio chanzo kikuu cha mapato katika kila wilaya ukiacha kodi za mabango na ushuru wa wafanyabiashara,” amesema Kuyeko.

Hata hivyo, utaratibu wa kukusanya kodi za majengo utaanza katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na baadaye kwenye manispaa zote.

Kuyeko amesema, manispaa yake imepanga kufikia bajeti ya Sh. 85 Bilion na zaidi kwa mwaka 2016/17 na kwamba kama serikali itatekeleza hatua yake ya kupoka kodi za majengo, itakuwa imevuruga bajeti hiyo.

Mwanahabarihuru, mwanahabari mwenye tuzo hebu onesha weledi wako katika hili. Hebu tupe kwa kina 'madudu'haya ya ccm. Kwanza utueleze mpaka uliopo kati ya serikali kuu na serikali za mitaa. Naomba utuambie kama kuna sheria yeyote au mamlaka ya kikatiba ambayo serikali ya ccm inayakiuka katika hili inalotaka kulifanya. Hebu tupe historia inayoanzia mwaka 1992 kuhusu utaratibu wa ukusanyaji kodi ya majengo ukoje,ulibadilika au umekaaje kaaaje. Hebu tupatie idadi ya mapato angalau ya halmashauri mbili mwaka wowote, halmashauri moja ikiwa inaongozwa na chama chochote cha upinzani na moja ikiongozwa na ccm tupate kuona (1) Uwezo wa uongozi wa hizo halmashauri kukusanya mapato (2) Tuone kiasi gani kitakacho ondoka mikononi mwa halmashauri kwenda serikali kuu. Baada ya hapo eleza hizo halmashauri ulizozitaja zinapokea fedha kiasi gani kutoka serikali kuu katika kujiendesha. Mwanahabari huru onesha umahiri wako ili ule uzushi kuwa eti mwanahabari huru ni mwanahabari wa kutengeneza uongo ufilie mbali
 
Haya uliyoandika ni kupanic tuu subiri tutatoa uozo wote mliofanya
 
Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) jijini Dar es Salaam vimeanza kufilisiwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mpango wa Serikali ya Rais John Magufuli kupoka vyanzo muhimu vya mapato ambavyo awali vilitumika kuendesha halmashauri za jijini humo, umekamilika na sasa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndiyo inayotarajiwa kuwa mbadala katika ukusanyaji mapato.

Vyama vinavyoumizwa na hatua hiyo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF) ambavyo ndivyo vilivyo na wabunge na madiwani Dar es Salaam.

Charles Kuyeko, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pia Diwani wa Kata ya Bonyokwa (CHADEMA) amesema, tayari manispaa yake imearifiwa kwamba, kodi ya majengo kwenye manispaa hiyo itakusanywa na TRA na sio manispaa kama ilivyokuwa awali.

Hatua hiyo anasema itazuia shughuli ama ahadi zao kutotekelezeka kwa namna ambavyo walitaka iwe huku akikosoa hatua hiyo na kuihusisha na uhasama wa kisiasa jijini humo.

Hata hivyo amesema, wapo kwenye mazungumzo na serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kwamba, serikali haioneshi dhamira ya kubadili msimamo wake.

Kuyeko amesema, ni vema serikali ikaachana na suala hilo kwani itakuwa chanzo cha kurudisha maendeleo nyuma na kuvuruga bajeti iliyopangwa na manispaa hiyo.

“Kwanza tunasikitishwa na hatua hiyo ambayo imeanza kutekelezwa baada ya Umoja wa Katiba ya Wananchi – UKAWA kuingia madarakani. Siku zote walikuwa wapi? Ni dhairi kuwa nia yao ni kutaka kuturudisha nyuma ili bajeti yetu ikwame.

“Kodi ya mapango ndio chanzo kikuu cha mapato katika kila wilaya ukiacha kodi za mabango na ushuru wa wafanyabiashara,” amesema Kuyeko.

Hata hivyo, utaratibu wa kukusanya kodi za majengo utaanza katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na baadaye kwenye manispaa zote.

Kuyeko amesema, manispaa yake imepanga kufikia bajeti ya Sh. 85 Bilion na zaidi kwa mwaka 2016/17 na kwamba kama serikali itatekeleza hatua yake ya kupoka kodi za majengo, itakuwa imevuruga bajeti hiyo.
HIVI UKIWA hamna akili na mipango MIPYA! Tumewajaribu ili tuone ni kitu gani kipya mnaweza kukileta hadi sasa hakuna ....MKO MULE MULE walikopita CCM...Mara Kodi ya mapango....mara ushuru wa kwenye MIGAHAWA... Bora tubaki na CCM wameshiba kupita hawa WAKIWA ...hawana JIPYA!
 
Ni sahihi kabisa, kuhakikisha hakuna mgongano wa mahesabu baina ya manispaa na TRA, mkakati mzuri kabisa.
Huo mgongano umeanza leo? Hebu acheni siasa katika issue muhimu. Serikali lazima itoe sababu kwa nini imeamua kufanya hivyo na Halmashauri hizi zitajiendesha vipi. Else wavunje tu halmashauri na Serikali kuu ndiyo isimamie kila kitu.
 
Haya uliyoandika ni kupanic tuu subiri tutatoa uozo wote mliofanya

Hee tena! Na mimi nimo kwa kuwa nimeomba utumie weledi wako kunifahamisha? Hata kama hivo ndivyo unavyodhani huoni basi kwa kufanya hivyo nilivyokuomba ungetunaufaisha wengi? Mimi nakusihi toa uozo woooote wa watu hao na pia toa ukweli wooooote ili uongo ujitenge na wewe weledi wako uhishimike
 
Kama ni utaratibu mpya wa kukusanya mapato kwa usahihi ni sawa lakini hayo mapato yaelekezwe moja kwa moja kwenye Manispaa na Halmashauri ni sawa.

Lakini zikiwa zinakusanywa alafu haziendi kusaidia halmashauri na Manispaa husika basi huo utakuwa ni uzandiki mkubwa.
 
Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) jijini Dar es Salaam vimeanza kufilisiwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mpango wa Serikali ya Rais John Magufuli kupoka vyanzo muhimu vya mapato ambavyo awali vilitumika kuendesha halmashauri za jijini humo, umekamilika na sasa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndiyo inayotarajiwa kuwa mbadala katika ukusanyaji mapato.

Vyama vinavyoumizwa na hatua hiyo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF) ambavyo ndivyo vilivyo na wabunge na madiwani Dar es Salaam.

Charles Kuyeko, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pia Diwani wa Kata ya Bonyokwa (CHADEMA) amesema, tayari manispaa yake imearifiwa kwamba, kodi ya majengo kwenye manispaa hiyo itakusanywa na TRA na sio manispaa kama ilivyokuwa awali.

Hatua hiyo anasema itazuia shughuli ama ahadi zao kutotekelezeka kwa namna ambavyo walitaka iwe huku akikosoa hatua hiyo na kuihusisha na uhasama wa kisiasa jijini humo.

Hata hivyo amesema, wapo kwenye mazungumzo na serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kwamba, serikali haioneshi dhamira ya kubadili msimamo wake.

Kuyeko amesema, ni vema serikali ikaachana na suala hilo kwani itakuwa chanzo cha kurudisha maendeleo nyuma na kuvuruga bajeti iliyopangwa na manispaa hiyo.

“Kwanza tunasikitishwa na hatua hiyo ambayo imeanza kutekelezwa baada ya Umoja wa Katiba ya Wananchi – UKAWA kuingia madarakani. Siku zote walikuwa wapi? Ni dhairi kuwa nia yao ni kutaka kuturudisha nyuma ili bajeti yetu ikwame.

“Kodi ya mapango ndio chanzo kikuu cha mapato katika kila wilaya ukiacha kodi za mabango na ushuru wa wafanyabiashara,” amesema Kuyeko.

Hata hivyo, utaratibu wa kukusanya kodi za majengo utaanza katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na baadaye kwenye manispaa zote.

Kuyeko amesema, manispaa yake imepanga kufikia bajeti ya Sh. 85 Bilion na zaidi kwa mwaka 2016/17 na kwamba kama serikali itatekeleza hatua yake ya kupoka kodi za majengo, itakuwa imevuruga bajeti hiyo.
Okey, payroll yenu ishafika ufipa. Tomorrow is a payday.
 
Back
Top Bottom