Vipepeo weusi season 2: From Zurich with rules

Vipepeo weusi season 2: From Zurich with rules

VIPEPEO WEUSI


SEASON 1 – FROM ZURICH WITH RULES



Ilipoishia Episode 14…


“I think i have said enough… its your turn now! What happened to you? How did you get shot?” Akauliza huku anatoa tabasamu hafifu.

Nikakumbuka siku tatu zilizopita niliporejeshwa hotelini kwangu kutoka kule Wipkingen. Nikakumbuka kilichotokea masaa ishirini yaliyopita. Nikajiuliza kama ni sahihi kwangu kumuamini huyu mtu na kumueleza kila ambacho kilitokea. Nikakumbuka msemo wake wa fumbo kuwa “Kuna deni anataka kuwalipa Hudini”. Nikakumbuka alivyoeleza kuwa amekuwa akinitafuta kwa miaka kadhaa kwa kuwa aliamini akinipata mimi atawapata Hudini hasa kiongozi wao wa sasa, ambao alikuwa amekorofishana nao.

Nikakumbuka namna ambavyo hakunitambua mara ya kwanza na kutaka kuondoka. Nikakumbuka namna ambayo baada ya kumwambia mimi ni mmiliki wa hili jengo aliniita jina langu. Nikajiuliza kama alifahamu jina langu, na pia alifahamu mimi ni mtoto wa Charles kajuna, ameshindwaje kuijua sura yangu? Iweje anitafute miaka yote kama anavyosema na asiwahi kuona hata picha yangu?

Nikajiuliza tena kwa nini anieleza siri zote hizi. Kuanzia tatoo yake kifuani. Uanachama wake ndani ya Hudini. Shughuli za Hudini na hata ugomvi walio nao na juhudi zake za kuwapata ili “awalipe deni” kama anavyosema.

Nikajiuliza kama hakuna mtego hapa nimewekewa.

Nilikuwa nawaza haya huku nimejiinamia. Nikainua uso kumtazama. Alikuwa ananiangalia huku anatabasamu kama vile anaisoma akili yangu.

“What happened Ray? How did you get shot?” Akauliza tena huku anatabasamu.

Nikavuta pumzi ndefu na kuishusha. Isingelikuwa jeraha tumboni mwangu, ningeweza kuinuka na kutimua mbio.


Masaa 36 Yaliyopita…

Nilikuwa nimetoka usingizini baada ya kulala kwa masaa mengi tangu alfajiri ambapo nilirejeshwa na vijana wa Hudini.

Baada ya kuoga, kubadili nguo na kuonja kidogo chakula ambacho nilikuwa nimeletewa muda si mrefu na muhudumu wa hoteli nilikaa kitandani na kuanza kuchambua lundo la nyaraka ambazo nilipewa na Hudini siku ya Jana usiku kwenye like jumba lao linalonuka damu. Au niseme mzee ambaye kwa wakati huu nilikuwa nikiamini kwamba jina lake alikuwa ni Hudini.

Lilikuwa ni lundo la nyaraka pamoja na ile picha ya jamaa wa kizungu akiwa na Rais Albert Kafumu na picha nyingine akiwa na cheupe pamoja na baba yake.

Nikaziweka picha pembeni na kisha kuanza kupitia hizi nyaraka moja baada ya nyingine. Kwa namna fulani nyaraka hizi zilikuwa zinafanana na zile ambazo nilizikuta kwenye vault ndogo kule kwenye jengo ambalo nilisikiliza ujumbe wa marehemu baba yangu kwenye video.
Zilikuwa nyaraka ambazo ziliorodhesha umiliki wa mali ambazo nilikiwa sizijui, majengo, akaunti za benki. Pia kulikiwa na lundo la anuani za sehemu mbali mbali ambazo sikuelewa mara moja ni wa wapi na kulikuwa na maana gani.

Nilipitia nyaraka zote moja baada ya nyingine, lakini mpaka nilipofika karatasi ya mwisho bado nilikuwa naona maluelue tu. Ni kitu gani hasa ambacho nilikuwa natakiwa kukifanyia kazi kwenye nyaraka hizi? Niliona kila kitu orodha ya mali na majengo ambayo siyajui yalipo na wala sijawahi kuyaona. Niliona pia makumi ya namba za akaunti za benki! Napaswa kuchnguza moja baada ya nyingine? Niliona pia mamia ya anuani mbali mbali! Je napaswa pia kuchunguza kila anuani ambayo imeorodheshqa kwenye nyaraka hizi? Si itanibidi kukaa Zurich mwaka mzima?

“Fuuucckk.!!” Niling’aka peke yangu… huu ni zaidi ya uwendawazimu.

Nikainuka kutoka kitandani na kuanza kutembea kuelekea dirishani. Pembeni ya dirisha kulikuwa na kijimlango fulani hizi chembamba cha kioo ambacho nilikifungia na kutokezea kwenye ‘balcony’ ya chumba changu cha hoteli.

Nilisimama kwenye balcony na kuutazama mji wa Zurich. Namna mataa ambavyo yalikuwa yanang’ara usiku kama huu. Kulikuwa na manyunyu fulani ya mvua inayoanza. Kama ingelikuwa siku nyingine, nyakati nyingine ambayo haikuwa na maswali na mafumbo kichwani mwangu kama ilivyo sasa. Kama ingelikuwa siku nyingine Cheupe akiwa pembeni ya ubavu wangu, muonekano huu, kusimama hapa kwenye balcony na kutazama mataa ya Zurich usiku huu ingekuwa ni wasaa wa furaha tele. Lakini kwa muda huu kitu pekee ambacho kilikuwa kinauwezo wa kunipatia furaha na amani ndani ya moyo ni kufumba macho ya kuvuta kumbukumbu. Kumbukumbu ya enzi za utoto, nyumbani kwa shangazi yangu Mwembechai.

Nikafumba macho kukumbuka namna ambavyo siku ambazo zilikuwa na mvua kama hivi namna asubuhi yake kunavyokuwa kukimya. Namna ambacho jua linachomoza taratibu kujipenyeza dirishani na kumulika usoni kama vile linanijaza uhai wa siku hiyo. Naomna ambavyo asubuhi ya siku ya mvua pazia dirishani inakuwa tulivu kama vile imeninginizwa kwenye nyumba ambayo haina wakazi kwa miaka. Namna ambavyo masikio yanafurahi kusikia sauti hafifu za ndege wa asubuhi wakiimba kutokea mbali. Namna ambavyo bati linadondosha matone magodo ya maji taratibu kutokana manyunyu hafifu ya mvua inayokaribia kukoma.
Namna ambavyo nikitoka nje siku ya asubuhi ya mvua mtaa wote unakuwa kimya kabisa, mtaa wenye fujo lakini ukionekana kama hauna wakazi. Lakini japokuwa hakuna vingi vya kuviona, kuna vitu lukuki vya kuvihisi.

“There is much to be felt, and little to be seen.!” Nikatabasamu nikikumbuka msemo wangu huu wa utoto. “There is much to be felt, little to he seen.!” Nikaurudia tena na tena kichwani huku natabasamu.

Kadiri ambavyo nilikuwa naurudia kichwani ndivyo ambavyo kuna ‘taa’ ilikuwa inawaka kichwani mwangi. “There is much to be felt, little to be seen”. Kuna kitu nilihisi akili yangu imekihisi lakini sikujua ni kitu gani. Nikaurudia tena na tena ule msemo kichwani huku narudi ndani ya chumba cha hoteli. “There is much to be felt, and little to be seen.!”

Jicho langu lilitua juu ya lundo za nyaraka pale kitandani. ‘Taa’ ikawaka zaidi. Yes, ni hili lundo la nyaraka… nilikuwa nahangaika muda wote kutafuta kitu ndani yake chenye jibu la moja kwa moja kumbe labda ni ‘detail’ ndogo tu ndiyo nilikuwa natakiwa kuifahamu. Detail ambayo yawezekana akili yangu ilishaihisi. Jawabu halikiwa kwenye huu uwingi wa anuani na orodha za akaunti za benki. Bali suala fulani dogo tu. “There is much to be felt, and little to be seen.!” Nikaurudia tena msemo kichwani na kuanza kuzipekea tena kwa pupa.

Nilihisi kabisa kuna kitu hapa ambacho nilikidharau mwanzoni lakini ndicho ambacho kinaweza kuwa na majawabu ya kila kitu.
Nikapekua karibia dakika tatu nzima. Hatimaye nikakutana nacho. Au niseme kwa mujibu wangu nilihisi ndicho hicho.

Kulikuwa na karatasi moja tu ambayo ilikiwa maandishi ambayo uamefutwa kwa wino mweusi na katikati ilikuwa na kapicha kadogo cha ‘black and white’ ambacho kimechapwa kwenye karatasi. Yaani karatasi juu ilikuwa na ‘paragraph’ kadhaa ambazo zimefutwa kwa wino mweusi katika mtindo unaofanana kabisa na karatasi za mambo ya ujasusi na intelijensia huwa zinazibwa maandishi kwa wino mweusi ili kilichiandikwa kisisomwe.
Katikati kulikuwa na hicho kipicha cha ‘black and white” kisha chini yake kulikuwa na maelezo ambayo nayo yalifutwa kwa wino mweusi.

Nikaitazama hii picha kwa makini. Ni picha ya eneo. Sehemu ambayo naifahamu kabisa hapa Zurich. Ni ule mgahawa wa kichina ambao nilienda siku ya kwanza na kuchomwa kemikali nikapoteza fahamu. Nikaiangalia picha kwa makini zaidi. Nilikiwa sijakosea ni penyewe.

Maelezo ya hii picha yalikuwa yamezibwa kwa wino mweusi kama ilivyo kwa paragraph za juu yake. Lakini kwenye maelezo hayo yote yaliyofichwa kulikuwa na neno moja tu limeachwa na nina imani liliachwa kwa makusudi kabisa. Sikuelewa kwa nini liliachwa, na wala sikuelewa lilikuwa lina maanisha nini. Lakini kwenye karatasi hii kila kitu kilikuwa kimefutwa kwa ustadi kwa wino mweusi na kuachwa hii picha na neno moja tu;

“MELCHIZEDEK ”

Mvua nje ilikuwa imeshika kasi. Na safari hii nikaanza kuiskia radi ikipiga. Japokuwa mvua ilikuwa ni kubwa na radi lilipiga kwa nguvu lakini kitu nilikuwa nahisi ukimya wa ajabu ndani ya chumba cha hoteli. Kuna hisia mbaya nilianza kuisikia mpaka vinyweleo vilisisimaka. Ule ukimya. Sijui kama ulikuwa ukimya ndani ya chumba cha Hotel au ukimya kwenye nafsi yangu. Lakini nilihisi ukimya kiasi kwamba hata tone la maji linedondoka ningelisikia.
Kuna kitu hakikuwa sawa humu ndani ya hoteli.

Nikatazama ile karatasi na maandishi yake yaliyofutwa futwa kwa wino mweusi. Nikatazama ile picha ya mgahawa wa kichina katikati. Nikasoma tena yale maandishi yaliyoachwa.

” MELCHIZEDEK ”

Nilihisi nimepata wazo nianzie wapi kufumbua fumbo lililonileta hapa Zurich. Lakini bado nilipata hisia, kuna kitu hakikuwa sawa ndani ya hiki chumba cha hoteli. Ukimya ndani ya nafsi yangu ambao ulihamia mpaka kwenye chumba nilichomo ulikuwa ni ukimya wa kutisha.



Itaendelea…



THE BOLD
 
VIPEPEO WEUSI


SEASON 2 – FROM ZURICH WITH RULES


EPISODE 16


Mara nyingi sana katika maisha kadiri ambavyo utakuwa unahangaika kutoka kwenye jambo ndivyo ambavyo unakuwa unapalilia kina cha kuzama. Ni kama vile kuzama kwenye bwawa lililojaa tope tupu, kadiri ambavyo utahangaika kujiokoa ndivyo ambavyo unazama zaidi na zaidi.

Ndivyo namna ambavyo maisha yanakupa kitendawili mara nyingi, kitendawili ambacho jawabu lake ni fumbo na kadiri ambavyo utaling’amua hilo fumbo ndivyo unaingia kwenye sintofahamu ya fumbo kubwa zaidi.

Unapozama kwenye bawa lenye tope tupu, busara ni ipi? Utulie tu na kushuhudia nafsi yako ikiondokewa na uhai au uhangaike na kuzama zaidi ndani ya tope?

Ni ajabu kwa kiasi gani maisha yanaweza kugeuka na kuwa uwanja wa mahangaiko… kadiri tunavyohangaika kuboresha maisha yetu ndivyo kadiri ambavyo tunazidisha msongo vichwani.
Ni ajabu namna gani ambavyo kadiri tunavyojitahidi kujifunza na kufahamu ndivyo ambavyo maswali mengi zaidi yanaibuka vichwani.
Ni ajabu ni namna gani ambavyo tunapenda ndivyo ambavyo tunazidi kuumiza mioyo yetu.

Ni ajabu ni namna gani tumezaliwa na kupewa aina ya maisha ambayo hatukuiomba. Maisha ambayo yanahitaji mapambano kuyajaza fahari. Mapambano ambayo muda mwingine yanaweza kuchukua miaka yetu yote ambayo tutaishi hapa duniani.

Ni ajabu kwa nini tumetengewa maisha ambayo tunayo.!


Japo tayari zilikuwa zimepita karibia dakika tano tangu nifike nje ya mgahawa huu wa kichina lakini bado nilikiwa nashindwa kufanya uamuzi wa nini hasa cha kufanya.

Mlango wa mgahawa ulikuwa umefungwa na kibao kilichosomeka “CLOSED” kilikuwa kinaning’inia mlangoni. Japokuwa mgahawa huu mbele ulikuwa na vioo tupu lakini sikuweza kuona ndani kutokana na giza na taa zake kuzimwa. Kuna hisia fulani nilikuwa naipata kwamba kulikuwa na uwezekano mgahawa huu ulikuwa haujafunguliwa kwa siku kadhaa, labda pengine tangu siku ile nilipofika hapa. Haikuwa sawa sawa kwa mgahawa hapa Zurich kufungwa muda huu kwa sababu hata saa tatu usiku ilikuwa haijafika bado.

Mvua bado ilikiwa inanyesha na nilikiwa naloa nikiwa nimesimama hapa nje ya mgahawa najiuliza ni nini hasa natakiwa kufanya ingawa hata nilikuwa sijui ni kwa nini hasa nilikuwa hapa. Mfukoni mwangu nilikiwa na kijipande cha karatasi nilichokitoa kwenye lile lundo la makabrasha nililoacha hotelini. Nilichukua kipande hiki tu cha karatasi ambacho kilikuwa na maandishi yaliyofutwa futwa yote yakiacha neno moja tu “MELCHIZEDEK”, pamoja na Picha ya mgahawa huu.

Kwa hiyo sababu pekee ambayo ilikuwa imenileta hapa ilikuwa ni kwa sababu picha yake mgahawa huu ilikuwa kwenye makabrasha ambayo nilikabidhiwa na Hudini. Sikujua ni nini hasa nilikuwa nakitafuta lakini niliamini tu kwamba ingeweza kunifumbua macho juu ya lengo langu la kuwa hapa Zurich.

Katika muda kama huu ndivyo ambavyo nilijikuta kwa kiwango fulani nilikuwa najuta kwa nini nilikuja hapa Zurich? Nafsi yangu mara kadhaa nilijikuta kama kuna sauti inaniuliza, kwa nini uko hapa?

Yote kwa ajili ya kukonga kiu yangu ya kutaka kujua. Yote kwa sababu ya kukonga kiu yangu ya fumbo ambalo marehemu baba yangu alinifumba siku ambayo alijitoa uhai wake mbele yangu.
” Au labda kuna lingine la zaidi akilini mwangu ambalo naogopa kulikiri hata kwa nafsi yangu mimi mwenyewe?” Nilijikuta najiuliza moyoni mwangu. Kwamba labda kuna jambo la zaidi kuhusu The Board ambalo nafsi yangu ilikuwa imeshawishika lakini nilikuwa nashindwa kukiri ndani ya nafsi yangu.

Nikaliondoa hilo wazo haraka kichwani mwangu. Nikarejesha akili yangu kwenye lililo mbele yangu, mgahawa huu wa kichina.

Mvua bado ilikuwa inanyesha kwa fujo, ikimiminika mwilini mwangu kama vile wingu lilikuwa juu ya kichwa changu.

Kama ilivyo kwa mgahawa mingine yote niliamini kabisa kwamba pia hata mgahawa huu wa kichina lazima nao utakuwa na mlango wa nyuma. Mlango ambao unaenda moja kwa moja jikoni kama ilivyo ada kwenye mgahawa mingine yote.

Sikuwa na hakika sana mlango huu nilikiwa nauhitaji kwa sababu gani lakini hulka yangu ya kutorudi nyuma ilikuwa inanisukuma kufanya hivyo. Baada ya kufika hapa tu mgahawani japokuwa nimeukuta umefungwa lakini kwa namna nilivyo si jambo ambalo linawezekana kwangu kugeuza na kurudi hotelini kwangu bila kufanya chochote kile.

Mgahawa huu ulikuwa kwenye Jengo lenye kama ghorofa tano juu ambalo sikujua kama juu lilikuwa linatumika kama makazi ya watu au maofisi. Pembezoni kwa jengo kulikuwa na uchochoro unaoingia na kufanya kama unazunguka nyuma ya jengo. Niliamini kabisa kama kulikuwa na mlango wa nyuma wa kuingia jikoni basi mlango huo utakuwa kwenye uchochoro huu.

Sikutaka kupoteza muda, nikaanza kutembea kuufuata huu uchochoro.

Mvua bado ili kuwa inaendelea kunyesha na nilikuwa naendelea kuloa.

Sauti ya ngurumo ilivyokuwa inapiga, radi ikimetata meta kila baada ya dakika kadhaa, matone yenyewe ya mvua mfululizo, kila kitu kilikuwa kinafanya nafsi yangu kujipa tathimini. Kila tone la mvua ambalo nilikuwa nalisikia likitiririka kutoka kichwani, shavuni na kisha mwilini, yalinikumbusha machozi yote ambayo nimewahi kuyasababisha kwa watu kutokana na maamuzi ambayo nimewagi kuyanfanya na nilijikuta najiuliza kwa hiki ninachokifanya sasa hapa Zurich huko mbeleni nitasababisha machozi kwa watu wangapi?

Na kila ambapo sauti ya ngurumo ikilia ilinifanya nijisikie hasira. Hasira juu ya nafsi yangu mwenyewe, hasira juu ya maamuzi ninayoyafanya kila siku ambayo yanaweza kuleta vidonda visivyo pona nafsini. Lakini kila baada ya dakika kadhaa radi ilipiga. Japokuwa mwanga wake uliangaza kwa kasi kuweza macho yangu kuufaidi nuru yake, lakini kila muda mwanga wa radi ulipooiga nilijikuta moyoni najipa moyo, najifariji kwamba labda iko nuru mbele, liko tumaini. Kwamba maumivu yote haya yanastahili ilo kufikia nuru hiyo.

Nikaendelea kuufuata ule uchochoro. Kulikuwa na malundo kadhaa ya mifuko mikubwa ya plastiki, meusi ambayo ilikuwa imejaa taka za vyakula. Moyoni nikajipongeza kuwa nilikuwa sahihi, uchochoro huu ulikuwa unaelekea moja kwa moja kwenye mlango wa nyuma wa mgahawa kuingia jikoni.

Nikatembea hatua kadhaa kupita ile mifuko ya plastiki ya kuwekea taka. Nilipoipita na kutembea kama hatua tano tu nikakutana na mlango. Mlango wa chuma kama geti dogo tu la kawaida la rangi nyeusi. Nilipoufikia tu mlango bila kujiuliza mara mbili au kufikiri sana nilinyoosha mkono na kuujaribu kufungua. Mlango ulifunguka.

Nilishangaa. Ilimaanisha kwamba mlango ulikuwa umeegeshwa tu bila kufungwa na funguo. Kwa hiyo ilikuwa na maana kwamba kulikuwa na watu huku ndani jikoni japokuwa mgahawa ulikuwa umefungwa kule mbele.

Nilipiga hatua na kuanza kuingia ndani kwa tahadhari kubwa sana. Nilihakikisha kuwa kila hatua ambayo nilikuwa nakanyaga chini haikuwa inasikika. Nikaingia ndani na kuufunga mlango kama ambavyo nilikuwa nimeukuta. Ndani taa zilikuwa hazijawashwa hivyo kulikuwa na kiza kikubwa. Nilitamani ninyoonye mkono ukutani kupapasa kutafuta swichi ili niwashe taa, lakini sikutaka kufanya chochote kile tofauti na namna ambavyo nilipakuta hapa ndani kwa kuwa nilihofu uwepo wa watu wengine humu.

Nilisimama ka karibia dakika mbili kuyapa macho yangu muda wa kuzoea kiasi hali hii ya giza ili niweze kung’amua vitu japo kwa uchache.

Nikaanza kuona japo kwa mbali sana na kwa uhafifu. Nilikuwa kwenye korido ambayo kama hauta saba kutoka nilipo kulikuwa na mlango unaoingia kulia ambako niliamini kwamba huko ndiko kwenye jiko. Hatua kama tano hivi kutoka mlango huo kulikuwa na mlango mwingine ambao nao ulikuwa mkono wa kulia ambao nao nilihisi kwamba ulikuwa unaelekea mgahawani kule mbele ambako hukaa wateja.


Mkono wa kushoto kulikuwa na mlango mmoja tu ambao sikujua hasa ulikuwa ni mlango wa nini.

Nikaanza tena kutembea kwa kunyata nikihakikisha hakuna hata hatua yangu moja ambayo ilikuwa inasikika nikikanyaga hapa sakafuni.

Nikatembea haraka haraka lakini kwa tahadhari kubwa sana na kisha nikakunja kulia kwenye mlango wa kwanza ambao niliamini kuwa ulikuwa ni mlango wa jikoni. Kutokana na kuukuta ule mlango wa nje uko wazi nilikuwa na imani kubwa sana kuwa japokuwa humu kulikuwa na giza lakini sikuwa peke yangu. Kuna sababu kwa nini mlango ule umeachwa wazi.

Kutokana na kitete changu cha kutembea haraka haraka, nikajikuta nimekanyaga kitu sakafuni… sijui ilikuwa ni sufuria, sijui ni sahani lakini ninachokumbuka ni kwamba kilitoa mlio mkubwa. Moyo ulipasuka na kutulia kimya kabisa kusikilizia kama nitasikia mtu yeyote anakuja.

Sikusikia mtu akiwa anakuja, wala sikusikia purukushani yoyote ile, nilishituka tu taa ikiwa imewashwa na kijana wa kichina aliyevalia suti nyeusi na bastola mkononi akiwa amesimama mbele yangu.

“…#####%%&&&&&&&#…”

Sikuelewa alichokuwa anakiongea. Alikuwa anaongea kichina kwa jazba huku ameinua bastola na kuninyooshea.
Nilibakia nimetumbua macho na kuinua mikono huku natetemeka.

“Don’t shoot. Don’t shoot.!” Niliongea huku nimeinua mikono juu natetemeka.

“…#&#$&$&#&$…!”

Aliongea tena kwa jazba bado bastola ikiwa imeelekea upande wangu.

“Melchizedek.!! I’m looking for Melchizedek.!” Nilijikuta naropoka bila hata kuelewa kama nilikuwa sahihi au ni kwa namna gani kutaja jina hilo la Melchizedek kungenisaidia mchina huyu aliyepandwa na mori asinitandike risasi.

Lakini nilipotaja tu jina la Melchizedek niligundua kwamba alipatwa na mshituko ghafla usoni.

“..&$%*##&$##..!” Aliongea kitu fulani hivi kwa kichina lakini alikiongea kwa taratibu huku amenikazia mamcho. Nilihisi alisema “Umesemaje?”

“Melchizedek.! I’m looking for Melchizedek.!” Nikarudia tena kujibu.

Hakunisemesha kitu chochote kile. Alinifuata haraka pale nilipo na kunikunja shati kifuani na kuanza kunivuta kutoka mule jikoni.

Alinivuta huku anatembea haraka mpaka tukafika koridoni. Kote huku nako taa zilikuwa zimewashwa. Aliendelea kunivuta tukauvuka ule mlango unaopinda kulia kwenda mgahawani kwenyewe, alinivuta mpaka kwenye mlango ambao ulikuwa upande wa kushoto. Hakukuwa na chumba bali kulikuwa na ngazi kuelekea ghorofa ya juu.

Tulipanda ngazi haraka haraka huku akiendelea kunivuta shati kwa nguvu mpaka tukatokezea juu ghorofani ambako mbele yetu kulikuwa na mlango. Akagonga mlango kwa haraka kama kulikuwa na dharura fulani hivi. Mlango ukafunguliwa na akanitutusa na kunitupia ndani.

Kulikuwa na lijichumba likubwa mno. Karibia nusu ya ‘floor’ yote ilikuwa ni lichumba hili au ‘hall’ naweza kusema.

Kulikuwa na makorokoro mengi sana lakini mengi yakiwa ni maboksi yaliyotengenezwa kwa mbao ambayo sikujua mara moja yalikuwa na nini hasa ndani yake.

Upande mmoja kulikuwa na meza na kiti kama ofisi na juu ya kiti alikuwa ameketi yule mzee wa kichina. Ni mzeebyule yule ambaye alinichoma sindano ya kemikali siku ya kwanza nilipokuja hapa na nikazimia na kuja kuzinduka nikiwa kwenye jengo kule mtaa wa Hardstrasse. Pamoja na yeye kulikuwa na vijana wengine wenye asili ya kichina kama kumi hivi.


“….##&&$&##%#&##&…Melchizedeck…!”

Yule jamaa ambaye alinikwida na kunileta hapa msobesobe alizungumza kichina na nilifanikiwa kung’amua neno “Melchizedek” kwenye sentensi zake.

Wote mle ndani akiwemo yule mzee wa kichina niliwaona wameshituka ghafla baada ya yule mwenzao kutamka jina la “Melchizedek”.

Yule mzee wa kichina aligeuka na kunikazia macho kwa karibia dakika tatu bila kusema neno lolote lile. Alikuwa kama anatathimini kitu fulani hivi. Nadhani uwepo wangu hapo na kile ambacho mwenzake alikuwa amemueleza.


“Is it true?” Aliniuliza bado akiwa amenikazia macho.

“What? I didn’t understand what he said!” Nikamjibu huku nikijitahidi nionyeshe taswira ya kujiamini.

“Is it true that Melchizedek sent you here?” Hakupepesa macho hata kwa sekunde. Aliniuliza huku ananiangalia moja kwa moja akiwa amekaza macho.

Sikuwa na muda wa kufikiri au kutafakari nitoe jibu gani. Kwa jinsi ambavyo alikuwa amenikazia macho kama ningethubutu kutafakari japo kwa sekunde tu basi angehisi nilikuwa nadanganya. Na kwa kuwa hakutaka nidanganye basi nikachukua uamuzi wa kumdanganya. Bila kufikiria sana nikajikuta tu nimeropoka,

“Yes! Melchizedek sent me here..!!”

Niliona mshituko wake usoni. Mara moja alisimama kutoka pale kwenye kiti ambako alikuwa ameketi. Sikujua kama ilikuwa ni hasira au alikuwa kwenye mshangao. Nakumbuka tu aliinuka haraka na kwa taharuki na kuanza kutembea kwa haraka kunifuata pale nilipo.

Nilianza kutamani labda nisingesema uongo. Lakini kwa kuwa tayari nimeshaanza na uongo niliousema basi napaswa kusimamia uongo huo. Lakini mtihani niliokuwa nao ni kwamba hata huyo Melchizedek sikumjua ni nani au anafanya nini au ilikuwa na maana gani.

Japokuwa mzee huyu anajifanya kufanya biashara ya mgahawa uliopo hapo chini lakini kwa hakika kabisa biashara yake halisi ilikuwa ni suala fulani la hatari au uhalifu kutokana na hawa vijana alionao ambao kwa mtindo ambao walikuwa wamevaa makoti yao ya suti nilikuwa na hakika kabisa kila mmoja wao alikuwa na silaha ya moto kiunoni.

Mzee alitembea mpaka mbele yangu kabisa tukawa tunaangaliana uso kwa uso.

“Where is the package?” Aliniuliza huku amenikazia macho na anapumua kwa hasira.

Nilitamani nimuulize “mzigo gani?” Lakini nikajua kuwa ndio nitaharibu kabisa. Nahitaji kutoka jibu la maana kabla hawajajua nadanganya na hata kile nilichotumaini kukipata hapa ili kinisaidie kwenye hizi harakati zangu nikakikosa.!!


Itaendelea…


THE BOLD
 
1d3ea48aa066ee3994d056633d2ad0ac.jpg



VIPEPEO WEUSI



SEASON 2 - FROM ZURICH WITH RULES




EPISODE 17

"Where is the package??" Yule mzee aliniuliza tena kwa kunikazia macho huku ananisogelea karibu baada ya kukaa kimya aliponiuliza mara ya kwanza.

Nilijua kabisa sipaswi kukakaa kimya, natakiwa nitoe jibu haraka kabla hawaingiwa na wasiwasi wowote na kunitilia mashaka.
Lakini pia sikutaka kutoa jibu la kukurupuka na kuharibu kabisa. Uhalisia ni kwamba sikuwa nimetumwa na 'Melchizedek' na wala sikufahamu Melchizedek ni nani au kitu gani. Jibu moja tu lisilo sahihi lingesababisha kuharibika kwa kila kitu.

Nilitamani kumvimbia na kumwambia kuwa "siwezi kumpa mzigo mpaka ajibu maswali yangu" lakini kuna upande fulani wa roho yangu ulikuwa unakataa kutoa jibu la namna hii. Kuna asilimia fulani ndani yangu ilikuwa inaamini kwamba swali hili lilikuwa ni swali la fumbo, swali la utambulisho. Yaani kwamba, kuna namna fulani ambayo wamejiwekea kwamba kama ni kweli wewe ni mtu kutoka kwa 'Melchizedek' basi utajibu swali hili kwa jibu mahususi ambalo wenyewe wamekubaliana liwe hivyo. Kwa maana ya kwamba swali lake hili "where is the package?" Hakuwa hasa anahitaji nimpe mzigo fulani kutoka kwa 'Melchizedek' bali alikuwa anataka nifumbue fumbo!
Lakini hii yote ilikuwa ni moja tu ya nadharia ambayo nilikuwa naiwaza kichwani mwangu, sikujua hasa kwa uhakika ni jibu gani nitoe, ni nini hasa maana ya swali lake? Ni kweli anataka mzigo kutoka kwa 'Melchizedek' au lilikuwa ni swali la fumbo ambalo nilipaswa kutoa jibu mahususi?

Yote haya nilikuwa nayafikiria kwa kasi kubwa kichwani mwangu, kama ndani ya sekunde tano tu ndizo ambazo nilitumia kuwaza hii sintofahami kichwani. Yule mzee bado alikuwa amenikazia macho bila kupepesa hata mara moja japo hata kwa sekunde tu.

"Come on man! Really??" Nikaongea huku navuta mdomo pembeni kuashiria kana kwamba ameuliza swali la kijinga, nikijitahidi kujenga picha kwamba alikuwa anafanya 'utoto' kwa kuniuliza swali la mtego kama hilo kwa kuwa mimi ni 'mwenzao' na twende kwenye mazungumzo moja kwa moja badala ya haya maswali. Lakini pia nilitamka katika namna kwamba kama alikuwa anamaanisha nimpe mzigo kutoka kwa Melchizedek pia alikuwa anafanya 'utoto' kwa kuutaka kirahisi rahisi hivyo! Kwa hiyo niliongea sentesi moja ambayo haikuwa na maana dhahiri moja kwa moja lakini niliamini kwamba tafsiri yake ingetokana na huyu mzee alikuwa na maana gani hasa kwa kuniuliza swali 'where is the package?"

Mzee wa kichina alinikazia macho zaidi. Hakusema chochote kile, hakupepesa macho wala kuonyesha hisia yoyote ile kana kwamba hakusikia chochote kile ambacho nilikuwa nimeongea.
Sikutegemea aseme chochote wala kujibu chochote lakini nilitamka nilichokisema ili nijipe walau muda mwingine kiduchu wa kutafakari ni nini haswa ambacho natakiwa kujibu.

"I'm going to ask you one last time… where is the package?" Aliniuliza huku akiwa serious zaidi safari hii na akiwa amekaza macho kifedhuli kuashiria kwamba uvumilivu wake ulikuwa unakaribia kikomo.

Kwa namna ambavyo alinitazama nilipoongea sentesi yangu ya kuzugia "come on man, really??" na namna ambavyo safari hii aliuliza tena "where is the package?" Niliamini kwa asilimia kubwa zaidi kwamba hili lilikuwa ni swali la fumbo na nilipaswa kutoa jibu mahususi ili kuthibitisha kwamba ni kweli nimetumwa hapa na 'Melchizedek'.

Nilitamani kama muda urudi nyuma dakika chache niwe hotelini kwangu na nipange mkakati maridhwa zaidi. Nilihisi nimejiingiza kwenye mtego wa simba bila kujiandaa namna gani ambavyo nitajinasua na kutoka.

Kwa muda wa kama sekunde kumi tu akili yangu ilifanya kazi kwa haraka na kasi kubwa ili walau nipate cha kutamka mdomoni.
Ndani ya sekunde hizo hizo kumi sikujua ni nini kilinipata lakini nikajikuta akili yangu inaanza kufikiri juu ya ile picha ya mkewangu Cheupe utotoni akiwa na baba yake na yule bwana mzungu ambaye sijamfahamu mpaka sasa ni nani na ana uhusika gani katika hiki kitendawili kinachonikabilo.
Lakini akili yangu ilipowaza tu picha ya Cheupe utotoni nikakumbuka namna ambavyo tangu utoto wake baba yake ekuwa akipenda kumita 'malkia'… neno malkia lilipoibuka kichwani mwangu sikujua ni kwanini lakini moja kwa moja nikajikuta nimehisisha malaika na jina hili 'Melchizedek' na nilipounganisha tu vitu hivi viwili 'Melchizedek' na malaika nikajikuta akili yangu inakubali kwamba niko sahihi japokuwa upande mwingine wa akili yangu ilikuwa inaniambia kuwa naota ndoto za mchana.

Lakini kuna picha nyingine ilikuwa inanijia kichwani, picha ya 'crown', kofia ya kifalme ya kale ambapo sikumbuki kwa usawia ni wapi niliiona kama ni kwenye nembo ya mgahawa huu au lile lundo la makaratasi nililonalo hotelini kwangu. Lakini akili yangu ilikuwa ina uhakika kwa asilimia kubwa sana kwamba kuna mahala nimeona mchoro wa kofia ya kifalme ya kale, kuna picha ina huo mchoro wa crown, haijalishi kama ni kwenye nembo ya mgahawa huu hapo nje au kwenye lundo la makaratasi niliyoyaacha hotelini, ninachokumbuka ni kwamba kuna mahali nimeona huo mchoro wa kofia ya kale ya kifalme.

Kwa haraka akili yangu ikahisi imeng'amua kwamba kwa namna fulani watu hawa wameamua kumuita mtu au wameamua kuweka fumbo la mawasiliano kwa jina la 'Melchizedek' kwa kuakisi 'Melchizedek' Mfalme wa ambaye hadithi yake niliisoma miaka mingi iliyopita nikiwa sekondari katika somo la biblia kwamba kwamba Mfalme huyo wa kusadikika alimtokea Ibrahim na kumbariki. 'Melchizedek' huyo huyo mahala mwingine kwenye hadithi za biblia anaitwa kuwa ndiye kuhani mkuu huko mbinguni.

Kwa namna fulani nikaanza kujihisi labda nilikuwa naanza kuchanganyikiwa kwa kuhusisha masuala ya biblia na changamoto na kitendawili kilichopo mbele yangu.
Lakini bado upande mwingine wa akili yangu ulikuwa unaniambia kwamba niko sahihi na uwendawazimu wangu. Nikajikuta najiuliza kama niko sahihi, huyo Melchizedek ndivyo vivyo wanavyomaanisha, je fumbo hili lina kipande gani ambacho napaswa kukijua??
Nikajijibu mwenyewe, kwamba kwa mujibu wa hadithi hizo nilizosoma huko sekondari ni kwamba Melchizedek ndiye kuhani mkuu pekee huyo mbinguni ambaye anaweza kuingia mahala patakatifu pa hekalu.


Nikahisi nimepata jawabu la fumbo hili ambalo lilikuwa nahisi natakiwa kulitengua. Sidhani kama nimewahi kuhisi kwamba mimerukwa na akili kama sekunde hizi kumi za maisha yangu. Kwanza kabisa sikuwa na hakika kama ni kweli swali hili la "where is the package?" Mzee huyu alikuwa anauliza kama fumbo au kulikuwa na mzigo kweli ambao alikuwa anautegemea kutoka kwa 'Melchizedek'? Lakini akili yangu ikanipa moyo kwamba hilo lilikuwa ni fumbo.
Lakini pili lilikuwa ni jibu la hilo fumbo, hakuna namna ambayo naweza kubuni jibu la fumbo la watu kuwasiliana kwa siri alafu niwe sahihi, lilikuwa ni kama vile nipatie namba ya siri ya mtu ya kufunga simu yake au labda namba yake ya siri ya kadi yake ya benki, hakuna namna ambayo naweza kutoa jawabu sahihi la fumbo hili la wao kutaka kunithibitisha kama kweli nimetumwa na Melchizedek. Lakini nikajipa moyo, kile nilichokifikiri ndani ya sekunde hizi kumi ndicho hicho ambacho nitakijibu.

Nikalirudia tena kichwani lile swali aliloniuliza yule mzee, "Where is the package?"

Nikavuta pumzi na kuishusha, kisha kwa kujiamini nikamuangalia machoni na kumjibu,

"The package is at the holly place.!!"

Sikumbuki kwa usahihi zaidi ni kwa muda gani alinitazama machoni bila kupepesa, lakini ilikuwa ni zaidi ya dakika moja tulikaziana macho baada ya kutoa jawabu langu hili.
Japokuwa usoni nilikuwa nimekaza macho na kuonyesha kujiamini lakini moyo ulikuwa unanienda mbio kama nimekimbia marathoni ya kilomita mia. Kijasho chembamba kilikuwa kinanivuja ndani ya nguo.

Baada ya kama dakika nzima ya kutazamana kwa kukaziana macho hatimaye nilimuona yule mzee anatikisa kichwa katika namna ya kuitikia, yaani kukubali. Maana yake kwamba nimetoa jawabu sahihi.!!!

"what the fuuuccckk!!" nilijikuta najitamkia mwenyewe kichwani mwangu kimya kimya. Nilihisi kama vile naota… kilichotokea ni kitu ambacho hata mtu ninaye muamini angenisimulia nisingeamini!! Inawezekanaje???
Nimepambana na The Board na kuwadondosha, nimeunda moja ya taasisi bora zaidi nchini Kwetu Tanzania, lakini hakuna siku ambayo nilijitukuza mwenyewe na kukubali jina la 'kichwa' kama siku hii ya leo. Nilihisi kama vile nastahili kutunukiwa tuzo ya Nobel au labda jina langu kuandikwa sambamba na majina ya akina Albert Einstein, Newton, Galileo na wanaofanana nao.
Nilijitahidi nisionyeshe mshangao wangu usoni… uzuri mapigo ya moyo yalirudi kuwa kawaida na kijasho kilichokuwa kinanitoka awali kilikauka.

"Go back to your hotel and wait.!"
Yule mzee wa kichina akaongea.

"What.!?" Nikamuuliza nikiwa kama nimezinduka kutoka usingizini.

"I said go back to your hotel and wait…. ##-@+@%$-$+#&@-&@%@-@%@"

Yule mzee akaongea huku akimalizia na kichina anamuambia yule kijana ambaye alinileta huku juu akiwa amenikwida kutoka 'floor' ya chini.

Nilitamani nimuulize yule mzee "wait for what?" Lakini nilihisi kwamba nikiuliza tu swali hilo wanaweza kung'amua kwamba sijatumwa hapa na Melchizedek na wala nilikuwa sijui ninachokifanya.
Kwa hiyo sikuongea chochote nikaanza zangu kuondoka huku yule kijana aliyenileta akinifuata kwa nyuma. Nilielewa kuwa yule mzee alimuamuru 'aniescort' mpaka nje ya jengo nisije kuwafanyia uhuni fulani labda.

Nikashuka mpaka chini nikiwa nasindikizwa na yule kijana, akanifungulia ule mlango wa nyuma wa jikoni kisha nikatembra na uchochoro mpaka kutokea barabarani mbele ya jengo la huu mgahawa.

Kitu cha kwanza tu nilipofika mbele ya jengo nikaangalia 'logo' ya mgahawa na yale maandishi yake ya kichina. Katika nembo pale kulikuwa na mchoro fulani hivi uliorembwa wa Kofia ya kifalme ya kale.
Nikajikuta natabasamu peke yangu kwa sababu tangu siku ya kwanza naona mgahawa huu sikuwahi kuhisi au kutilia maanani nembo hii kiasi cha kujua kulikuwa na mchoro huo wa Kofia ya kifalme lakini ajabu ni kwamba ubongo wangu ulihifadhi sawia mchoro huo na kuniletea hiyo kumbukumbu pale nilipohisi kuhitaji.

Japokuwa nilitabasamu kutokana na kujinasua kwenye mtego, lakini kichwani maswali yalizidi maradufu! Melchizedek ni kitu gani hasa? Yule mzee ameniambia nirudi hotelini na kusubiri, nasubiri nini? Ni nini hasa kinaendelea??
Kwa kiwango fulani nikaanza kujutia uamuzi wangu wa kuja hapa Zurich, lakini nilijutia zaidi uamuzi wangu wa kufungua bahasha ambayo nilipewa na marehemu baba yangu… nikajikuta naanza kuwaza Cheupe ana hali gani nyumbani Tanzania, vipi kuhusu mwanangu?
Japokuwa hatukuwa na maelewano mazuri na Cheupe mpaka siku naondoka Tanzania, lakini nilijikuta natamani angekuwa hapa usiku huu… nilitamani kama nirejeapo hotelini nimkute! Anikumbatie nilale kama mtoto mchanga na kunifarini kuwa kila kitu kitakuwa sawa… nilijikuta natamani nipae na kutua Tanzania na kumwambia nampenda mkewangu licha ya sintofahmu ya mahusiabo yetu. Nikakata shauri kwamba nikirejea tu hotelini nimpigie simu kabla ya kufanya lllotr lile.

Nikatembea kurejea hotelini huku nimeinamisha kichwa nikiwaza na kuwazua juu ya kila kinachoendelea katika maisha yangu.


Kutoka na kutembea taratibu nikitafakari nilitumia karibia dakika arobaini nzima kufika hotelini kwangu. Nilipofika tu mlangoni na kuingiza funguo kwenye tundu lake nikaisikia ile hali ambayo niliisikia awali kabla sijaondoka, kwamba siko peke yangu. Mwili ulikuwa unanisisimuka nikihisi kama vile kulikuwa na mtu mwingine ndani ya chumba changu. Vinyweleo vilisimama na mwili ulikuwa unasisimuka kama chaji ya umeme inapita.

Nikafungua mlango taratibu na kuingia ndani. Nilipoingia tu mara moja puani nikaanza kusikia harufu fulani hivi hafifu. Kama harufu ya kemikali au labda manukati ya bei chee.


Harufu fulani hivi ambayo nilikuwa naijua lakini nilishindwa kukumbuka sawia ni harufu ya nini. Nikageuka na kutazama huku na huko nione labda naweza kupata jawabu lakini wapi. Niakingia chumbani, nako kulikuwa na hiyo harufu ya kemikali au manukato ya bei ya chini lakini kila kitu kilikuwa vile vile kama ambavyo nilikiacha. Nikapekuwa mkoba nilioweka makabrasha na makaratasi yangu, yalikuwa vile vile kama ambavyo niliacha.
Nikarejea tena sebuleni, hakukuwa na mabadiliko yoyote tofauti.

Nikaelekea bafuni… nilipoingia tu moja kwa moja macho yangu yalitua kwenye 'sink' la kunawia uso na kupiga mswaki… kila kitu kilikuwa sawa kasoro kitu kimoja tu ambacho kilinifanya ning'amue hii harufu ilikuwa ni harufu ya nini! Miswaki ilikuwepo sawa kabisa, dawa ya meno, dawa ya kunyolea ndevu na sabuni.! Lakini pamoja na hivi kulikuwa na kikopo cha 'WINDEX'. Maji maji (kemikali) ya kusafisha madirisha na milango na meza za vioo. Kikopo kilikuwa kwenye mtindo wake ule ule ambavyo vibatengenezwa na mbele kuna kimshikio ambacho ukiminya vimaji maji vinaruka.

Nikajiuliza tena na tena, hiki kikopo kilikuwa hapa kabla sijaondoka?? Jibu nikawa sipati kwa sababu ni suala ambalo sikutilia maanani awali… lakini swali lingine linanijia kuwa harufu hii ninayosikia ni ya hii Windex kwa maana kwamba muda mchache uliopita imetumia kusafisha vitu humu chumbani, nikajiuliza kama hilo suala linawezekana, chumba cha Hoteli kusagishwa usiku huu bila mimi kuomba? Na nilishangaa kwa nini harufu iwe kila mahala, kama ingetumia kusafisha vioo vya madirisha tu nisingeweza kuisikia… lakini pia kwa nini hiki kikopo kiachwe hapa? Kwa ninavyojua wakimaliza usafi lazima waondoke nacho kusafisha vyumba vingine!!!

Mwili ukaanza kunisisimuka nikihisi kabisa hapa kuna jambo haliko sawa.

Nikakibeba kile kikopo kwa haraka na kwenda nacho mpaka chini mapokezi…

"You guys forgot this in my room!" Nikamuambia yule binti wa mapokezi huku natabasamu.

"What do you mean?" Akaniuliza kwa mshangao.

"I found this inside my room so I assume its yours…" nikaongea tena huku natabasamu.

"No its not ours?" Yule binti akanijibu kwa kujiamini.

"What? What do you mean?" Nikauliza kwa mshangao.

"First we don't use that brand… we use 'Glass Plus'… and second its not likely for us to forget it in your room and if so we would have came and picked it up since afternoon!"

"I assumed may be you guys forgot it this evening!"

"No way! We only do the cleaning in the morning unless requested by the customer!"

Nikabaki namuangalia tu huku nahema juu juu. Kuna kitu nilianza kuking'amua kichwani na sikukipenda. Kiliniogopesha.!!

"Sir is everything OK?" Yule binti akaniuliza kwa udadisi.

"I am perfect! Thank you!!"

Nikamjibu huku naondoka kwa kasi bila kuangalia nyuma. Moyo nilikuwa nausikia unadunda kama vile unataka kutoka. Niliogopa mpaka miguu ikawa inagongana nikitembea. Nilielewa ni nini kimetokea chumbani kwangu. Na kwa nini harufu hiyi ilitawala chumbani kwangu kila mahala.
Kutokana na mapambano yangu na The Board mwaka mmoja uliopita yalinipa uzoefu wa kujua mambo mengi ambayo watu wengi hawayajua. Nilielewa nini kimetokea kwenye chumba changu cha hotel na kila nilivyozidi kuunganisha nukta nilitamani nipae nipotee au ardhi ipasuke nisionekane.

Kemikali ya kusafisha vioo (glass cleaner) ndio njia bora zaidi ya kufuta alama za vidole kwenye kitu chochote. Ukifanya tukio lolote na hutaki kubakisha alama za vidole ili usije kubainika basi tumia glass cleaner kufuta kila mahala ulikoshika.
Hii ilimaanisha kwamba muda mchache kabla sijarejea hapa hotelini kuna kitu kimefanyika chumbani kwangu na baada ya kitu hiki kufanyika walioyekeleza wamefuta alama zao za vidole.!!

"What the *** is going on here?"

Niliongea kwa sauti kubwa na kwa hasiri huku natetemeka ma kuvuja jasho.

Kichwani nilikuwa na lundo la maswali ambayo hayana majibu na sasa nilianza kuhisi hatari juu ya maisha yangu mimi mwenyewe.!!




ilItaendelea…



Habibu Anga 'The Bold' - 0718 096 811
To Infinity and Beyond

Pls: WhatsApp, follow and subscribe
 
e0f90dcf75982dce4b3fbf379d3abd89.jpg




VIPEPEO WEUSI



SEASON 1 - FROM ZURICH WITH RULES



EPISODE 18


Nilikuwa bado nimesimama katikati ya chumba changu cha hoteli nikitazama na kujaribu kufikiri. Bado nilikuwa naisikia ile harufu ya windex kwa mbali sana puani kwangu. Nilijiuliza kama huyu mtu ambaye aliingia chumbani kwangu humu na kufanya kile ambacho alikifanya na kisha kufuta alama zake za vidole kwa sababu ambayo sijaijua mpaka sasa, nilijiuliza hilo kopo la hii windex alisahau kwa makusudi au bahati mbaya. Kuna nini kilikuwa kinaendelea? Safari yangu ya kuja hapa Zurich imekuja kunichanganya zaidi akili na kuniacha na maswali mengi kuliko majibu. Nilidhani uwepo wangu hapa Zurich ungelisaidia kunitoa gizani rohoni mwangu, giza ambalo limekaa nafsini mwangu kwa takribani mwaka mzima tangu siku ambayo baba yangu alijipiga risasi mbele yangu. Lakini safari yangu hapa Zurich kwa sasa nilihisi imeniingizia giza zaidi nafsini badala ya mwanga niliokuwa nautarajia.

Niligeuka tena huku na huko pale chumbani. Kichwani sikuwa napata jawabu lolote la nini hasa kilikiwa kinaendelea. Kitu pekee nilichokuwa nakihisi ni ukimya. Kwa mara ya kwanza nikahisi labda ukimya huu ninao hisi kila mara hauko kwenye chumba hiki bali upo nafsini mwangu. Ukimya wa upweke na ukimya wa kujihisi kupotea.

Nikaitazama simu yangu niliyoiweka juu ya meza pale katikati ya sebule, niliitazama kwa sekunde kadhaa nikitamani walau ilie na juu yake kwenye kioo nione namba kutoka Tanzania, namba ya mkewangu Cheupe. Lakini zilikuwa zimepita siku kadhaa bila kuona simu ya Cheupe na mimi sikujua ni kitu gani ambacho kilikuwa nafsini mwangu lakini nilishindwa kuinua simu na kumpigia.

Nikafumba macho kwa nguvu huku nikiinua viganja vya mikono na kujifunikanavyo usoni. Ilikuwa kana kwamba ulimwengu wangu wote unadondoka mbele yangu huku nikiutazama nisijue ni nini cha kufanya.

Kuna muda mtu unatamani labda ungeliweza kuandika namna gani unataka maisha yako yawe. Unatamani uandike kama riwaya tamu kuhusu maisha yako na hayo ndio yawe maisha yako halisi. Upweke ambao uko nao nafsini ujazwe na kufunguka na nyuso za tabasamu. Hofu ulizo nazo zigeuke kuwa uimara wa kuitafuta kesho nyingine yenye furaha zaidi. Kiza ambacho kimeijaza nafsi yako ukiondoe kwa nyakati murua za nuru.
Unatamani uwe mwandishi mahiri wa riwaya halisi ya maisha yako. Unatamani kila kitu kiwe sawia vile ambavyo unaota usiku.

Lakini hatukujaliwa karama hii ya kuandika maisha yetu tunataka yaweje, tumepewa maisha ambayo hatukuyachagua. Hatuwezi kuchagua maumivu gani tuyapitie katika maisha. Hatuwezi kuchagua mateso, hatuwezi kuchagua mafarakano, hatuwezi kuchagua taharuki, hatuwezi kuchagua machozi, na wala hatuwezi kuchagua moyo mgumu. Na ndio maana katika nyakati za fadhaa kama siku hii ya leo kila siku usiku ni swali moja tu tunajiuliza kichwani, kwa nini? Kwa nini hatukujaliwa karama ya kuwa waandishi wa maisha yetu tuyatakayo.

Ukiwa katika fadhaa namna hii kuna muda unashindwa kuona uhalisia, uhalisia wa kwamba maumivu haya ndio ambayo yanafanya furaha ya kesho iwe na ladha tamu na nzuri zaidi. Maumivu haya yakishapita na kuona ni namna gani maisha yanaweza kuwa sio kumbukumbu ya yalikuwaje, ndipo hapa ambapo unageuka nyuma na kukumbuka siku hizi za fadhaa, siku hizi za upweke, siku hizi za kujihisi umepotea na kumshukuru Mungu kwa sababu bila maumivu haya ya leo usingeweza kuona utamu wa furaha ya kesho na uimara wa moyo wako.

Nikageuka tena huku na huko kutazama sebule na chumba hiki cha hoteli. Bado nilikiwa nahisi ule ukimya, bado puani nilikuwa nasikia harufu ya ile windex ya kusafishia vioo vya madirisha. "Go back yo your hotel and wait", nikakumbuka kauli ya mwisho ya yule mzee wa kichina.

"Wait for what.!?"

Nikajikuta nang'aka peke yangu kwa hasira. Tangu nimefika hapa Zurich imekuwa ni mfululizo tu wa kupokea amri na maagizo nisiyoyaelewa ambayo yananichanganya akili siku baada ya siku. Mara ya kwanza nilipewa maelekezo ya kwenda kwenye lile jengo la HARDSTRASSE 201, 1985. Huko nako nikakutana na ujumbe wa kurekodi wa marehemu baba yangu ambao ulinifikisha mpaka kwa kikundi cha Hudini. Kule nako nimepewa lundo la nyaraka bila maelezo yoyote yale. Na hata baada ya kung'amua japo ukweli mdogo kwenye zile nyaraka na kisha kufika kwenye ule mgahawa wa kichina bado huko nako napewa maagizo ambayo siyaelewi. Ati "go back to your hotel and wait.!?"

"Wait for what??" Nikang'aka tena huku nikiinuka kutoka kwenye sofa na kuanza kutembea pale sebuleni kwa hasira.

"Wait for what?" Nikaongea kwa hasira zaidi nikitembea kutoka upande mmoja wa sebule mpaka mwingine na kurudi tena.

Kichwani mwangu nikaanza kujewa na hisia kwamba kama nitaendelea kufuata maelezo haya ambayo siyaelewi na kwa kiaisi fulani nikiyaona kama hayanisaidii ninaweza kukaa hata mwaka mzima hapa Zurich na nisifanikishe chochote kile. Nikaanza kujewa na hisia pia kwamba labda inawezekana watu hawa wanataka kunitumia ili kufanikisha lengo lao fulani ambalo labda wanashindwa kulifanikisha bila mimi. Kwa sababu inawezekanaje nipewe lundo la nyaraka pamoja na picha alafu anayenipa anadai kwamba hajui chochote kile kuhusu nyaraka hizo au picha hizo.

Nikaanza kuvuta kumbukumbu ya zaidi ya mwaka mmoja uliopita, namna ambavyo nilipambana na kuidondosha jumuiya ya siri ya The Board mimi mwenyewe pekee. Moyoni nikaanza kujawa na ushujaa, kama niliweza kufanya vile kipindi kile nawezaje kushindwa kufanya hivyo sasa?

"Nimekuja Zurich kutafuta majibu sio kupata vitendawili zaidi… am done taking orders from anyone!"

Nikatembea kwa hasira mpaka chumbani na kuanza kutoa mabegi yangu ya safari kutoka kwenye kabati. Nikapanga vitu vizuri pamoja na lile lundo za nyaraka nilizozitoa kule kwenye nyumba ya baba yangu au yangu kama nilivyoelezwa pamoja na nyaraka ambazo nilipewa na Hudini.

Nikarudi sebuleni mezani ambako kulikuwa na ile chupa ya windex niliyoikuta bafuni. Nikaitazama kwa sekunde kadhaa kisha nikakata shauri kwamba nayo niichukue. Nikafungua tena begi na kuiweka ndani.

Sikutaka kupoteza muda, kwa haraka kabisa nikatoka chumbani humu na kushuka mpaka chini mapokezi.

"Are you checking out, Sir?" Muhudumu wa pale mapokezi aliniuliza huku akiwa na uso wa mshangao.

"Yes!" Nikamjibu kwa kifupi tu.

"Sir, are you sure?" Akaniuliza tena huku akiwa na uso wa mshangao zaidi ambao alikuwa anajitahidi kuuficha. Nilikuwa naongea naye huku nikimuangalia na nikibofya bofya simu yangu. Lakini nilipoona mshangao wake pale usoni ilinibidi niache kubofya simu na kumuangalia kwa makini zaidi.

"Is there a problem mam?" Nikamuuliza huku nimemkazia macho kwa makini zaidi.

Nilimuona namna ambavyo alikuwa anajitahidi kuficha uso wake wa mshangao na wasiwasi. Nilianza kuhisi kama kuna kitu fulani binti huyu alikiwa anakijua ambacho kilimfanya ashangae kuona naondoka na awe na wasiwasi huo. Nikamkazia macho zaidi kwa umakini niweze kumsoma anachowaza.

"Are you ok?" Nikamuiliza baada ya kumuona kama amepatwa na kitete hivi baada ya kujitahidi sana kuficha hisia zake usoni.

"I am fine, thank you sir..! aah here is your bill, sign here please..!" Alijitahidi kupeleka mazungumzo kwenye muelekeo mwingine lakini bado nilikuwa nahisi wasiwasi na taharuki yake usoni.

Kwa muda wa kama nusu sekunde tu hivi kwa haraka sana nikamuona ametupa jicho nyuma yangu, kama kuna kitu hivi alikuwa anatazama nyuma yangu lakini hakutaka nijue ni kitu gani. Kwa hiyo aliangalia kwa haraka sana na kisha kurejesha macho pale kwenye 'kaunta' ambako aliniwekea karatasi nisaini kwa sababu nilikiwa natoa fedha tasilimu.


Nikavuta ile karatasi na kuanza kuandika. Nikajaza haraka haraka na kisha kuingiza mkono mfukoni, nikatoa hela na kumpa…

"Keep change…"

"Thank you sir and thank you for staying at……"

Nikamsikia anaongea kwa mbali lakini akili yangu hata haikuwa inamsikiliza tena. Niligeuka haraka ili nione ni kitu gani hasa ambacho alikuwa ametupa jicho na kukitazama kwa haraka haraka huku akijaribu kuficha nisijue anacho kiangalia.
Pale mapokezi mbele yake kulikuwa na eneo kubwa la kupumzika. Kulikuwa na masofa makubwa kama sita hivi ya kukaa watu wawili wawili na mawili ya kukaa watu watatu au wanne. Katikati kulikuwa na meza nadhifu ya mbao ambayo ilionekana ilikuwa ghali na adimu. Pembeni karibu na ukuta kulikuwa na 'water dispenser' pamoja na sehemu ya kahawa ambako niliona watu kama watatu hivi, wawili wakitengeneza kahawa na mmoja akichukua maji.

Kwenye moja ya sofa kubwa kulikuwa na mama pamoja na watoto wake wawili mmoja akiwa amekaa naye kwenye sofa na mwingine amekaa sakafuni akichezea mdoli. Kwenye sofa lingine moja kulikuwa na vijana wawili wa kizungu, mmoja wa kike na wa kiume. Kutokana na walivyokuwa wanaongea kwa kudalizana daliazana ni dhahiri kabisa kwamba walikuwa ni wapenzi.
Lakini macho yangu yaliganda kwenye sofa lingine dogo la kukaa kama watu wawili hivi lakini lilikuwa limekaliwa na mtu mmoja. Mtu huyu ndiye ambaye mara moja nilihisi kwamba yule muhudumu alikuwa amemuangalia kwa kuibia ibia kwa haraka nisijue.

Mtu huyu ndiye alikuwa mtu mweusi kati ya wote ambao walikuwa hapa mapokezi. Au kwa usahihi zaidi niseme mimi na yeye ndio ambao tulikuwa watu weusi pekee. Alikuwa kichwani amevalia kofia nyeusi ya 'pama' pamoja na koti jeusi refu ambalo lilifika mpaka chini kidogo ya magoti. Alikuwa ameinamisha kichwa chake akisoma gazeti ambalo amelishikilia mikononi mwake katika namna ambayo nilishindwa hata kuona sura yake. Alikuwa ametulia kimya kabisa kiasi kwamba kama alikuwa haoni chochote cha zaidi pale mapokezi zaidi ya gazeti lake ambalo alikiwa ameinamisha kichwa kulisoma.
Kwa asilimia zote nikahisi kabisa kwamba huyu ndiye ambaye yule muhudumu alikuwa anamuangalia. Nikaanza kujiuliza ni nani huyu? Au ndiye ambaye alikuwa amepekuwa chumbani kwangu na kisha kufuta alama zake za vidole kwa windex? Anataka nini?

Lakini kabla ya huko kote swali la msingi zaidi likaninia kichwani, kwa nini huyu muhudumu alimuangalia kwa kificho? Kwa nini muhudumu huyu wa mapokezi alipata taharuki aliponiona nimekuja mapokezi 'kucheck out'? Kuna kitu gani ambacho alikuwa anakijua?
Muhudumu huyu ndiye yule yule ambaye dakika kadhaa zilizopita niliposhuka kuja kuuliza kama wamesahau windex chumbani kwangu, ni yeye huyu ambaye nilimkuta hapa mapokezi. Kuna nini kilikuwa kinaendelea?

Nikageuka kumtazama tena yule muhudumu. Kumbe alikuwa ameganda ananitazama muda wote huu… nilipogeuka tu na macho yetu kugongana akalazimisha tabasamu na kisha kugeuka pembeni akijifanya kuendelea na shughuli zake nyingine. Kichwani nilipata kiaisi fulani cha uhakika kwamba muhudumu huyu kuna kitu anakifahamu. Lakini sikuwa na muda zaidi wa kupoteza. Nikabeba mabegi yangu na kutoka nje ya hoteli. Nikatembea hatua kadhaa mpaka barabarani na kuita Taxi.

"Where are we going Sir.!" Muendesha Taxi akaniuliza kwa tabasamu mara tu baada ya kupanda kwenye Taxi.

"Just drive..!" Nikamjibu huku macho yangu yakiwa yanaangalia kwenye kioo cha gari cha kutazama nyuma.

"What?" Dereva akauliza tena huku ananiangalia kwenye kioo kwa sura ya kukereka.

"Hey man!! Just drive?" Nikaongea kwa kufoka.

Niliona uso wa mshangao wa dereva akiniangalia kwenye kioo… hakusema chochote, aling'oa gari na kuanza kuendesha. Macho yangu bado yalikuwa yameganda kwenye kioo cha kutazama nyuma nikiangalia pale hotelini nilikotoka.

Kama sekunde thelathini tu baada ya gari kuondoka pale Hotelini nikiwa bado naangalia nyuma kwa kioo, niliwaona wale vijana wawili wa kizungu waliokaa pale kwenye sofa, wa kike na wakiume ambao walionekana kama wapenzi nao walitoka hotelini haraka haraka wakasimamisha Taxi na kuanza kuja uelekeo huu huu ambao sisi tulikuwa tunaelekea.


Official Robot: Moyo ukanilipuka, nilihisi kabisa hawa vijana wananifuatilia mimi. Nilipokuwa pale mapokezi sikuwatilia shaka yoyote bali shaka yangu ilikuwa kwa yule jamaa mweusi mwenye kofia ya 'pama' na koti refu akisoma gazeti.

Dereva alipoendesha gari umbali wa kama dakika moja hivi nikamuamuru asimame. Nilifanya hivi ili nione ile Taxi ya wale vijana nyuma yetu itafanya nini. Ajabu nayo ikasimama kama hatua ishirini hivi kutoka pale tuliposimama sisi.

"Sir, what's going on?" Dereva aliniuliza kwa wasiwasi.

"Wait a little bit" niliongea huku nimegeuka nyuma nikiitazama Taxi ya wale vijana ambayo ilikuwa imesimama nyuma yetu kama umbali wa hatua ishirini. Walisimama kwa muda wa kama dakika moja hivi kisha sikujua kwa nini lakini walionekana kubadili mawazo. Nikaona Taxi yao ikiondoka na kutupita pale tuliposimama.
Haraka haraka nikaingiza mkono mfukoni haraka haraka na kutoa noti mbili ambazo sikumbuki zilikuwa za faranga ngapi, nikamkabidhi dereva na kushuka kwenye Taxi.

"Keep change!" Nikaongea huku nimeanza kuondoka.

Nikatembea kwa miguu kurudi kule tuliko toka, hotelini. Sikujua ni kwa nini nilikiwa narudi, lakini akili yangu iliniambia kwamba nirudi hotelini… nilihisi kabisa kuna suala la zaidi ambalo nahitaji kuling'amua.
Kutokana na kwamba hatukuwa tumeenda mbali sana na Taxi kwa hiyo kama baada ya dakika tano tu nilikuwa nimefika Hotelini. Nikafungua mlango wa mbele na kuingia mapokezi.

Yule mama mwenye watoto wawili alikuwa pale pale na watoto wake. Pale kwenye kutengeneza kahawa na maji ya kunywa safari hii kulikuwa na mtu mmoja tu akitengeneza kahawa. Ajabu ni kwamba yule jamaa mweusi, mwenye kofia ya pama, na koti jeusi alikuwa amekaa pale pale na katika 'pozi' lile lile akiwa anasoma gazeti.

Nikageuka kutazama mapokezi. Macho yangu yaligongana na ya yule muhudumu. Safari hii alishindwa kabisa kuficha mshituko wake. Alinitazama kwa mshangao mkubwa aliponiona nimeingia tena hotelini usoni akiwa na taharuki kama vile alikuwa kama vile ameona jini. Nikamkazia macho na kuanza kutembea kwa haraka kuelekea pale alipo. Kila nilivyokuwa napiga hatua ndivyo ambavyo alizidisha taharuki usoni. Akaanza kuniangalia mimi alafu anahamisha macho anamtazama yule jama mweusi mwenye kofia na koti. Ananitazama mimi, kisha yule jamaa. Tena na tena kana kwamba kuna kitu alikuwa anategemea kitokee.
Nikaelewa kwamba hisia zangu za awali sikukosea, mwanzoni huyu muhudumu alipotazama nyuma yangu alikuwa anamuangalia jamaa huyu mweusi. Nikajiuliza tena, kama huyu jamaa ndiye wa kumtilia shaka, wale vijana wa kizungu walionifuatilia nyuma na Taxi ni akina nani?

Nikaendelea kupiga hatua kwa haraka kuelekea pale mapokezi. Kila hatua ambayo nilikuwa napiga ndivyo ambavyo nilianza kuelewa ni nini kilikuwa kinaendelea hapa…


Itaendelea…


The Bold - 0718 096 811
To Infinity and Beyond

Pls: WhatsApp, Follow and Subscribe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom