Vipepeo weusi season 2: From Zurich with rules

Mkuu The Bold sikukuu inaisha bila bila? Kama kuna chochote kirushe Mkuu tuendelee kufurahia sikukuu.
 
Jamaa kafichwa na

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nifa tafadhali tunamuhitaji The Bold, aje haya asalimie tu basi.
 
VIPEPEO WEUSI

SEASON 2 - FROM ZURICH WITH RULES

EPISODE 32

"…wanasema tunajifunza kwa makosa ya awali, si kweli. Tunafanya makosa, tunahisi tumejifunza, kesho tunafanya makosa tena, tunahisi tena tumejifunza lakini mtodogoo tunafanya makosa kwa mara nyingine. Ni asili ya mwanadamu, kupungukiwa utimilifu. Japokuwa ni asili ya binadamu lakini bado haiondoi maumivu tunayoyasikia pale udhaifu wetu wa asili unaposababisha machozi kwa wale ambao wanatupenda zaidi, haiondoi kujuta pale ambapo udhaifu wetu unapopelekea usaliti na kuumiza nafsi za wanaotupenda sawa sawa na maisha yao. Ni maumivu haya ambayo yanafanya tukiona machozi ya watupendao tuhisi kama uhai umetutoka nafsini mwetu, tusikie hatia mioyoni mwetu kiasi kwamba tunasikia mpaka harufu ya kifo.
Ni nini basi cha kutuokoa na udhaifu huu wa asili? Je tunapaswa kuishi tukiukubali udhaifu huu? Tuendelee kufanya makosa? Tuendelee kuwaumiza wanaotupenda? Labda pengine maumivu haya yanasababishwa na ulimwengu kutegemea makubwa kutoka kwetu. Labda ujasiri wanaona tunao unawafanya wadhani ni watimilifu, labda wingi wa akili tulizonazo unawafanya wahisi hatupaswi kukosea na pengine labda vipawa adhimu tulivyojaaliwa vinawapofusha wasione ukweli, ukweli dhahiri kabisa, ukweli usiopaswa kupuuzwa kwamba licha ya ujasiri wote, licha ya akili zote, licha ya vipawa vyote…. *I am only human.!!* Tunakosea, tunajifunza, kesho tunakosea tena, tunajifunza… na iko siku tutakosea tena..!"

*Mtaa wa Hardstrasse, Zurich*

Nilikuwa nimeamka tena kwa mara ya pili hii ndani ya siku hii hii moja. Ilikuwa inakaribia saa kumi jioni, na kilichoniamsha ilikuwa ni mlio wa simu. Simu ilikuwa imeita mara mbili hapo awali na sikuijibu lakini safari hii niliamua niamke ili kuijibu.

"still sleeping?" Ilikuwa ni sauti ya Winnie upande wa pili wa simu.

"I was… morning!" Nilimjibu huku napiga mihayo.

"Its evening idiot! Are you coming?" Winnie aliongea kwa sauti ya utani aliponiuta 'idiot' lakini aliponiuliza kama naenda sauti ilibadilika akionekana kumaanisha.

"Did you get it?" Nikamuuliza kwa shahuku.

"Yap… got it!"

"On my way!" Nikakata simu.

Tangu awali ambapo simu ilikuwa inaita japo sikuangalia lakini nilijua kabisa lazima simu hiyo itakuwa ya Winnie. Nafsini mwangu nilikuwa sina ujasiri kabisa wa kuongea nae kutokana na kile ambacho kilitokea baina yetu jana usiku. Nilikuwa nasikia mzigo wa hatia moyoni. Japokuwa hatukufanya tendo la ngono kabisa lakini kitendo cha kutomasana tu kiasi kile ambacho tulifikia moyoni nilikuwa nasikia hatia ya kumsaliti mkewangu Cheupe. Nilitamani niinue simu nimtwangie mkewangu nyumbani Tanzania lakini moyo ulikuwa haupati ujasiri.
Lakini pia kila ambapo nilifikiria kuonana tena na Winnie moyo wangu ulikuwa unapasuka vipande. Nawezaje kumtazama tena usoni? Ajabu ni kwamba sikuwa nasikia aibu kwa kutomasana vile bali nilikuwa najisikia aibu kwa kumchombeza na kumtomasa na kisha kuishia njiani bila kufanya tendo lenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini hii ilikuwa ni tofauti kabisa na winnie kwa namna ambavyo alikuwa anaongea kwenye simu utadhani kama vile hakukuwa na chochote kile kilichotokea jana usiku. Nilihisi kwamba hakutaka kuwe na 'tension' katikati yetu ukizingatia hii dhahama tuliyonayo. Alikuwa anajitahidi kwa nguvu zote kufanya mazungumzo nami kwa namna ya kawaida kana kwamba hakuna chochote ambacho kimetokea.

Tangu jana usiku tulipoishia katikati ya mchezo ambao tulikuwa tunataka kuufanya Winnie hakuwahi kuniuliza kwanini sikutaka kufanya nae ngono wala kugusia kwa namna yoyote ile mazungumzo yenye mlengi huo. Badala yake jana ile usiku alichepusha maongezi na kunipeleka kwenye basement ya ile nyumba ya mtaa wa Affoltrenasse. Kwenye basement ambayo alinionyesha vitu ambavyo mpaka muda huu ubongo wangu umekuwa mzito nikiogopa hata kuviwaza.

Wazo hili la kumbukumbu ya vitu ambavyo niliviona kwenye basement lilivyoanza kurejea kichwani niliacha kulifikiria haraka na kuinuka kutoka kwenye sofa ambayo ndio naitumia kama kitanda changu kwenye jengo hili la hapa Hardstrasse. Niliinuka haraka haraka na kuanza kuvaa nguo ili niweze kuelekea chuo kikuu cha Zurich alipo Winnie. Kwa hakika kabisa nilikuwa sitaki abadani kuonana na Winnie lakini taarifa ambayo alikuwa ananieleza kuwa anayo ilikuwa ni ngumu kuipuuza nisiende kutazama hicho alichokipata.

Tulipoachana asubuhi kutoka pale affoltrenasse nilimueleza kwamba sikutaka kufikiria chochote kile kuhusu kile ambacho alikuwa amenionyesha kule chini kwenye basement. Nilikuwa nataka tufanyie kazi mfululuzo wa picha ambazo nimekuwa nazipata kuanzia zile ambayo niliikuta kwenye bahasha niliyoachiwa na marehemu mzee wangu, ile niliyopewa na Hudini na hii ambayo nilipewa jana na yule mzee wa kichina. Katika picha zile zote kulikuwa na kitu kimoja kikuu ambacho kiko kwenye picha zote… Delani. Yule mzungu anayeonekana kwenye picha akiwa na Rais Albert Kafumu kwenye eneo lenye makontena, ni yeye pia alikuwa kwenye ipe picha pamoja na Cheupe na baba yake na ni yeye pia alikuwa kwenye picha ambayo nilipewa jana na yule mzee wa kichina ambayo inamuonyesha Delani akiwa na yule jamaa mwenye kuvaa kofia ya pama na koti refu jeusi.

Ilikuwa ni dhahiri kwamba kwa namna yeyote ile nilikuwa napaswa kuonana na Delani ambaye anaonekana ni kiunganishi cha watu wote hawa. Lakini kwa muda wa miaka miwili sasa hakuna ambaye anajua Delani yuko wapi. Wazo la pili ambalo tulilizungumza na Winnie ni kujaribu kumpata mmoja kati ya watu wale ambao anaonekana kwenye mojawapo ya zile picha. Ilikuwa haiwezekani kumpata Rais Albert Kafumu. Winnie akapendekeza nizungumze na Cheupe. Nikamkatalia. Cheupe alikuwa haungi mkono safari yangu ya hapa Zurich, kwahiyo napaswa kutafuta wakati mujarabu haswa ili kumuuliza kuhusu picha hiyo ya yeye akiwa mtoto pamoja na baba yake na bwana Delani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo mtu pekee sahihi ambaye walau alikuwa ana uwezekano wa kumpata alikuwa ni yule jamaa wa kofia ya pama na koti refu jeusi. Walau huyu tulikuwa tunajua pasina shaka yeyote kwamba yuko hapa Zurich. Kama tukiweza kumtafuta na kumpata jamaa huyu walau tutakuwa na matumaini hata kiduchu na mwongozo wa kumpata Delani.
Ndipo hapa ambapo tulikubaliana kutumia namba ya taxi ambayo yule jamaa wa kofia ya pama aliitumia kuja nayo pale chuoni na kupaki ng'ambo ya geti kuu la kuingilia chuo juzi wakati ambapo nilikuwa naongea na Winnie. Kwa bahati nzuri wakati taxi inaondoka nilifanikiwa kunakili namba yake, ZH 45789.

Nilikuwa na imani kwamba kama nitaweza kumpata dereva taxi ambaye alikuwa anamuendesha yule jamaa siku ile basi naweza kumng'ang'aniza hata kwa hongo aniambie alimpeleka wapi yule jamaa walipotoka pale chuo na nikifahamu mahali ambako alimpeleka basi tunaweza kuanzia hapo kufuatilia nyendo za yule jamaa.
Lakini ili tumpate yule dereva taxi, tunapswa kufahamu taxi ile ni ya kampuni gani, na ofisi zao ziko wapi na jina la dereva taxi ambaye alikuwa anaendesha taxi siku ile. Uzuri ni kwamba taarifa zote siku hizi ziko kwenye mifumo ya kompyuta. Lakini hatuwezi kuipata taarifa hiyo kwa urahisi pasipo ruhusa ya wenye kampuni. Tunapaswa kufanya uhuni mpaka tuipate.
Winnie alinieleza kwamba chuoni kwao anawafahamu baadhi ya wanafunzi kutoka Nigeria ambao ni watundu wa mifumo ya Tehama.

Tukakubaliana kwamba aipeleke namba hii ya taxi kwa wanafunzi wenzeke hao na wakimpa majibu stahiki ndipo anipigie ili tuanze mchakato wa kumtafuta huyo dereva taxi na hatimaye yule jamaa wa kofia ya pama.

Maongezi haya tuliyaongea asubuhi wakati tunatoka kwenye nyumba ya affoltrenasse ambako tulilala jana usiku. Na sasa ilikuwa tayari saa kumi jioni na Winnie ananieleza kwamba tayari anayo taarifa kuhusu ile taxi ambayo yule jamaa wa kofia ya pama aliipanda juzi alipokuja pale chuoni.

Nilichukua simu yangu tena na kuingia mtandaoni na kufungua tovuti ya kampuni ya uuzaji 'fast food' ambayo iko karibu na mtaa huu wa hardstrasse. Niliagiza pizza niletewe. Kama ambavyo tulikubaliana na Jimmy kwamba nikimuhitaji basi niweke boksi la pizza nje ya mlango wa jengo hilo na akiliona usiku atakuja hapa nikiwepo. Nilikuwa namuhitaji Jimmy, nilikuwa namuhitaji anisaidie kung'amua kile ambacho nilikiona kwenye basement ya nyumba ya kule affoltrenasse.

Kama dakika saba baadae nilisikia mlango unagongwa. Uzuri nilikuwa nimemaliza pia kujiandaa. Nikachukua simu yangu na kutoka mpaka nje.

"Keep change!" Nilimlipa kijana wa pizza na kuipokea. Alipoondoka nilifunua upande wa juu wa boksi kwa ndani na kuandika "i need a doctor". Nikiamini kabisa kwamba Jimmy atahisi kwamba nahitaji aje aniangalie kidonda changu cha risasi tumboni. Hii ingemfanye aje haraka na bila kukosa.
Japo ilikuwa ni kweli nilimuhitaji aniangalie maendeleo ya kidonda… lakini nilimuhitaji zaidi kwa ajili ya kile ambacho nilikiona affoltrenasse. Mwili ulinisisimka kila ambapo nilikumbuka ile basement.

Nikaweka boksi la pizza chini mlangoni na kuondoka kuelekea chuo kikuu cha Zurich kuonana na Winnie.

Itaendelea…

Habibu B. Anga "The Bold"
To Infinity and Beyond

Sent using Jamii Forums mobile app
 
VIPEPEO WEUSI

SEASON 2 – FROM ZURICH WITH RULES

EPISODE 33

Tofauti na juzi ambapo mimi ndiye nilikuwa wa kwanza kufika na kumsubiri Winnie, leo hii nilimkuta tayari amefika pale kwenye lango la kuingilia chuoni kwao akinisubiri.

“you are late!” aliongea huku anatazama saa kwenye simu yake.

“sorry! Had a few things to attend first!”

Tuliongozana moja kwa moja na kuingia ndani ya eneo la chuo. Hostel zao wanazoishi zilikuwa kama mwendo wa dakika saba hivi kutoka pale kwenye lango kuu la kuingia ndani ya chuo. Muda wote huo ambao tulitembea kutoka pale getini mpaka kufika kwenye hosteli Winnie hakuongea neno lolote lile. Muda wote alikuwa anabofya simu yake.
Mwanzoni nilihisi labda alikuwa anajisikia aibu kutokana na kile ambacho kilikuwa kimetokea jana usiku, lakini nilipomtazama usoni nilimuona akiwa anatabasamu kila mara huku anaendelea kubofya simu yake. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza nikiwa na Winnie kumuona akiwa ‘bize’ na simu kana kwamba sikuwepo pale, nilisikia karoho kaniniuma kwa mbali lakini nikajitahidi kutoonyesha hisia zozote zile usoni. Tulitembea namna hiyo mpaka kwenye jengo la hostel ambalo alikuwa anaishi.

“Karibu.!” Winnie alinikaribisha kwa kuongea neno la Kiswahili fasaha kabisa tulipofika nje ya chumba chake. Nilitabasamu na kumjibu

“Asante sana!” nikamjibu pia kwa Kiswahili.

Tukaingia ndani.

kilikuwa ni chumba cha ukubwa wa wastani, kama futi kumi kwa futi kumi. Mtindo wake wa namna ambavyo kilipangiliwa ulikuwa unafanana sana na vyumba vya wanafunzi nyumbani Tanzania na kwa dakika kadhaa nikajikuta nakumbuka nilipokuwa mwanafunzi chuo kikuu Mzumbe miaka kadhaa iliyopita. Kulikuwa na kitanda cha futi nne kwa sita kwa namna ambavyo nilikadiria haraka haraka. Tofauti kubwa ya chumba hiki na nikikumbuka vyumba vya hosteli zetu za Mzumbe kilikuwa na nyongeza ya sehemu ya jiko, bafu na unadhifu wa vyumba hivi. Nilipotupa jicho kwenye meza yake ya kusomea nilijikuta napatwa na hasira fulani ya ghafla. Kulikuwa na mtu, mwanaume amekaa na kompyuta mpakato akibofya bofya.

“Ray! This is Dafa… he is the one who is helping us with the issue.!” Winnie alinitambulisha mara baada ya kuingia.

“hey man! Nice to meet you!” nilimpa mkono kumsalimia huku nikilazimisha kutoa tabasamu. Nilikuwa nachukia hali ya wivu ambayo ilikuwa inanikaba rohoni kumuona mwaume mwingine kwenye chumba cha Winnie.
“So what have you got?” nikamuuliza huku navuta kiti kilicho karibu na kukisogeza karibu yake pale mezani na kuketi.

“it was tricky at first but then I figured out…” yule jamaa niliyetambulishwa kama Dafa akaanza kunielezea kile ambacho alikuwa amefanikiwa kukipata baada kupatiwa ile nambari ya gari.

Kama ilivyo kawaida ya wataalamu wa mambo ya kiufundi, hasa wataalamu wa teknohama, alianza kubwabwaja masuala ya kiufundi ambayo nilikuwa siyaelewi wala sihitaji kuyajua. Akanieleza kuhusu namna ‘alivyocheza’ na proggramu za kompyuta mpaka kufikia kudukua taarifa kutoka kwenye mifumo ya serikali na hatimaye kwenye kampuni inayomiliki ile taxi.

“Did you find our guy?” nikamuuliza kwa kukereka baada ya kumuona hamalizi kubwabwaja msuala ya kiufundi aliyokuwa ananieleza.

“easy… easy! Found him… here!!” aliongea na kunionyesha kwenye kioo cha kompyuta.

Nikaanza kusoma kwa makini. Maelezo pale kwenye kioo cha kompyuta ambayo yalionyesha kwamba, taxi ile yenye namba za usajili ZH 45789 inamilikiwa na kampuni ya usafirishaji hapa Zurich inayoitwa Alp Limo. Baada ya maelezo hayo kulikuwa na maelezo mengine mengi mno ambayo nilikuwa siyaelewi.

“Where is our guy.!?” Nilimuuliza kwa mshangao kwa sababu kulikuwa na maandishi mengi sana yanayofuata baada ya jina la kampuni ambalo liliambatana na ile namba ya taxi.

“Look closer.!” Aliongea huku ananionyesha kidole kwenye kioo cha kompyuta.

Nikatazama tena kwa makini zaidi na ndipo ambapo nikagundua kuwa maelezo yale yalikuwa kama ‘log book’… ratiba fulani hivi au kumbukumbu. Ilikuwa inaonyesha taxi gani ilikuwa inaendeshwa na dereva gani na siku ipi. Nikaangaza macho yangu kwenye jedwali ambalo lilikuwa linaonyesha nambari za taxi. Nikayapepesa kwa kushuka chini mpaka nilipoiona namba ZH 45789. Nikaangaza pembeni yake mpaka siku ya juzi na kutazama jina la dereva ambaye alikuwa anaendesha taxi hiyo…

“Vihaan Singh!” Nilisoma pale juu ya kioo na kumtazama Dafa. “Is this our guy?” nikamuuliza.

“That’s your guy!” alinijibu huku anabofya bofya tena kompyuta… “found his address too… here it is!”

Nilitoa simu yangu haraka haraka na kunakili anuani ambayo ilikuwa inaonekana pale kwenye kompyuta. Anuani ilikuwa inaonyesha kwamba Vihaan Singh anaishi mtaa wa Peterstrasse karibu kabisa na Uwanja wa ndege Zurich.

“Thank you Dafa!” Winnie alimshukuru yule jamaa huku nikimuona akimkabidhi noti kadhaa za faranga za Uswisi.

Yule jamaa lizipokea wakaagana na kisha akuondoka. Tukabakia mimi na Winnie pekee.

“Thank you for this Winnie!”

“It’s ok! We are in this together..” alinijibu huku anakaa kwenye kiti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
“I think we should get moving right now!”

“sorry Ray I won’t be joining you today… I have an appointment with someone!”

“A date?” nilimuuliza kwa utani lakini ajabu ni kwamba nilimuona anajiinamia chini kwa aibu fulani hivi kumaanisha kwamba kile ambacho nilikuwa nakisema kilikuwa sahihi. Nilisikia kama vile moyo wangu unawaka moto.

“My boyfriend is going to be in town today… I have to meet him.” Winnie aliongea huku akiwa amejiinamia chini.

Nilisikia kama kisu cha moto kimepenya moyoni. Mithiri ya kisu cha moto ambacho kinapita kwenye siagi. Mimi na Winnie hatukuwa wapenzi rasmi, lakini kulikuwa na kitu fulani katikati yetu, kitu ambacho kadiri ambavyo tulikuwa tunaepuka kukiongea ndivyo ambavyo kilikuwa kinazidi kuwa na nguvu zaidi. Moyo uliniuma niliposikia ametamka “my boyfriend”.

“Wow! Sounds cozy.” Nikajitahidi kuongea kwa sauti iliyo kawaida lakini kigugumizi kilikuwa dhahiri kabisa katika mwambo wa sauti. “so… see you later?” nikauliza kwa mashaka kabisa nikijua kabisa jibu ambalo nitalipata.

“No! ’ll see you tomorrow.!” Alinijubu na kuinua kichwa kuniangalia.

“send him my regards… will keep you posted!” Niliaga na kuanza kuondoka.

Winnie hakunijibu chochote alijiinamia tena chini, hakuinuka hata kunisindikiza. Hatukuwa wapenzi lakini dhahiri kabisa alikuwa anajisikia aibu kunieleza kuwa leo ataonana na mpenzi wake na watalala wote. Niliondoka roho ikiwa inafukuta, moyo kama vile unawake moto. Nilijisikia hasira na aibu kwa wakati mmoja. Nilisikia hasira kwa kuwa na wivu ambao ulikuwa unanijia kila ambapo nikifikiria kwamba leo hii Winnie atakuwa mikononi kwa mwanaume mwingine. Lakini wakati huo huo nilisikia aibu kwa mume wa mtu, mume wa mwanamke ananyenipenda kwa dhati kabisa kuruhusu hisia za namna hii juu ya mwanamke mwingine kukua moyoni mwangu.

“Stay focused kichwa… stay focused!” nilijisemesha mwenyewe nikiwa napanda taxi kutoka chuoni kwa Winnie kuelekea mtaa wa pertstrasse ambako Vihaan Singh alikuwa anaishi.

Kama dakika kumi na tano baadae taxi ilikuwa imesimama kwenye mtaa wa peterstrasse. Nikalipa na kushuka kuanza kutafuta namba ya nyumba ambayo ilikuwa kwenye anuani. Nilitembea kama dakika mbili hivi mpaka hatimaye nikaipata. Nikasogea mlangoni na kubofya kengele mlangoni. Nilibofya kengele kama mara tatu hivi ndipo niliposikia mtu akifungua mlango.

“Hello.!” Alikuwa ni mwanaume wa kihindi mtu mzima wa makamo ya kama katikati ya miaka arobaini hivi.

“Hello… ’m looking for Mr. Vihaan Singh!”

“This is him… who are you?” alinijibu kwa kingereza kilichojaa lafudhi nzito ya kihindi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
“My name is Ray, would like to ask you a few questions.” Niliongea huku mwenyewe nikihisi kabisa nilitumia sentesi ambayo haikuwa sahihi sana. Niliuliza kama mtu mwenye mamlaka fulani hivi.

“Who are you? Police?” aliniuliza kwa woga.

“No no no! ’m not with the police… if we can just speak for a few minutes.”

“what is it about?” aliniuliza huku ananiangalia kwa mashaka.

“can I come in?”

“No you can’t! what is it about?” aliniuliza huku nikiona kabisa mashaka yakiongezeka usoni mwake.

Nilikuwa nimefungua maongezi haya kwa sentesi ambazo hazikuwa sahihi kabisa na sasa nilikuwa nimebananishwa kwenye kona.

“its about a passenger you drove day befor…..”

“No no no man! I can’t share with you that kind of information unless you are with the polce.!” kAlinikatisha kabla sijamaliza kuongea na aliongea kwa hasira na kisha kufunga mlango kwa nguvu.

Nikabaki pale nje nimeduwaa tu. Taarifa ambayo nilikuwa nahitaji anipatie ilikuwa ni kinyume na maadili ya kazi yake kabisa na mbaya zaidi nilikuwa nimemuuliza kwa urahisi rahisi kama vile naomba maji ya kunywa. Nikachakata akili haraka haraka.

“it’s a job offer… hundred francs per hour!” niliongea kwa msamiati wa fumbo nikiamini atanielewa kabisa kwamba nataka kumpa hongo ili anipatie taarifa hiyo.

Ulipita ukimya wa kama sekunde thelathini hivi kisha nikasikia mlango unafunguliwa tena kwa nguvu.

“What do you want man?” aliongea kwa hasira kiasi.

Sikutaka kuchelewesha mambo. Nikaingiza mkono mfukoni na kuhesabu faranga hamsini haraka haraka na kumkabidhi mkononi, “You get another fifty after we talk.!” Niliongea huku nimemkazia macho.

Vihaan aligeuka kuangalia kushoto na kisha kuangalia kulia na kisha kufungua mlango niingie.

“you guys go to your room!” Vihaan aliwaambia watoto kama watatu ambao ambao walikuwa pale sebuleni mara baada ya sisi kuingia. “have a seat!” Vihaan alinikaribisha nikae kwenye sofa pale sebuleni. “what is your name again?”

“It’s Ray.!”

“Which customer exactly are you talking about!” aliniuliza huku naye akikaa kwenye sofa.

Nilielewa wazi kabisa kwamba anahudimia watu wengi kwa siku kwa hiyo nilihitaji kumueleza kwa ufasaha mno mpaka kumkumbuka ni mteja gani hasa ambaye nilikuwa namlenga. Lakini ajabu ni kwamba nilipoanza tu kumueleza kuhusu safari yake ya juzi chuo kikuu chA Zurich alimkumbuka ni nani ambaye nilikuwa namlenga.

“You want to know where I took that guy with a black hat and a long over coat?” aliniuliza huku anatabasamu.

“yes yes.. that guy. Wow you have a good memory!”

“Nah not good memory! I remember that guy well because you are not the first one to ask where I took him!”

“what? Someone else asked you about him? Who?” nilipatwa na mshituko wa ghafla kiasi kwamba kama ningekuwa nimesimama ningeliweza kudondoka. Kuna mtu kabla yangu amekuja kwa Vihaan kuuliza kuhusu yule jamaa wa kofia ya pama na koti refu jeusi. “who?” nikamuuliza tena.

“I will do this for three hundred francs!” Vihaan aliongea huku anatabasamu kifedhuli. Alijua kuwa amenibananisha kwenye kona na kwa muda huu nilihitaji taarifa hiyo zaidi ya nilivyokuwa nahitaji oksijeni.

Sikutaka kufikiri mara mbili. Uzuri nilikuwa nimejiandaa tangu nilipotoka hardstrasse, nilijua kuwa lazima nitahitaji fedha kumshawishi dereva taxi ili anipe taarifa hizo kitendo ambacho ni kinyume kabisa na maadili yake ya kazi.
Nikaingiza mkono mfukoni na kutoa kibunda cha fedha. Nikahesabu faranga mia tatu na kuziweka mezani.

“Now tell me where you took him and who is asking questions about him?”

Itaendelea…

Habibu B. Anga “The Bold”

Mkuu ubarikiwe sana
 
Shukran sana mkuu.

Asante sana mkuu..nawezaje kuipata hii kitu kwa watsap?na ile ya The other half?siwezi kuteseka nmna hii aiseeh.uvumilivu umenishinda kabisa.[emoji41]
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom