Virusi vya Corona vyatua Afrika, mgonjwa mmoja kutoka China abainika kuwa navyo

digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
7,894
14,353
Maofisa wa afya wanamshuku mgonjwa mmoja nchini Ivory Coast kuwa na virusi vya Corona, Waziri wa afya ametangaza.

Mwanafunzi ambaye jina lake halikutajwa, alikuwa ametokea China, mjini Beijing na kurudi kwao Afrika magharibi siku ya jumamosi, sasa anafanyiwa vipimo zaidi baada ya kukutwa na mafua, ambayo ni moja ya dalili za ugonjwa wa Corona.

Imethibitishwa kwamba mgonjwa huyo atakuwa wa kwanza barani Afrika kufanyiwa vipimo hivyo vya virusi hatari.

Virusi hivyo vilibainika kwa mara ya kwanza katika mji wa China wa Wuhan, na sasa watu 2000 wana virusi hivyo na 56 wamefariki tayrari.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 34, ametengwa kwa sasa, maofisa walisema.,

Virusi vya Corona vinasambaa kabla ya dalili kuanza kujitokeza

Virusi vya Corona vyaenea kwa kasi, Rais Xi Jinping

Mwanamke mhuyo anadaiwa kuishi China kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, kwa mujibu wa taarifa ambayo ilitolewa na wizara ya afya ya Ivory Coast na kusema kuwa alionyesha dalili za mafua kabla hajapanda ndege akiwa anaelekea Abidjan.

"Kuna hali ya wasiwasi kuwa dalili alizokuwa nazo zina uhusiano na virusi vya corona."

Majibu ya vipimo vya mwanamke huyo yanatarajiwa kutolewa siku ya jumapili jioni.

Kwa sasa virusi hivi vinavyofahamika kama 2019-nCoV, vinadaiwa kuwa maambukizi mapya kuwapata binadamu.

Tangu mlipuko wa ugonjwa huo kuanza Wuhan, mataifa kadhaa ya Afrika yalianzisha vipimo vya kuangalia virusi vya corona kwa wat wanaotoka China.

Eee mola tusaidie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali inatakiwa idhibiti watu wanaoingia hapa kutoka china wapimwe kwanza ndio waruhusiwe kuingia nchini la sivyo ugonjwa utaingia hapa na wachina wanaingia hapa nnchini kama njugu ni wengi sana, pia wafanya biashara wengi wanaenda china na kurudi tujipange la sivyo tutaisha

pia wachina wapunguze uchafu, wanakula vitu vya ajabu sana kuanzia panya, nguruwe, popo hadi wadudu, watailetea dunia mikosi hawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenza ramli tena mkuu,wewe ongelea ugonjwa hayo mambo ya kina furani yanini tena?
Mungu atusaidie maana vikifika Tanzania tutakufa wengi kwa uzembe wa wachache! Simply because kuna watu hawatatikiwa kuripoti taarifa sahihi hadi zipite kwa akina flani, sio waziri wala mbunge ataweza kutoa takwimu! Mungu tunusuru

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
China inaitega dunia. no body should be allowed to travel out of china until they sort out the mess.
 
Hivi virusi vinasadikika kutoka kwa nyoka
serikali inatakiwa idhibiti watu wanaoingia hapa kutoka china wapimwe kwanza ndio waruhusiwe kuingia nchini la sivyo ugonjwa utaingia hapa na wachina wanaingia hapa nnchini kama njugu ni wengi sana, pia wafanya biashara wengi wanaenda china na kurudi tujipange la sivyo tutaisha

pia wachina wapunguze uchafu, wanakula vitu vya ajabu sana kuanzia panya, nguruwe, popo hadi wadudu, watailetea dunia mikosi hawa

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu atusaidie maana vikifika Tanzania tutakufa wengi kwa uzembe wa wachache! Simply because kuna watu hawatatikiwa kuripoti taarifa sahihi hadi zipite kwa akina flani, sio waziri wala mbunge ataweza kutoa takwimu! Mungu tunusuru

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata hizo data za vifo China ni za kupika siyo halisi....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
serikali inatakiwa idhibiti watu wanaoingia hapa kutoka china wapimwe kwanza ndio waruhusiwe kuingia nchini la sivyo ugonjwa utaingia hapa na wachina wanaingia hapa nnchini kama njugu ni wengi sana, pia wafanya biashara wengi wanaenda china na kurudi tujipange la sivyo tutaisha

pia wachina wapunguze uchafu, wanakula vitu vya ajabu sana kuanzia panya, nguruwe, popo hadi wadudu, watailetea dunia mikosi hawa

Sent using Jamii Forums mobile app
Siyo kukazana kuanza kupima wanaotoka China peke yake bali ipime wanaoingia nchini kutokea popote pale duniani na pia itafute uwezo wa kuweka utaratibu wa kuwafanyia screening wananchi wote.
 
Sikilizeni huu ugonjwa ni hatari sana kama ukifika afrika vuta picha kama ni China nchi yenye kila kitu na bado wanashindwa kuudhibiti unaenea kwa kasi sana watu na viongozi wao ni waelewa wanajilinda na kujitunza wemezuia mikusanyiko wamefuta safari RAIA wanajikinga na kufata taratibu zote na bado maambukizi yanaendelea na watu wanakufa hapo sio sana

Kaa alafu vuta picha uje afrika tena nchi masikini yoyote ile ufike nakuambia watu watakufa kama kuku
TUSIOMBE YATUKUTE JAMANI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom