Mwaka 2008, Nilikuwa Mbeya Tukuyu Kikazi, Nilikuwa nimetokea Mbeya Mjini ambapo Kuna baridi, Dose yangu ilikuwa Tusker Kumi,
Kwenda Tukuyu Nikaendelea na dose ileile bila kugundua kuwa Hali ya hewa ya Tukuyu Ni Tofauti na Mbeya Mjini. Na Pombe. Hukolea kwenye Joto, Tukuyu Kuna Joto.
Mzee Mzima Nikavesha Kama kawaida, mpaka saa tano FULANI hivi, Sasa kimbembe Nikasahau Guest, Nikaenda kugonga Nyumba ambayo Inaangaliana na Guest Huku Povu likinitoka kwanini wafunge na Mimi bado sijarudi.
Ebwana mlango ulifunguliwa na Mbaba mmoja akiwa na njemba tatu (Watoto wake) Nilichezea vitasa vyakutosha kila nikiweka Gurd wapi.
Niliokolewa na Staff wenzangu Baada ya kuhisi kuwa sijarudi na wanasikia kelele za sauti yangu.
Asee hiyo ilikuwa moja Ila Pombe kuacha bado nafikiria.