Vipepeo weusi season 2: From Zurich with rules

Vipepeo weusi season 2: From Zurich with rules

Winnie alibakia ametumbua macho asielewe kile ambacho kilikuwa kinaendelea. Hakuelewa kuhusu hili neno la fumbo ambalo nilipewa siku yangu ya kwanza tu kuingia Zurich ambapo nilitakiwa kufika kwenye mgahawa huu na kuwaambia wahudumu waniletee ‘dragon wings’. Siku ambayo hapa hapa mgahawani baada ya kuwaambia neno hilo la siri nilikutanishwa na yule mzee wa kichina ambaye alinichoma sindano ya kemikali na kupoteza fahamu na kujikuta nimeamka kwenye lile jengo mtaa wa Hardstrasse.

Yule kijana wa miraba mine alisogea pale mlangoni na kutupisha tuingie jikoni. Lilikuwa ni jiko la kisasa la ukubwa wa wastani. Kulikuwa na wapishi kama watano hivi wakiwa na ‘apron’ zao za upishi kila mmoja akioneakana kuwa ‘bize’ kuandaa chakula. Katika wapishi hawa watano mmoja wao alikuwa yule mzee wa kichina ambaye nilikutana naye hapa nilipokuja siku ile ya kwanza.

“Give us some privacy!” yule mzee aliongea na wapishi wengine na wote kwa haraka na heshima kubwa walitoka jikoni.

Yule kijana wa miraba mine ambaye awali alikuwa ametuzuia tusiingie pale mlangoni alifunga mlango kwa ndani. Kwa hiyo ndani ya jiko tulibakia mimi, Winnie, yule mzee na kijana huyu wa miraba minne. Winnie taharuki iliongezeka usoni mwake baada ya mlango wa jiko kufungwa.

“PUUUUUUUUHH.!!!” Nilikuwa nimegeuka nikimuangalia yule kijana akifunga mlango na ghafla nilishitukizwa kwa ngumi nzito ya uso iliyonifanya nijiinamie nikishikilia mdomo na kugugumia kwa maumivu.

“That’s for Ivanka!” yule mzee wa kichina aliongea huku nikimuona akivuta kasi ili kunidondoshea ngumi nyingine.

“PUUUUUUUUHH.!!!” Alinidondoshea ngumi ya pili ambayo ilinipata tumboni.

Nilidondoka chini na kujinyongorota kwa maumivu.

“That’s for Luke…” mzee aliongea kwa kukereka.

“what…the ***…are you doing!” niliongea kwa taabu nikijinyongorota kwa maumivu pale chini sakafuni.

“stupid kid… get up!” mzee alifoka na kuja kuninyanyua mzobe mzobe na kunikalisha kwenye moja ya kiti pale jikoni. Alikuwa ni mzee wa makamo lakini nilishangaa namna ambavyo alikuwa mkakakamavu.

Nilikaa kwenye kitu huku nikiwa kama niko ‘disorriented’. Nilikuwa naona maluweluwe tu. Alikuwa amenishambulia kwa kunishtukiza na sikuwa namuelewa maana ya kile ambacho alikuwa anakisema.

“I told you to go back to the hotel and wait motherfucker! Is that hard?” mzee alifoka huku amenikwida shati uso wake akiwa ameusogeza karibu kabisa na wa kwangu.

Nilibakia nimetumbua macho tu nisijue ni kitu gani hasa niongee. Nakumbuka mara ya mwisho tulipoonana alinipa maagizo hayo. Siku ile ambayo nilikuta mgahawa umefungwa na kuzunguka mlango wa nyuma. Kijana wake wa ulinzi aliponikamata nilimueleza kuwa nimetumwa na ‘melchizedek’. Baadae aliniuliza swali la mtego ambalo nililijibu kwa usahihi. Na kisha akanieleza “go back to the hotel and wait”. Lakini nilipofika hotelini na kukuta chumba kizima kinanukia harufu ya windex na pia kukuta kopo hilo la dawa ya windex imesahauliwa chumbani kwangu niliamua kuondoka na kuhamia kwenye jengo la Hardstrasse. Ni kweli sikufanya kama vile ambavyo alikuwa amenieleza, lakini sikuelewa hiki kipigo chote na kunitajia majina ya Ivanka na Luke alikuwa na maana gani hasa.

“do you know what you have done you son of bitch!! You killed them both..!” mzee alifoka huku akiniachia kwa nguvu shati ambalo alilkuwa amenikwida na kunifanya nisukumwe nyuma nusura nidondoke tena ardhini.

“I don’t understand!” niliongea kwa sauti ya kutetema kwa hasira na uoga.

Yule mzee alienda mpaka upande mmoja wa jiko ambako kulikuwa na makorokoro akapekua pekua na kisha kutoka na bahasha mbili za kaki.
Akatembea haraka haraka kwa hasira mpaka pale nilipo. Kwa hasira kubwa aliweka zile bahasha mbili kwenye meza ya karibu yangu. Kisha nikamuona anafunua lile apron lake la upishi na kisha anapeleka mkono wake kiunoni. Alipotoa mkono alikuwa ameshikilia bastola mkononi.
Sikujua kama nikimbie au nifanye nini. Wote wawili, mimi na Winnie tulibakia tumetumbua macho huku tukitetemeka kwa hisia ambayo tulikuwa nayo kichwani yule mzee alichokuwa anataka kukifanya.
Lakini ajabu ni kwamba aliigeuza ile bastola na kuishika mdomoni huku mshikio akiuelekeza kwangu kwa maana ya kwamba alikuwa ananikabidhi ile bastola. Niliipokea huku mikono inatetemeka. Akachukua na zile bahasha mbili ambazoa likuwa ameziweka pale mezani awali nazo pia akanikabidhi.

“this is the package that I delivered for you at Radison Blue but you were not there.!” Mzee aliongea kwa hasira huku amenikazia macho.

“I don’t understand!” nilimjibu huku bado nikiwa natetemeka.

“Now you are on your own Ray! Don’t ever come back here… if I ever see you here again I swear to God I’m gonn’ skin you alive!” mzee aliongea kwa hasira na kwa msisitizo akionekana kumaanisha kila neno ambalo alikuwa analiongea.

Nilibakia nimemkodolea macho kwa karibia nusu dakika. Niligeuka kumuangalia Winnie, alikuwa ananiangalia kwa woga kama vile ameona kifo mbele yake.
Nikageuka kumuangalia tena yule mzee.

“I don’t understand!” nikamweleza tena.

“Get the *** out of here before I cut off your haed!” mzee aliongea huku ameanza kupiga hatua za taratibu kunifuata tena.

“Let’s go Ray!” Winnie aliongea kwa upole huku ananishika mkono kuniondosha. Nahisi alikuwa amegunduka kwamba kutokana na kilichokuwa kimetoka hapa haraka haraka, akili yangu ilikuwa imesizi ghafla na sikuwa nawaza sawasawa, nilikuwa kama niko kwenye bumbuwazi na uwepo wangu hapa ulikuwa unaendelea kumtia hasira huyu mzee.

Tulitoka jikoni na moja kwa moja kutokea sehemu ya mbele ya mgahawa ambayo tulikuwa tumekaa awali. Tulitembea haraka haraka na kutoka nje mpaka kwenye gari ya Winnie ambayo alikuwa amekuja nayo na kuingia ndani haraka.
 
Ulipita ukimya wa karibia dakika tatu nzima tukiwa ndani ya gari pasipo yeyote kusema neno wala kung’oa gari. Nilikuwa nimefumba macho na kujilaza kwenye siti nikijaribu kuiweka akili yangu iwaze vyema sawa sawa. Nilishtushwa na mikono laini ambayo ilikuwa imenigusa usoni kama inanipapasa.

“Let me take a look at that!” Winnie alikuwa amenishika kichwa na kukigeuza kutaka kuangalia vyema lile aneo ambalo yule mzee alikuwa amenipiga ngumi. Mwanzoni pale jikoni sikutambua ila sasa hivi ndio niligungua kuwa palikuwa pamechanika na kulikuwa na damu kidogo zilitoka japo kwa sasa zilikuwa zimekoma kutoka.

“Leave it alone… its ok!” nilimtoa mikono yake usoni na kuinuka na kukaa vyema wima.

Kilipita kimya kingine cha dakika moja nzima bila yeyote kuongea lakini wote wawili tulijua kabisa ni kitu gani ambacho tunapaswa kukizingumza.

“what’s going on Ray?” Winnie aliuliza hatimaye na aliuliza kwa sauti ya upole kabisa na utulivu kana kwamba alikuwa ananionea huruma.

“I don’t even know where to start!” niliongea huku nimefumba macho.

“Start from where you said this was a trap!”

Nilitafakari kwa muda wa kama sekunde ishirini hivi kisha nikaanza kumueleza Winnie. Kwanza nilimueleza kwa kifupi kuhusu uwepo wa kikundi cha HUDINI na namna ambavyo wanapaswa kunipa taarifa ambazo zimenifanya nije hapa Zurich. Kisha nikamueleza wasiwasi wangu kwamba kuna uwezekano kuna watu wengine nje ya HUDINI nao walikuwa wanaitaka taarifa hiyo ambayo HUDINI wanayo. Nilimueleza ni kwa namna gani ambavyo maelezo alinipa juzi kwamba kuna watu wamekuwa wakimfutilia kwa muda wa wiki tatu zilizopita kwa kupaki gari nje barabarani kwenye ile nyumba mtaa wa Affoltranasse. Nilimueleza kwamba nina imani kubwa waliomuajiri ni mawakala wa HUDINI kwa hiyo hawana sababu ya kumfutilia kwa hiyo hii ilimaanisha kwamba watu ambao wanamfuatilia ni wengine nje ya HUDINI. Nikamweleza Winnie pia kwamba HUDINI hawana sababu ya kunifuatilia mimi kwa sababu walikuwa wanajua naishi wapi hapa Zurich na mambo mengine yote. Kwa hiyo kitendo hiki cha kufuatiliwa kilikuwa kinaonyesha dhahiri kabisa kwamba kulikuwa na watu wengine wapinzani wa HUDINI. Lakini pia nilimweleza kuhusu mauaji ya Luke na Ivanka siku mbili tu baada ya mimi kuonana nao iliashiria dhahiri kabisa kwamba Ivanka na Luke kuna uwezekano mkubwa walikuwa ni mawakala wa HUDINI na waliuwawa na wapinzani wao.
Baada ya hapo nilimueleza kwa nini nilihisi kwamba kuitwa kwake hapa kulikuwa ni mtego… kwanza kabisa nikamueleza kwamba ahiingii akilini mtu amuite kumwambia sentesi moja tu kuwa “kamwe asimruhusu mtu kuingia ndani ya nyumba ile ya mtaa wa Affoltrenasse”. Kwa hiyo hisia yangu ni kwamba HUDINI walikuwa wanafanya ‘counter-survaillance’, kwamba walikuwa hawajui kinagaubaga adui yao ni nani kwahiyo walimtumia yeye kumuita hapa wakijua kuna uwezekano mkubwa na yeye kuniita mimi hapa ili wote tukiwa sehem moja ni chambo kizuri cha hao watu wanaotufuatilia kufanya hivyo na papo hapo HUDINI kutumia mwanya huo kuwang’amua wabaya wao.

Nakumbuka Winnie aliniuliza kwa nini HUDINI wasinipe tu hiyo taarifa ninayotakiwa kuwa nayo ili niondoke na kuepusha madhila yote haya. Nikamjibu kwamba hisia yangu ni kwamba HUDINI walikuwa wanaogopa kunipa taarifa hiyo kienyeji au kirahisi rahisi kwa kuhofia taarifa hiyo inaweza kuchukuliwa kwa urahisi kutoka kwangu na hao maadui zao.
 
“I know it doesn’t make any sense but that’s what is in my head!” nilijitetea baada ya kuhisi ufafanuzi wangu ni wa kuunga unga mno.

“No, actually it make sense some how.” Winnie akanitia moyo japo sikudhani kama alikuwa anamaanisha kweli maana hata mimi mwenyewe nilikuwa na wasiwasi na nadharia yangu.

“So what made you go to the kitchen and get your ass beaten?” Winnie aliongea huku anatabasmau. Tulijikuta wote tumeangua vicheko.

“I have this principle… stall, confuse, deflect!”

Nikamueleza ni namna gani ambavyo mara nyingi nikiwa kwenye mazingira ninayohisi kuwa natumika kama chambo au nashawishiwa nichukue hatua fulani huwa napenda kufanya kitu ‘random’ ambacho huyo mtu anayenifuatilia alikuwa hakitegemei ili kumchanganya asiweze kuelewa hatua ambayo niyaichukua tena baada ya hapo.

“stall, confuse, deflect! I like that!” wote tukatabasamu. “so what’s up with those envolopes and the gun.”

“that part I tottaly don’t understand… it was a surprise even to me!”

Aliponiuliza kuhusu zile bahasha nilihisi huu ulikuwa muda muafaka wa mimi kuzifungua bahasha hizo kujua kulikuwa na nini ndani yake.
Nikaifungua bahasha ya kwanza.ndani yake kulikuwa na picha ya Delani na mkewe wakiwa pamoja na Luke na Ivanka wakiwa watoto. Ilikuwa ni picha sawasawa kabisa na ile picha ambayo niliichukua siku ile kwenye nyumba ya kule Affoltranasse.

“I know this photo!” Winnie alihamaki.

Naam sikushangaa Winnie kusema anaijua picha hii kutokana na uwepo wa picha kama hii kule kwenye nyumba ya Affoltrenasse ambayo niliiba siku kadhaa zilizopita.
Nikafungua bahasha ya pili. Ndani yake kulikuwa na picha ya Delani akiwa pamoja na yule jamaa ambaye nimekuwa nikimuona mara kadhaa, yule jamaa anayevaa kofia ya pama na koti refu jeusi. Tofauti pekee kwenye picha alikuwa anaonekana hana lile kovu alilonalo sasa usoni.
Nikamweleza Winnie kwamba ninazo piacha nyingine kadhaa zikimuonyesha Delani akiwa na watu wengine tofauti tofauti. Nilihisi kwamba siri yote ambayo natakiwa kuijua imefichwa kwenye hizi picha. Natakiwa kuzitazama picha zote hizi na kisha kujaribu kutafsiri kile ambacho kimejificha kwenye picha hizi maana ndicho kitu pekee kinachoonyesha kina umuhimu mkubwa kwenye kisanga chote hiki.

“I agree with you but we need to get a safe place and rest for the night!” Winnie alinijibu.

“Sure! The problem is I don’t think if its safe anymore for me to go back to Hardstrasse or for you to go back to your place!”

“you said stall, confuse, deflect! That’s what we going to do… I have an idea.!” Winnie aliongea huku anatabasamu kwa bashasha na kung’oa gari.

Japokuwa tulikuwa kwenye dhahama kubwa lakini kulikuwa na kitu fulani kikubwa juu ya Winnie kilikuwa kinajengeka moyoni mwangu. Nilihitaji ‘upako’ wa ziada niweze kumshinda shetani kwenye kile ambacho nilihisi kinaweza kutokea kati yangu na Winnie siku si nyingi.



Itaendelea…


Habibu B. Anga ‘The Bold’
To Infinity and Beyond
 
VIPEPEO WEUSI

SEASON 2 – FROM ZURICH WITH RULES


EPISODE 29


Nilifika mtaa wa Freatch West karibia majira ya saa mbili na nusu usiku. Mtaa ulikuwa kimya tofauti na kawaida kama ambavyo niliufahamu kipindi bado nakaa hoteli ya Radison Blu. Nilihisi labda ni kutokana na matukio ya maujai ambayo yametokea ndio yalifanya watu wawe na hofu kutembea usiku katika mtaa huu. Nilishuka kwenye taxi umbali wa kama hatua ishirini kutoka mahala ambako ule mgahawa wa kichina ulipo ambapo Winnie alinielekeza kuwa yuko ndani yake. Nilihitaji kuyasoma mazingira kabla ya kuingia ndani ya mgahawa huu.

Nilitembea na kufika kama hatua kumi kutoaka ulipo malango wa mgahawa. Uzuri ni kwamba upande huu wa barabarani wa mgahawa kama ilivyo desturi ya migahawa mingi ya nchi za magharibi ulikuwa ni wa kioo tupu kwa hiyo niliweza kuona ndani bila wasiwasi kabisa. Japo kuwa ilikuwa ni mapema kabisa saa mbili unusu usiku, lakini ndani ya mgahawa kulikuwa na watu wachache sana. Niliweza kumuona Winnie akiwa amekaa kwenye meza ya peke yake kukiwa na kikombe cha kahawa mezani. Winnie alikuwa amevalia sweta la mikono mirefu na alikuwa amelivuta mpaka kufunika viganja vya mikono. Kwa namna ambavyo alikuwa amekaa tu mtu yeyote angeweza kuhisi woga ambao Winnie alikuwa nao.

Meza kama ya tatu kutoka aliko Winnie alikuwa amekaa mzee wa kichina na mkewe ambao walionekana wanapata mlo wa jioni kama kawaida. Meza nyingine kulikuwa na kijana wa kizungu, mwanaume ambaye pia alikuwa anapata kahawa. Nilijaribu kuangaza macho huku na huko labda niweze kung’amua huyo mtu ambaye Winnie alidai anamfuatilia lakini sikuweza hata kuhisi… nje ya mgahawa kulikuwa hakuna mtu yeyote yule na watu wote ambao walikuwa ndani ya mgahawa hakuna ambaye alinifanya nimtilie mashaka.
Nikaufuta mlango wa ngahawa na kuingia ndani.

“Hey… you ok?” nilimuuliza Winnie huku nikikaa kwenye kiti baada ya kufika kwenye meza ambayo aliketi.

“No I’m not… I’m far from ok!” Winnie aliongea kwa wasiwasi huki analivuta vuta sweta lake viganjani.

“What are you doing here?” nilimuuliza. Ilikuwa ni jambo la ajabu sana kwangu Winnie aliponiambia kuwa yuko kwenye mgahawa huu hasa baada ya kuonana tu na mimi masaa machache yaliyopita.

“They called me again!” alinijibu huku ananiangalia kwa uso wa wasiwasi

“Who called you?”

“The guy who gave me the job… the one I told you about earlier today!” Winnie alinijibu.

Nilimuelewa kwamba alikuwa anamaanisha yule jamaa ambaye alimpigia simu miaka miwili iliyopita na wakakutana katika mgahwa huu huu na kumpa kazi ya kusafisha nyumba ile ya mtaa wa Affoltentrasse.
Wanasema tano watu wa mjini wenye kujielewa,,chukua gwala broo
 
Ulipita ukimya wa karibia dakika tatu nzima tukiwa ndani ya gari pasipo yeyote kusema neno wala kung’oa gari. Nilikuwa nimefumba macho na kujilaza kwenye siti nikijaribu kuiweka akili yangu iwaze vyema sawa sawa. Nilishtushwa na mikono laini ambayo ilikuwa imenigusa usoni kama inanipapasa.

“Let me take a look at that!” Winnie alikuwa amenishika kichwa na kukigeuza kutaka kuangalia vyema lile aneo ambalo yule mzee alikuwa amenipiga ngumi. Mwanzoni pale jikoni sikutambua ila sasa hivi ndio niligungua kuwa palikuwa pamechanika na kulikuwa na damu kidogo zilitoka japo kwa sasa zilikuwa zimekoma kutoka.

“Leave it alone… its ok!” nilimtoa mikono yake usoni na kuinuka na kukaa vyema wima.

Kilipita kimya kingine cha dakika moja nzima bila yeyote kuongea lakini wote wawili tulijua kabisa ni kitu gani ambacho tunapaswa kukizingumza.

“what’s going on Ray?” Winnie aliuliza hatimaye na aliuliza kwa sauti ya upole kabisa na utulivu kana kwamba alikuwa ananionea huruma.

“I don’t even know where to start!” niliongea huku nimefumba macho.

“Start from where you said this was a trap!”

Nilitafakari kwa muda wa kama sekunde ishirini hivi kisha nikaanza kumueleza Winnie. Kwanza nilimueleza kwa kifupi kuhusu uwepo wa kikundi cha HUDINI na namna ambavyo wanapaswa kunipa taarifa ambazo zimenifanya nije hapa Zurich. Kisha nikamueleza wasiwasi wangu kwamba kuna uwezekano kuna watu wengine nje ya HUDINI nao walikuwa wanaitaka taarifa hiyo ambayo HUDINI wanayo. Nilimueleza ni kwa namna gani ambavyo maelezo alinipa juzi kwamba kuna watu wamekuwa wakimfutilia kwa muda wa wiki tatu zilizopita kwa kupaki gari nje barabarani kwenye ile nyumba mtaa wa Affoltranasse. Nilimueleza kwamba nina imani kubwa waliomuajiri ni mawakala wa HUDINI kwa hiyo hawana sababu ya kumfutilia kwa hiyo hii ilimaanisha kwamba watu ambao wanamfuatilia ni wengine nje ya HUDINI. Nikamweleza Winnie pia kwamba HUDINI hawana sababu ya kunifuatilia mimi kwa sababu walikuwa wanajua naishi wapi hapa Zurich na mambo mengine yote. Kwa hiyo kitendo hiki cha kufuatiliwa kilikuwa kinaonyesha dhahiri kabisa kwamba kulikuwa na watu wengine wapinzani wa HUDINI. Lakini pia nilimweleza kuhusu mauaji ya Luke na Ivanka siku mbili tu baada ya mimi kuonana nao iliashiria dhahiri kabisa kwamba Ivanka na Luke kuna uwezekano mkubwa walikuwa ni mawakala wa HUDINI na waliuwawa na wapinzani wao.
Baada ya hapo nilimueleza kwa nini nilihisi kwamba kuitwa kwake hapa kulikuwa ni mtego… kwanza kabisa nikamueleza kwamba ahiingii akilini mtu amuite kumwambia sentesi moja tu kuwa “kamwe asimruhusu mtu kuingia ndani ya nyumba ile ya mtaa wa Affoltrenasse”. Kwa hiyo hisia yangu ni kwamba HUDINI walikuwa wanafanya ‘counter-survaillance’, kwamba walikuwa hawajui kinagaubaga adui yao ni nani kwahiyo walimtumia yeye kumuita hapa wakijua kuna uwezekano mkubwa na yeye kuniita mimi hapa ili wote tukiwa sehem moja ni chambo kizuri cha hao watu wanaotufuatilia kufanya hivyo na papo hapo HUDINI kutumia mwanya huo kuwang’amua wabaya wao.

Nakumbuka Winnie aliniuliza kwa nini HUDINI wasinipe tu hiyo taarifa ninayotakiwa kuwa nayo ili niondoke na kuepusha madhila yote haya. Nikamjibu kwamba hisia yangu ni kwamba HUDINI walikuwa wanaogopa kunipa taarifa hiyo kienyeji au kirahisi rahisi kwa kuhofia taarifa hiyo inaweza kuchukuliwa kwa urahisi kutoka kwangu na hao maadui zao.
Hapa ndipo ray akili yake imekuwa kubwa
 
VIPEPEO WEUSI


SEASON 2 – FROM ZURICH WITH RULES



EPISODE 31


Winnie ndiye ambaye alikuwa amekaa kwenye usukani akiendesha gari na mimi nikiwa kwenye siti ya abiria. Alikuwa amekata kona kuingia mtaa wa Affoltrenasse. Kichwani nilikuwa tayari nimehisi ni wapi ambapo tulikuwa tunaelekea. Alipokata kona tu kuingia mtaa wa affoltrenasse nilimuangalia na kutabasamu na yeye alinikata jicho na kutabasamu pia. Tulikuwa tunaelekea kwenye ile nyumba ambayo ameajiriwa kufanya usafi, nyumba ambayo masaa machache yaliyopita alionywa kwamba asimkaribishe mtu yeyote yule ndani.
Tangu ambapo tulitoka kule kwenye mgahawa wa kichina mpaka kufika hapa affoltrenasse kulikuwa na ukimya fulani umetawala kati yetu. Ukimya ambao ulikuwa kana kwamba unabembeleze kitu fulani kisemwe. Kitu ambacho hakipaswi kusemwa na hakikuwa na ulazima wa kusemwa kwa sababu wote kati yetu kilianza kujengeka mioyoni mwetu. Kitu kilichokuwa kinafanya ukimya huu kati yetu kwa dakika chache kuwa kama bakshikshi ya kuchochea uthibitisho wa kile ambacho tulikuwa tumeanza kukihisi mioyoni mwetu lakini tukifanya juhudi za kutaka kukizima.

Tulikuwa tayari tumefika mbele ya nyumba mtaa wa affoltrenasse na kupaki gari. Kulikuwa na kimvua fulani chepesi kimeanza kunyesha.
Tulikaa kimya kwenye gari kwa karibia dakika tatu nzima bila yeyote kati yetu kusem chochote. Sikujua kama Winnie alikuwa anatafakari namna ambavyo tulikuwa tunaelekea kuvunja agizo alilokuwa amepewa kwamba asimkarinishe mtu ndani ya nyumba ile au kama alikuwa anawaza kile ambacho nilikuwa nakiwaza mimi kichwani mwangu… nini kitatokea kati yetu leo hii gizani?

“are you ready for this?” Winnie aliniuliza nikiamini kwamba alikuwa anamaanisha kuhusu kuingia ndani ya ile nyumba kinyume na maagizo ambayo alikuwa amepewa.

“not so sure!” nilimjibu huku natabasamu.

“Let’s do this!!” aliongea na mara moja akafungua mlango na kutoka nje ya gari, nami nikafanya hivyo.

Kutokana na ile mvua ndogo ambayo ilikuwa inanyesha Winnie alikuwa amejikumbatia mikono akiiweka kifuani mwake huku anakimbia kuelekea kwenye mlango wa nyumba. Sijui kama ni kwasababu ya mvua au kutokana na umbo lake lakini nilihisi kama vile nguo zake zimekuwa nyepesi zaidi mwilini mwake na kumfanya akiwa anakimbia mwili wake ulivyokuwa unatikisika kufanya nisikie kama cheche zinapita mwilini mwangu. Nilijikuta nasikia wivu namna ambavyo matone ya mvua yalikuwa yanatiririka mwilini mwake nikitamani kana kwamba matone yale ya mvua yangelikuwa ni kiganja changu cha mkono kikiambaa ambaa mwilini mwake namna ile.

“Are you coming or what?” Winnie alinigutusha kutoka kwenye mgagaziko uliokuwa umenikuta ghafla nikivuta hisia na kujikuta nimesimama bila kutembea katikati ya mvua nikimtazama bila kujijua.
 
“Coming.!” Nikaanza kukimbia kutoka kwenye mvua na kuelekea kwenye mlango wa nyumba.

Pembezoni mwa nyumba kulikuwa kuna maua ambayo yalikuwa yamaeoteshwa kwenye bakuli kubwa za udongo za urembo. Winnie alitembea mpaka kwenye bakuli kama ya nne hivi kutoka mlangoni na kuifunua na kisha kuingiza mkono chini yake na kutoka na funguo.

“Oh so there is where you keep the keys!” nilongea kwa utani.

“Yap! For emergencies..” Winnie alijibu huku anakimbia kutoka pale kukwepa mvua na kurudi mlangoni.

“Emergencies!?”

“Yeah! Like today.”

Tukacheka kisha Winnie akafungua mlango tukaingia ndani.

“I’m such a bad girl!” Winnie aliongea kwa sauti ya utani.

“Why is that?” nikamuuliza

“First date and I’m taking you back home.” Akaoongea tena kwa utani

“I like naughty girls!” nikamjibu pia kwa utani.

Yalikuwa ni maneno ya utani lakini kichwani mwangu nilikuwa namaanisha kila neno ambalo nililisema. Nilitamani kwamba naye kchwani mwake awe japo na asilimia fulani ya kumaanisha kwa haya maneno ya utani ambayo ameyasema.

“Don’t turn on the lights.” Niliongea kwa sauti ya kunong’ona.

“why?”

“that’s the easiest way for someone to know that we are inside.”

“I bet they already know we are inside.” Winnie alinijibu lakini hakuwasha taa kama ambavyo nilitaka.

Japokuwa kulikuwa na giza lakini niliweza kuona kwa mbali mule ndani. Kulikuwa kama ambavyo nilipaona siku ya kwanza. Nadhifu na pamepangiliwa sawia kabisa kana kwamba kuna watu wanaishi ndani yake.
Nilikuwa natamani kuichunguza hii nyumba nukta baada ya nukta nikiamini kabisa kwamba kuna baadhi ya maswali ambayo nitayapatia majawabu. Lakini nilikuwa nashindwa kabisa kubandua macho yangu kutoka kwa Winnie ambaye alikuwa amesimama kwenye moja ya dirisha kuangalia nje barabarani kana kwamba anahakikisha hakukuwa na mtu ambaye alikuwa anatufuatilia.
Kutokana na giza ambalo lilikuwa humu ndani lilifanya pale dirishani ambapo alikuwa amesimama na mwanga hafifu ukimmulika kutokea nje kulifanya apendeze zaidi kumuangalia umbo lake ambalo nguo zilikuwa zimeshika mwili sawia kutokana na mvua ndogo ile ambayo ilikuwa imemnyeshea.

Damu illikuwa imeanza kunichemka nikisikia mshawasha wa cheche ukitembea mwilini.
 
“what are you looking at!” Winnie aliongea kwa sauti ya nyororo ya ushawishi kama ananong’ona bila kugeuka kuniangalia. Nilihisi kabisa namna ambavyo hata yeye mwili wake unawaka moto wa matamanio muda huu.

Sikujibu. Nilipiga hatua za taratibu kumfuata pale dirishani ambako alikuwa amesimama. Nilikuwa nahema taratibu lakini niliusikia moyo namna ambavyo ulikuwa unadunda kwa nguvu kama unakaribia kutoka nje ya kifua. Winnie alinisikia namna ambavyo nilikuwa namsogelea lakini hakugeuka, aliendelea kusimama vile vile akiwa amenipa mgongo.
Nilisogea mpaka kufika nyuma yake kabisa tukigusana, makalio yake yakinigusa katikati ya mapaja yangu, uso wangu ukiwa nyuma ya kichwa chake ukiparaza nywele zake laini. Winnie hakusogea wala kutikisika, kitu pekee ambacho nilikisikia ni namna ambavyo alikuwa anahema kwa nguvu kama vile anapanda mlima. Taratibu nikapenyeza mikono yangu ubavuni kwake mpaka mbele kifuani kwake na kumkumbatia kwa nguvu nikimvuta kwangu. Japokuwa alikuwa ameloa kiduchu na ile mvua lakini mwili wake ulikuwa ni wa moto kana kwamba alikuwa amebanikwa kwenye jiko la mkaa.
Niliusikia namna ambavyo mwili wake ulikuwa unaitika kwa kulegea nyang’anyang’a kana kwamba ulikuwa unapasuka vipande vipande. Nilihisi namna ambavyo alikuwa ameishiwa nguvu… akalaza shingo yake begani kwangu.

“you are so beautiful!”

Nilimnongoneza taratibu sikioni kama vile namng’ata. Niliusikia mwili wake namna ambavyo ulisisimkwa nilipokuwa nanong’ona sikioni mwake. Alikuwa anahema kwa nguvu nikihisi ameishiwa nguvu kiasi kwamba alikuwa kuna kitu anataka kusema lakini alishindwa na kuishia kutoa miguno tu…

“Mmmmmhhhh.!”

Nilimkumbatia kwa nguvu zaidi huku mikono yangu kifuani kwake nikiipa uhuru wa kubinya chuchu za matiti yake taratibu. Alikuwa anajinyonganyonga kana kwamba anataka kujinasua mikononi mwangu lakini kwa namna ambavyo utamu ulikuwa umemkolea nilihisi alikuwa anataka zaidi.
Akaanza kwa kupeleka mkono wake mpaka juu ya suruali yangu na kuanza kuushika mkuki akipeleka mkono juu na kurudisha chini. Nilihisi kama vile suruali ilikuwa inakaribia kuchanika kwa namna ambavyo mkuki ulichachamaa ndani ya suruali. Nikamvuta tena kwangu kwa nguvu zaidi… bado tulikuwa hatuangaliani uso kwa uso. Alikuwa amegeukia dirishani na mimi nimekumbatia mgongoni.
Nilikuwa nimepandwa na mori iliyochanganya hasira na matamanio na hamu kubwa haswa ya kutaka kuusulubisha mwili wake usiku mzima wa leo.
Nilimvuta kwa nguvu haswa na kuzama shingoni mwake nikiilamba na kuimungunya shingo kama pipi. Winnie alikuwa anajinyonga nyonga kama vile nyoka aliyemwagiwa mafuta ya taa huku anatoa miguno mikubwa akiendelea kuhema kwa taabu sana. Taratibu niliusikia mkono wake akiuzamisha ndani ya suruali yangu na kwenda kuushika mkuki akifanya kama mwanzoni akiupeleka mkono juu na kuushusha chini.
Uzalendo ulinishinda nikamkamata kwa nguvu na kumgeuza tukawa tunaangaliana.

Alikuwa anahema kwa nguvu kama anataka kukata roho. Nilijikuta ghafla kwa hasira na mori ya matamanio nimeikamata blauzi yake na kuichana kwa nguvu kutoka kifuani mwake. Sikujua kama Winnie alikuwa hajavaa braa au kama niliichana pamoja na ile blauzi, lakini ninachokumbuka ni Winnie alikuwa mbele yangu kifua wazi matiti yakiwa yamesimama kama kigoli wa miaka kumi na saba. Hii ilikuwa ni moja ya nyakati chache ambazo niliweza kusifu ufundi na umaridadi wa aliye juu katika uumbaji wake. Katika wakati huu kama ningepewa kontena lililojaa dhahabu na mwili wa Winnie, hakika
 
ningelichagua mwili huu ambao ulikuwa mbele yangu muda huu nikiutazama. Namna ambazo matiti yake yalikuwa yamejaa sawia kifuani mwake, chuchu zikiwa zimesimama kama mwali wa kimanga, na tumbo lake tambarare kama sakafu ambalo lilijiunga vyema kwenye kiuno chembamba ambacho kilikuwa kinashawishi kukimata na kukisulubisha … kwa hakika alipoumbwa muumbaji alitulia.
Winnie alikuwa bado anahema kwa nguvu… alinishika shingoni kwa nguvu na kunivuta midomoni mwake. Niliibusu midomo yake na kuinyonya ndimi yake kana kwamba ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kwenye maisha. Morali na mshawasha ambao tulikuwa nao ulifanya tunyonyane ndimi kama vile tulikuwa tunapigana. Mkono wake ulizama tena ndani ya suruali yangu na mimi nilikuwa natembeza mikono yangu mgongoni mwake, kushuka mpaka kiunoni na mpaka chini ya kiuno kwenye ‘mitungi’ miliwi iliyounganishwa na kiwili wili chake chini ya kiuno. Nikaanza kumvua kisuruali chake taratibu mpaka ilipofika magotini ambako alimalizia mwenyewe kuivua kwa kuikanyaga na upande mmoja na mguu na ilipovuka upande mmoja akakanyaga tena upande mwingine.

Winnie alikuwa amesimama mbele yangu akiwa mtupu kabisa isipokuwa nduo ya ndani tu. Mimi nilikuwa kifua wazi na suruali mkanda ukiwa tayari umefunguliwa. Tulikuwa tunanyonyana ndimi kwa nguvu na morali huku mkono wangu mmoja ukipapasa ‘mitungi’ yake na kumvua nguo ya ndani taratibu.
Sijui ni nini ambacho kilinitokea lakini nilipoanza kumvua Winnie nguo ya ndani sura ya mkewangu Hasnat, Cheupe wangu ghafla ilikuwa inanijia akilini… nilijikuta nimejinasua kukota kwenye mikono ya Winnie.

“I can’t do this!” niliongea huku nahema.

Winnie akafanya kama vile hajanisikia. Alinirukia na kunivuta tena mdomoni mwake na kuingiza tena mkono ndani ya suruali.

“No no no! stop..!” nilijinasua tena kutoka mikononi mwake huku nikihema kwa nguvu.

Winnie naye alikuwa anahema kwa nguvu huku amenikodolea macho akishangaa akiwa haamini kile ambacho nilikuwa nakisema.
Sikujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kinanisibu lakini haijalishi ni kwa kaisi gani nilijitutumua kiume kupoteza nisimuwaze cheupe kwa wakati huu nilishindwa na sura yake ilikuwa imejaa kwenye akili yangu. Nilijisikia hatia moyoni kiasi kwamba hata morali ya ‘kumsulubisha’ Winnie ilipotea. Ule mshawasha wa mapenzi wote uliyeyuka ghafla… nilibakiwa na hatia tu moyoni.

“I’m so sorry Winnie! I can’t do this..!!” niligeuka pembeni kwa aibu.

Hakuna kitu kibaya kama kumvua nguo zote mwanamke alafu uhairishe kufanya tendo lenyewe. Nilimuona Winnie akijisikia aibu kiasi kwamba nilihisi alitamani akimbie kutoka mle ndani. Alikaa chini na kujikunyata akificha matiti yake kwa viganja vya mikono huku anazoa zoa nguo zake kutoka sakafuni. Sidhani kama nimewahi kujisikia aibu kwa kiasi kile. Nilijisikia aibu na hasira kwa nafsi yangu kwa hiki ambacho kilikuwa kinatokea.

“I’m sorry!” niliomba tena radhi huku nikienda upande mwingine wa sebule na kukaa chini nikijiinamia.

Winnie hakusema chochote kile, nilimsikia tu akiwa na purukushani za kuvaa nguo haraka haraka. Alipomaliza kuvaa nguo naye alikaa chini sakafuni lakini hakujiinamia… alikuwa ananitazama kwa hasira bila kusema chochote. Nilikosa hata ujasiri wa kumuangalia. Nikajiinamia chini.
Tulikaa hivyo kwa muda wa kama dakika kumi nzima bila yeyote kati yetu kuongea. Winnie akiwa ananitazama kwa hasira na mimi nimejiinamia chini.
Nikamsikia Winnie amesimama na anagusa gusa funguo mkononi.

“There is something I want to show you… I think might help us… come with me!” aliongea bila kuniangalia huku anaanza kutembea.

Nilishtuka kutoka kwenye kujiinamia kwa mawazo na kuinuka na kuanza kumfuata ambako alikuwa anaelekea… kwenye ‘basement’ ya nyumba.



Itaendelea…


Habibu B. Anga ‘The Bold’
To Infinity and Beyond
 
Shukrani sana Mkwe!

Hii ya leo kali, mpaka mitungi na mikuki imehusika!

[emoji39][emoji39][emoji39]
 
Shukran mkuu Habibu.

Kuna watu wana uthubutu, hii ya Ray mimi siiwezi. Winnie lazima angemalizwa.
 
Tafadhali ndugu yangu The bold naomba uniweke kwenye tag list yenu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom