Vipepeo weusi season 2: From Zurich with rules

Vipepeo weusi season 2: From Zurich with rules

Nimepata wasiwasi na uhai wa huyu muanzilishi wa huu uzi
Jamaa yupo sema kuna mawili:-
1.Pesa mbele kwamaana baada ya kutulambisha humu kwa ncha ya kisu sasa anataka tununue kitabu kama wanavyofanya wengine so ilikuwa ni promo tu kuleta Riwaya humu.
2.Amefulia yaani hana idea mpya so ule mzuka wa utunzi umesepa
 
VIPEPEO WEUSI

SEASON 2 – FROM ZURICH WITH RULES


EPISODE 29


Nilifika mtaa wa Freatch West karibia majira ya saa mbili na nusu usiku. Mtaa ulikuwa kimya tofauti na kawaida kama ambavyo niliufahamu kipindi bado nakaa hoteli ya Radison Blu. Nilihisi labda ni kutokana na matukio ya maujai ambayo yametokea ndio yalifanya watu wawe na hofu kutembea usiku katika mtaa huu. Nilishuka kwenye taxi umbali wa kama hatua ishirini kutoka mahala ambako ule mgahawa wa kichina ulipo ambapo Winnie alinielekeza kuwa yuko ndani yake. Nilihitaji kuyasoma mazingira kabla ya kuingia ndani ya mgahawa huu.

Nilitembea na kufika kama hatua kumi kutoaka ulipo malango wa mgahawa. Uzuri ni kwamba upande huu wa barabarani wa mgahawa kama ilivyo desturi ya migahawa mingi ya nchi za magharibi ulikuwa ni wa kioo tupu kwa hiyo niliweza kuona ndani bila wasiwasi kabisa. Japo kuwa ilikuwa ni mapema kabisa saa mbili unusu usiku, lakini ndani ya mgahawa kulikuwa na watu wachache sana. Niliweza kumuona Winnie akiwa amekaa kwenye meza ya peke yake kukiwa na kikombe cha kahawa mezani. Winnie alikuwa amevalia sweta la mikono mirefu na alikuwa amelivuta mpaka kufunika viganja vya mikono. Kwa namna ambavyo alikuwa amekaa tu mtu yeyote angeweza kuhisi woga ambao Winnie alikuwa nao.

Meza kama ya tatu kutoka aliko Winnie alikuwa amekaa mzee wa kichina na mkewe ambao walionekana wanapata mlo wa jioni kama kawaida. Meza nyingine kulikuwa na kijana wa kizungu, mwanaume ambaye pia alikuwa anapata kahawa. Nilijaribu kuangaza macho huku na huko labda niweze kung’amua huyo mtu ambaye Winnie alidai anamfuatilia lakini sikuweza hata kuhisi… nje ya mgahawa kulikuwa hakuna mtu yeyote yule na watu wote ambao walikuwa ndani ya mgahawa hakuna ambaye alinifanya nimtilie mashaka.
Nikaufuta mlango wa ngahawa na kuingia ndani.

“Hey… you ok?” nilimuuliza Winnie huku nikikaa kwenye kiti baada ya kufika kwenye meza ambayo aliketi.

“No I’m not… I’m far from ok!” Winnie aliongea kwa wasiwasi huki analivuta vuta sweta lake viganjani.

“What are you doing here?” nilimuuliza. Ilikuwa ni jambo la ajabu sana kwangu Winnie aliponiambia kuwa yuko kwenye mgahawa huu hasa baada ya kuonana tu na mimi masaa machache yaliyopita.

“They called me again!” alinijibu huku ananiangalia kwa uso wa wasiwasi

“Who called you?”

“The guy who gave me the job… the one I told you about earlier today!” Winnie alinijibu.

Nilimuelewa kwamba alikuwa anamaanisha yule jamaa ambaye alimpigia simu miaka miwili iliyopita na wakakutana katika mgahwa huu huu na kumpa kazi ya kusafisha nyumba ile ya mtaa wa Affoltentrasse.
 
Nilijiuliza kichwani kama hii ilikuwa ni bahati mbaya ama vipi? Kwa nini mtu huyo ampigie simu Winnie siku ya leo baada ya Wiinie kuonana tu na mimi?

“What did he want?” nikamuuliza Winnie huku kichwani nikiendelea kuchekecha mfululizo huu wa utokeaji wa matukio.

“it’s strange.. he called me and wanted to meet him up here and then he only said one sentence and then he left.!”

“What didi he say?” nikauliza kwa shauku.

“He just said… ‘don’t invite anyone inside the house’.!”

“What!!”

“That’s all that he said and then he left!”

“He could have said that over the phone… why did he want to meet!”

“I don’t know… am really confused!”

Ilikuwa haiingii akilini kwamba mtu huyo alitaka kuonana na Winnie ili aongee sentesi moja tu kwamba ‘winnie asiruhusu mtu yeyote kuingia ndani ya nyumba’. Alikuwa anaweza kumwambia suala hilo kupitia simu, kwa nini alitaka waonane. Au huu ulikuwa ni mtego ? Mtego wa nini?

“You said someone was following you?” nikamuuliza Winnie kwa kunong’ona.

“Yes.. that guy over there!” Winnie aliongea kwa kunionyesha kwa ishara ya macho.

Nilifuata uelekeo wa macho ya Winnie na alikuwa ananionyesha kwenye ile meza ambayo alikuwa amekaa kijana wa kizungu ambaye alikuwa anakunywa kahawa. Kwa mara hii ya pili baada ya Winnie kunionyesha na kumuangalia vizuri yule kijana ndipo ambapo sura yake ikaanza kuingia kwenye akili yangu na kuhisi kama nimewahi kumuona mtu huyu mahala fulani japokuwa alikuwa anaonekana ni wa kawaida kabisa ambaye mtu usingelimtilia mashaka. Alikuwa amevalia suruali ya jinzi na sweta lenye kofia waitazo ‘hood’ kwa umombo.

“Are you sure?” nilimuuliza Winnie.

“Hundred percent sure… I saw that guy’s car when I was on my way here… and then after I got here he also parked outside and has since been sitting there. I think he is waiting for me to leave so that he can do the same!”

Nikainua tena shingo kumtazama yule kijana wa kizungu. Hakika nimewahi kumuona mahali, japo kumbukumbu ilikuwa inakuja na kuondoka.

“What is going on Ray?” Winnie aliniuliza kwa sauti ya woga.

“I don’t know… did you call the police like you said earlier today?” nikamuuliza
 
“I wanted to but I couldn’t.”

“Why?”

“Well you said it might get you into trouble if the police get involved in this!” Winnie alinijibu huku ananiangalia kwa macho ya huruma.

Moyoni niliumia kweli kweli. Binti huyu japo tumejuana kwa siku chache tu lakini alikuwa anajali usalama wangu kiasi hiki. Alikuwa anahatarisha maisha yake kwa kutotoa taarifa hii ya kufuatiliwa na watu wasiojulikana polisi na anafanya hivyo ili tu kunilinda nisiingie kwenye matatizo na polisi. Na sasa mimi ndiye mtu pekee ambaye ni tegemeo lake kumnasua kwenye kizaazaa hiki ambacho amejikuta yumo. Moyo ulikuwa unaniuma kwa kuwa nilikuwa sijui nifanye nini, nilikuwa bado sijui hata adui yetu halisi alikuwa ni nani.

Nikiwa nawaza hivi ghafla mlango wa mgahawa ulifunguliwa na aliingia binti mrembo wa kizungu. Alikuwa amevalia kigauni kifupi sana cha rangi nyekundu. Kigauni kilikuwa kifupi kiasi kwamba sehemu kubwa ya mapaja yake yalibakia wazi. Chini alikuwa amevalia viatu virefu vya rangi nyekundu pia. Shingoni alikuwa amevalia mkufu wenye kumeremeta kwa vito vya thamani ambao ulionyesha ulikuwa wa bei ghali si kidogo. Nilipomtazama usoni macho yetu yaligongana, akatabasamu. Naama ndipo hapa ambapo niling’amua, nimewahi pia kumuona huyu binti… yes, nimewahi kumuona. Nilibakia nimemkodolea macho tu… binti alitembea kwa mwendo wa madaha kama mwanamtindo na kwenda kukaa kwenye kiti pale ambapo yule kijana wa kizungu ambaye Winnie alisema kuwa alikuwa anamfutilia alikuwa ameketi. Naam, sasa kumbukumbu yangu ilinijea sawia kabisa, niwahi kuwaona hawa watu… ni siku ile pale Radisson Blu Hotel… siku ile ambapo nilikuwa nabishana yule muhudumu Erica, pale kwenye eneo la kupumzika pale mapokezi kulikuwa na mama mwenye mtoto, alafu kulikuwa na yule jamaa mwenye kuvaa kofia ya pama na koti refu jeusi na pia kulikuwa na hawa wapenzi wawili. Ni hawa hawa ambapo nilipochukua taxi na kuondoka nao walichukua taxi nyingine na kunifuatilia kwa nyuma. Kisha nilipomuamuru dereva asimamishe gari nao walimama kwa muda wa kama dakika moja hivi na kisha kuamua kuondoka wakitupita kwa kasi pale tuliposimama. Naam, ni hawa hawa. Mapigo ya moyo yalinienda mbio.

“What is it?” Winnie aliniuliza.

Alikuwa ameona namna ambavyo nilibadilika mara baada ya yule binti wa kizungu kuingia humu mgahawani na kwenda kuketi pale kwa yule kijana wa kizungu.

“I know them!” nilimjibu bila kumuangalia. Macho yangu bado nilikuwa nimeyakaza kuwatazama wale vijana wa kizungu.

“Who are they?” Winnie aliniuliza kwa shauku.

“I don’t know who they are but this is not the first time I see them!”

Nikiwa najiuliza kichwani ni nini kilikuwa kinaendelea na watu hawa ni akina nani, mara yule kijana wa kiume alimuita muhudumu na kisha kumlipa. Wakainuka yeye na mwenzake yule binti aliyekuja hapa dakika chache ziliopita na kisha wakatoja nje ya mgahawa na kuondoka.
 
Nilihisi kichwa kinataka kupasuka, nilihisi maluweluwe mbele yangu. Kwa nini waondoke? Si Winnie amenieleza huyu kijana amekuwa anamfuatilia.? Kwa nini wameondoka na kutuacha hapa?
Nikawaza haraka haraka lakini sikupata jawabu.
Kwa nini huyo mtu aliyemuita Winnie waje kukutana kwenye mgahawa ule ule ambao mimi niliitwa pia siku ya kwanza tu nilipowasili hapa Zurich na kutolewa damu na kudungwa sindano ya usingizi? Lakini Winnie anadai pia ni mgahawa huu huu ambao aliitwa miaka miwili iliyopita, hii maana yake kwamba yeye alishawahi kufika hapa hata kabla ya mimi kufikiria kuja Zurich.
Lakini kwa nini mtu huyo amuite tena leo hii, baada ya mimi na Winnie kuonana mchana, na kwa nini amuite ili kuongea sentesi moja tu? Papo hapo Winnie afuatiliwe, na ghafla tu wanaomfuatilia waondoke?

Kuna mtu alikuwa anacheza na akili yangu. Sikujua alikuwa na lengo gani lakini ilikuwa dhahiri kwamba alikuwa hatua elfu kadhaa mbele yangu. Alikuwa ananichezesha ngoma ambayo nilikuwa siijui.

“It’s a trap!” nilimwambia Winnie huku nikiangaza macho mle ndani ya mgahawa huku na huko kama vile kuna kitu natafuta.

“What?” Winnie aliniuliza kwa mshangao.

“This is a trap! Come with me.” nilimwambia tena huku namshiika mkono na kuanza kuinuka kutoka pale ambako tulikuwa tumekaa.


Itaendelea..


Habibu B. Anga ‘The Bold’
To Infinity and Beyond
 
VIPEPEO WEUSI

SEASON 2 – FROM ZURICH WITH RULES


EPISODE 30


“Where are we going Ray?” Winnie aliniuliza huku ametoa macho anashangaa.

Nilielewa mshangao wake. Alikuwa anategemea kwamba tungetoka nje ya mgahawa tofauti na nilichokuwa nakifanya kumvuta kuelekea nyuma ya ‘kauta’ ambako kuna jiko. Kitendo cha wale vijana wawili wa kizungu ambao niliwahi kuwaona Radison Blu Hotel kuwepo hapa mgahawani na kisha kuondoka ghafla tu kilinipa mashaka. Kulikuwa na mtego ambao ulikuwa mbele yetu. Sikuelewa kwa haraka ni kwa nini walikuwa wanafanya haya lakini kwa mbali nilikuwa nimeanza kupata wazo mazingira ambayo yalikuwa yanatengenezwa. Ilikuwa haiingii akilini watu hawa kunifuatilia mimi au Winnie, kwa sababu nilikuwa na hakika kabisa wanajua mahala gani naishi na walikuwa wanajua pia Winnie anaishi wapi. Nilikuwa na hakika kabisa wanajua mambo mengi kuhusu mimi na hata kuhusu Winnie. Kwa nini walikuwa wanatufuatilia? Kulikuwa na jawabu moja tu ambalo lilikuwa na mashiko…

“stop being stubborn… just come with me.!” Niliongea huku naendelea kumvuta Winnie mkono kuelekea kule jikoni kwa huu mgahawa.

“Please explain it to me… what’s going on here?”

“I will explain later… we don’t have much time… just come!”

Tulifika mpaka kwenye malango wa jiko la mgahawa. Kulikuwa na kijana wa Kichina ambaye alikuwa amevalia suti nyeusi na mwili wa miraba minne uliojengeka kwa mazoezi alikuwa amejaa mlangoni akituzuia tusipite. Nikamuangalia kwa kumkazia macho nikimaanisha kwamba asogee pembeni na kunipisha nipite lakini hakutikisika wala kupepesa macho. Kitendo chake cha kubakia kuziba mlango tu ili tusiingie jikoni lakini kushindwa kutuondoa pale kwa nguvu kilinipa moyo kwamba mtu huyu hakuwa na hakika hasa kichwani mwake kama atuondoe au aturuhusu kuingia.

“Step aside.!” Niliongea kwa kujiamini huku nimemkazia macho. Winnie alikuwa amesimama pembeni yangu kwa utulivu mkubwa na kwa uoga.

Yule kijana wa kichina bado alikuwa amesimama pale mlangoni bila kutikisika wala kupepesa macho.

“I need my dragon wings.!!” Niliongea kwa sauti kubwa nikitaka watu walioko huko jikoni wanisikie.

“What are talking about??” Winnie alihamaki huku ametumbua macho akishangaa kile ambacho nilikuwa nimekisema.

“Shut up! Just wait and see…!” nilimnyamazisha Winnie “I need my dragon wings.!!” Nilirudia tena kuita kwa sauti.

“Let him in.!” sauti iliyojaa lafudhi ya kichina iliongea kutokea ndani ya jiko.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom